Abiria
waliokuwa katika ajali ya meli nchini Korea Kusini wamesimulia
walichokishuhudia na kukisikia wakati meli hiyo ilipoanza kuyumba na
kuzama.Abiria hao wamesimulia katika nyakati tofauti lakini kwa mujibu wa BBC maelezo yao yamekuwa yakifanana.“Kwa
kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikaanza kuegemea uapande
mmoja. Watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli,
lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka.” Amesema
Kim Song-Muk.
Kikosi
cha walinzi cha Pwani ya Korea kusini kimesema abiria watatao mia tatu
hawajulikani walipo. Imeripotiwa kuwa watu wawili wamepoteza maisha na
watu 164 wameokolewa.
Bado
haijafahamika chanzo kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo ambayo
ilikuwa na jumla ya watu 460 na wengi wao wakiwa wanafunzi wa sekondari
waliokuwa wakielekea katika kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.
0 comments:
Post a Comment