Meli, helikopta na ndege zinashiriki katika zoezi la kuitafuta ndege ya shirika la ndege la Malaysia Airlines iliyopotea usiku wa ijumaa kuamkia jumamosi, machi 8 mwaka 2014. |
Juhudi
za kutafuta ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines iliopotea
usiku wa ijumaa kuamkia jumamosisaa ikiwa na abiria 227 zimeendelea
kushika kasi mapema leo asubuhi katika eneo la kisiwa kilichopo nchini
Vietnam ambapo inashukiwa huenda mabaki ya ndege hiyo yakapatikana
katika eneo hilo.
Baada ya masaa zaidi ya 48, matumaini ya kupatikana kwa ndege MH370 yameanza kukosekana.
Ndege hio
ya aina ya Boeing 777, ilikua ikitokea Kuala Lumper ikielekea Beijing
nchini China ikiwa na abiria 227 kutoka mataifa 14, wakiwemo 153 wa
China, raia 4 wa Ufaransa na timu ya watu 12 wakiwa ni wafanyakazi wa
ndani ya ndege hio.
Mamlaka
ya usafiri wa anga wa Vietnam imeendesha uchunguzi jana jioni na
kugundua vifaa viwili ambavyo huenda vilidondoka kutoka kwenye ndege hio
kwenye umbali wa kilomita 80 katika kisiwa cha Tho Chu.
“Lakini
hakuna taarifa yoyote kuhusiana na vifaa hivyo iliyotolewa”, amesema
Abdul Rahman, katika mkutano na waandishi wa habari.
Meli
mbili zimetumwa katika kisiwa cha Tho Chu, ili kuendelea na uchunguzi
zaidi, naibu mkurugenzi wa mamlaka ya anga ya Vietnam, Ngo Van Phat,
amelithibitishia shirika la habari la Ufaransa AFP.
Wakati
juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo zikiendelea, utata umeibuka juu
ya abiria ambao walikuwa wanatumia vitambulisho bandia.
Viongozi
wa Malaysia, ambao wameanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa tukio la
kigaidi kufuatia kupotea kwa ndege hiyo, baada ya kugundulika kua watu
wawili ambao walikua wakisafiri ndani ya ndege hio walikua na passport
bandia, wameendelea kuendesha msako katika maeneo yaliyo karibu na taifa
lao, kusini mwa kisiwa cha Thoi Chu.
Mkurungenzi
wa idara ya Usafiri wa anga nchini Malyasia Azharuddin Abdul Rahman
amesema hadi sasa hawajafaanikiwa kupata mabaki ya ndege hiyo licha ya
taarifa kutoka Vietnam.
0 comments:
Post a Comment