Friday, December 13


  Abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli  Mh Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Arusha leo mchana. 
 
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua, ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria.

"Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.
Mh Lowassa ni mbunge wa Monduli, jimbo ambalo anatoka Waziri Mkuu aliyekuwa kipenzi Cha mwalimu Nyerere na watanzania hayati Edward Moringe Sokione.Sokoine aliyefariki katika ajali ya gari mwaka 1994.

0 comments:

-