Thursday, August 8



Rafiki zangu, kama nawe unawaza hivyo unakosea sana. Mapenzi si rahisi kama wengi wanavyofikiri. Ni hisia zinazotesa na na kuumiza kuliko kawaida.
Kwa faida ya ambao hawajui undani wa mapenzi leo wanakwenda kuwa wapya kabisa baada ya kusoma mada hii. Hebu twende tukajifunze.


WENGI huwa hawapati muda wa kutafakari kwa kina japo kidogo tu kuhusu hisia za mapenzi.
Wapo wanaofikiri mapenzi ni kukutana kimwili halafu baasi! Wengine wanadhani kwamba mapenzi ni jambo la kawaida tu.

KWA NINI TUNAJADILI?
Yupo msomaji mmoja alinitumia meseji akiomba ushauri. Aliandika: “Kaka Jose, naomba msaada wako. Mimi  ni msichana mwenye umri wa miaka 19, nimeishia darasa la saba tu.
“Kwa bahati nzuri nilifaulu lakini kwa sababu wazazi wangu hawana uwezo sikuweza kuendelea na elimu ya sekondari. Nipo nyumbani sasa kwa muda wa miaka mitatu.
“Hivi karibuni nilikutana na kijana mmoja mtu mzima kiasi lakini hajaoa. Amesema ananipenda na lengo lake ni kuoa kwa ndoa, nikamweleza juu ya kiu yangu ya kusoma akasema yupo tayari kunisomesha.
“Ukweli ni kwamba moyoni mwangu hayupo hata kidogo lakini nahitaji anisaidie kunisomesha. Unanishaurinini kaka yangu?

                      ”

UMEONA?
Yaani anajua kabisa hampendi lakini anataka kuwa naye kwa ajili ya malengo ya kusoma. Hili ni kosa kubwa sana. Wengi wanafanya hivi lakini mwisho wake hauwi mzuri hata kidogo.
Kama nawe upo katika mkumbo huu ni vizuri ukaacha kwa faida yako mwenyewe. Hisia za mapenzi hazichezewi hata siku moja. Moyo hauchezewi.

MAPENZI NI KUWEKEZA
Ngoja nikuambie rafiki yangu, mapenzi ni kuwekeza. Ukiona mtu yupo tayari hata kutumia gharama zake kwa ajili ya mtu tena kwa matarajio ya baadaye ujue yupo tayari kufanya ‘investment’.
Siku zote mtu anayewekeza katika biashara hategemei kupata hasara. Uwekezaji mara nyingi huwa una lengo la kupata faida. Sasa kama mwenzako amewekeza akitegemea kupata mke bora, mke msomi hapo baadaye, vipi akija kugundua tofauti?
Unadhani atakuwa tayari kweli kupoteza miaka minne au zaidi kumsubiri ‘mke’ anayesoma kwa gharama zake halafu baadaye eti anabadilika na kumkataa?
Nini kitatokea unadhani? Ni matatizo ambayo yangeweza kuepukika. Bado kuna mengi ya kujifunza katika mada hii, wiki ijayo nitakuwa hapa kwa mwendelezo wake, USIKOSE!

0 comments:

-