Tuesday, April 15

                   

Jaji mkuu wa Tanzania Othman Chande katika mjadala huo.
 Sehemu ya wajumbe wakifuatilia kwa makini
 Wajumbe wengine


 Picha ya pamoja juu na chini

Kutoka kulia ni mshiriki kutoka Marekani, katikati ni Dr.Edward Hosea na wa mwisho ni Jaji mkuu wa Tanzania Othman Chande wakibadilishana mawazo.


Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini imeandaa mjadala kuhusu sheria ya ushahidi ili kutatua kero za wananchi na kutoa haki.

Mjadala huo unaofanyika jijini Mwanza katika Hoteli ya Malaika na unahusisha Majaji wa Mahakama ya rufani Nchini na wataalamu kutoka chuo kikuu cha Northwest cha Nchini Marekani.

Mkurugenzi wa TAKUKURU Dk. Edward hosea amesema wameamua kushirkiana na taasisi mbalimbali ili kuboresha utoaji haki kwa wananchi.

Jaji mkuu wa Tanzania Othman Chande amesema hiyo ni fursa kwa majaji ambao kazi yao ni kutafasiri sheria kuboresha mapendekezo yaliyotolewa na Takukuru kupata sheria mpya ya ushahidi.

0 comments:

-