Monday, April 28

Mchezaji wa timu ya Barcelona Dani Alves, arushiwa ndizi akiwa uwanjani na kuitwa nyani na baadhi ya mashabiki waliokuwa uwanjani katika mechi iliyochezwa jazi usiku dhidi ya Villarreal
Baada ya mmiliki wa timu ya kikapu ya LA Clippers, Donald Sterling, kumwaga kauli za kibaguzi zilizosababisha reaction kutoka kwa watu mbali mbali akiwemo Raisi Obama, jana nimeshuhudia aina hiyo hiyo ya ubaguzi kutoka kwa mashabiki kwenda kwa mchezaji wa timu ya Barcelona "Dani Alves".


Alves alirushiwa ndizi hiyo akiwa katika harakati za kupiga kona, ndipo yeye alipoamua kuichukua ndizi hiyo na kuimenya na kuila kisha akaendelea kupiga kona.Barcelona mpaka dakika ya mwisho walishinda kwa mgoli 3-2.

 nakumbuka maneno ya Obama aliyoyasema jana kuwa "tunajitahidi sana kukomesha hali hii ya ubaguzi lakini, naamini tutaendelea sana kukutana nayo kila siku zinavyozidi kwenda" ndo haya sasa

0 comments:

-