Kwa
mujibu wa mdogo wake na mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha
ITV, Ufoo Saro aitwaye Goodluck aliyekuwepo wakati wa tukio la mauaji
lililotokea asubuhi ya jana, ambapo mchumba wa Ufoo alimuua mama yake
mtangazaji huyo, na pia yeye kujeruhiwa kabla ya mtu huyo aitwaye
Anthery Mushi kujiua pia.
“Tulisikia
sauti ya risasi sebuleni…na hapo mama akawa anatuita anasema njooni
hapa nakufa, tulipotoka nje tukakuta na dada nae ndo yuko chini,
akatuambia rudini ndani anataka kutuua wote hawa, ndo tukarudi ndani.
Baada ya kurudi ndani ndo akaanza kupiga risasi milangoni na madirishani
akawa anasema tokeni nje nataka niwauwe,” Goodluck alikiambia kituo cha
radio cha Times FM.
“Na
sisi tukakimbia tukapanda juu dalini baada ya kusikia mlango wetu
umeshapigwa sana risasi na dirishani, tukapanda juu ya dali, baada ya
kupanda juu dalini tukasikia mlio wa risasi mbili zinalia tena sebuleni
na hatukuwezi kutoka kule juu dalini. Baadae akatoka akaenda kufungua
gas akawasha moto wa gas, sasa moshi ukawa unakuja kule juu dalini na
hatuwezi kupumua, tukaja tukakuta jiko la gas lile limewaka liko karibu
na pikipiki.
Baada
ya polisi kuja na kuzunguka nyumba tukakuta mtu mwenyewe amekaa kwenye
kochi na yeye kajiripua risasi. Tukaulizia dada yuko wapi tukaambiwa
wamemuona dada mmoja hapa amechafuka damu amepelekwa Tumbi na pikipiki,
ndo baada ya kufuatilia ndo tunasikia amepelekwa Muhimbili.”
Ufoo
Saro amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na tayari
amefanyiwa upasuaji. Jana kamishina msaidizi wa upelelezi kanda maalum
ya Dar es Salaam Hemed Msangi,amesema kuwa Ufoo amejeruhiwa eneo la
mkononi, begani na tumboni na hali yake inaendelea vizuri.
Sababu
za tukio hilo bado hazijafahamika lakini kwa mujibu wa chanzo kimoja,
linaweza kuwa limetokana na ugomvi wa kimapenzi kati yao.
“Alikuwa
mume mtarajiwa wa Ufoo ila jamaa alikuwa akifanya kazi UN nchini Sudan
Kusini ingawa kitengo chake bado hakijafahamika ila kwa habari za mtaani
zisizokuwa na uhakika wanasema alikuwa mwanajeshi. Anaitwa Mushi. Bwana
mushi alikuwa na mgogoro na Ufoo mpenzi wake ila mama mkwe akawa
anamtetea Ufoo. Huyu dada alikuwa na mtu wa pembeni ikabuma. NIPO ENEO
LA TUKIO,” kimesecha chanzo hicho japo binafsi moshonomedia
haijazithibitisha.
Jana Jamii Forums waliandika:
Inasemekana
kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na
ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) ili
awasuluhishe.
Baada
ya usuluhishi kuanza na kuonekana kuwa tatizo liko kwa mwanaume,
mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa na mazoea ya
kumtetea mwanae na ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo
Saro risasi ya kichwa na kumuua papo hapo…. Alipomuua mama huyo,
mwanaume huyo alimpiga Ufoo Saro risasi mbili, moja ya tumboni na
nyingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha
kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
Inadaiwa
kuwa kufuatia tukio hilo polisi waligawanyika katika timu tatu ambapo
moja ipo Muhimbili, ya pili Kibamba yalipotokea mauaji na ya tatu
inashughulika mtaani kutafuta taarifa muhimu za mauaji.
Source: Jamii Forums, ITV, Michuzi, Mchomeblog, Times FM Blog
0 comments:
Post a Comment