Sheria
mpya inatengenezwa Kenya sheria hiyo itawataka wanaowazungumzia wakuu
wa serikali kufanya mazoezi ya kutosha kwani sheria hii ikipitishwa basi
inamaana kwamba Rais,Naibu wake na wake zao pekee ndiyo watakao pewa
jina Mtukufu au His/Her Excellency.
Unaambiwa yeyote atakaye kosa kuzingatia hilo adhabu yake atafungwa
mwaka mmoja Gerezani au kutozwa faini ya shilingi milioni moja pesa za
Kenya sawa na dola elfu 12 za Marekani.
Yeyote atakaye vunja sheria ya kukosa kumuita Mbunge kwenye bunge la
kitaifa Mheshimiwa au Honorable
atafungwa mwaka mmoja au faini ya
shilingi milioni mbili pesa za Kenya.
Kwenye mpangilio Rasmi wa Itifaki ama pecking order Rais atafatiwa na
Naibu wake kisha Spiker wa bunge la taifa,Jaji mkuu,Seneta,Mbunge wa
Jimbo na wa mwisho ni Gavana.
Sheria hiyo pia inapendekeza kwamba spika wa bunge la taifa kuitwa
Right honourable ama Mheshimiwa mkuu na Jaji mkuu kuitwa
his/herloadship,itakua kosa vile vile kumuita mwakilishi wa Jimbo
Mheshimiwa hilo ni jina la Mbunge wa Bunge la Taifa peke yake.
Muswada huo uliotungwa na kuwasilishwa Bungeni na Mbunge Mheshimiwa
Aden keynan anaye sema kwamba sheria hiyo itasaidia kutoa mpangilio wa
vyeo kwa Taifa pia anapendekeza kwamba watumishi wa umma watakao
jilimbikizia vyeo watatozwa faini ya Dola milioni mbili.
Mswada huo unajadiliwa Bungeni wakati magavana serikali ya kitaifa,
wabunge na mahakama wako kwenye vita vya kubaini ni nani anauwezo wa
kutekeleza majukumu na mamlaka ya kutoa muelekeo kwenye maswala mbali
mbali yanayo husu usimamizi.
0 comments:
Post a Comment