Tuesday, August 13

bilionea

Mfanyabiashara tajiri wa madini kutoka Mirerani Erasto Msuya aliyeuwawa kikatili wiki iliyopita huko Kilimanjaro, azikwa jana (August 12) huko nyumbani kwao eneo la Kairo Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.


Kwa mujibu wa Mwananchi, marehemu Msuya alizikwa kifahari huku jeneza lake linalofunguka kwa ‘rimoti’ pamoja na gari la kuubeba mwili viliagizwa kutoka Nairobi, Kenya. Jeneza pamoja na gari hilo viliagizwa kutoka kampuni ya kutoa huduma za mazishi ya Montezuma & Monalisa Funeral Home ya Nairobi Kenya na kugharimu Tshs M8.
Jeneza hilo la aina yake lilionekana kuwaacha na mshangao maelfu ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wakati wa ibada iliyofanyika nyumbani kwa marehemu , Kwa Iddi, wilayani Arumeru.
Kamati ya Maandalizi ya mazishi hayo inayoongozwa na kaka mkubwa wa familia ya Msuya, Gady, ilisema zaidi ya Sh100 milioni zilipangwa kugharimia shughuli za maombolezo na mazishi.
Chakula, vinywaji, mapambo na magari ya kukodishwa kutoka Arusha kwenda Mirerani na kurudi yanatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh80 milioni.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani Arusha imeendelea kuwahoji wafanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro, wakidaiwa kuhusika na kifo hicho.
Msuya anayeaminika kuwa wafanyabiashara wa Mirerani wanaoongoza kwa utajiri aliuwawa kwa kupigwa risasi 20 (August 7) wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro.
Source: Mwananchi. Isome zaidi taarifa hiyo hapa


0 comments:

-