Sunday, April 20

 

1.DIamond platinum
 Ukiachilia mbali wingi wa wasanii wanaofanya vizuri kwenye tasnia mbali mbali apa bongo, sio wote wanaobahatika kukubalika na kupokelewa vizuri na Jamii/mashabiki. Hawa ndio wasanii wenye mvuto zaidi na wanaoongoza kwa kupendwa na mashabiki.
Anaweza akawa sio muimbaji mzuri kama Alikiba au barnaba, ila haina ubishi huyu ndiye msanii wa kiume kwa upande wa bongo fleva anayeongoza kwa kupendwa zaidi na mashabiki, jina lake linazidi kukua siku hadi siku na kazi zake zinafanya vizur karibia east Africa nzima.

2. Wema sepetu

Sio muigizaji mzuri kumshinda Johari, wala hana filamu nyingi sokoni kuliko Irene uwoya, ndio maana hata waandaji wa tunzo za filamu hawajawahi kum nominate hata kwenye category ya msanii chipukizi bora, hiyo haijafanya jina lake lishuke kwenye Tasnia hiyo, Bado haina ubishi wema ana nyota Kali na anapendwa kuliko msanii yeyote. mwenyewe anajiita ENDLESS FAME.



 
 
 
 
 
3. LADY JAYDEE

Kiuno chake kina mfupa, hana mauno makali kumzidi Snura mushi, sauti yake nzuri na kipaji cha pekee alichobarikiwa kimemfanya apendwe zaidi na mashabiki kibao. Unadhani ana pesa sana kuliko ruge? Hakustahili kabisa kushindana naye , ila jeuri ya mashabiki aliyonao ilimfanya ajione malkia , nadhan unakumbuka Team anaconda ilifanya nini pale Nyumbani Lounge. Jide ana nyota Kali sana.




4. JB

Kipaji chake hakikumfikia marehemu kanumba(r.I.p),sio director mzuri kama Jackson kibirigi, ubunifu alionao kwenye filamu zake umemfanya apendwe zaidi na mashabiki kuliko msanii yeyote wa kiume kwa upande wa filamu apa bongo.




5.Lulu Michael

Hajawahi kuigiza vizuri kama Diana kimaro(Danija,Kigodoro) ila ana nyota nzuri sana, licha ya umri mdogo alionao , anapendwa na ana mashabiki wengi zaidi.




6.Monalisa












Hana umbo kama masogange, kipaji cha kipekee alichonacho na umakini alionao kwenye uigizaji umemfanya ajiongezee mashabiki wengi zaidi.




7. Ray kigosi
















 
 Sio muigizaji mzuri kumshinda Gabo, kampuni makini aliyonayo na aina ya waigizaji anaowatumia imemfanya kazi zake zinunuliwe zaidi kuliko kampuni yeyote apa bongo. Steps ilishawahi kusema kuhusu kazi za waigizaji zinazonunuliwa kama njugu, ray alishika namba mbili akitanguliwa na kanumba.


8.Johari


Hana swagger kama wema sepetu, kazi zake na umakini alionao kwenye uigizaji , vimemfanya apendwe zaidi na mashabiki , ndo maana hadi Leo kazi zake zipo juu.
credit : swahilitz

0 comments:

-