Tuesday, September 3


Katika jitihada za kuhakikisha kuwa inawezekana kuweka kumbukumbu ya kila kitu kinachoendelea katika maisha ya binadamu masaa yote bila kupumzika kwa kutumia njia ya picha, Kampuni ya Memoto ya nchini Sweeden chini ya Martin Kaellstroem, wamefanikisha kutengeneza ki-camera kidogo ambacho huweza
kuvaliwa na mtu katika mavazi yake ya kawaida na kuendelea kurekodi kila kitu katika mishe zake bila kusimama.


Kicamera hiki ambacho kinatambulika kwa jina Memoto Camera, Ambacho kipo katika mfumo wa ipod ndogo, hukusanya picha za matukio yote kwa kutegemea location ya GPS ambayo mtumiaji yupo kwa wakati huo, muda na kiasi cha mwanga pia na kuzistream moja kwa moja katika mtandao.

Njia hii imetajwa kama teknolojia mpya ambayo itasaidia sana kuweka kumbukumbu ya mambo na matukio na kupunguza kazi ya kuweka rekodi hizi katika diary.                              
Kizuri zaidi kuhusiana na camera hizi ni kuwa, unaweza kuunganisha mfumo wa kumbukumbu za matukio haya na picha hizi zikawa zinaenda moja kwa moja katika mitandao kama twitter na facebook

0 comments:

-