Huyu ni Omar Borkan Al Gala, mwigizaji
na pia mpiga picha wa huko Dubai ambaye kwa mujibu wa taarifa, yeye
pamoja na wenzake wawili wamefukuzwa huko Saudi Arabia kutokana na kuwa
na muonekano mzuri kupitiliza
(Yaani ma-handsome kupita kiasi) ili kuepusha kuwaingiza katika tamaa wanawake ambao hushindwa kujizuia kuwashobokea.
Omar alitolewa na maafisa wa polisi na
kunyimwa kuhudhuria katika tamasha ambalo hufanyika kila mwaka nchini
humo ambalo huusisha mbio za Ngamia, Janadriyah Festival ambalo kwa
sehemu kubwa huhudhuriwa na matajiri, na baadhi ya vyanzo vya taarifa
vinasema Omar alitolewa kutokana na mualiko wa msanii wa kike maarufu
kutoka Falme za Kiarabu ambaye walihofia angeweza kutengeneza mahusiano
naye.... na wengine wakisema ni hofu ya wakubwa kuibiwa mademu wao.
0 comments:
Post a Comment