Wednesday, October 23

                              
NI wakati mwingine tena marafiki tunakutana katika safu yetu murua kabisa ya kujadiliana mambo ya mapenzi na maisha kwa ujumla. Naamini mpo tayari kupokea kitu kipya kabisa kutoka kwangu.
Marafiki zangu, katika kipindi hiki cha Sayansi na Teknolojia, uzungu umekuwa mwingi sana kwenye uhusiano. Kwa bahati mbaya, mazoea hayo yamekuwa tatizo katika jamii yetu.
Kutokana na wengi kujifanya wataalamu wa kuiga, wamejikuta wakitumbukia kwenye michezo michafu ambayo mwisho wa siku inaathiri afya zao.
Hapa nitachambua aina za mazoea mabaya na madhara yake, ambapo mwisho wa siku, kama ni mmoja wa walio katika michezo hiyo hatari, utaamua kusuka au kunyoa baada ya kumaliza kusoma mada hii.


KINYUME NA MAUMBILE
Mchezo huu umeingia kwa kasi sana kwenye jamii yetu. Waanzilishi wakuu wa ujinga huu ni wanaume. Kiukweli, baadhi ya wanawake wamejikuta kwenye wakati mgumu kwenye mapenzi, baada ya wanaume wengi kucharukia kuanza kufanya mapenzi kwa njia hii isiyokubalika.
“Kaka Shaluwa, mpenzi wangu ananing’ang’aniza sana nifanye naye huu mchezo, anasema eti amesikia marafiki zake wakisema tukifanya, eti mapenzi yataongezeka! Sijui kama kuna ukweli wowote, hebu niambie kaka yangu,” huyu ni msomaji wangu kutoka Iringa ambaye aliniomba ushauri kwa njia ya simu.
Ipo mifano mingi, lakini yupo dada mmoja aliwasiliana nami, akaniambia kwamba anafanya mchezo huo kwa mwaka wa tatu sasa kwa lengo la kulinda usichana wake. Nilizungumza naye mengi na kumweleza madhara makubwa ambayo anaweza kuyapata kwa kuendekeza mchezo huo.
Kifupi si tabia nzuri kuiendekeza na husababisha madhara makubwa sana kiafya.

ATHARI ZAKE NI ZIPI?
Zipo athari za moja kwa moja ambazo mhusika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo huu hatari. Kwanza inakupasa ujue kwamba, njia hiyo ni maalum kwa ajili ya kupitisha kinyesi tu na siyo kitu kingine chochote.
Mwanamke anaweza kupata magonjwa ya uambukizo ya njia ya haja kubwa. Mafuta mepesi yaliyopo kwenye njia hiyo muda wote kwa lengo la kupitisha kinyesi kirahisi, yatakauka kutokana na matumizi mapya ambayo mhusika atakuwa ameyaanza.
Kukauka kwa mafuta hayo husababisha choo kutoka kwa tabu na hatimaye kuacha mikwaruzo ambayo husababisha vidonda – mwisho wake kupata maambukizi ya virusi ambavyo humea siku zote kwenye njia hiyo.
Hii ndiyo sababu mwanamke hushauriwa kutawaza akianzia sehemu ya haja ndogo kuelekea haja kubwa ili kuepusha maambukizi ya virusi vilivyopo kwenye njia ya haja kubwa. Zaidi ya yote ni vidonda na maumivu makali wakati wa kupata haja kubwa.
Misuli inayodhibiti haja kubwa hulegea na hivyo kuwepo kwa hatari ya kutokwa na haja bila taarifa. Kwa maneno mengine, mfanyaji wa kitendo hicho anajiweka kwenye hatari ya kuanza kutumia nepi akiwa mtu mzima!
Zaidi ya yote, wakati wa kujifungua mwanamke hupata tabu kubwa kwa sababu hatakuwa na uwezo wa kusukuma mtoto na hivyo kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa kujifungua kwa njia ya upasuaji, jambo ambalo si jema kiafya.
Ukiachana na wanawake, wanaume pia wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata maradhi ya kuambukiza (rejea hapo juu). Kadhalika mwanaume anakuwa kwenye nafasi kubwa ya kupata magonjwa mengine ya njia ya mkojo, kama mrija kuziba na mengineyo ya kitaalam ambayo matibabu yake wakati mwingine huhitajika kufanyika upasuaji.

MASWALI YA KUJIULIZA
Una haja gani ya kuingia kwenye matatizo makubwa kiafya? Una sababu gani ya kuwa kwenye hatari kubwa kiasi hiki? Kimsingi hakuna starehe yoyote ya maana inayopatikana kwa kufanya mapenzi kinyume na maumbile (labda kwa sababu ya ushetani unaweza kuona tofauti).
Mbaya zaidi, hakuna kitabu chochote kitakatifu kinachounga mkono tabia hii. Imani zote zinakinzana na ufanyaji wa mapenzi kinyume na maumbile.
Hebu ufike wakati sasa wa kuyatazama madhara haya kama somo, ikiwa unafanya mchezo huu, achana nao mara moja maana upo kwenye hatari kubwa sana.
Kama hujawahi, ONDOA FIKRA HIZO KABISA. Ni bora kuachana na mwanaume anayelazimisha mchezo huo kuliko kuwa naye kwa kuogopa kukosa ndoa.USIKOSE SEHEMU YA PILI YA MADA HII KESHO!!!

by GPL

0 comments:

-