Taasisi
ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu ‘’UTT Projects and Infrastructure
Development Plc’’ (UTT-PID) ni Taasisi inayomilikiwa na Serikali ya
Tanzania na kuendeshwa chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.
Menejimenti
ya UTT-PID imesikitishwa na kitendo cha moja ya gazeti la kila wiki
linalotoka hapa Tanzania katika matoleo yake mawili yaliyopita ya mwezi
wa Machi 7 na Machi 14, mwaka huu kwa kuandika habari zisizo sahihi bila
kupata maelezo ya Taasisi husika kinyume na maadili ya uandishi wa
habari yanayovitaka vyombo vya habari kuzingatia usahihi, haki na usawa
katika kutoa habari yoyote.
Tunapenda
kuujulisha Umma wa Watanzania kuwa baada ya Taasisi kufuatilia chimbuko
la taarifa zisizo sahihi zinazotolewa na baadae kuandikwa kwenye gazeti
hilo ilitoa taarifa kwa vyombo vya dola ambavyo vinafanyia uchunguzi
suala zima la tuhuma na nani anazisambaza tuhuma hizo ambazo kimsingi
zina lengo la upotoshaji na kuichafua UTT-PID.
Aidha
Menejimenti ya UTT-PID inawashauri waandishi wa habari na wahariri wa
habari wajikite kwenye weledi, ukweli na maadili ya tasnia ya habari,
wafanye utafiti wa kina na kutoa taarifa zilizo sahihi na kwa umakini,
uhakika na kutokubali kamwe kutumiwa na watu au makundi ambayo yana
agenda binafsi katika kufikisha ujumbe wenye matakwa yao.
Mwisho
tunawasihi wadau wetu katika miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya
usimamizi wa UTT-PID, wateja wetu pamoja na Umma kwa ujumla kuendelea
kuwa na imani na Taasisi ya UTT-PID kwa kuwa habari hizo ni za uzushi na
zenye lengo la kuichafua Taasisi.
Tazama MO tv, kuona taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa UTT-PID, Dk. Gration Kamugisha:
RSS Feed
Twitter
March 18, 2016
Unknown
0 comments:
Post a Comment