Friday, March 14


Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite
Serikali ya Uchina imechapisha picha zilizonaswa na mtambo wake wa satelite zikionyesha mabaki ya kitu kipana kikielea katika bahari ya Kusini mwa Uchina.Picha hizo zilipigwa siku ya Jumapili, saa ishirini na nne baada ya ndege ya abiria ya Malaysia kutoweka ikiwa na abiria 239, lakini haijabainika ikiwa vifaa hivyo ni vya ndege hiyo.Huku ikiwa na raia wake 154, ambao walikuwa abiria kwenye ndege hiyo ya Malaysia, serikali ya Uchina imetuma mitambo kumi ya satellite kusaidia katika harakati za kutafuta ndege hiyo.Picha za vifaa hivyo vitatu, ambavyo moja ina upana wa takriban mita 24 kwa 22, zilichukuliwa siku ya Jumapili, siku moja tu baada ya ndege hiyo kupotea, lakini zilichapishwa siku ya Jumatano.


Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite
Ubawa wa ndege hiyo iliyopotea ina upana wa mita sitini na moja.
Picha hizo za satellite zimeweka vifaa hivyo takriban maili mia moja kutoka kwa njia iliyotarajiwa kutumiwa na ndege hiyo na sio mbali kutoka kwa kisima kimoja cha mafuta, ambako mfanyakazi mmoja aliripoti kuona kitu kilichokuwa kikichomeka angani siku ya Jumamosi asubuhi.
Lakini siku chache zilizopita, kumekuwa na fununu kadhaa kuhusiana hatma ya ndege hiyo lakini zote zimekuwa uongo.
Makundi ya uokozi hiyo vile vile wanatafuta mabaki ya ndege hiyo katika maji inayokaribiana na rasi ya Malaysia, kwa sababu wanaamini kuwa ndege hiyo ya Malaysia ilibadili mkondo na kuelekea Magharibi.


Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite
Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite





New developments: This map shows the two areas where the search for flight MH370 was focused in green. The blue X marks the spot where the large debris has been spotted by Chinese satellites. The black circle is where the New Zealand oil worker witnessed a plane burning in the sky

Checking: Chinese state broadcaster CCTV said that ships & planes were on their way to help search for MH370 after China's satellite found possible debris. They tweeted this picture and said that verification was in progress

Floating: These images from the Chinese satellite dated March 9 appear to show what could be fuel resting on the surface of the South China Sea and were taken in the zone where the three pieces of large debris were recorded

0 comments:

-