Lagos, Nigeria MWIGIZAJI wa
kike wa Ghana, Yvonne Nelson, amesema wiki kadhaa zilizopita katika
mahojiano kwamba mwanamuziki wa Nigeria, Iyanya, ndiye mtu kwa kwanza
ambaye aliuvunjavunja zaidi moyo wake kwa penzi kubwa ambalo
alilolionyesha kwake.
Hata hivyo, mwanamuziki huyo alipofanya mahojiano na kituo cha
televisheni cha MTV, alisema japokuwa kweli alikuwa na uhusiano motomoto
na Yvonne Nelson, lakini hakuwa mtu wa kwanza kumpagawisha kimapenzi.
"Tulipoanza uhusiano na Yvonne Nelson, sikuwa na furaha kwani kila
mtu alikuwa anafikiri kwamba mimi nilikuwa ndiye shetani aliyempagawisha
mwanamke huyo.
Watu wananizungumzia mimi hadi leo, lakini, mbona hawawazungumzii
wanaume wengine ambao walimpagawisha kabla yangu?” aliuliza Iyanya.
Aliongeza kwamba pamoja na penzi lao kukoma, bado ni marafiki wa
kawaida.
No comments:
Post a Comment