Saturday, April 26


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono 
wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya 
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika
 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na
 nje ya nchi.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.

 Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa
aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano.



 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

 Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.

 Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia 
kichwa na mikono.

 Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya
 umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.

 Kikosi cha Wanamaji 

 Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho
 ya Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha  Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.

 Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi
 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli .

 Maandamano ya Pikipiki.

 Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano .

Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu waliorusha njiwa hao nao wametimiza miaka 50.

0 comments:

-