Friday, August 16




Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.

Mwenyekiti Alex Mgongolwa amesema kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba wakati alikuwa na mkataba na (Azam) hivyo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.

Kamati imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo ikitokea akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.

mbali na sakata la ngasa pia wachezaji wa kigeni kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza mpaka watakapopata hati za uhamisho wa kimataifa(ITC) na vibali vya kufanya kazi nchini(Work Permits

0 comments:

-