Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kubadili tarehe ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara… TFF imefanya maamuzi hayo kufuatia kubadilishwa kwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na jukumu la kuifundisha Timu hiyo akapewa Charles Borniface Mkwasa.
Ligi Kuu Tanzania ilikuwa
ianze August 22 2015 lakini kw sasa itakuwa hivi, Ligi itaanza Septemba
12 2015 kwa lengo la kumpa muda wa kutosha Kocha Mkwasa wa kukinoa kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza na timu ya taifa ya Nigeria Septemba 5.
Mchezo wa Ngao ya Jamii (Community Shield) ambao utazikutanisha timu za Yanga na Azam FC utapigwa August 22 badala ya August 15 kama ilivyokuwa imetangazwa awali.
Ratiba ya Ligi Kuu sasa inafanyiwa
marekebisho na mechi zitakuwa zinachezwa katikati ya wiki na siku za
weekend kasoro Oktoba 25 2015 ambapo hakutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu
wowote ili kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge Tanzania.
Klabu zinazoshiri Ligi hiyo zimeandikiwa
barua kupewa taarifa hiyo na wamiliki wa viwanja wameandikiwa barua
kukarabati viwanja hivyo ili viweze kukidhi vigezo vya kutumika katika
michezo ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza vinginevyo havitaruhusiwa
kutumika.
No comments:
Post a Comment