Mzungu
aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae amekamtwa
kikomandoo akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki.

Kwa
mujibu wa taarifa zilizonaswa na mtandao huu hatari kwa habari za
uchunguzi zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi
ya Euro hizo feki 700 mwandishi mwandamizi wa blog hii na DTV Bw.
Livingstone Mkoi mwanzoni mwa januari mwaka huu kisha kufungua kituo cha
polisi Oysterbay nakupatia kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA
KWA NJIA YA UDANGANYIFU,pamoja na Kutoa Euro Feki.
Baada
ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi
lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa
akishirikiana na wadada wawili ambao ni araia wa Cameroon na Nigeria
pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya tukio la kukatwa mwenzao
wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake
anaoshirikiana nao.ananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa
kufanikisha kukamatwa mzungu huyo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi kupigwa na mzungu huyo basi wafike haaka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo..Imeandaliwa na
Livingstone Mkoi
Livingstone Mkoi
RSS Feed
Twitter
March 06, 2014
Unknown
0 comments:
Post a Comment