Kwa mara ya pili mfululizo timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani
kutoka Tanzania imetinga fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la
Watoto wa Mitaani baada ya kuchachafya timu ngumu ya Marekani magoli 6
kwa 1, kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya mashindano haya hapa
Rio de Janeiro.
Tanzania ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya pili ya
mchezo goli likifungwa na Michael, baada ya kuingia goli hilo Marekani
waliweza kupoteana na kuwafanya vijana wa Tanzania waliokuwa wakitandaza
soka safi kufunga magoli mengine matatu ya haraka haraka na kufanya
matokeo ya mchezo kuwa magoli manne kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Tanzania ilizidi kuishambulia marekani na
kufanikiwa kufunga magoli mengine mawili ya haraka haraka na kuifanya
Tanzania kufikisha magoli sita katika mchezo huo wa nusu fainali huku
mshambuliaji wa Tanzania Michael akifunga magoli manne nakuweza kuibuka
nyota wa mchezo.
Goli la Marekani lilifungwa na katika dakika za mwisho za mchezo
baada ya kipa wa Tanzania Emmanuel kuutema mpira mkali uliopigwa
kuelekea golini kwake na baadae mchezajiwa Marekani kuukwamisha wavuni.
Tanzania leo imetandaza soka safi la kuvutia huku wakipiga mikwaju
hatari kuelekea goilini kwa Marekani, waioonekana kupotea kabisa. Mpaka
wanaingia nusu fainali Marekani walikuwa hawajapoteza mchezo wowote, na
waliweza kuwafunga wenyeji Brazil magoli matani kwa matatu kwenye mchezo
wao wa robo fainali.
Timu nyingine iliyoingia kwenye fainali ni Burundi baada ya
kuifunga Pakstani magoli 4 kwa matatu, hadi kipindi cha kwanza
kinamalizika Pakistani walikuwa wanaongoza kwa magoli 3 kwa moja,
kipindi cha pili Burundi waliweza kurudisha magoli yote na kuweza
kuongoza na kushinda jumla ya magoli manne kwa matatu.
Hivyo Tanzania itacheza na Burundi kwenye mchezo wa fainali hapo
kesho kwenye uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense katikati
ya Jiji la Rio de Janeiro huku mgeni rasmi wa mechi hii akiwa Waziri wa
fedha wa Uingereza, George Osborne, Waziri wa jinsia na Watoto na pia
Meya wa Jiji la Rio de Janeiro.
Ikumbukwe kuwa katika mechi ya kwanza katika kundi 2 la michuano
hii Tanzania ilicheza na Burundi na kutoka sare ya magoli mawili kwa
mawili. Huku Burundi ikirejesha magoli yote mawili katika kipindi cha
pili. Mechi ya fainali kesho itakuwa ngumu sana kwani Burundi wana
wachezaji wengi waliozidi umri, na wanatumia nguvu kubwa sana. Tanzania
itawatengemea wachezajia wake wanaocheza kitimu zaidi na wenye kuweza
kupiga mashuti langini mwa timu pinzani.
0 comments:
Post a Comment