Serikali
ya Tanzania imesaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za
Kimarekani milioni 665 na Wadau wa Maendeleo ili kusaidia Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini
nchini.
Mkataba
huo ambao umetiwa saini jijini Dar es Salaam unawataka watendaji kuweka
utaratibu ambao unaenda sambamba na Mpango wa utekelezaji bila
kuingilia majukumu ya mamlaka ya Serikali katika utekelezaji wa TASAF wa
kunusuru kaya masikini.
Akizungumzia
mkatraba huo mara baada ya kusaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania,
Katibu Mkuu Wiazara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile amesema
kuwa mpango huo unaosimamiwa na TASAF unalenga kuziwezesha kaya
masikini nchini kujiongezea kipato na kupata chakula cha kutosha pamoja
na kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Katika
kutekeleza mpango huo wa TASAF uwe wa tija kwa kaya masikini kulingana
na malengo tarajiwa, mpango umegawanyika katika maeneo makuu manne
ambayo yanatarajiwa kuboresha hali za watu wanaoishi katika hali duni
nchini.
Maeneo
hayo yanayotekelezwa ni pamoja na kuhawilisha fedha kwa kaya masikini
hasa zile zenye watoto ili ziweze kupata huduma za elimu kwa kuwawezesha
watoto walio katika shule za msingi na sekondari kupata mahitaji muhimu
shuleni pamoja na kupata huduma za afya na kuongeza kipato kwa kaya
masikini kupitia uwekaji akiba na shughuli za kiuchumi.
Maeneo
mengine ya utekelezaji huo ni kutoa ajira ya muda kwa kaya masikini
zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi wakati wa kipindi cha njaa na
majanga yakiwemo ukame na mafuriko pamoja na kujenga uwezo katika ngazi
zote za uteklelezaji wa kutoa mafunzo yatakayoboresha utekelezaji wake.
Mpango
wa Kunusuru Kaya Masikini nchini umekuwa na mafanikio nchini ambapo
hadi sasa umeshahawilisha kwa walengwa mizunguko 14 ya malipo ya jumla
ya fedha zote zilizohawilishwa kufikia bilioni Sh. 224 na kuandikisha
kaya milioni 1.1 tangu uanzishwe mwaka 2012 na kuhudumia halmashauri
159 Tanzania Bara pamoja na halmashauri 11 Tanzania Zanzibar.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Wadau hao wa Maendeleo nchini ambaye pia ni
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania,
Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird amesema kuwa makubaliano
yaliyotiwa saini yataboresha uhusiano na kuendeleza majadiliano baina ya
Serikali na wadau kuhusu kunusuru kaya masikini na kutoa msaada wa
kitaalamu utakaohitajika ili kufikia malengo yanayotarajiwa.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus
Mwamanga amewahakikishia wadau hao wa maendeleo kuwa fedha walizotoa kwa
mfuko huo zitatumika kwa malengo yaliyowekwa ili kuwasaidia Watanzania
wanaoishi katika hali duni waweze kuinua hali zao kiuchumi na kupata
mahiji yao ya kila siku.
Wadau
waliotia saini mkataba huo wa makubaliano ya kunusuru kaya masikini ni
pamoja Benki ya Dunia, Ubalozi wa Sweden, Shirika la Maendeleo la
Uingereza (DFID), Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mtaifa (UNDP), Shirika
la Misaada la Marekani (USAID), Shirika la Watoto la Umojas wa Mtaifa
(UNICEF), Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika la Watu wa Umoja wa
Mataifa (UNFPA), Wizara ya Fedha na Mipango na TASAF kwa upande wa
Tanzania.
RSS Feed
Twitter
March 18, 2016
Unknown
0 comments:
Post a Comment