taarifa kutoka Kiambu
Kenya ambapo hisia tofauti zimetolewa kuhusiana na picha ya askari wa
kike wa usalama barabarani iliyofanya mabosi wake kumkemea.
Sababu kubwa ni picha ya Trafiki huyo aliyekua amevalia sketi fupi
iliyombana huku akiongoza doria wakati wa mashindano ya magari katika
kaunti ya kiambu ilisababisha picha iliyopigwa na mwanahabari wa gazeti
moja nchini Kenya kuzua mjadala kwenye mitandao ya kijamii Redioni na
Televisheni nchini Kenya.
Linda Okello ni afisa wa trafiki mwenye cheo cha koplo
aliitwa
ofisini na mkuu wa Trafiki kaunti ya kiambu James Mugeria na kumkemea
vikali akitaja kwamba vazi hilo linakiuka maantiki ya kikazi katika
kikosi cha polisi.
Baadhi ya watu waliotoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii wamesema
Trafiki huyu alilengwa na wakuu wake bila kosa ikizingatiwa kwamba sare
ama magwanda ya maafisa wa polisi hutolewa kwao na serikali na pia
kumekua na madai kwamba Linda alikua amepewa uhamisho kaunti ya Mandera
japo maafisa wakuu wa polisi wemekanusha madai hayo.
Haya yanajiri miezi kadhaa baada ya Naibu wa Inspekta mkuu wa polisi
Grace kaindi kuwaonya vikali maafisa wa kike wa polisi dhidi ya kutumia
lipstick, kuvalia mavazi ya kimtindo, bangili na vipuri virefu wakiwa
kazini.
Kifupi taarifa kwa mafisa wa polisi iliyotolewa ilisema afisa yeyote
atakayepatikana na mavazi yaliyopigwa marufuku atakua amevunja sheria
Nambari 37 na sheria kwa maafisa wa polisi wa mwaka 2011 kipenge numbari
87-88 na atakabiliwa kisheria.
0 comments:
Post a Comment