Wachezaji wa Young Africans Sports Club
Bao
la dakika ya 82 ya mchezo liliowekwa wavuni na Naodha wa timu ya Young
Africans Nadir Haroub "Cannavaro" limepelekea watoto wa Jangwani kuvunja
mwiko wa Waarabu baada ya dakika 90 za mchezo za mwamuzi Bezez
Haileysus kumalizika na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliofanyika
dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo tangu ianze kushiriki mashindano ya Klabu
Bingwa Barani Afrika ilikuwa haijawahi kupata ushindi katika mchezo
wowote zaidi ya kutoka sare, leo imeushangaza umma na dunia kwa ujumla
kwamba ni timu nzuri na inaweza kupamabana na timu yoyote.
Mashabiki
wa soka walijitokeza kwa wingi leo kuipa sapoti timu ya Young Africans
kutokana na kuwa na imani kwamba uwezo wa kikosi cha Young Africans
umekamilika kila idara na ndivyo hali ilivyokuwa katika dakika 90 za
mchezo.
Washambuliaji wa Young Africans walikosa nafasi zaidi ya
nne kipindi cha kwanza kutokana na kutokua makini na kukuta mashuti yao
yakiokolewa na walinzi wa Ah Ahly na mlinda mlango wao Sherif Ekramny.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Al Ahly.
Kipindi
cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko kwa lengo la
kuhakikisha wanapata mabao ya mapema lakini mabadiliko hayo yaliisadia
Young Africans zaidi kuweza kumiliki mchezo na kutawala eneo la ulinzi.
Baada
ya Young Africans kufanya mashambulizi langoni mwa Al Ahly mlindao
mlango Ekramny alianza kupoteza muda huku wachezaji wa ndani ndao
wakijiangusha mara kwa mara wakifikira kupoteza muda na mchezo
kumalizika kwa sare.
Dakika ya 82 ya mchezo kona iliyopigwa na
Saimon Msuva ilitua kichwani kwa Nahodha Nadir Haroub "Cannavaro" na
kuukwamisha wavuni na kuwaacha mabingwa watetezi Al Ahly na benchi la
Ufundi wakiduwaa.
Bao hilo liliamsha shangwe kwa washabiki,
wapenzi na wanachama kwa ujumla na kuwafanya Al Ahly kupoteana uwanjani
na kama umakini wa washambuliaji wa Young Africans ungekua makini basi
wangeweza kuongeza bao la pili.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 1 - 0 Al Ahly.
Mara
baada ya mchezo kocha wa Young Africana amesema anashukuru vijana wake
wamecheza vizuri mchezo wa leo, walipata nafasi nyingi lakini
walishindwa kuzitumia na kutumia nafasi moja iliyopelekea kupata bao
hilo la ushindi.
Kocha Hans amesema ameona mapungufu
yaliyojitokeza katika mchezo wa leo watayafanyia kazi kuanzia jumatatu
mchana kabla ya safari ya kuelekea Cairo nchini Misri katikati ya wiki
tayari kwa mechi ya marudiano siku ya jumapili Januari 09 mwaka huu.
Young Africans:
1.Deo Munish "Dida", 2.Mbuyu Twite, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub
"Cannavaro", 5.Kelvin Yondani, 6.Frank Domayo "Chumvi", 7.Saimon Msuva,
8.Haruna Niyonzima, 9.Emmanuel Okwi, 10. Mrisho Ngasa/Said Bahanuzi,
11.Hamis Kiiza/Didier Kavumbagu
RSS Feed
Twitter
March 01, 2014
Unknown
0 comments:
Post a Comment