Friday, August 16

1. Calvin Harris - $46 million [74,267,000,000Tshs]
Huyu ndio top DJ... wa kwanza kwa kulipwa pesa ndefu duniani kwa mujibu wa Forbes, king wa kuspin/scratch/mix electronic dance, Ndani ya
kipindi cha miaka miwili anatajwa kusaini mikataba ya kupiga mziki kwenye shows kubwa zaidi ya 70.. dili za pesa ndefu, Mbali na U-DJ pia ni Producer na Mwandishi wa nyimbo ambaye amekwishapiga kazi na mastaa kama vile Rihhana, Katty Perry na wengine.

2. Tiƫsto - $32 million [51,664,000,000Tshs]
Huyu kwa mwaka jana pekee amefanya zaidi ya showz 140 na ni moja ya Ma-DJ's wanaoheshimika sana na anagonga muziki katika Club kubwa kabisa huko Las Vegas Marekani.

3. David Guetta - $30 million [48,435,000,000Tshs]
DJ ambaye alianza kwa kugonga muziki katika klabu ndogo huko Paris kabla ya kuhamia katika Radio na kuanza kuchukua contract za shows, Anagonga ngoma na pia anacheza katika nafasi ya back up artist kwa wasanii na pia amekuwa ni mtu mwenye mchango mkubwa katika Tour ya Dunia ya Rihhana.

4. Swedish House Mafia - $25 million [40,362,500,000Tshs]
Hii inaunda na washkaji watatu Sebastian Ingrosso, Axwell and Steve Angello, Kundi hili kwa sasa tayari limekwishavunjika na tokea mwezi March kila mmoja anafanya mambo yake kivyake, lakini wanaingia katika orodha hii kutokana na pesa walizotengeneza wakiwa pamoja.

5. Deadmau5 - $21 million [33,904,500,000Tshs]
ID ya umaarufu wake ni mask ya umbo la Panya, Ni DJ wa Club na pia anatengeneza pesa nyingi kupitia showz kubwa za muziki.

WENGINE NI;

6. Avicii - $20 million [32,290,000,000Tshs]

7. Afrojack - $18 million [29,061,000,000Tshs]

8. Armin van Buuren - $17 million [27,446,500,000Tshs]

9. Skrillex - $16 million [25,832,000,000Tshs]

10. Kaskade - $16 million [25,832,000,000Tshs]

0 comments:

-