Abiria wakitoka kwenye gari hiyo baada ya kupinduka
Abiria wakisaidiwa na wasamaria wema kutoka kwenye gari hiyo
Hapa abiria wengine wakijiokoa wenyewe kutoka kwenye gari hilo.
FRANK KIBIKI, IRINGA
ZAIDI
ya watu kumi, wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya
rufaa ya Mkoa wa Iringa, baada daladala waliyokuwa wakisafiria kutoka
Frelimo kwenda Tumaini, mjini Iringa kuacha njia na kuanguka.
Ajali hiyo
imetokea mchana huu majira ya saa saba mchana, baada ya gari hiyo
kushindwa kupanda mlima, na badala yake kurudi nyuma kabla ya kutumbukia
kwenye mto.
Mwitikio
imewashuhudia wasamaria wema wakiokoa majeruhi waliokuwa wamepanda
daladala hiyo yenye namba za usajili, T 106 ABP ambao wote
wamekimbizwahospitali kwa ajili ya matibabu.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea
kwa ajali hiyo kwamba taarifa zaidi itatolewa baada ya uchunguzi
kukamilika
0 comments:
Post a Comment