Wednesday, April 26

Mataifa ya Asia yameanza sheria kuthibiti ulaji wa nyama ya Mbwa na Paka
Taiwan imepiga marufuku uuzaji na ulaji wa paka na mbwa kufuatia visa kadhaa vya ukatili dhidi ya wanyama na kuzua ghadhabu ya umma.
Sheria mpya ya kulinda wanyama imeweka adhabu ya faini pauni 6,500 kwa yule anayepatikana akiuza, kula au kununua nyama hiyo.Wanaopatikana wakiwadhulumu wanyama nao watapigwa faini ya Pauni 52,000 na miaka miwili gerezani.
Taiwan ndilo taifa la kwanza kuweka marufu hii Barani Asia.
Sheria mpya inanuia kukabili baadhi ya imani kuhusu ulaji mbwa. Kwa mfano kuna baadhi wanaamini kumla mbwa mweusi wakati wa msimu wa baridi kunamsaidia mtu kupata joto mwilini.
Sheria hii imeungwa mkono na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen, ambaye ana mbwa watatu na paka wawili.
Korea Kusini imefunga soko kubwa la kuuza mbwaUlaji wa paka na mbwa umeendelea kupungua wakati jamii ikibadilisha jinsi inavyoshughulikia wanyama wanaofugwa nyumbani. Shirika linalotetea mslahi ya wanyama 'Humane Society International', limetaja mataifa ambayo yana desturi ya kula mbwa na paka.
Haya ni pamoja,Thailand, Laos, Vietnam, Cambodia na jimbo la Nagaland nchini India. Aidha desturi hii iko katika nchi za China, Korea Kusini na Ufilipino.

CHINA
Licha ya kutokuwepo na takwimu rasmi, China inaaminika kuongoza duniani katika ulaji na uuzaji wa mbwa na paka. Kila mwaka karibu mbwa na paka milioni 10 wanaaminika kuchinjwa nchini China.
Shirika linalotetea maslahi ya wanyama linasema wanyama wengi wanaibwa wakati wakionekana barabarani bila wamiliki wao.

Katika mji wa Yulin huko China mwezi Juni husherekea sherehe maalum ya mbwa na paka. Inakadiriwa mbwa na paka 10,000 huchinjwa mwezi huu kwa tamasha hiyo. Mwaka uliopita sherehe hizo zilikumbwa na maandamano kupinga kuwajicha mbwa na paka.

KOREA KUSINI
Nchini Korea Kusini, nyama ya mbwa ni maarufu sana kiasi cha kitoweo chake kupewa jina la 'Gaegogi'. Inaaminika taifa hilo lina mashamba 17,000 yanayowafuga mbwa na kuuzwa kuwa chakula. Hata hivyo shinikizo za mashirika ya kutetea maslahi ya wanyama zimeanza kuzaa matunda.
Hapo mwezi Februari, soko kubwa zaidi la mbwa lilifungwa katika eneo la Seongnam, kabla ya Korea Kusini kuandaa michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi.

VIETNAM
Takriban mbwa milioni tano wanaaminika kuchinjwa na kufanywa kitoweo nchini Vietnam kila mwaka.
Ongezeko la wateja wa nyama hii limepelekea kuwepo na biashara ya magendo ya nyama ya mbwa katika nchi jirani za Thailand, Cambodia na Laos.
Taiwan imepiga marufuku uuzaji na ulaji wa nyama hii
Shirika linalotetea haki za wanyama la 'Asia Canine Protection Alliance', limeshinikiza serikali kujaribu kumaliza biashara ya nyama ya mbwa.
Shirika hilo limesema lina ushahidi kwamba nyama ya mbwa ni hatari kwa afya ya binadamu,na huenda ikasabaisha ugonjwa wa kichaa cha mbwa miongoni mwa watu wanaokula nyama yake.

Korea Kusini imesema sehemu muhimu za mfumo wa ulinzi wa Marekani wa kukinga makombora zimeshawekwa nchini humo, baada ya hasimu wake Korea Kaskazini kuonyesha nguvu zake za kijeshi. Ni hatua pia iliyoikasirisha China.
Marekani inaisisitiza China - ambayo ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini- kuchukua hatua zaidi za kuidhibiti nchi hiyo. Lakini taifa hilo kubwa barani Asia limeitikia wito huo kwa hasira, kutokana na hatua ya Marekani ya kuweka mfumo wa kukinga makombora unaojulikana kama THAAD katika ardhi ya Korea Kusini.
China ina wasiwasi  mfumo huo wenye nguvu kubwa unaweza kupenya katika ardhi yake na kudhoofisha usalama wa nchi yake, pamoja na usalama wa kanda hiyo. China inaupinga mfumo huo wa kukinga makombora katika kanda hiyo ya Asia.
Aidha, China imeichukulia Korea Kaskazini hatua kadhaa, ikiwa ni pamoja na kupiga marufu makundi ya ziara nchini mwake.
Akizungumza katika mkutano wake wa kila siku na waandishi habari, msemaji mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya China, Geng Shuang, amesema China inaitolea wito Marekani na Korea Kusini kuondoa mfumo huo wa kukinga makombora.
"Tunatarajia kwamba pande zote, ikiwa ni pamoja na Japan, zitashirikiana na China ili kulipatia suala hili azimio la amani la mapema. Tunatarajia kwamba pande zote zitachukua jitihada kama ilivyo wajibu wao," amesema Geng Shuang.
Donald Trump und Xi Jinping (picture alliance/AP Photo/A. Brandon) Rais wa Marekani Donald Trump, akiwa na Rais wa China Xi Jinping
Marekani na mshirika wake Korea Kusini wanasema uamuzi wa kutuma wanajeshi, ulikubalika tokea mwaka jana, na una lengo la kuzuia  kitisho cha makombora ya Korea Kaskazini iliyo na silaha za kinyuklia.
"Na tunaendelea katika ngazi zote mbili kujijenga na kuwa tayari hata tukihitajika kupigana usiku wa leo. Kwa upande wa zoezi hili na katika kazi yangu hii ya miaka ishirini, sijawahi kuona zoezi la aina hii.. la kitaaluma zaidi na lenye uwezo zaidi wa mifumo ya silaha ambayo imejumuishwa pamoja na yenye uwezo wa kufyatua risasi kwa wakati mmoja .. kama nilivyoona katika zoezi hili hapa," amesema Luteni Kanali wa Kimarekani Matthew Harner, akiuzungumzia mtambo huo wa kukinga makombora.
Rais wa China, Xi Jinping alizungumza na Rais wa Marekani Donald Trump juzi kwa njia ya simu na kumtaka ajizuie katika suala hili la Korea Kaskazini.
Viongozi wa ulinzi wa Marekani pamoja na maafisa wengine a ngazi za juu, leo wanatarajiwa kuwa na mkutano wa siri na maseneta wote wa Marekani kuhusu suala hilo la Korea Kaskazini. Ni mkutano usio wa kawaida katika ikulu ya Marekani ya White House.


Je, Falsafa ya Kuanzishwa kwa Mbio za Mwenge wakati wa Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/1961 imepitwa na wakati??? Je, kuna wakati utafika misingi ambayo taifa hili lilijengwa kwahiyo, itapitwa na wakati? Je, tuachane na mbio za Mwenge kwa sababu za gharama kuwa kubwa - wengine wanasema mwenge ni Jipu na Rais Magufuli alitumbue? Au Mbio za Mwenge zina umuhimu na ni sehemu ya msingi ambao taifa hili lilianzishwa na ni kumbukumbu ya mapambano ya kumletea mabadiliko na maaendeleo Mtanzania? Yote haya nitayatolea ufafanuzi kwenye Penyenye Fupi Fupi.
Falsafa ya Mwalimu Julis Kambarage Nyerere kuhusu mwenge wa Uhuru ilikuwa ni: “Sisi Watanganyika, tunataka  kuuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau”.
Je, Falsafa ya Kuanzishwa kwa Mbio za Mwenge wakati wa Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/1961 imepitwa na wakati??? Ikumbukwe kwamba falsafa hii ni sehemu ya misingi ya Taifa letu..tangu ilipoanzishwa na waasisi wetu. Mataifa yaliyoendelea yameendelea kuenzi misingi iliyojenga Mataifa hayo kwa gharama zozote zile. Tutakubaliana sote kuwa Watanzania bado tunahitaji kujikwamua kutoka kwenye ujinga, maradhi, na umaskini. Tunahitaji kujikwamua kutoka kwenye dhuruma na chuki ambazo, ukizingatia dhana ya mazingira na wakati, zimekuwa ni tofauti zaidi ukilinganisha na wakati wa Uhuru. Japokuwa wakati wa Uhuru kulikuwa na dhuruma, ufisadi, chuki nakadharika, bado hata sasa hivi tuna ufisadi, dhuruma na chuki tena zilizoenda mbali sana. Katika dhama hizi za Magufuli, zilizotofauti kabisa na nyakati za Kikwete, Mkapa, Mwinyi na zile za wakati wa Baba wa Taifa. Tumejionea uozo wa hali ya juu kuliko ambavyo tumewahi kushuhudia. Neno hili siyo geni tena kwetu – “Tanzania ilikuwa ni shamba la bibi”.  Mwenge wa Uhuru unapaswa kutukumbusha kila mara kuwa vita dhidi ya ubadhirifu, chuki, na dharau bado inaendelea. Tena falsafa ya Mwalimu ilikuwa inataka huu Mwenge umulike hadi nje ya mipaka yetu. Hii inanipeleka kwenye penyenye yangu inayofuata – Kuingiliwa kwa Uhuru wa Taifa letu na Mataifa ya Magharibi.
Tutakumbuka kuwa hivi karibuni sakata la MCC 2 lilishika kurasa nyingi sana. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Marudio wa Zanzibar na kuhusiana na ile sharia ya makosa ya Kimtandao. Taasisi ya MCC ni kibaraka wa umagharibi, pia ina kila lengo la kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu. Maitaifa ya Magharibi kuingilia mambo ya ndani ya nchi za kiafrika limekuwa ni jambo la kawaida sana. Tumekuwa ni nchi ya amani isiyokiuka haki za binadamu, sasa kuiingiliwa kwenye mambo ya ndani ya nchi ni jambo linakiuka hadhi yetu ya kuwa Sovereign State. Mwenge wa Uhuru unatukumbusha maneno ya Mwalimu Julius Nyerere kuwa “… tunataka kuuwasha Mwenge na kuuweka juu yam lima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu...” Je msingi huu wa kuanzishwa kwa Taifa letu umepitwa na wakati, hasha.. msingi huu bado uko na unaendelea. Na kama taifa lazima tusimame kidete. Mwenge huu inabidi tuumulike ili sisi kama Watanzania tujikumbushe, na hayo mataifa ya nje yaliyo karibu nasi na yaliyo Magharibi au Mashariki. Pia ninaungana na kauli ya Mh. Rais Dk. John Joseph Magufuli kuwa ni bora kuishi kwa kula mihogo kuliko kula mkate ya masimango.
Je, kuna wakati utafika misingi ambayo taifa hili lilijengwa kwayo, itapitwa na wakati?
Mwalimu Julius Nyerere, alipohutubia Watanganyika kwa mara ya kwanza kama Waziri Mkuu wa Tanganyika, alielekeza kuwa Tanganyika iko vitani dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini. Ni nukuu baadhi ya maneno yake: “…matatizo haya, hayanitishi mimi, hayawatishi wenzangu, na wala hatuombi kwamba yawatisheni ninyi. Tunayaona kwamba ni jaribio tu…Mara nyingi sana, nimesema nayi juu ya umaskini, ujinga, na maradhi, lakini kwa kweli adui yetu mkubwa ni umaskini. Tukiweza kumshinda adui huyu, tutakuwa tumeweza kupata silaha itakayotuwezesha kuushinda ujinga na maradhi. …tunaweza kupigana vita vya umaskini. Namuomba kila raia wa Tanganyika, aape kiapo cha kuwa adui wa umaskini. Amshambulie adui huyo mahali popote atakapoonekana.”
Japokuwa Tanganyika ilipata Uhuru wake bila mapambano dhidi ya mkoloni yaliyohusisha kumwaga damu. Msingi tuliachiwa na Baba wa Taifa ni kuwa nchi iko kwenye mapambano dhidi ya umaskini. Kila Mtanzania anapaswa kuwa vitani wakati wowote. Nikiiweka hoja hii kwenye muktadha wa Mwenge wa Uhuru ambao unajengwa kwenye msingi wa kumulika ubadhirifu na dhuruma. Tumeshuhudia ambavyo viongozi au watumishi wetu katika kada mbalimbali wakiwa mstari wa mbele kwenye ubadhirifu wa mali za umma. Kuingia mikataba isiyokuwa na tija wala maslahi ya Taifa. Watu hawa wamekuwa wakiturudisha nyuma sana kwenye vita dhidi ya umaskini ambao mwalimu alitutaka kila Mtanzania kuapa kupambana nao kila sehemu atakapoukuta. Ila katika juhudi za Mtanzania maskini kujitafutia njia za kutoka kwenye umaskini na wengine kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi, wachumia tumbo wamekuwa na mtindo wa kujinufaisha wao na vizazi vyao. Kinyume kabisa na misingi ya Taifa letu. Kila Mtanzania akiwa vitani dhidi ya umaskini inamaanisha kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato na serikali itatimiza wajibu wake kuwaletea wananchi bidhaa za umma. Ndiyo maana katika dhama hizi za Magufuli utumbuaji wa majipu unaturudisha kwenye ile vita dhidi ya dhuruma, ufisadi, na uonevu. Mwenge lazima uendelee kumulika, falsafa na itikadi ya kuwa tuko katika mapambano lazima iendelee kumulikwa.
Je, tuachane na mbio za Mwenge kwa sababu za gharama kuwa kubwa - wengine wanasema mwenge ni Jipu na Rais Magufuli alitumbue? Au Mbio za Mwenge zina umumhimu na ni sehemu ya msingi ambao taifa hili lilianzishwa kwayo na ni kumbukumbu ya mapambano ya kumletea mabadiliko na maaendeleo Mtanzania?
Kama nilivyelezea hapo juu nia, falsafa na matokeo ya kuwepo kwa mbio za Mwenge wa Uhuru bado hazijabadilika. Changamoto ambazo zilikuwepo wakati wa Uhuru wa Tanganyika, bado zipo katika kipindi cha Tanzania ya karne ya 21, na inawezekana Tanzania ya vizazi vijavyo itakutana na changamoto zinazofanana na hizi lakini kadika mazingira na wakati wa vizazi vya wakati huo.
Kama Taifa misingi ya kuanzishwa kwa Taifa lazima iendelezwe, kwani wanaosema kuachana na misingi hiyo huwezi fahamu ajenda yao iliyojificha ni mimi. Taifa lisilo na misingi ya kuanzilishwa kwake ni dhaifu. Taifa linaloweza kutupilia mbali misingi ya kuanzilishwa kwake, linaweza kuwa katika hatari kubwa sana ya siku moja kutoweka, au kuingia katika virugu na matatizo ambayo ni vigumu kuweza kurudi katika hali ya awali. Bado tunaihitaji misingi ya Taifa letu. Bado tunaipenda misingi ya Taifa letu. Gharama ya mbio za Mwenge siyo hoja, maana misingi ya kuanzishwa kwa Taifa lazima ilindwe kwa gharama zozote zile. Ufisadi uliokuwa unaendana na kukimbiza mbio za Mwenge wa Uhuru ndiyo unaotakiwa kupigwa vita kwa juhudi zote. Mwenge kwa sababu unamulika na kuangaza palipo na ufisadi, udharimu, dharau, na chuki. Mbio za Mwenge wa Uhuru zitumike kutumbulia kila linapokuwa limemulikwa jipu, kwenye miradi ambayo imekuwa ni utamaduni kutumika kuizindua nchi nzima yaani mikoa 31 na Halimashauri 173.
Kumbukumbu ya kumletea Mtanzania mabadiliko ya kiuongozi na uundwaji wa mfumo wa utawala bora utakao ridhishwa kizazi hadi kizazi, ni jambo linalopaswa kuwa sehemu ya ujivuni wa kuwa na Mwenge wa Uhuru. Mwenge ni alama ya Uhuru wetu kuona mapungufu yetu. Mwenge ni alama ya kutuunganisha Watanzania na kupambana na uovu, udharimu, wizi, na ufisadi. Mwengi ni alama ya Uzalendo na kila Mtanzania nia akiuona anapaswa kuukumbuka wakati wa uhai wake wote, na kuwafundisha watoto na watoto wa watoto wake kuwa hiyo ndiyo ishara ya Uzalendo wa Mtanzania. Ndiyo ishara la tumaini la Mtanzania lilioanza tangu na kabla baada ya kupata Uhuru na lilikuwepo kabla ya kupata Uhuru. Wanaoupiga vita Mwenge wa Uhuru wamepoteza tumaini na wanataka Watanzania nia pia wapoteze tumaini pamoja nao. Ninachoamini mimi ni kuwa mtu aliyepoteza tumaini safari yake inapaswa kuishia kaburini. Tena kwa sisi tuliona tumaini la kizazi hiki na kutambua ukuu wa Mungu, tunaamini hata baada ya Kaburi tunatumaini kuwa siku moja tunauna uso wake. Sasa iweze sisi Watanzania tukubali mawazo haya finyu kuwa Mwenge ni Jipu, ninadhani kupoteza Tumaini ni Jipu, na dawa ya jipu ni kulitumbua na Mwenge unamwangaza kwa kutosha kumulika wakati wa Utumbuaji wa Jipu hilo.
Mnyela Jonathan N.


c79015a227b446e15f181d145a9ed4a7_XL
Katika kuadhimisha Miaka 53 ya Muungano wa Tanzania tarehe      26 Aprili, 2017 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-
  • Wafungwa wote ambao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu (1/3) linalotolewa chini ya Kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58, wawe wametumikia nusu (½) ya vifungo vyao vilivyobaki, isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2(i – xxi).
  • Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, Kifua kikuu (TB) na Saratani (Cancer) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa hawa wathibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.
  • Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi. Umri huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.
  • Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.
  • Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (Physical disability and mental disability). Ulemavu huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.
  1. Aidha, Msamaha huu wa Mheshimiwa Rais hautawahusu wafungwa wafuatao:-
  • Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa.
  • Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani.
  • Wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
  • Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya kama vile cocaine, heroin, bhangik.
  • Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na uombaji na upokeaji au utoaji rushwa.
  • Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya unyang’anyi na unyang’anyi wa kutumia silaha au kujaribu kutenda makosa hayo (robbery with violence, armed robbery and attempt robbery).

  • Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na silaha, risasi au milipuko isivyo halali (fire arms, ammunitions and explosives).
  • Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya shambulio la aibu, kunajisi, kubaka na kulawiti au kujaribu kutenda makosa hayo.
  • Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari na ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
  • Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi wa magari na pikipiki, uharibifu wa miundombinu au kujaribu kutenda makosa hayo.
  • Wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole (Act. No. 25/1994) na Sheria ya Huduma kwa Jamii (Act. No. 6/2002).
  • Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao.
  • Wafungwa waliowahi kupunguziwa kifungo na Msamaha wa Mhe. Rais na bado wangali wanaendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.
  • Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kupata masomo.
  • Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, kupoka na kufanya biashara ya binadamu (Human Trafficking).
  • Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu.
  • Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na nyara za Serikali na ujangili (poachers).
  • Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya wizi/ubadhirifu wa fedha za Serikali.
  • Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi halali.
  • Wafungwa walioingia gerezani baada ya tarehe 16/03/2017.
  • Wafungwa warejeaji wa makosa/wafungwa waliowahi kufungwa gerezani (Recidivists).
  1. Wafungwa 2,219 watafaidika na msamaha huu na wataachiliwa huru. Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.
Meja Jenerali  Projest Rwegasira
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
26/04/2017

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli akiwa katika Gari maalum na kuwapungia mkono Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakati wa sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri,[Picha na Ikulu.]26/04/2017
2
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania katika Uwanja wa Uhuru zilizofanyika leo,ambapo Mgeni rasmi akiwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli,[Picha na Ikulu.] 26/04/2017
3
Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ,pamoja na Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakiwa katika Uwanja wa Jamhuri,wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo,Mgeni rasmi akiwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli [Picha na Ikulu.] 26/04/2017
…………………………………………………………….
Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 April 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama lililoandaliwa kwa heshma yake, Rais Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa yeye na Rais wa Zanzibara Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.
”Muungano ndio silaha yetu. Ni nguvu yetu. Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda Muungano  kwa nguvu zote. Yeyote atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye” amesema Rais Magufuli.
Aidha Dkt. Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.
Rais Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuuunda taifa moja lenye nguvu.
Aidha amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe. Rais ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa uchumi na kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira,kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini,reli  na nchi kavu.
Aidha Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa demokrasia nchini.
Kwa mara ya kwanaza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Maadhimisho ya Sherehe za Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu ya Serikali ikiwa ni ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na chama cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha makao makuuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.
”Niwahahakikishie wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla  kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi tena, na  kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali yote itakuwa imehamia hapa” amesema Rais magufuli.
Sherehe za miaka 53 ya Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyere Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na viongozi wa chama na serikali.
Kauli mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni ”Miaka 53 ya muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii”
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
26 Aprili, 2017




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 April 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama lililoandaliwa kwa heshma yake, Rais Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa yeye na Rais wa Zanzibara Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.
''Muungano ndio silaha yetu. Ni nguvu yetu. Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda Muungano  kwa nguvu zote. Yeyote atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye'' amesema Rais Magufuli.
Aidha Dkt. Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.
Rais Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuuunda taifa moja lenye nguvu.
Aidha amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe. Rais ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa uchumi na kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira,kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini,reli  na nchi kavu.
Aidha Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa demokrasia nchini.
Kwa mara ya kwanaza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Maadhimisho ya Sherehe za Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu ya Serikali ikiwa ni ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na chama cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha makao makuuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.
''Niwahahakikishie wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla  kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi tena, na  kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali yote itakuwa imehamia hapa'' amesema Rais magufuli.
Sherehe za miaka 53 ya Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyere Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na viongozi wa chama na serikali.
Kauli mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni ''Miaka 53 ya muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii''

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
26 Aprili, 2017


-