Theluthi mbili ya watu wote
waliobakwa nchini Liberia mwaka jana wa 2013 walikuwa ni watoto. Hayo
yameelezwa na serikali ya nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika. Wizara ya
Jinsia na Maendeleo ya Liberia imetangaza kuwa asilimia 65 ya kesi 1,002
za ubakaji zilizoripotiwa mwaka jana zilikuwa za watoto wenye umri wa
kati ya miaka mitatu na kumi na nne. Taarifa ya Wizara ya Jinsia na
Maendeleo ya Liberia imesema, watoto kumi kutoka kaunti nane waliokuwa
na umri kati ya miaka mitatu na 14 walifariki dunia mwaka jana baada ya
kubakwa.
Hii ni katika hali ambayo ni wabakaji 49
tu ndio walioweza kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kati ya jumla ya
kesi za ubakaji 137 zilizoripotiwa mahakamani mwaka jana huko Liberia.
Wizara ya Jinsia na Maendeleo ya Liberia imesema kuwa idadi ya watenda
jinai hiyo ya ubakaji ingekuwa ya juu iwapo wazazi wa watoto wanaobakwa
wasingekuwa wakifikia maridhiano na kumaliza kesi hizo, kwa kuwa wengi
wa wabakaji huwa ni ndugu wa karibu au marafiki.
0 comments:
Post a Comment