HALI
ya Mtangazaji wa Channel 10, Salumu Mkambala aliyepata ajali alfajiri
ya leo kwa kugongana na lori akiwa safarini kuelekea Morogoro inaendelea
vizuri katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza
na mwandishi wetu hospitalini hapo, mdogo wa mtangazaji huyo, Ramadhani
Mkambala alisema kaka yake alikuwa akielekea Morogoro na alipofika
maeneo ya Vigwaza aligongana na lori alfajiri saa 10. 30 akiwa yeye na
mtu mmoja aliyempa lifti.
Hata
hivyo, chanzo cha ajali hiyo kilitajwa na Ramadhani kuwa ni kutokana na
barabara ya eneo hilo kuwa na mashimo mengi hali iliyosababisha gari la
kaka yake kuhama upande wake na kulivamia lori
Chanzo: GPL
RSS Feed
Twitter
March 02, 2014
Unknown
0 comments:
Post a Comment