Pale ambapo alijitokeza jamaa mmoja
na kwenda mpaka Mahakamani kupinga kitendo cha Biblia ambacho ni kitabu
kitakatifu cha Mungu kutumika kwenye shughuli za kuwaapisha Watumishi wa
Umma na kwenye Mahakama kuapisha mashahidi.
Taarifa mpya inasema Mahakama ya
upeo nchini Kenya imetupilia mbali kesi hiyo na kusema Mlalamikaji wa
kesi hiyo ambae ni David Gitahi hakutoa sababu zozote za kikatiba
kulazimu Mahakama kutoa uamuzi wa kuondolewa kwa Bibilia.
Mlalamikaji Gitahi alisema ametumwa
na Mungu kushughulikia changamoto na matatizo ya kiroho yanayo kabili
taifa la
Kenya lakini alipingwa na mwanasheria mkuu wa serikali Githu
Muigai aliesema kipengee cha katiba namba 74 kinaeleza ni lazima wakuu
katika serikali kuapishwa kabla hawajaanza kazi katika nyadhifa zao
tofautitofauti.
Kwenye lalamiko jingine Gitahi
alitaka viongozi wa Serikali wasitumie kiapo cha Biblia kwa sababu
wanashindwa kutimiza majukumu yao kama walivyoapa na hiyo inabebesha
nchi dhambi mbele za Mungu.
0 comments:
Post a Comment