FRANK W.A MUHALIFU TAPELI MWENYE HISTORIA YA PEKEE FBI
Heri ya Mwaka Mpya 2018. Si makusudi yangu kusifia Uhalifu lakini katika
Ulimwengu huu kuna akili za ziada au vipaji ambavyo watu wanavyo sema
tu matumizi yake ndo huwa yanakuwa ya kihalifu. wazungu wenzetu bado
hukaa chini na kutathmini faida na hasara ya akili za watu flan flan
hata kama walikuw awahalifu. leo hii tunamzungumzia Frank Williams
Abagnale Jr ambaye baadaye FBI ilibidi wamwajiri baada ya kumkamata na
kustaajabishwa na uwezo aliokuwa nao.
Kwa wale ambao wamewahi kutizama movie inaitwa Catch me if You Can
au kusoma kitabu chenye jina hilo hilo bila shaka watakuwa wamewahi
kusikia kisa cha Tapeli/Msanii mmoja mwenye akili kuwahi kupata kutokea
Duniani. Huyu jamaa aliyekuwa akifahamika kwa jina la Frank W. Abagnale
Jr. Akiwa na miaka 15 alianza shughuli za kufanya utapeli au usanii
kiasi kwamba mama yake ilibidi mapeleke shule ya watoto watukutu. Frank
alipomaliza shule aliamua kutafuta ajira hasa baada ya baba yake kuyumba
kiuchumi na kusababisha awe na maisha magumu. vyuma vilikaza.
Frank aliamua kuondoka nyumbani akiwa na checkbook pamoja na Usd 200
katika account yake akielekea New York City kutafuta maisha. Akiwa huko
akawa anaishi na familia ya kijana mmoja ambaye walikutana kwenye train
wakati wa safari yake basi akamuuzia uzia chai wakawa marafiki na badaye
akafikia kwao. Haikuchukua muda mrefu alifanikiwa kupata kazi katika
kampuni moja ya stationery akitumia uzoefu alioupata aliupokuwa akifanya
kazi katika kampuni ya baba yake.
Frank aligundua ilikuwa ngumu sana kuishi maisha mazuri katika jiji la
new York hasa hasa ukiwa hujasoma angalau kuwa na elimu ya kwa ngazi ya
Diploma. Na ili kuweza kuishi vizuri pale jijini basi alipaswa angalau
aweze kupata zaidi ya Usd 1.50 kwa saa kiasi ambacho alikuwa akipata.
Hivyo alianza kuchangamsha akili kuwa afanye nini ili aweze kuongeza
kipato.hakuchagua kuwa punga.no. alichagua kuwa Msanii. Alifanikiwa
kupata wazo ambalo lingemsaidia kupata kipato cha ziada na hivyo
kusababisha miezi ikutane.
Akaamua kuchezea leseni yake ya udereva. Ambayo mara ya kwanza ilikuwa
inaonesha alizaliwa mwkaa 1948 akarudisha nyuma na kuifanya ioneshe
amezaliwa mwaka 1938. Miaka 10 zaidi ya umri wake.hii mbinu ilifanya
kazi.watu walikuwa wakimwona ni mtu mzima kutokana na yeye kubehave na
kuonekana hivyo na pia hata urefu wake wa futi 6 na mvi za urithi ambazo
zilikuwa zimeanza kumtoka.basi ilikuwa ni rahisi kumdhania kuwa ni mtu
mzima. Frank hakuishia hapo. Kaanza kujifanya kama ni mtu ambaye amesoma
sana akijua hii ingemsaidia katika kuongeza mshahara wake. Hata hivyo
aligundua hata pamoja na kufanya sarakasi zote hizo yaani za kuongeza
umri na kudanganya kuhusu elimu yake bado hakuweza kupata pesa ambayo
ingemsaidia kuishi maisha mazuri kama alivyokuwa ametegemea.akaamua
kuchemsha tena akili.
Atafutaye hachoki. Frank alikumbuka kuwa alikuja New York akiwa na
chekcbook na alipofika new York alifungua check account kupata blank
checks. Akadhamiria kutumia hizo checks kwa hali ambayo ingempa faida
Zaidi kuliko ambavyo ilikusudiwa.yaani kufanya usanii/utapeli.
Frank akafanya maamuzi magumu. Akaamua kuacha kazi na kuanza kufanya
utapeli kwa Mabank kwa kujiandikia check feki. Alishafanya jambo hili
hapo kwanza na hivyo akawa ameendeleza huu mchezo wa kujiandikia check
feki na kuvuta mapene kutoka bank.akijipatika Madollar kibao. Lakini
alishtuka kuwa si muda mrefu mapolisi watakuwa wanafaham mchezo wake
hivyo akaamua kuondoka kwenda sehemu nyingine na kubadilisha jina.
Mpango wa Kujifanya Rubani wa Shirika kubwa la Ndege Duniani.
Frank W akiwa na mtoto mmoja mkali baada ya kutoka kumgegeda.
Alipata wazo la kujifanya rubani hasa baada ya kushuhudia mara nyingi
marubani walivyokuwa wakipata heshima katika jamii. Alishashuhudia
marubani wengi wakiwa nje ya Hotel ya Commodore wakila bata na
mademu wakali wa kibongo,kitasha,kihindi,kiarabu na kilatino aka admire
sana ile life style na siku zote alikuwa akiwaza maisha yale ya kula
bata kwa kwenda mbele.Na akaona ili sasa aweze kuzi cash zile bad checks
zake bila bugudha au kutiliwa mashaka basi inabidi ajifanye naye ni
rubani. Hapo tayari alikuwa ameshaziandika cash kadhaa ambazo inabidi
akazi cash.
Basi akaamua kupata sare za marubani wa Shirika la ndege la Pan Am (Pan American) na kujifanya yeye ni mmoja wa Marubai wa Panam. Akaanza kufanya mchakato mtoto wa mjini… wanasema "kuku hafi kwa utitiri "na ndivyo ilivyo kwa mtoto wa mjini hafi kwa njaa. Akampigia simu wakala wa manunuzi wa Pan American Airlines Corporate
makao makuu na kuwaambia kuwa yeye ni Rubani(pilot) wa Kampuni hiyo ya
Panam na kuwa katika Hotel aliyokuwa anaishi walipoteza Sare yake ya
kazi. Jamaa kule wakamwambia hamna noma basi aende kuchukua hiyo sare
katika Kampuni ambayo wao wame specialize katika kutengeneza uniform za
Pan Am mtaa wa 5th Avenue. Naye pasipo kuchelea alifanya hivyo. Siku
hiyo hiyo aliafanikiwa kupimishwa Sare na akawapa namba ya Mfanyakazi
ambayo aliibuni alipokuwa akijaza form.
Hatimaye frank alitoka katika lile jengo akitabasamu kimoyo moyo akiwa
ameshikiria sare yake mkononi akiwa amefanikiwa kuvuka kikwazo kimoja
wapo katika mchakato wake. Ili sasa kujihakikishia nafasi ile akaamua
kutengeneza na kitambulisho cha Pan Am. Baada ya kuangalia katika vile
vitabu vya simu maarufu kama Yellow Pages frank aligundua kuwa 3M ndo
ilikuwa Kampuni inayohusika na utengenezaji wa Vitambulisho kwa
Makampuni Mengi ya Ndege ikiwepo Pan Am. Akawasiliana na kampuni hiyo
akijifanya yeye ni Afsa manunuzi ambaye amedhamiria kutengeneza
vitambulisho vipya kwa ajili ya Kampuni yake. Akaomba wakutane na
mhusika wa 3M kwa ajili ya maongezi Zaidi. Akakutana na afsa wa Kampuni
anayehusika na mauzo na huko akapewa catalogs mbalimbali za vitambulisho
walivyo navyo.katika hilo akagundua kitambulisho ambacho kinafanana na
vinavyotumiwa na Pan Am. Akamwambia mhusika wa ile Kampuni alitaka apewe
copies za sample za vitambulisho ambacho kitawekwa picha na details
zake kama mfano ili akawaoneshe wafanyakazi wenzie vitambulisho vile
vitakuwaje. Kitambulisho kile kilifanana kabisa na vile vya Pan Am
isipokuwa ilikosekana Logo tu.akatengenezewa akachukua akawaoneshe
wafanyakazi wenzie kama alivyojinasibu kwa yule jamaa.
Frank alitatua tatizo hilo la kukosekana nembo kwa kuamua kununua mfano
wa ndege ya Pan Am. Yaani toy ambapo katika hilo akanyofoa hiyo alama
ambayo ni famous sana na kwa umakini akaibandika kwenye kitambulisho
chake na kilionekana kama vile vile ambavyo vinatumika na maruban wa Pan
Am. Kikwazo kingine akawa amekivuka. Sasa ana sare na kitambulisho. Safari yake ya kuelekea kula bata ikawa inazidi kukaribia.
Akawa amaebakiwa na maeneo mawili Zaidi ya ku clear. Alitakiwa kuwa na leseni ya FAA ambayo
kila rubani anapaswa kuwa nayo na pia awe na ufahamu kuhusiana na
shughuli za Airlines. Kwanza akaamua kutafuta habari nyingi kadri
awezavyo kuhusiana na usafiri wa anga,urubani na pia maneno au
terminologies ambazo zinatumika katika kada hii ya usafiri wa anga.
Akaanza kuwa anaingia library kujisomea ingawa alikuta vitabu vingi
vimekuwa outdated.lakini alijitahidi kupata ABCs za Urubani.
Akaona ili kuweza kupata habari za uhakika na za kuaminika basi aanze
kufanya utaratibu wa kupata habari hiz kutoka kwa wahusika wenyewe yaani
wafanyakazi na marubani.akaanza kuandaa mahojiano na wafanyakazi wa Pan
Am akijifanya yeye ni mwanafunzi anayefanya research project kuhusiana
na kampuni hiyo na marubani wake. Lilikuwa ni wazo bora kabisa lenye
akili. Alijipatia utajiri wa habari za uhakika pamoja na ufahamu
kuhusiana na sera,kanuni na taratibu kama msaidizi wa rubani. Co-pilot.
Aina ya ndege zinazotumika na njia za kimataifa zinazotumika.jamaa akawa
fiti sana katika eneo hilo.
Zaidi Zaidi alipata kufaham kuhusiana na deadheading. Deadheading ni
mfanyakazi wa ndege ambaye anapata kipaumbele cha kusafiri kwa kutumia
ndege nyingine kwenda sehemu mbalimbali bure kwa ajili ya kwenda kufanya
shughuli flani. Mwajiri ndo anayelipia hii safari kwa kila kitu.hapa
frank alitasabamu na kuona sasa ameuchinja.maana akiwa kama rubani pia
deadheading atakuwa sometime anasafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani
kwenda kula bata akilipiwa na kampuni. Mungu ampe nini Frank? Upele?
Elimu yote hii aliihifadhi kichwani mwake akiendelea kujikita Zaidi
katika kukamilisha mpango wake.
Issue iliyokuwa inafuatia sasa ilikuwa ni kupata leseni ya FAA aligundua
kuwa bila leseni hiyo asingeweza kujifanya yeye ni rubani.sababu wakati
mwingine marubani walitakiwa kuonesha leseni ya FAA ikiwa angepanda
ndege nyingine kama Staff yaani deadheading. Si unajua zile za kibongo
hata kwenye daladala wakati konda akidai mchango wa mafuta utasikia “mi stafu”
basi ndo na wao ili uonekane staff basi sometime utaulizwa tuoneshe
leseni yako ya FAA. Frank aligundua FAA walikuwa na Branch hivyo
akajiita Frank Williams na kuwa ametumwa akachukue documents za maelezo
ya vitambulisho baada ya kutumiwa mail ndugu yake ambaye ni rubani.
Akachukua ule mfano wa vitambulisho toka kwenye barua na vipeperushi vya
FAA akaiweka kwenye printer na kuifanya iwe ndogo akaibandika kwenye
karatasi maalum na kulaminate. Shabash ! frank alikuwa tayari
ameshaula.huwezi amini ilikuwa copy right kama zile zile za
marubani.alitabasamu tena na kurusha ngumi hewani ya kujipongeza huku
akianza kufurahia jinsi ambavyo atakuwa anakula bata na watoto wakali.
frank akiwaza amezungukwa na watoto wakali.
Frank sasa alikuwa amekamilika.ana kila kitu. Leseni ya FAA, leseni ya
urubani, Sare na Ufaham kuhusiana na kazi hiyo. Yaani kifupi alikuwa
yupo Gado Ile mbaya. Ukimcheck hivi we mwenyewe unaingia King kuwa jamaa
ni Rubani..mkipiga stories za mambo ya huko hewani ..unaweza jikuta una
come jinsi alivyokuwa fresh.
Safari tayari ya kuanza kula bata na kutapeli Mabank duniani
Basi mshkaji akakaza mwendo akiwa ametinga sare zake za kirubani na
vitambulisho vyake vyote akiwa anatumia jina la Frank Williams akaenda
mpaka Bank kwenda kufungua Account akiwa ametinga sare au uniform za
marubani akitembea kimikogo kabisa kwa kujiamini. katika mabenk yote
aliyopita walikuwa wakimheshimu sana maana miaka hiyo ya 1960s marubani
walikuwa wanatesa sana kitaa...kama una demu wako hajielewi elewi trust
me rubani angeweza kukupora kirahisi sana akamgonga akakuachia maumivu.
yaani walikuwa wanaonekana mambo safi sana na wanaheshimika ile
kinoma.tena Zaidi yeye kutoka Kampuni kubwa ya kimataifa. hawakujua.
hawakujua maskini, kuwa huyu alikuwa bwana mdogo tu tapeli msanii wa
kiwango cha standard gauge.
Frank akawa amekuwa mcharo ile mbaya. Mademu wengi walikuwa
wakimzimia..hasa wale mademu wafanyakazi wa kwenye ndege na si unajua
walivyo wakali… basi wengi wakawa wanamjia tu kwa nyuma "frank tunakuzimia"
n.k. jamaa hakuwanyima haki yao.akawa anawapa tu.anawapa,
anawagaia,anawakita na mashine,anawapa mkono,akawa anawacharaza
bakora,anawapiga kwa ukuni...si unajua ukishakuwa mwana utamaduni
humchapi mwanamke kwa fimbo...unamchapa kwa ukuni.watu wa kale toka
zamani.... Ikawa yeye ni mtu wa kuwa na list. Anatick tu huyu tayari,
huyu tayari..huyu bado next week. Kumbe aogope nini na uzushi upo
pembeni?
Kwa kujiamini kabisa akaamua kusafiri kama deadheading kuelekea
Miami..si umewahi zisikia beach za Miami ?(tamka mayami) alipanda pipa
ndege ya Eastern Airline 127 akiwa na sare zake na kujaza form akiweka
details zote. Akiwa huko ndani akaenda mpaka kukaa sehemu inaitwa
cockpit huko alikaa kwenye seat na kuwa tayari kwa swali lolote ambalo
angeulizwa na marubani. unajua kosa moja tu lingemfanya wamshtukie na
wampeleke segerea kunyea debe? Jamaa alikuwa anajiamini ile mbaya akakaa
mle ndani ame chill tu kama mtalaam ile kinoma.
Kinyume na matarajio yake marubani wala hawakujishughulisha naye kule
mbele kwenye chumba chao mwishowe wakatua Miami na hapo akashusha pumzi
za kushukuru..afadhali.kutoka hapo Frank akagundua sasa atakuwa kila
mara anasafiri kama deadheading kwa miaka kadhaa ijayo.ilikuwa bure na
alikuwa anaweza kwenda sehemu yoyote ya dunia ambako angeenda ku cash
zile check zake fake. Jamaa akawa anakula bata tu na watoto wakali toka
mataifa mbalimbali. Wakati anahojiwa anasema hivi vitu vitatu
vilimsaidia sana katika shughuli zake za utapeli hapa duniani.1.
mwonekano wake 2. Umakini wake katika kutambua mambo 3. Kufanya utafiti
wa kina kabla ya kufanya jambo lolote.
Anasema alijifunza jinsi ya kuweza kutapeli kwa kupitia cash baada ya
kufanya utafiti kwa kuangalia details flan flan kwenye check. Na
kuhakikisha kuwa anazichezea hizo namba katika namna ambayo itachukua
muda sana kugundua kuwa zile namba zimechezewa check ni fake. Hivyo
alikuwa akiziandika zionekane ni za mbali sana ili zichukue muda mrefu
kufuatiliwa na hvyo kumfanya aweze kujitolea pesa tena na tena katika
bank hiyo hiyo.
Zaidi Zaidi frank alikuwa anafanikiwa sababu alikuwa pia anafungua
akaunt ya ukweli kwa jina la kufikirika.na mara kadhaa alikuwa akitumia
check deposit ya ukweli na kuwapa bank address ambayo alikuwa kiishi au
sanduku la barua ambalo angepokea check husika. Hizo information
zilikuwa zinafanya transaction iwe ya kuaminika kabisa.akawa
anajiandikia check kwa jina lingine na kwend ku draw pesa katika banks
mbalimbali hapa duniani. Inawezekana hata bongo alifika…(ila sidhani
miaka hiyo tulikuwa bado sana). Na pale bank husika ilipokuja kugundua
kuwa check ilikuwa ni fake yeye alikuwa tayari ameshaondoka yupo pande
nyingine ya dunia...
..................................................................................................................................
SEHEMU YA PILI
Frank aliendelea kuishi maisha haya ya kuhama hama na kuwakwepa mapolisi
kila sehemu huku akiendelea kula bata na watoto wakali. Kiufupi maisha
yalikuwa yamemnyookea hasa, ingawa alikuwa anaishi kwa mashaka kiasi
flani lakini alikuwa smart sana. Maelfu ya dollar alizokuwa anatapeli
kwenye mabenk alikuwa anazificha kwenye masanduku salama ya kuhifadhia
pesa (safe deposit boxes) kila sehemu ya nchi ili hizo pesa
zitumike ikiwa atapata msala. Alishajua kuwa amechagua kuishi maisha ya
namna hiyo hivyo anapaswa kuwa tayar tayari wakati wowote akipata msala.
Mtu mwingine ungefikiria kuwa jamaa jinsi alivyokuwa na pesa ana
anavyokula bata na mademu kila sehemu alikuwa ana enjoy sana. Hapana.
Alifikia hatua akachoka maisha ya kuwakwepa mapolisi na akawa wakati
mwingine anakuwa mpweke sana.kwenye mahojiano anasema kila mtu
aliyekutana naye hakuweza kudumu naye maana alikuwa anajitambulisha kwa
fake name. si jina lake halisi.hivyo akawa hadumu na marafiki. Mademu
anagonga tu halafu anaanza mbele hataki kudumu na demu muda mrefu maana
ilikuwa ni risk sana.”hivyo ye anapita tu” ....
Frank alishajua kuwa yale maisha hayakuwa ya kudumu hivyo alikuwa
anaishi kwa umakini sana lakini alijua kuna siku tu angekamatwa. Kweli
siku hiyo ilifika. Alikuwa akisafiri kuelekea Miami akiwa kwenye ndege
kama kawaida deadheading..yaani anasafiri bure. Ndege aliyopanda ikatuka
Dade County na akiwa ndani ya ndege maofisa wa polisi watatu wakamfuata
na kuanza kumhoji. Yeye alikuwa amejenga utulivu mzuri tu akidai kwa
kujiamini kabisa kuwa yeye ni Frank William na kuwa ni Pilot bado wale
maofisa walimchukua kwa ajili ya mahojiano Zaidi.
Akiwa anahojiwa frank akatoa kitambulisho chake fake na kwa
kuwahakikishia kabisa akawapa majina ya marubani,wafanyakazi,masela
kibao wa kazini wengine wa PanAm aliokuwa anafanya nao kazi. polisi
walipowapigia jamaa hao waliwahakikishia kuwa jamaa ni mwana/mfanyakazi
mwenzao wapo naye kitambo tu wanapiga naye mzigo PanAm bila shida yoyote
tena mtu peace sana hana noma wala kokoro. Na Frank alikuwa mjanja sana
aliweza kujichanganya na wenzie kila alipokuwa akisafiri na wakamwamini
kuwa ni Rubani kweli kweli. Polisi walipopata huo uthibitisho kwa
masikitiko, wakamwomba msamaha kwa kumsumbua na kumchelewesha.
Akawaambia wasijali anajua wapo kazini na dunia imeharibika hivyo
wanatimiza wajibu wao. hamna noma peace and love.na polisi walihisi
pengine angeweza washtaki kwa kumharass..jamaa aliwahakikishia yale
yamepita na yaliyopita si ndwele wagange yajayo...wakapeana tano na
mapolisi akaondoka zake.kuanzia hapo akaamua kutulia kwanza kidogo kwa
muda flan kwa kiingereza tunaita ku lay low for a while. Atulie kwanza
kucheck hali ya hewa.
FRANK AWA DAKTARI WA WATOTO
Akiwa Atlanta Frank alifanikiwa kupata eneo flan limetulia sana ambalo
vijana wengi walikuwa wamechukua apartments akaamua naye apange eneo
hilo kwa mwaka mmoja. Na huko alijiandikisha kama ni doctor akiwa
anajaza mkataba wake wa kupanga hizo apartment. Na kudai ni daktari
ambaye alikuwa amekuja kupata mapumziko ya mudA mrefu kutokana na kupiga
kazi kwa muda kwa miaka mingi akiwa daktari wa watoto yaani
pediatrician. mshkaji alikuwa msanii kinyama.
Basi jamaa akawa amejenga utulivu maeneo hayo.anakula tu pesa zake za kuwaibia mabenk.wewe unahangaika kuwatapeli waswahili wenzio maskini laki laki zao.mwenzio anayaibia mabenki hata dhambi hapati sana.uongo?
Siku moja ametulia home anacheck zake movies akasikia hodi. Kwenda
kufungua akakutana na jamaa mmoja ambaye alijitambulisha kuwa ni doctor.
Frank akaona huu sasa msala kakutana na doctor mubashara kabisa kaja
kumtmbelea.maana alijua ishu yake ingebumbuluka.wakiwa katika maongezi
alijitahidi sana kutengeneza utulivu na mwishowe akaja kugundua yule
doctor hakuwa interested sana kuzungumzia masuala ya kazi.alikuwa
alikuwa mtu wa watoto sana… hivyo huko kwenye mademu sasa ndo akamkuta
frank kwenye profession yake kabisa aliyozaliwa nayo...sehemu husika ..
wakawa wanapiga sana stories kuhusu mademu na kuanza kuwagonga
..wakagundua wote ni wazee wa mabinti na hivyo wakawa marafiki sana.
Yule doctor akamwomba Frank siku moja amtembelee katika hospital
anayofanya kazi.pasipo kigugumizi frank alikubali. Na ikawa anamtembelea
kila mara na mwishowe frank akawa anafahamiana na wafanyakzi wengi tu
pale hospitalini. Si unajua mtoto wa mjini anavyojichanganya haraka na
watu.hii ilimsaidia sana maana aliweza sasa kujifunza juujuu kuhusiana
na udaktari wa watoto.mwishowe hata aliruhusiwa kuwa anaingia library
huko alijitahidi sana kujifunza udaktari wa watoto kama ambavyo alikuwa
akijinasibu.
Jamaa alionekana kufit sana kwenye hii nafasi alionekana anaipenda sana
kazi na mwishowe siku moja meneja wa ile hospital akataman aonane na
frank waongee kuhusu ajira pale kazini. Yaani alimpenda frank akapenda
naye afanye kazi katika ile hospital. Dah…. Frank akaona huu sasa
msala,ishakuwa noma.maana hakuwa daktari wa ukweli Zaidi ya usanii
tu.akawa anajaribu sana kukwepa hiyo hali lakini jamaa alikuwa
akimsumbua kila wakati kuwa waonane waongee. Mwishowe akakubali. Na yule
meneja akamwambia kitu ambacho zaidi kikamshangaza frank.alimwomba kuwa
awe anasupervise wanafunzi wa udaktari wanaokuja mafunzoni shift za
usiku kuchukua nafasi za daktari ambaye alikuwepo aliyepata
dharura.frank alikataa… lakini meneja alimshawishi sana.kabla ya hapo
frank alikuwa amepewa nafasi ya kuwasimamia wagonjwa mbalimbali pale
hospitalini baada ya kuwa amepata kibali cha kufanya kazi Jimbo la
Georgia.
Frank alikuwa na ujanja flan kukwepa maswali ambayo alikuwa hayafaham
pindi aulizwapo. Ikiwa ingetokea angeulizwa kitu ambacho hakijui basi
angekifanyia mzaha au utani na mwishowe kingepotezewa.yaani ilikuwa
huwezi mbananisha kwenye maelezo ambayo hayajui...atakuuzia uzia chai
mtacheka ishu itapita. Basi baada ya kuachia ile kazi ya usimamizi wa
wagonjwa kwa mhusika mwingine siku zote ule uwezo wake wa kufanya
masikhara na utani vilimsaidia sana kuficha ukweli kuwa hakuwa amesomea
udaktari. Zaidi zaidi wafanyakazi wengi walikuwa wakimpenda maana
alikuwa mtu wa chai sana na ucheshi kuwafanya wacheke muda mwingi kumbe
mshkaji ndo anafukia fukia mashimo kwa style hiyo.hakuwa na beef na mtu
wala ujivuni.alikuwa mtu wa watu sana.Basi aliendelea ku maintain ile
nafasi yake kama daktari msimamizi sababu hakuwa akilazimika kufanya
kazi yenyewe Zaidi ya kusimamia inavyofanywa na madaktari wengine.
Siku za mwizi ni arobaini. Siku moja mtoto aliletwa chumba cha
wagonjwa wa dharura akiwa amejeruhiwa mguu.frank akaitwa kwenda
kusaidia. Naye aligundua hapo ndipo rangi yake itajulikana kama ni
nyekundu au njano.akaona isiwe shida haraka naye akawaita wale vijana
waliokuwa mafunzoni akawakabidhi ile kazi halafu yeye akasimama serious
kuwaangalia wakipiga kazi.huku akikagua kagua.nao kwa kutaka kupata sifa
kwa msimamizi wao ambaye ni frank wakapiga ile kazi vizuri sana. Lakini
jambo hili lilianza kumpa shida kiasi kikubwa sana. Sasa alianza kuwaza
kuwa anacheza na maisha ya watu hivyo akaona si suala la kulifanyia
mchezo. Frank akaamua kuondoka hapo hospitalini maana alishagundua kuwa
angeweza kuhatarisha maisha ya mtoto.aliamua kujiuzulu baada ya muda
mfupi wa lile tukio alikuwa ameshafanya kazi kwa miezi kadhaa haukufika
mwaka. Akaamua kuelekea jimbo la Lousiana.
MAISHA YA FRANK LOUSIANA AKIWA NI MWANASHERIA
Frank akiwa Lousiana siku moja alikutana na moja ya mademu aliowahi
kuwagegeda miaka ya nyuma. Huyu dada alikuwa mfanyakazi wa kwenye ndege.
Frank alimwambia yule dada kipindi kile kuwa alikuwa ni co-pilot yaani
rubani msaidizi. sasa akwambia si hivyo tu ila pia alikuwa ni
mwanasheria. Alisomea urubani na pia alikuwa Mwanasheria.frank akawa
anaendelea kumgegeda yule mrembo kwa mara nyingine tena. anajilia tu
kiulani. ukitaka kupata mademu wakali unatakiwa uwe mjanja mjanja.
Siku moja wapo kwenye party usiku wakila bata yule dada akamkutanisha na
mwanasheria aliyekuwa akifanya kazi kwa mwanasheria mkuu pale jimboni.
Yule jamaa akavutiwa na Frank sababu Frank alidai kuwa yeye alipata Degree yake ya Sheria toka Chuocha Harvard.
Jamaa akaona hiki kichwa sana maana Harvard wanaosoma kule si watu wa
mchezo mchezo.ni Vipanga hasa si Chuo cha vilaza hata kidogo. Jamaa
akamwambia kuna nafasi katika ofisi ya Mwanasheria mkuu. Akamwambia
ambacho alipaswa kufanya ni kupeleka tu transcript yake kwa ofisi ya
mtihani na kuomba nafasi ya kufanya mtihani ili akifaulu aajiriwe kwa
hiyo nafasi.
Hii ilikuwa changamoto ambayo ilimpa hamu pia ya kujaribu, akiamini nayo
atashinda tu.baada ya kufanya maongezi na mwanasheria frank aliamua
kwenda kutengeneza transcript bandia/fake kutoka chuo kikuu cha Harvard.
Alifanya kwanza utafiti ni kozi gani zinafundishwa chuo cha
Harvard.alikusanya kila ambacho kilihitajika kwa ajili ya kutengeneza
mfano wa transcript hiyo. Aisee… mpaka amemaliza ile transcript ilikuwa
kama original.yaani mle mle….ingawa hakuwa amewahi kuiona transcript
halisi toka chuo cha sharia.ilionekana kuwa ni yenyewe kabisa na akaamua
kwenda kujaribu.
Hatua iliyofuatia ilikuwa ni kufanya mtihani .hivyo frank akanza
kujifunza sheria kwa week kadhaa kabla hajaenda kufanya mtihani.alipoona
na mambo mengi tayari anayafahamu aliedna kujiandikisha kwa ajili ya
kufanya mtihani.akawapa transcript yake ya magumashi. akaruhusiwa
kufanya.Alichemsha…si unajua hakuwahi kusoma sheria katika maisha yake
yote. Lakini alikuwa na advantage..ule mtihani uki fail unaweza tena
kuja kufanya tena na tena.unaruhusiwa kurudia.hivyo akarudia tena na
this time jamaa alipasua kinoma na akapewa leseni ya kufanya kazi kama
mwanasheria.
Na hapo hapo akaomba kazi kwa mwanasheria mkuu wa hilo jimbo ikafanyika
interview.akafanikiwa kuajiriwa kama legal assistant akiwa anafanya kazi
kama upande wa corporate law.akawa mbali na marupurupu mengine analipwa
mshahara wa usd 13,000 kwa mwaka miaka hiyo. Ulikuwa mshahara mkubwa
sana. Jamaa alionesha kipaji cha ajabu sana cha utapeli na usanii katika historia hapa duniani.katika
ile ofisi kulikuwa na mfanyakazi mwingine mpya aliajiriwa ambaye yeye
alisoma Harvard kiukwel kweli. Jamaa akawa ana mghasi sana kwa kutaka
kila mara wapige stories za chuo na kutaka kuzungumzia jamaa wengine
ambao walisoma pale chuo wakamaliza mwaka huo.akaona hii sasa itakuwa
issue jamaa asije akamuumbua bure. Akaamua kuachana na kazi yake hii ya
uana sheria na kuamua kutafuta kazi nyingine.
Akaamua kurudia ile kazi yake ya kwanza.lakini safari hii akaamua kuwa anafanya kazi shirika la ndege la Trans World Airways(TWA) hivyo
akajipatia sare,akatengeneza leseni mpya ya FAA,na kadi na kila kitu
kilichotakiwa kama alivyofanya kule PanAm. Akaanza kupiga kazi tena
akisafiri sehemu mbali mbali duniani na ku Cash bank mbalimbali ambazo
kipindi kile hakuzigusa.
FRANK AKIWA UTAH (Profesa wa Sociology)
Jamaa katika pita pita yake akafika mpaka Jimbo la Utah hili jimbo
lilimvutia kwa uzuri wake na pia kuw ana warembo wengi sana. Jamaa
akenda mpaka maeneo ya kampasi za chuo...daah aliona watoto wakali
sana.asikwambie mtu.udenda ulimtoka akajua hapo sasa inabidi kupiga
kambi ili aweze kuwagegeda ipasavyo watoto warembo. Nia alikuwa nayo ,uwezo (pesa) alikuwa nao na sababu pia alikuwa nayo.
Jamaa akaomba kazi chuoni ili afundishe. Alipata akawa anawapiga pindi
watoto warembo hapo chuoni.huku jioni anawapangia ratiba ya
kuwagegeda.apewe nini na shetani?acha awachape watoto warembo.
Jamaa akaamua sasa ahame kile chuo akaombe chuo kingine kufundisha chuo cha Brigham Young University. Akafanya appointment akijifanya yeye ni Profesa wa Sociology.
Akawa amewasiliana na Dean na kumwambia alifanya kazi ya kufundisha kwa
miaka kadhaa kabla hajaacha na kuwa Rubani. Na akasisitiza sasa anataka
kurudi katika kazi aliyokuwa akiipenda sana. Kazi ya ualimu. Yule dean
alivutiwa sana na uzoefu mbalimbali aliokuwa nao frank na pia uchangamfu
wake.
Akiwa na vyeti mbalimbali feki Frank akafanikiwa kupata interview na
Dean akaamua kumwajiri akiwa amevutiwa naye sana. Akakubali kumpa ajira
akiwa amepewa kozi moja aifundishe kwa semester nzima. Jamaa akaamua
kwenda library kujiandaa kwa ajili ya kufundisha kozi hiyo. Hatimaye
kwel akapewa mkataba wa kuajiriwa kwa semester moja awapige kipindi
watoto wa kidosi akiwa kama Profesa Frank.alionekana kufurahia
kazi hii mpya ingawa ilikuwa ni kwa muda tu maana hakuwa amepata mkataba
mkubwa. Anapiga vipindi lakini pia anapata muda jioni wa kuwagegeda
watoto wazuri ambao wanasoma pale chuoni na salary anapata kama kawa. Jamaa alikuwa anaua ndege wawili kwa jiwe moja.kazi na dawa.
Kazi hii hakudumu nayo sana kwa kuwa dean alimtaka kuwa asubiri nafasi
itokee ya kudumu kwa kuwa chuoni hawakutaka tena kuajiri walimu wa muda
mfupi.
SAFARI YA KWENDA CALIFONIA.
Frank akaondoka zake Utah huku akiwa amejilia kiasi cha kutosha nanii za
watoto wakali wabichi wa UTAH…akaamua kuelekea Califonia. (Unaukumbuka wimbo wa Tupac califonia Dream? Hili jimbo nalo lina maraha yake huko Marekani. Binafsi niliwahi fika huko kumekucha hasa)
akiwa anaelekea huko akafikiria kurudia tena kazi yake ambaya huifanya
vizuri zaid. Kuandika check za magumashi.kipindi hiki akawa amepata
uzoefu mkubwa zaidi katika kipengele hiki. Aliweza kuandika check kubwa
kubwa za maelfu Zaidi ya mara ya kwanza.aliweza kujikusanyia Zaidi ya
USD 100,000 kwa kipindi hicho. Ukiziconvert kwa sasa zinakuwa nyingi
Zaidi.
Alikuwa kijana mdpgo mwenye mkwanja wa kutosha kwa umri wake….alikuwa na
ukwasi mwingi tu huyu bwana mdogo.bado alikuwa na upweke kiasi
flani.maana kumbuka alikuwa ana vitambulisho mbalimbali.mara doctor,mara
mwanasheria,mara profesa,mara…. Yaani ili mradi jamaa aliweza kuwa kila
kitu.angeamua hata kufake kuwa yeye ni baba yako ungemwamini
nakwambia.angekuja angekueleza yeye ndo baba yako kweli kweli huyo uliye
naye siye..na angeweza hata kumshawishi mama yako…usiombee ukutane na
frank mtaalam.jamaa alikuwa kichwa hasa.
Basi katika pita pita zake akafanikiwa kumpata mtoto mmoja mkali
sana.wakapendana. huyo binti alikuwa ni mfanyakazi wa kwenye ndege. Na
nikuambie kitu? Ukitaka watoto wakali sana… angalia wafanyakazi wa
kwenye ndege,aisee ni wazuri sana..kama umepanda panda ndege wengi wao
ni wazuri sana.sema yale maumbo yetu ya miss bantu huyapati.
SEHEMU YA MWISHO.
Basi frank akawa amempenda sana yule mtoto na alitamani kabisa kuwa
waishi wote na katika kuzidiwa na mapenzi ye mwenyewe akaamua tu
kumwambia ukweli yule binti.akajichana ye mwenyewe. Unajua hakuna kitu
kigumu kama kukaa na siri…trust me ni ngumu sana yaani sometime
unatamani hata uende porini ukaseme siri yako then baada ya hapo
unajisikia kama umetua mzigo mkubwa.kama tu ile story ya mfalme aliyekuwa na masikio ya punda.
Yeye aliamini kwa kumwambia huo ukweli basi yule mwanamke atamsamehe na
kuyachukulia yale kama ni madhaifu yake na wakasonga mbele pamoja
wakiishi real sasa.maana jamaa alikuwa hata hujui leo ye ni frank au
john au abel....
Mshkaji alifanya kosa. Usiwaamini sana mademu… jamaa alitegemea kuwa
demu angemwona amekuwa mwaminifu na sasa wasonge mbele kumbe sivyo.dem
akaenda kumchoma FBI na kuwalezea alipo. bahati nzuri Jamaa wa machale
alifanikiwa kuwatoroka akawa tena anaishi maisha ya kimachale machale.
Jamaa akasafir mpaka ufaransa. Na akiwa katika ndege akakutana na demu
mmoja mkali mfanya kazi wa kwenye ndege wakaanza mahusiano. Aligundua
kuwa baba wa yule demu anamiliki duka la kuprint pictures na stationary.
So akawa anatamani sana akutane na baba wa yule binti.kweli ikatokea
akakutana na baba ya bint yule.frank akamwambia mzee kama atakuwa tayari
kupiga naye kazi.yaani waprint kazi moja yenye mshiko kwa ajili ya
PanAm.frank akamwambia mzee anampa tenda ya kuprint check 10,000 za
payroll kwa wafanya kazi wa PanAm.yule mzee hakuwa na hiyana akaona
mchongo si ndo huu. Akapiga kazi
Frank akazichukua hizo checks na kuanza kuzitumia katika Mabank kadhaa
hapo hapo ufaransa.akajikusanyia makwaru kwaru (pesa) kibao. Halafu
haraka sana akapanda mwewe kurudi USA ambako pia aliendelea kujikumbia
mkwanja kwa njia zake haramu za kimazabe mazabe.
Muda si mrefu baada ya kurudi US. Siku moja Manjagu wakambananisha
airport ya Boston akiwa anataka kupanda mwewe akale bata jimbo lingine.
Jamaa wakamweka kwanza korokoroni ili waendelee kukusanya ushahidi
mbalimbali kuthibitisha kama alikuwa ni yeye yule jamaa mtukutu sana
Frank A.jr hata hivyo Manjagu /polisi walishindwa kupata kwa usahihi
ushahidi wa kutosha yeye ni nani hasa. Walikuwa wamweka tu korokoroni
hajapelekwa hasa segerea kwenyewe.ushahidi wa kutosha ukawa umekosekana
na mwishowe akaachiwa kwa dhamana akiwa ameponea chupuchupu kuja
kukamatwa na FBI ambaye alikuwa ametumwa kwenda kumtafuta. Jamaa ikawa
kama wamempiga chura teke… si unajua humkomoi ukimpiga chura teke
unamwongezea mwendo. Basi akazidi kuwa jasiri badala ya kukatishwa tamaa
au kuingiwa woga.
Baada yu ya kutoka akaenda kuazima sare za walinzi au sercurity guard na
kwenda kusimama pale pale uwanja wa ndege ambako mamwela walimkamata
masaa kadhaa yaliyopita. Alikuwa ameshikiria mfuko mkubwa maalum ambao
alikuwa anasubiria watu waweke deposits/pesa zao kila wanapokuwa
wanapita au kusafiri kama ulivyo utaratibu. Wakawa hawana shaka wanaenda
wanaandikisha zinahesabiwa wanakuja wanaweka kwenye ule mfuko/begi
maalum alioshika frank wanaendelea na shughuli zao. Lile begi lilipoanza
kujaa aliamua kulibeba kupeleka kwenye gari alilokuwa amekodi. Lilikuwa
zito maana kulikuwa kumewekwa mapene kichele (pesa nyingi sana). Basi
wale jamaa wengine wakaamua kumsaidia mshkaji pasipo kujua wanamsaidia
mwizi katika mchakato wa kuondoka na pesa za wizi.jamaa siku ile ile
moja tu alipiga zaidi ya usd 60,000 akaweka begani akalala nazo
mbele.ilikuwa noma ile mbaya…. Polisi walikuja kumgwaya hapo baadaye si
kwa usanii ule.
Kukamatwa
Frank akawa anaonekana ameshindikana karibia kwenye kila kitu alichokuwa
akifanya.alifanikiwa kuwakwepa manjagu na hata FBI kwa kila mpango
mpya.aliendelea kufikiria namna ambavyo ataendelea kupiga mkwanja mrefu.
Akaja na wazo lingine.aliamua kuwa kwa sasa hatakuwa anasafiri peke
yake. Atakuwa anasafiri na warembo kibao. hii itasaidia aweze kuwa ana
cash mkwanja zaidi .maana unapokuwa umezungukwa na mademu watu
hawakutilii shaka hata kidogo hivyo akaona aibuke na mbinu hi ya
kutembea na watoto kadhaa wakali.
Akiwa anatembelea Arizona Frank akaweza kufanya mchakato wa
kuoana na Director/Mkurugenzi aliyekuwa anahusika na masuala ya
wanafunzi vijana katika vyuo vya serikali jimboni hapo.yaani kuwapeleka
vyuo mbalimbali wanapoomba na pia kushughulika nao wanapomaliza kwa
masuala ya ushauri na kazi. Akawa amaeongea naye uwezekanao wa kuajiri
wanawake wengi kama maafisa uhusiano kwa ajili ya PanAm. Na akamwambia
wanawake ambao atakuwa amewachagua watapata hata nafasi ya kwenda
kutembelea Ulaya kipindi cha majira ya joto. zaidi zaidi hao wanawake
watapewa mpaka uniforms au sare za PanAm,watapewa mshahara na barua za
ajira pindi wamalizapo tu masomo yao.
Ilikuwa patashika pale chuoni watoto wazuri wengi waliomba hiyo nafasi…
kila mtu alitamani awe mfanyakazi wa kwenye ndege..na si unajua watoto
wakali wanapenda maisha yale ya kuzunguka tu na mwewe angani huku wakial
bata sehemu mbalimbali duniani.katika kusagula sagula humo ndani
akajipatia watoto nane wakaliiiiiii balaa.hawa walikuwa wakisisimkwa na
vinyweleo kusimama wakiwaza jinsi ambavyo wataizunguka dunia ndani ya
mwewe.halafu wakawa wanawaza pia jinsi ambavyo watakuwa wanalipwa kula
bata. Just imagine unaenda kula bata na bado unalipwa
pia.hawakujua.hawakujua.
Lengo la Frank lilikuwa kuwatumia hao mademu wakali kwenda ku cash zile
check zake za kimagumashi hivyo akawa anaandika check za malipo makubwa
kuliko hata ya kawaida. Akiwa huko huko bado alikuwa anawala kwa zamu
tartiiiiibu.kama Analia vile.kwa hiyo muda wote akawa anazunguka nao
wakiwa wamevaa zile sare wakifurahia sana na akawa anaenda nao bank ku
cash zile pesa na huko hawakuweza kumtilia mashaka hata chembe maana
unawezaje kumtilia mashaka mshkaji amezungukwa na watoto wakali wa
kibongo,kilatino,kitasha n.k tena wamevaa sare za PanAm. Huwezi.kumbe
jamaa anawapa tu za chembe kimya kimya anafinya mpunga wa kutosha
kutokana na wao.inasadikiwa jamaa alikusanya mpunga wa zaidi ya usd
300,000 miaka hiyo. Si mchezo.
FRANK ANAHAMISHIA MASHAMBULIZI UFARANSA (MWANDISHI WA MOVIES ZA HOLLYWOOD)
Alipoona hii imefanikiwa akaamua tena apumzishe hii mbinu ili asije
akashtukiwa. Akaamua kwenda Montpellier huko Ufaransa. Haikuwa mbali na
alipokuwa amezaliwa mama yake. Akamua kutulia kwanza kwa muda kwenye
nyumba tu ya wastani akiwa amebadilisha jina anaitwa Robert Monjo na
akijifanya yeye ni mwandishi wa movies toka Hollywood.karibia mwaka
hivi alijitahidi kuishi maisha ya kawaida tu.alikuwa amechoka sana na
maisha ya kukimbia kimbia manjagu na FBI.
Siku za mwizi zilikuwa zinakaribia …na jamaa alishaacha hata kuzihesabu
maana si unajua wanasema siku za mwizi ni arobaini?so kama unaiba
hakikisha ukifika 39 unaacha. Jamaa mmoja mgwadu sana wa FBI alikuwa anaitwa Joseph Shea huyu
alikuwa amekomaa ile mbaya kumtafuta Frank kwa miaka na miaka.maana FBI
si kwamba walikuwa hawana taarifa zake.walikuwa nazo ila walikuwa bado
hawampata ile bumper to bumper wanamlia tu timing. zaidi zaid ya kusikia
tu mshkaji kapiga huku.wakienda hayupo,wanasikia tena kapiga bank flan
wakienda hayupo. Jamaa alisema ye atakomaa naye tu mpaka kieleweke iwe
mchana au usiku,iwe masika au kiangazi. Hakuna kulala.
Miezi kama minne hivi Frank akiwa France jamaa wa FBI alishapata taarifa
hizo. Unajua ilichukua miaka mingi sana kufahamu kuwa Frank hakuwa mtu
mzima ni bwana mdogo tu ambaye akili zimemzidia ameamua kuzitumia
kihuni. Yule FBI alikutana na mmoja wa wafanyakazi wa ndege ambao frank
alikuwa amewakamua. Akamwonesha picha kuwa anamtafuta jamaa.. yule demu
akakiri anamfaham jamaa na kuwa yupo ufaransa sehemu flan ame chill tu.
Manjagu wa Ufaransa wakatonywa kuwa kuna mshkaji mmoja hafai
ameshaziumiza banks mbalimbali Zaidi ya Usd 2.5 Million so yupo kitaani
kwao wakamcheck. Wale wafaransa wakaona hii sasa issue yule mpigaji yupo
nchini mwao.wakaanza mfuatilia na kuja kumkuta frank anafanya shopping
mtaani kwenye kigrocery flani karibu na maskani mwake. Wakamdaka
kumpeleka Montpellier Polce Station kumfungulia mashtaka kwa
makosa aliyokuwa amewatendea pale ufaransa. Baada ya mahojiano frank
alikuwabli kuwa yeye ni Frank A. Jr lakini akakataa kueleze kiundani
makosa yake yote.hakutaka kuwapa habari yoyote kuhusiana na makosa yake.
Ana bahati sana angekuwa ni mbongo halafu kakamatwa bongo akingepata
kisago cha mbwa mwizi mpaka angeanza kuimba.
Ndani ya week frank akawa amepelekwa kwa pirato huko ufaransa na kukutwa
na misala kibao..yaani alikutwa na madhambi au makosa mengi tu kwa
mujibu wa sheria yakiwemo hayo ya utapeli. Wakampeleka kunyea debe
segerea ya ufaransa kwa mwaka mmoja gereza moja la watu watukutu sana la Perpignan…. Aliishia tu kufungwa miezi sita. Ila hali ya mle ndani ilikuwa mbaya sana.wakamtoa.
Akapelekwa Sweden na baadaye Ufaransa. Huko akifanikiwa mara kadhaa
kuwatoroka Manjagu na FBI na kuanza kuishi maisha ya kimachale machale…
mwishowe akajikuta anasakwa ile mbaya.FBI wakamweka katika ile list yao
ya wanted. Akajikuta hana pa kujificha na mwishowe alikuja kukamatwa
akiwa amejificha huko New York si unajua mkono wa sheria ni mrefu sana.
Na wale manjagu walishaona huyu jamaa si saizi yao wakampeleka
kumkabidhi kwa wazee wa kazi wa FBI ( Female Body Intruder…
ha haha am kidding bwana si maana hiyo) huko wakampeleka kwa pilato ili
akapate stahiki zake kwa madhambi aliyowatendea wanagenzi mbalimbali.
Jamaa wakamhukumu kifungo cha miaka 12. Huko Virginia Gereza la Petersburg.
Na hata hivyo akapata parole akiwa na miaka 26 akiwa ametumikia miaka 5
nyuma ya nyondo. Yaani alikuwa mpaka muda huo amechezea mvua 5 tu
katika 12. Akaachiwa na kupata nafasi ya kuanza maisha mapya.
Baada ya kutoka segerea jamaa akaanza kuranda randa mtaani akitafuta
vibarua. Ila life lilishakuwa gumu kinoma jamaa hakuzoea ku hustle namna
ile na makashkash kibao akikimbizana na life.akawa anakamata kamata tu
vijikazi kiasi vya kumtoa angalau asilale na njaa.alikuwa mara nyingi
akijitahidi isijulikane kuwa alikuwa ni tapeli na alishawahi
fungwa.lakini mwishowe waajiri wake wakawa wanakuja kufaham ukweli na
kumfukuza.
Baada ya muda Frank akaanza kuwa frustrated … yaani kama kupagawa flani
hivi kimawazo sababu alijua kabisa ana kipaji ambacho sehemu flan mtu
anaweza akakihitaji. Hivyo akawa anawaza kutafuta mteja ambaye angekuwa
interested na ujuzi wake na hivyo kufaidika nao. Hivyo akaamua kutafuta
namna ya kujitangaza. Kwa kushangaza kabisa watu ambao wangefaidika naye
walikuwa ni FBI. Hawa FBI ndiyo ambao wangeweza faidika na kipaji
alichokuwa nacho. FBi walikuwa wanahitaji kufaham namna mbavyo wahaalifu
wanatumia akili kufanya uhalifu wao ili waweze kuwakamata wahalifu hao.
Frank akaanza kuwapa lecture bure.alijua pia kwa kutoa elimu hii
alikuwa analipa kwa jamii aliyokuwa ameiumiza kwa utapeli wake.kabla ya
muda mrefu kupita ikaja kazi ambayo ingeweza kumlipa elimu aliyokuwa
nayo ikawa inahitajika sana na makampuni mengi duniani. Makampuni mengi
yakagundua yanaweza kuokoa pesa nyingi mamilioni au mabillion kutoka kwa
matapeli ikiwa watakuwa na mtaalam wa utapeli ambaye atawasaidia. Hivyo
frank akawa ni mtu ambaye anatumika kwa ajili ya kuwapa taarifa muhimu
za kuzuia matapeli.
Jamaa akawa anaitwa huku na kule akawaelekeze na wanampa mkwanja wa
maana hasa. Na mpaka leo hii frank anaheshimika na makampuni mengi akiwa
amefungua kampuni yake ya kutoa ushauri na kulingana na website yake ya
www.abagnale.com
frank amekuwa akienda kupiga lecture,akifanya consultation duniani
nzima na kutoa semina na makongamano na vile vile akaamua FBI awe
anawapa ushauri bure kabisa ingawa wao walikuwa wanataka wamwajiri.yeye
aliona aitumikie FBI kwa nia hiyo ya kuwapa ushauri bure.
Jamaa ameandika vitabu vingi tu,Makala na mahapisho mbalimbali na ku
design check ambazo ni salama zinazotumika na wafanyabiashara mbalimbali
wakubwa duniani. Kiuhalisia hakuna shaka kabisa kuwa jamaa amekuwa
akijitahidi sana kusahihisha makosa aliyoyafanya miaka ile ya nyuma na
kipaji au akili yake kaipelekea katika mambo ya kujenga zaidi na si
kuwapiga wenye makampuni na bank kama zamani na kula papuchi tu muda
wote. Na jamaa ukimcheki amechange sana kwa sasa akiwa na mke ambaye
wameishi naye Zaidi ya miaka 25 na kufanikiwa kupata watoto wa3. Jamaa
amekuwa mtu wa dini sana kwa sasa. Anaenda church na kushirikiana na
wadau wengine katika kujenga taifa. Ukimcheck kwa kweli ame change sana.
Kwa sasa anaishi huko Midwest na mkewe na watoto wake vidume
watatu.anakula kihalali. tuacheni uhalisi ndugu zanguni.....
No comments:
Post a Comment