Sunday, August 4


Haya ndiyo maajabu manne ya mto Mori.
Mto Mori upo katika Mkoa Mara Wilaya ya Rorya.
Inaanzia Tarime na inamwaga Maji yake Ziwa Victoria.
Zamani wakati wa Ukoloni hapa Tanzania,kulitokea Mti moja wa ajabu kweli kandokando ya Mto Mori.
Huu mti ulipokatwa tu ili kusafisha hayo maeneo,ilianza kulia kwa nguvu huku ikipiga kelele na kutokwa na damu nyingi hiyo sehemu iliyokatwa.

Ilikuwa ikisema kwa Kijaluo.''UWIIII,ING'ADA NANG'O NYATHII DHAKO WADWA,ATIMONI ANG'OO 
MARACH YAWA.''Akimaanisha Unanikata kwa nini mtoto wa mwanamke Mwenzangu kwani nimekufanyia nini kibaya.

Huyo jamaa aliyekuwa anaukata akaogopa akakimbia kufika
kwake Akafa.

Siku iliyofuata watu wakaogopa kuukata huo mti Mzungu akawalazimisha wakagoma.

Mzungu kuanza kuukata Mti ukaanza kulalamika kwa Kiingereza na kutokwa damu nyingi hiyo sehemu
iliyokatwa,Mzungu naye kapoteza Maisha.

Mpaka sasa inasemekana huo mti bado uko hapo na hayo maeneo watu hawasongelei.

Maajabu mengine ya Mto Mori ni haya hapa.
Kuna sehemu ukiingia kama uataka samaki hasa kwa wale
Wavuvi,unawakuta kibao tena bila kutumia ndoano,Unachota tu.Utajaza matenga mpaka uchoke Mwenyewe.

Kitendo cha kuanza kutoka hapo na hao samaki ghafla inageuka usiku mnene na Bonge la Giza,Utaangaika mpaka ukome.

Na ukifanikiwa kutoka nje utakuta mchana kweupe na wale Samaki hufanikiwi kutoka nao hata moja.

Kingine ni kwamba huwa inajaa na kuwa Vigumu kuuvuka na mara nyingi sana inauwa Watu.Kila Mwaka lazima iue.

Hivyo basi kama wewe ni mpita njia na ukaona Maiti kwa huo mto,Usipige kelele Ukipiga kelele maiti itatoweka ghafla na hutoina tena na itaanza kukusumbua sana katika maisha yako.

Daima utakuwa unaona mauzauza.Unachotakiwa kufanya Ukiona Maiti katika Mto Mori ni kuisogelea na kuwa Jasiri ya kuivuta mpaka nchi kavu ndipo upige kelele ya kuopmba msaada.

Njia ya Pili ni kuiita tu kwa kuibembereza njoo,njoo muungwana,njoo Rafiki yangu unasema ''bii,biii Orinda,biii kikiluor,biii kuoma''Hayo ni maneno ya Kijaluo wanayotumia.Maya kweli ni maajabu kwa sababu
Maiti inakufuata mpaka ulipo kandokando ya mto!


0 comments:

-