NIENDE moja kwa moja kwenye mada yetu ya leo ambapo tunaangalia kwa kina jambo moja ambalo wanaume wengi wamekuwa wakichukizwa nalo na kufikia hatua ya kusitisha suala la ndoa kwa watu waliotokea kuwapenda.
Wanawake wana hulka karibu sawa, kwa upande wa wanaume ni tofauti kidogo, wanaume wana hulka tofauti kulingana na matakwa na utashi wao, japokuwa kuna baadhi ya vitu huwa wanakaribiana sana hasa katika kutoa uamuzi!
Wanaume wengi hufikiria sana kabla ya kufikia hatua ya kutoa uamuzi, baada ya kufanya hivyo huwa hawarudi nyuma.
Yaani wao ni mbele kwa mbele, tofauti na wanawake ambao huwa na uamuzi wa haraka lakini baada ya kukaa kwa muda na kufikiri sana hujiona wakosaji na kutaka kurekebisha uamuzi wao, wakati huo wanakuwa wamechelewa.
Nimetanguliza hayo kwa makusudi kabisa, unapaswa kufahamu kuwa mume wako au mchumba wako unapomfanyia mambo asiyoyapendelea, hukuvumilia kwa muda lakini kumbuka kuwa akitoa uamuzi siyo rahisi kurudi nyuma hiyo inamaanisha kuwa uwezekano wa kumkosa huwa mkubwa sana.
Unapaswa kujua vitu vinavyowakwaza wanaume, lakini pia unapaswa kufahamu ni vitu gani hasa ambavyo mumeo au mchumba wako anavichukia ili kukwepa kumchukiza na kusababisha mfarakano usio wa lazima katika uhusiano wenu.
Pengine unaweza ukawa na maswali mengi sana juu ya hilo, inawezekana unafanya makosa bila kufahamu kuwa ni kosa, sasa hebu tuliza ubongo wako katika kipengele hiki cha kujifanya wewe ni ghali kwa mpenzi wako na jinsi kinavyoweza kukufanya ukaishia kuachwa kisha wakaolewa wengine.
Hili limekuwa tatizo kubwa sana kwa baadhi ya wasichana, yaani hata kama maisha yake ni ya kawaida lakini kwa mpenzi wake atayafanya yaonekane ni ya ghali sana.
Akitolewa katika matembezi ya usiku kwa ajili ya kupata ‘dina’ au hata katika matembezi ya mwisho wa wiki, huagiza vyakula na vinywaji vya bei kali, badala yake tafsiri inayokuja hapo ni kwamba unakuwa na mpenzi huyo kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe kumbe wakati mwingine inaweza isiwe hivyo.
Wanaume wengi hawapendi kabisa tabia hiyo, ila huvumilia kwa muda lakini tambua kuwa siku akitoa maamuzi utayajutia.
Kimsingi mwanamke mwenye matarajio ya kudumu na mwanaume wake, ikiwa ni pamoja na kuishi naye katika ndoa takatifu, hawezi kumkomoa mpenzi wake kwa kuhitaji vitu vya gharama kubwa sana ambavyo ni kama hasara kwa mpenzi wako.
Mwingine anaweza akapewa ofa ya kwenda kufanya ununuzi wa nguo dukani, lakini akifika huko hufanya vurugu tupu, huchagua nguo za bei kali kiasi kwamba inakuwa kero kwa mpenzi wake.
Kikubwa hapa ni mwanamke kujitahidi kukijua kipato cha mpenzi wake. Usijifanye wa ghali bali ishi maisha ya kawaida, labda kama atakushawishi kuchukua au kutumia vitu vya gharama kubwa.
Elewa kuwa kwa kufanya hivyo unakuwa unamwogopesha mwanaume huyo kuwa na fikra za kutaka kuishi nawe katika ndoa, badala yake utaendelea kuwa chombo cha starehe siku zote, badilika ndugu yangu.Kevyclarity.blogspotl.com
0 comments:
Post a Comment