Wednesday, April 9

Maiti ikipambwaDuna hii imejaa matukio mengi sana na ya ajabu,huko Indonesia kuna utamaduni ambao si wa kawaida na pengine ni wa ajabu wa kufufua maiti kaburini  na kisha kuwapamba upya na kuwavisha nguo za thamani wavalie kama walivyokuwa hai.
Wakazi hao wa Jimbo la Twaraj huko  Indonesia wanakusanyika na kumfanyia sherehe kubwa maiti kabla ya kuanza msafara wa kumtembeza katika mitaa na kumrejesha kaburini alipokuwa amezikwa, wakazi hao wanamini kwamba watu waliyokufa wanahaki ya kuendelea kuishi na kujumuika nao.


 Na ili   kufanikisha zoezi hilo la kihistoria ambalo wanaimani kwa lazima kufanya ili kuonesha hishima kwa maiti na kulinda mapenzi ya kweli kwa mtu aliyekufa, kabla ya kumzika maiti anavishwa kitambaa maalum ili kuzuia mwili wa marehemu kuoza.

0 comments:

-