kevy: Haya ndugu yangu za masiku hatuonani ila mimi nakuona tu kwenye luninga.
AYO: Aiyaa….! Wakuu ni aje ni kitambo kimepita hatujaonana ila mimi niko poa tu nakaza buti.
kevy: Usiende
mbali tunajua uko bize lakini hebu kaa kitako uzungumze na mhariri
wangu kuhusu mawili matatu watu wasio yajua kuhusu wewe.
kevy: Nini kimeshawahi kukutokea maishani ambacho huwezi kukisahau na wasikilizaji na watazamaji wako hawakifahamu.
MILLARD AYO: Nilishawahi
kupata ajali mbaya kiasi kwamba watu wengi wasingekuwa wananifahamu
hivi leo. Ni ajali ambayo iliondoka na rafiki zangu wanne.
kevy: Pole sana na tuna muomba Mwenyezi Mungu Mwenye Rehema Awarehemu.
MILLARD AYO: Amina.
Tulikuwa
tunasafiri na basi katika safari za kishule, tulikuwa 60 hivi kwenye
basi tukapata ajali ‘Ngongoro crater’ bonde la ufa sehemu inaitwa
‘Malanjo Cross’ ni sehemu hatari sana, yaani tuliingia bondeni, yaani
sidhani kama leo ningekuwa hai.
kevy: Hebu Millard tufafanulie zaidi tukio hilo la ajali lilikuaje..?
MILLARD AYO: Yaani
sina la kusema ila kama Mungu asingependa mimi nisingekuwepo duniani,
lakini kwa sababu alipenda, ndio maana nipo, hata hili kovu katika
kichwa upande wa kushoto lipo. Hapa iliingia chuma, unajua mabasi ya
zamani yalikuwa na chuma, sasa ile chuma ilikatika wakati basi
likijipiga kwenye mawe kama unavyojua kule ni crater.
Kwa
kweli ninachokumbuka ni kuwa gari lilipotulia watu walikuwa wakilia na
damu zinatiririka na mimi nilikuwa nimebanwa katika hiyo chuma na
nilipotolewa sikukumbuka tena nini kiliendelea.
Ilikuwa
mbaya sana kwa sababu lile basi lilikuwa likibiringika kama chupa,
hivyo watu wanatupwa madirishani na kisha gari linawalalia ndio
mazingira watu walivyopoteza maisha.
OMG…!!!
kevy:
Kitu kingine ambacho kevyclarity ingependa kufahamu ni kuondoka kwako ITV,
fununu zinasema kuwa ulikuwa ni mtiti, ni ya kweli haya?
MILLARD AYO: Ningependa watu wakifahamu ni kuwa mimi sina ugomvi na ITV wala sikuondoka kwa ugomvi.
Kwanza
kufanya kwangu kazi ITV naamini Mungu alikuwa anaona na alipanga ndio
maana hata hivi sasa kuna uwezekano kuwa nafasi nyingine nilizo nazo
maishani kwangu nisingezipata, pengine hata ‘Clouds’ wasingeniona na
wasingenifuata.
ITV ndio ilimtambulisha Millard Ayo.
ITV niliondoka vizuri ndio maana nitawaheshimu na nitazidi kuwatangaza vizuri popote nitakapokwenda.
Kwa sasa hapa ‘Clouds Radio’ nafanya show yangu ya ‘Amplifaya’ ambayo ina sehemu inayohusisha Blogs, Facebook na Twitter.
Katika kipengele hicho nasoma sana habari zao wanazo zi’tweet’ na nasema nimezitoa ITV.
kevy: Zungumzia mahusiano yako na viongozi wa ITV na wafanyakazi wake.
MILLARD AYO: Nasema
ukweli kuwa sina kinyongo na Mkurugenzi Mkuu wa ITV Joyce Mhaville tena
namwambia asante sana kwa kunilea, sina matatizo na waliokuwa
wafanyakazi wenzangi wa ITV na Radio One na tunaendelea kuwasiliana kama
kawaida na nawaambia tuko pamoja na nawapenda sana.
Wengine
tunakutana na tunakuwa ‘good times’ pamoja na bado nitaendelea
kuwaheshimu kote nilikotoka ikiwemo ITV, WAPO RADIO na TVZ, hata kama
kuna mapungufu, hakuna sehemu isiyokuwa na mapungufu.
Wasikilizaji
wa ‘Amplifaya’ msisite kusikiza kipindi hiki kwa sababu kila
unachokipenda utakipata humu na pia mimi kama Millard Ayo nasema “KEVYCLARITY MO BENEFIT”.
Msomaji
wa Blog hii usikose SEHEMU YA TATU ya mahojiano ya KEVYCLARITY na MILLARD
AYO ambapo amezungumzia maisha yake ya kimapenzi na suala tata
linalovuma hivi sasa la ‘FREEMASON’.
0 comments:
Post a Comment