Thursday, March 13

Muimbaji wa muziki aliyewahi kuhit na wimbo wake ‘Binti Kiziwi’ Z-Anto amesema aliwahi kumkanya aliyekuwa mke wake, Sandra (msichana aliyeigiza kwenye video ya wimbo wake Binti Kiziwi), kuachana na makundi hatarishi aliyoanza kuwa nayo baada kupata umaarufu ambayo yalimfelisha kimaisha ikiwemo kufungwa jela nchini China baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya.
Z-Anto na Sandra siku ya ndoa yao
“Alishindwa kujicontrol na maisha ya ustaa hiyo ndio ikawa shida, akapata kampani za ajabu ajabu,” Z-Anto alimwambia jana mtangazaji wa kipindi cha Mseto cha Radio Citizen ya Kenya, Willy M Tuva.

Muimbaji huyo amekumbushia kuwa wiki moja kabla ya msichana huyo kusafiri kwenda China, ndio kipindi ilipotokea ajali ya Sharo Milionea, na kulikuwa na tetesi pia kuwa Sandra naye alipata ajali na kupoteza maisha na hivyo kumlazimu kufuatilia undani wake.
“Mwisho wa siku kama siku tatu nikampata, akaniambia ‘mbona mimi niko fresh’, nikamuuliza ‘mbona nimesikia umepata ajali’ akasema ‘hapana mimi niko sawa tu ila natarajia kusafiri kuna sehemu naenda kibiashara’. Nikasema ikiwa kama inafika hatua watu wanakuzushia kitu kama hiki hapa, yawezekana kuna kitu ambacho kinakuja. Lakini ilikuwa ni kweli kwamba kuna tatizo lilikuwa linakuja mbele yake na aliposafiri kwenye hiyo safari ndio alienda zake huko China kwa issue ya madawa, kufika zake kule kweli matatizo yamemkuta. Kwahiyo nikasema ni kweli ilikuwa ni ishara ya ajali kwake.” Z-Anto amesema mke wake huyo wa zamani alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela.
Bongo5

0 comments:

-