
SIRI NYETI ZAVUJA
Wakati
Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikiendelea na hekaheka za vikao vya uteuzi wa
wagombea ili kumpata mgombea atakaye peperusha chama hicho katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, jaribio jipya lakutaka kumzuia kada wa
chama hicho ndugu Edward Lowassa imefahamika.
Habari
kutoka vikao vya ndani vya siri vilivyo kaa kuanzia juzi, jana, na leo
vimeripoti kuwa mkakati huo mahususi na wa siri uliowakutanisha vigogo
wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) umeazimia kumshinikiza msajili wa vyama vya
siasa nchini Jaji Francis Mutungi kuandaa taarifa itakayo mtia hatiani
ndugu Edward Lowassa kwa kuonesha kuwa alianza kampeni kabla ya wakati.
Mkakati
huo wenye Baraka za vigogo wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) umeratibiwa kwa
umakini mkubwa kwa msukumo wa wagombea wanatajwa kwa majina ya Bernard
Membe, Mizengo Pinda, Januari Makamba na John Pombe Magufuli, ambao pia
wamepata Baraka kutoka kwa baadhi ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi.
RSS Feed
Twitter
July 10, 2015
Unknown
0 comments:
Post a Comment