Wednesday, March 12

Kutoka kwenye mitandao tofauti ya Marekani kuna stori zimemake headline zinazowahusisha Jay Z na Kanye West ambao ni washkaji walioshirikiana kufanya album moja ya Watch the Throne ambayo ilitoka August 08 2011.
Story hiyo inasema kuwa Jay Z amegoma kuwa best man kwenye harusi ya Kanye west na mpenzi wake Kim Kardashian.
Miongoni mwa sababu zilizotajwa ni  kusemekana kuwa Jay Z hapendi na hayuko tayari kutokea na kuonekana kwenye Reality Tv show,Jiga ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 44 ni mume wa Beyonce na tayari ni baba wa mtoto wa miaka 2 aitwae Blue Ivy.
Kwa sababu hizo ni kwamba Jay Z hatapenda kutokea kwenye show ya maisha ya familia ya Kardashian maarufu kama The Kardashians,gazeti la Daily Star limeandika kuwa Jay Z ndiye msanii rafiki mkubwa wa Kanye West na anavigezo vyote kuwa msimamizi wake,
Masharti aliyoweka Jay Z amedai atakubali kuwa Best man wa Kanye West endapo kama hapatakuwa na mpiga picha yoyote wa kipindi hicho cha Kim K,mpaka sasa waongozaji wa kipindi cha Kim K na mabosi wa kituo cha E wako tayari kutoa hata dola milioni 1 ilikupata Picha za Jay z na Beyonce kwenye harusi hiyo.

0 comments:

-