Mtanzania
yeyote ambae anajua utaratibu wa usafirishaji kwenye nchi zilizoendelea
kama South Africa, Uingereza na mataifa mengine duniani, anaweza
kushawishika kutamani utaratibu huo ungekua unapatikana pia na nyumbani
Tanzania.
Nilikua natazama TBC1 nikaona interview fupi ya Waziri wa uchukuzi
Harrison Mwakyembe na nikafanikiwa kuipata akisema itajengwa reli nchini
Tanzania kwa nguvu ya Uingereza baada ya kuona umuhimu wa matumizi ya
reli kusafirisha mizigo na abiria ili kuepukana
na yote yanayotokea
barabarani.
Taarifa ilisema pia kuna mpango wa baadae wa kuleta treni za kisasa
zinazotumia umeme ambazo zina sifa ya kufanya kazi kwa uharaka na
uhakika kote duniani.
Una chochote cha kusema kuhusu hili?
0 comments:
Post a Comment