Mshambuliaji
wa kimataifa wa timu ya Taifa Uganda na klabu ya Young Africans
Emmanuel Arnold Okwi leo ameruhiswa ramsi kuanza kuitumikia timu yake
katika michezo ya Ligi Kuu na Mashindano ya klabu Bingwa Barani Afrika
kufuatia shirikisho la soka nchini TFF kuiandikia barua klabu ya Young
Africans.
Okwi ambaye alisajiliw aa Young Africans mwishoni mwa mwaka jana na
kucheza michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya, alisimamishwa na
Shirikisho la Soka la Nchini TFF wakati wakisubiria kupata udhibitisho
wa usajili wake kutoka FIFA.
Mara baada ya barua hiyo, Okwi
anatarajiwa kuungana na wenzake mwishoni mwa wiki mara timu itakaporejea
kutoka Visiwa vya Comoro na ataanza kuonekana katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom dhidi ya Ruvu Shooting siku ya jumamosi Februari 22 mwaka
huu.
Uongozi wa Young Africans
unawashukuru wanachama, wapenzi na wadau kwa ujumla kwa kuwa wavumilivu
wakati wa suala na hili na hatimaye limepatiwa ufumbuzi.
RSS Feed
Twitter
February 14, 2014
Unknown

0 comments:
Post a Comment