Baada ya kugoma kuendelea kuhudhuria vikao vya bunge la katiba
Dodoma, Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoongozwa na Profesa
Ibrahim Lipumba na Freeman Mbowe ulitangaza kufanya mkutano Zanzibar
Jumamosi ya leo kuwaeleza wananchi kilichotokea ambapo baadae
wangetembea nchi nzima.
Mkutano huo ilikua waufanye leo April 19 2014 ambapo kutokana na
sababu za kiusalama zilizotolewa na Jeshi la Polisi Tanzania mkutani huo
haukufanyika.
YAH: TAARIFA YA KUSITISHWA MKUTANO WA HADHARA
Naomba urejee barua yangu Kumbu. Nam. W/MGH/SO/7/2/A/4 ya tarehe 17 Aprili, 2014 inahusika.
Ninakujulisha rasmi kuwa mkutano huo uliokuwa ufanyika tarehe 19
Aprili, 2014 hapo Viwanja ya Demokrasia Kibanda Maiti umesitishwa kwa
sababu za
KIUSALAMA WA NCHI.
Kwa barua hii unatakiwa kuwajulisha Wanachama na wapenzi wote wa
Chama kuwa watulivu kwa muda huu hadi hapo hali itakapo ruhusu kufanyika
tena kwa mkutano huo.
Tafadhali nawasilisha.
RAMADHANI S. NGAMIA – SSP
MKUU WA POLISI,
WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.
Katika Taarifa ya habari iliyosomwa kupitia TBC1 imeeleza kuwa Jeshi
la Polisi Zanzibar limesitisha mikutano yote ya hadhara ya vyama vya
siasa visiwani humo ambapo hiyo imesemwa na kamishna wa Polisi Zanzibar
Hamdan Omar Makame wakati alipokutana na viongozi waandamizi wa vyama
vya CCM na CUF katika makao makuu ya Jeshi la Polisi Ziwani Zanzibar.
Kabla ya kutolewa tamko hilo UKAWA walipanga kufanya mkutano kama
ilivyoelezwa hapo juu wakati UVCCM walipanga kufanya mkutano wa hadhara
kesho April 20 Jumapili katika eneo la Mabata.
0 comments:
Post a Comment