Monday, October 23

 



Wako watu ambao uwepo wao katika ulimwengu wamechangia kwa namna moja au nyingine kuufanya huu ulimwengu uwe jinsi ulivyo. Wako wengine ambao wamechangia kwa kiwango kikubwa kuifanya 'mifumo' ya dunia iwe jinsi ilivyo. Mara nyingi watu hawa tunawasoma kwenye vitabu endapo kama waliishi miaka mingi iliyopita na endapo kama bado wako hai huwa ni watu tunao wahusudu na kuwachukulia kama mifano ya kuigwa.

Lakini wako watu ambao ni vigumu kuwahusudu au kuwaandika katika vitabu vya historia kutokana na jinsi ambavyo walichangia kubadilisha mifumo ya kimaisha dunia. Moja wapo ya watu hawa ni Wezi ambao mimi binafsi napenda kuwaita 'Wezi wa Daraja la kwanza' (First Class Thieves). Hawa wamekuwa toka enzi za kale na wamekuwa wanaushangaza ulimwengu kwa kiwango cha akili walichotumia na uthubutu walionao katika kutekeleza matukio.

Moja wapo kati ya wezi hawa ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha mifumo ya kiusalama ni mtu ambaye ameandika historia katika ulimwengu na hususani taifa la ufaransa kwa kutekeleza tukio kubwa zaidi la ujambazi na lenye thamani kubwa zaidi ambayo mpaka leo hii bado hajatokea mtu mwingine katika nchi ya ufaransa aliyefanikiwa kutekeleza tukio kubwa kama hilo na kwa mafanikio. Yeye binafsi hakuiba ili tu apate kutajirika pekee na kuishi maisha ya anasa bali pia aliiba kwa kuwa aliamini huo ndio wito wake (destiny) na aliiba ili kuudhihirishia ulimwengu kuwa anaweza. Jina lake aliitwa Albert Spaggiarri.




May 1976: Nice, Ufaransa


Alfred Spaggiari moja ya watu mashuhuri kwenye jiji la Nice nchini ufaransa na swahiba mkubwa wa Meya wa jiji la Nice Bw. Jacques Medécin, Spaggiari ambaye shughuli zake alikuwa amebobea kwenye upigaji picha za mitindo na matukio muhimu zaidi ya kiserika na binafsi alikuwa ameitisha kikao kilichohudhuriwa na watu wapatao ishirini katika nyumba yake ya mapumziko ya mwisho wa wiki iliyopo nje kidogo ya jiji la Nice. Kikao hicho hakikuhusu upigaji picha au siasa bali aliitisha kikao hicho cha siri na aliwaalika wahalifu kadhaa ili awashirikishe mpango wa siri aliokuwa nao. Kati ya watu hao 20 watu watano walikuwa ni wawakilishi wa ukoo wa Mafia wa usisili ( Sicilian Mafia) aliowaakika kutoka Italia.
Akiwa anafungua kikao hicho Spaggiari aliwaeleza kuwa amewaita hapo ili awashirikishe kwenye tukio la wizi la kihistoria na ambalo anaamini litakuwa na thamani kubwa sana kiasi kwamba hawataitaji kuiba tena maishani mwao ili kuishi maisha ya hali ya juu waliyoyapenda.

Spaggiari akawaeleza kuwa amedhamiria kuiba katika Kuba (vault) ya benki ya Société Générale. Ambayo ndiyo ilikuwa benki kubwa zaidi katika nchi ya ufaransa kwa kipindi hicho na moja ya benki kubwa zaidi duniani.
Lakini kabla hajaendelea zaidi na 'hotuba' yake watu kadhaa waliokuwepo kwenye kikao hicho waliangua kicheko cha dharau na kusema kwamba walidhani kuwa wameitwa kwenye kikao hicho labda 'celebrity' Spaggiari alikuwa ana ugomvi na 'celebrity' mwenzake kwahiyo alitaka awalipe wakamfanyie 'umafia' lakini kamwe hawakutegemea mtu 'mboga saba' kama Spaggiari ati atake kuwashirikisha wao kuhusu tukio la ujambazi kwani wanaamini kuwa Spagiari hajui chochote kuhusu uhalifu wala hajui hata "a e i o u" za matukio ya ujambazi.
Spaggiari aka kaa kimya kwa sekunde kadhaa huku macho yake yakiangaza kwa wahudhuriaji wote wa kikao hicho na macho yake yakakutana na mzee mmoja wa makamo aliyekuwepo pia kwenye kikao hicho ambaye walifahamiana vyema na Spaggiari. Spaggiari akampa ishara kuwa awaeleze watu hao waliohudhuria kikao hicho kuwa yeye ni nani, yeye Spaggiari halisi ni nani, awaeleze kiundani wamfahamu Spaggiari zaidi ya yule wanayemsoma kwenye magazeti, zaidi ya Spaggiari 'mboga saba' wanaye mjua.



UTAMBULISHO MFUPI WA "MPIGA PICHA" ALBERT SPAGGIARI

Albert Spaggiari alizaliwa Desemba 14, 1932 katika mji mdogo wa Hyerés ambapo mama yake alimiliki duka kubwa la mavazi ya ndani ya wanawake (lingerie).
Akiwa bado yuko katika shule ya upili, katika shule yao Spaggiari alitokea kumpenda msichana ambaye alikuwa ni mtoto wa Mkuu wa shule. Mara nyingi Spaggiari alijikuta anaingia kwenye matatizo na walimu kutokana na kumshushia kipigo kijana mmoja wa kisenegali ambaye alipata ufadhili wa kusoma shuleni hapo lakini naye alionyesha hisia za kumpenda binti huyo. Kutokana na Spaggiari kuingia kwenye matatizo mara kwa mara na walimu hakufanikiwa kumaliza shule kwani alifukuzwa baada ya walimu kuchoshwa na tabia zake.

Licha ya kutokuwepo shuleni Spaggiari aliendeleza uhusiano wake na yule mtoto wa Mkuu wa shule
Katika juhudi za Kutaka kumuonyesha huyo binti kwamba yeye sio hoe hae Spaggiari akamuahidi huyo binti kumnunulia pete ya almasi yenye thamani kubwa sana. Uhalisia ni kwamba Spaggiari hakuwa na hela lakini kutoka moyoni alipania kuitekeleza ahadi huyo ili azidi kumfanya mpenzi wake ampende zaidi.

Hivyo basi Spaggiari akamshawishi rafiki yake mmoja kuwa usiku wa siku moja ana mpango wa kuiba pete ya almasi katika duka mojawapo hapo mjini kwao.. Rafiki yake akakubali na wakapanga siku wakatekeleza tukio lakini kwa masikitiko makubwa wakakamatwa.
Baada ya kukamatwa na kushtakiwa mahakamani, Spagiarri alihukumiwa kwenda jela.
Lakini kutokana na umri wake mdogo wa miaka 17, serikaki na Spagiarri wakakubaliana kuwa akajiunge na jeshi badala ya kukaa jela.
Hivyo basi Spaggiarri akajiunga na jeshi kitengo cha wanajeshi wa kutumia parashuti.

Mwaka 1953 Spaggiari alishiriki katika vita ambayo majeshi ya Ufaransa yaliivamia koloni lao la Indochina (Vietnam ya sasa na maeneo yanayoizunguka). Spaggiari alikuwa ni mwanajeshi hodari na aliwahi kujeruhiwa mara mbili katika mapambano na kutokana na uhodari wake alitunukiwa nishani ya heshima.
Lakini ni kana kwamba wizi ulikuwa ndani ya vinasaba vya Spaggiari kwani akiwa huko huko Vietnam na kabla vita haijaisha yeye pamoja na rafiki yake walivamia duka moja mjini Hanoi na baada ya upelelezi walibainika.
Hii ilipelekea Spaggiari kufukuzwa jeshini na kurudishwa ufaransa na kufunguliwa mashtaka na akahukumiwa miaka mitano.

Spaggiarri akatumikia kifungo na mnamo mwaka 1957 akarudi uraiani.
Baada ya kurudi uraiani Spaggiari akajihusisha na kufanya kazi katika viwanda vya kutengeneza makabati ya kuhifadhi vitu vya siri (Safes) na pia akafanikiwa kupata msichana mrembo aliyeitwa Marcelle Audi ambaye kwa kipindi hicho alikuwa anafanya kazi kama Nesi na akafanikiwa kumuoa.
Baada ya kumuoa waliondoka ufaransa na kuelekea nchini Senegal ambapo kwa kipindi hicho bado lilikuwa ni koloni la Ufaransa na wakaishi mjini Dakar. Kwa bahati mbaya hawakufanikiwa kukaa sana Senegal kwani mwaka 1960 Senegal ilipata Uhuru na ikawalazimu warejee tena Ufaransa.

Baada ya kurejea Ufaransa Spaggiarri akaanza kujihusisha na vikundi vya uzalendo vya nchi za ulaya ambavyo vilikuwa vinapinga wazungu kuachia makoloni ya Africa.
Kikundi ambacho kilimvutia sana Spaggiarri kiliitwa OAS (Organisation de al'rmée Secrète). Kikundi hiki kilijihusisha na shughuli za kishushushu kusaidia kushawishi serikali ya ufaransa isiachie koloni la Algeria na pia kilifanya shughuli zake kudhoofisha harakati za watu wa Algeria kudai Uhuru. Spaggiari akajiunga na kikundi hiki mwaka 1961.
Rais wa ufarasa wa kipindi hicho (Rais De Gaulle) mwanzoni alikiunga mkono kikundi hiki lakini kadiri muda ulivyoenda na kuonekana wazi kuwa suala la kuipatia Uhuru Algeria haliepukiki, Rais De Gaulle akakipiga marufuku kikundi cha OAS na vikundi vingine vyote vyenye mlengo huo.

Baada ya harakati zao za OAS kupigwa marufuku Spaggiari akabakia na kinyongo kikubwa sana dhidi ya Rais De Gaulle. Hivyo basi mwaka huo huo wa 1961 akasafiri mpaka nchini Hispania kwenda kuonana na mmoja wa waanzilishi wa kikundi cha OAS mzee aliyeitwa Jenerali Pierre Lagaillarde. Sababu kubwa ya kumfuata ni kwamba Spaggiari alikuwa anahitaji apewe ruhusu ya kumdungua kwa risasi Rais De Gaulle ili kulipiza kisasi kwa "kuwasaliti" OAS na 'raia' wa Ufaransa kwa kuunga mkono Algeria kupewa Uhuru.
Jenerali Pierre akamwambia kuwa ampe 'ramani' yake jinsi alivyopanga ni namna gani atampiga risasi Rais De Gaulle.
Bila kusita Spaggiari akamueleza mpango wake, kuwa msafara wa Rais De Gaulle huwa unapita katika mji mdogo wa Hyerès na huwa wanapita mbele ya duka la mama yake Spaggiari (mama yake Spaggiari alikuwa ni mfanyabiashara wa mavazi ya ndani ya akina mama (langarie)). Hivyo Spaggiari akamueleza Jenerali Pierre kuwa atakaa juu ya paa la duka la mama yake na atakaa na bunduki ya wadunguaji na Msafara wa Rais ukupita atampiga risasi Rais De Guelle.

Jenerali Pierre akakubaliana naye kuwa arudi ufaransa na akatekeleze mpango huo lakini akampa onyo kuwa siku hiyo atayotakaa juu ya paa la duka la mama yake, asifyatue risasi kabla hajapata amri ya moja kwa moja kutoka kwake (direct command). Spaggiari akakubali na kurejea ufaransa.
Siku ya siku ikafika, Spaggiari akakaa juu ya paa la duka la mama yake, msafara wa Rais ukapita mbele ya duka, Spaggiari akasubiri 'direct command' kutoka kwa Jenereli Pierre ili amfyatulie risasi Rais De Guelle, akasubiri na kusubiri, amri haikuja na msafara wa Rais ulitokomea mbali na macho yake.
Wiki chache baadae Spaggiarri akakamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kujihusisha na vikundi vya 'kigaidi'. Spaggiarri akagundua kuwa Jenerali Pierre 'alimuuza'.
Mahakama ikamuhukumu kifungo cha miaka minne jela. Spaggiari akatumikia miaka yote.

Siku ya kutoka jela ni mke wake Audi pekee aliyemkuta nje ya geti la jela akimsubiri waende nyumbani. Spaggiari akamuapia mkewe kuwa hataki tena kujihusisha na harakati zozote wala siasa. Kuanzia sasa kitu pekee anachokitaka ni kuwa mume bora kwake.
Spaggiarri hakuwa anatania, akafungua ofisi yake ya upigaji picha katika jiji la Nice. Akafanya kazi kwa bidii usiku na mchana na ndani ya miaka michache akaibukia kuwa ndiye mpiga picha bora zaidi katika jiji la Nice, na harusi zote za hadhi ya juu ni Spaggiari ndiye alipiga picha, matukio yote muhimu ya kiserikali na binafsi, tenda ya kupiga picha alipewa Spaggiari. Punde si punde Spaggiari akawa moja ya watu mashuhuri zaidi katika jiji la Nice, na akafahamiana na kila mtu muhimu kwenye jiji la Nice. Mpiga picha Spaggiari akawa moja ya raia wanaoheshimika zaidi jijini Nice.
Lakini licha ya mafanikio na heshima yote, kana kwamba uhalifu umeandikwa kwenye vinasaba vyake, roho ya Spaggiari ilitaka zaidi! Sio pesa zaidi, sio umaarufu zaidi, hapana roho ya Spaggiari ilitamani kuiba! Kufanya tukio moja kubwa kuudhihirishia ulimwengu umahiri wake katika wizi.
Roho ya Spaggiari iliwasha kwa kiu ya kutaka kuiba, na alijua bayana roho yake haitotulia mpaka pale atakapo tekeleza walau tukio moja maridadi la wizi. Na ili kujiridhisha Spaggiari akaamua kuwa atafanya tukio la wizi ambalo litasimuliwa vizazi na vizazi.



Turejee kwenye Kikao cha "Mpiga Picha" Spaggiari na wenzake


Baada ya wote waliokuwepo kwenye kikao hicho kusikia historia hiyo ya Spaggiari walishikwa na bumbuwazi. Wote waliduwaa kwani baadhi yao waliwahi kusikia minong'oni mtaani kuwa mpiga picha Spaggiari ni 'mtundu mtundu' lakini hawakutegemea kama huo 'utundu' wake aliwahi kuhusika kwenye maisha ya hatari kama jinsi ambavyo wamesimuliwa kwenye kikao hicho.
Kwa ufupi kwa historia hiyo fupi, Spaggiari alivuna heshima kutoka kwa watu wote ambao walikuwa wamehudhuria kikao hicho lakini swali moja likabaki hewani, je mpango wake ni upi juu ya utekelezaji wa kuiba benki hiyo ya Société Générale, naye Spaggiari akawajibu kuwa hicho ndicho alichowaitia hapo kuwa wakae chini wote watoke na mpango kabambe wa kuiba katika benki hiyo na yeye yuko tayari kusikia mawazo yao kwanza.

Baadhi ya waliokuwepo kwenye kikao kile hasa wale wanachama watano kutoka ukoo wa Mafia wa usisili, wakatoa maoni yao. Wakasema kuwa kama anaweza kuwapa uhakika kuwa katika tarehe fulani mahususi benki hiyo itakuwa na kiwango kikubwa cha fedha basi wao wanaweza wakasaidia wapate silaha na kuweka mpango madhubuti wa kuivamia hiyo bank na kupora hela. Baada ya wanachama hao wa Mafia kutoa maoni hayo Spaggiari akawapa jibu la kuwashangaza sana, kuwa hakubaliani na mkakati huo kwasababu anataka kwamba tukio hilo watakalotekeleza anataka waweke mpango wa kutumia akili zaidi badala ya kutumia mabavu na silaha.

Baada ya maoni hayo kukataliwa wengine nao wakatoa maoni kwamba labda wamteke mtoto au mke wa meneja wa benki kisha watumie kigezo hicho kumshawishi meneja awasaidie kuiba katika benki yake. Wazo hili nalo lilipingwa na Spaggiari na akawaeleza kuwa hataki ukatili wowote utumike katika kutekeleza tukio hili. Mzee mmoja veterani wa kikundi cha OAS ambaye alikuwepo yeye akasema kuwa anatamani afahamu siku ambayo benki yoyote kubwa inakuwa na kiwango kikubwa cha fedha kisha wailipue ili kuikomesha serikali kwa 'kusaliti' kikundi chao cha OAS. Spaggiari akamjibu kwa kifupi tu kuwa kama akitaka afanye tukio lolote kwa ufanisi anatakiwa aweke hisia za chuki pembeni. Hivyo wazo lake hilo la kulipua benki kwa kisasi alikuwa analipinga.

Wale jamaa watano wanachama wa ukoo wa kihalifu wa Mafia, ambao walisafiri kutoka Itali kuja kuhudhuria kikao hicho wakainuka wote kwa pamoja na kumwambia Spaggiari kuwa wanaondoka. Wanahisi kuwa licha ya kuwa ni kweli kama walivyosikia kwenye kikao hicho kuwa amewahi kushiriki katika mipango ya hatari katika maisha yake lakini wanahisi kuwa kwasasa Spaggiari ana ndoto za mchana na hayuko kwenye uhalisia kwasababu kama anakataa maoni yote yaliyotolewa hawaoni uwezekano wowote wa kikao hicho kuzaa mkakati wenye uhalisia wa kutekeleza tukio la ujambazi.
Spaggiari akawasisitiza kuwa wakae chini wasikilize maoni mengine yakiwemo maoni yake lakini wanachama hao wa Mafia wakamwambaia kuwa hawako tayari kuendelea na kikao hicho kwani wanadhani mkakati wowote utakaowekwa hapo utakuwa ni kana kwamba wanaenda kujitoa sadaka kwani haiingii akilini watu muwe na dhamira ya kuiba benki alafu msitumie silaha. Mafia hao wakainuka, wakaaga na kuondoka.

Kwahiyo Spaggiari akabakia na watu 15 pekee kwenye kikao hicho wengi wao wakiwa ni wanachama wa zamani wa kikundi cha OAS. Na alivyowaangalia nyuso zao aligundua dhahiri kuwa ndani ya dakika chache kama hatowapa mpango wowote wa kuwashawishi kuhusu hilo tukio nao wangeweza kuinuka na kuondoka.
Spaggiari akaenda mpaka kwenye kabati la pembeni lililopo kwenye sebule hiyo na kutoka na boksi dogo la saizi ya kati na kulibeba kwa mikono miwili mpaka kwenye meza iliyokuwepo katikati ya sebule na kisha akawaomba wote wainuke na kusogea karibu na meza.
Baada ya wote kusogea karibu na meza Spaggiari akatoa makaratasi kadhaa kutoka kwenye lile box na kayatandaza juu ya meza.

Makaratasi yale yalionyesha ramani na mpango mji wa jiji la Nice. Kuna makaratasi yalionyesha nyumba kwa nyumba na jengo kwa jengo kwa jiji lote la Nice. Makaratasi mengine yalionyesha juu ya mifumo ya barabara ya jiji zima. Makaratasi mengine yalionyesha juu ya mfumo ya maji taka ya jiji zima na hapa katika karatasi hizi za mifumo ya maji taka ndipo hasa Spaggiari aliwataka awaeleze kuhusu mpango wake anao ufikiria. Katika karatasi hiyo inayoonyesha mfumo wa maji taka, Spaggiari akawaonyesha mahali ambapo benki ilipo na akaweka alama kwenye karatasi kisha akawaonyesha mfereji wa maji taka wa chini kwa chini ( Sewer) ambao unapita karibu kabisa na benki hiyo na pia akaweka alama kwenye mfereji huo kisha akawafafanulia zaidi. Akawaeleza kuwa upande ambapo mfereji huo unapita na kupakana na benki ni takribani mita 5 tu kutoka kwenye mfereji mpaka kwenye Kuba (Vault) ya benki. Hivyo basi kama wataweza kuchimba shimo la chini kwa chini (tunnel) lenye urefu wa mita 8 kutoka kwenye mtaro huo wa maji taka kuelekea upande wa benki basi watakuwa wamefika katikati ya sakafu ya vault ya benki ya Société Générale na kitu pekee kitakachobaki ni kutoboa tundu dogo kwa kwenda juu na watakalolitumia kuingilia ndani ya vault kutoka kwenye tunnel walilochimba kutoka mtaroni. Huo ndio ulikuwa mkakati wake.
Spaggiari aliwaangalia nyuso za wale waliokuwepo kwenye hicho kikao na alikuwa na uhakika kuwa wamevutiwa na mkakati huo ingawa walikuwa na maswali kadhaa.

Spaggiari akatoa fursa waulize maswali na swali la kwanza lililokuwepo kwenye vichwa vya wengi lilikuwa je, watakapokuwa chini wanachimba hilo shimo (tunnel) hawatashtukiwa kutokana na makelele na mitetemo watakayo sababisha. Spaggiari akawajibu kuwa japokuwa tunnel la urefu wa mita 8 wanaume kama wao 15 wana uwezo wa kulichimba ndani ya siku hata 3 lakini ili kuzuia kusababisha kelele na mitetemo amepanga kuwa shimo hilo litachimbwa taratibu kana kwamba wanakula chakula kwenye sahani kwa kutumia kijiko. Haijalishi itachukua wiki au miezi mingapi.

Swali lingine lilikuwa je itakuwaje kama vault ina 'sensors' za kuhisi mitetemo au sauti? Spaggiari akawajibu kuwa kuhusu hilo wampe kama siku tatu atafahamu hiyo vault ina 'sensors' zipi na ni namna gani watakavyo jiahami nazo.

Spaggiari akauliza kama kuna swali lingine. Hakukuwa na swali. Kisha akawaukiza, "who is in?" ("Nani atashiriki nami kwenye hili?") wote 15 waliobakia kwenye kikao hicho walikubali kushiriki katika tukio hilo.
Spaggiari akawaeleza kuwa anawapa wiki moja kila mtu akamalize ratiba zake alizokuwa nazo, mwenye familia akaage na kudanganya anavyoweza kwani wakikutana baada ya hiyo wiki moja watakuwa na wiki kadhaa au pengine miezi kadhaa ya kutekeleza tukio hilo ambalo halijawahi kufanyika kabla.
Wakaagana, wakatawanyika.



SPAGGIARI NA GENGE LAKE WANAINGIA 'KAZINI'



Wakati wenzake wakiwa wamerudi makwao kuaga familia zao ili warejee baada ya wiki moja kwa ajili ya 'kazi', yeye Spaggiari kesho yake alifika mpaka kwenye benki ya Société Générale na akaomba kuwa mteja afunguliwe sanduki jipya kwa ajili ya kuhifadhi vitu vyake vya faragha/siri ( safe deposit box) katika vault. Baada ya kukamilisha taratibu zote za kujaza nyaraka za maandishi na kulipia gharama za huduma hiyo hatimaye akapelekwa na muhudumu wa benki mpaka kwenye vault na kuonyeshwa kisanduku ambacho kitakuwa chake. Kisha muhudumu akatoka nje ya mlango ili kumpa faragha Spaggiari ahifadhi vitu vyake. Baada ya kuachwa peke yake Spaggiari akatoa saa kubwa ya muito (alarm clock) ambayo ilikuwa kwenye kibegi kidogo alichokuja nacho. Saa hii ilikuwa na ukubwa wa kufanana kabisa na saa kubwa ya ukutani. Lakini ilikuwa nzito zaidi. Na ilitengenezwa kuwa saa ya muito ambayo muda uliotegeshwa ukifika Saa inaita na kutetema (vibration). Spaggiari akaitegesha saa hiyo iwe inaita usiku wa manane. Kisha akaiweka kwenye kisanduku chake alichoonyeshwa. Kisha akakifunga kisanduku, akatoka nje akakabidhi funguo ya kisanduku kwa muhudumu na kurudi nyumbani.

Baada ya wiki moja kupita na wenzake kurudi kwa ajili yakuanza kazi, kwanza kabisa Spaggiari akawapa muhtasari juu ya alichofanikisha mpaka mda huo. Akawaeleza kuwa hawahitaji kuhofu kuhusu 'sensor' za mitetemo au sauti kwakuwa ameng'amua kuwa vault hiyo haina 'sensor' zozote zile. Walipo muuliza amejuaje, akawaeleza kuhusu Saa ya muito aliyoiweka kwenye hiyo vault na kuitegesha iwe inaita muda wa usiku. Na akawaeleza kuwa kwa siku kadhaa amekuwa akichunguza na hajaona taharuki yoyote kutoka kwa walinzi au alarm za ulinzi za benki zikilia hivyo ana uhakika kabisa hakuna 'sensors' zozote kwenye hiyo vault.

Spaggiari alikuwa sahihi kabisa kwani vault hiyo ni kweli haikuwa na sensor zozote, wenyewe wenye benki waliamini kuwa vault hiyo ilikuwa haiingiliki kwa namna yoyote (utterly impregnable) kwasababu mlango wake wa chuma ulikuwa mnene zaidi ya kuta tatu za nyumba ya tofali zikiunganishwa pamoja na mtu alihitajika kuingiza namba maalumu (combination) na kutumia funguo kubwa mbili maalumu ili aweze kuufungua. Pia kuta za hiyo vault zilikuwa haiwezekani hata mtu kuzigusa akiwa nje kwani vault ilikuwa kati kati ya jengo la benki na kuta zake zilikuwa nene kiasi kwamba zinazidi hata unene wa kuta tatu za nyumba ya kawaida.

Baada ya Spaggiari kuwapa wenzake muhtasari huo, kawaeleza kuwa hivyo basi saa hiyo ya muito watakuwa wanaitumia kama muongozo wa ziada ili wawe wanachimba kwa usahihi zaidi kuekekea chini ya sakafu ya vault (pinpointing). Baada ya kupeana muhtasari, Spaggiari akaondoka na wenzake ili akawaonyeshe eneo la kazi.

Walitumia boti ndogo kusafiri katika mto Rivera mpaka mahali ambapo kiwango kidogo cha maji ya mto yanachepuka na kuingia katika mtaro mkubwa wa maji taka unaokusanya maji na kupita karibu na benki waliyotaka kuiba. Walipofika hapa walitumia maboya kuelea juu ya maji machafu ya mtaro yaliyojaa kinyesi cha binadamu na uchafu mwingine, walielea kuelekea mbele kwa takribani dakika ishirini wakiwa na ramani zao mikononi mpaka walipofika sehemu waliyoihitaji.

Baada ya kufika hapo Spaggiari akawapa maelekezo kuwa wanatakiwa wachimbe moja kwa moja bila kupindisha hata kidogo kwenda mita 8 ndani na kama watakuwa sahihi baada ya kufikisha mita 8 hizo alarm aliyoiweka kwenye vault ikilia basi wataisikia juu ya vichwa vyao, ikimaanisha kwamba wako chini ya sakafu ya vault.
Pia Spaggiari akawagawanya wenzake kwenye shift za kufanya kazi. Akawaambia kuwa kutakuwa na makundi mawili, kila kundi litafanya kazi kwa masaa kumi wakati huo wengine watakuwa wamelala na akawasisitiza kuwa ni lazima walale kwa masaa kumi. Kwahiyo shifti zilikuwa mbili, masaa kumi kazini na masaa kumi kulala. Pia akawakataza wasiguse kabisa pombe au kahawa kwa muda wote ambao watakuwa wanafanya hiyo kazi.

Siku iliyofuata kazi ilianza. Kazi ilifanyika bila papara, taratibu na kwa umakini mkubwa. Kazi ikaendelea kwa siku kadhaa, wiki kadhaa na baada ya miezi miwili hatimae walifikisha tanuru (tunnel) la urefu wa mita 8. Baada ya kufikisha umbali huo Spaggiari akawaambia wasubiri usiku wa manane kusikiliza saa ya muito ili wajue kama wako sahihi au la. Ilipofika usiku wa manane alarm ya saa iliyowekwa kwenye vault na Spaggiari iliita, na waliisikia juu ya vichwa vyao kabisa. Wakapongezana kwani sasa walikuwa na uhakika asilimia mia moja kuwa wako sahihi, walikuwa wako chini ya sakafu ya vault na kilichobakia ilikuwa ni kutoboa hiyo sakafu na kuchukua 'mwali wao'.
Spaggiari akawaambia wenzake kuwa inabidi wapumzike kwa siku mbili kuisubiria Bestille Day ndipo watoboe sakafu na kuchukua mwali wao.

Bastille Day (siku ya Uhuru wa Ufaransa) ambayo husheherekewa kila mwaka tarehe 14 July na kwa mwaka huu 1976 ilikuwa inaangukia siku ya alhamisi, hivyo hii ilifanya kuwe na siku nne za mapumziko (alhamisi na ijumaa (sherehe za Bastille Day) Jumamosi na jumapili (mapumziko ya mwisho wa juma)). Kwahiyo Spaggiari alitaka wapate muda wa kutosha kwa siku nne ili wachukue fedha na vitu vingi kadiri wawezavyo.

Hatimaye alhamisi ikawadia na Spaggiari na genge lake wakamalizia kutoboa sakafu ya vault na kuingia ndani. Jambo la kwanza walilolifanya baada kufanikiwa kuingia ndani ya vault ni kuchomelea mlango wa vault kwa ndani ili mtu aliyepo nje asiweze kuufungua.
Kazi ikaanza na Spaggiari kwa kutumia uzoefu aliokuwa nao wa kufanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza 'safes' akawaongoza wenzake katika zoezi la kufungua visanduku. Kazi ilifanyika mchana na usiku kwa siku ya kwanza ya alhamisi na kesho yake siku ya Ijumaa Spaggiari akawaambia wenzake wapumzike kwa masaa machache ili nao washerehekee sikukuu ya Bastille kama wenzao walioko huko mitaani. Hivyo basi Spaggiari akatoka kwenye vault na kurudi mtaani kununua mvinyo pamoja na vyakula vya anasa na kurudi navyo kwenye vault kwa ajili ya kusheherekea. Baada ya kumaliza kula na kunywa kazi iliendelea usiku na mchana siku hiyo ya ijumaa, jumamosi na ilipofika jumapili mchana walikuwa wamefanikiwa kufungua yapata visanduku 400 vilivyokuwa na fedha taslimu, vito vya thamani, hati fungani na vitu vinginevyo vya thamani kubwa. Inakadiriwa kuwa thamani ya 'mzigo' wote ambao Spaggiari na genge lake walipata unafikia Faranga Milioni 60 za ufaransa (60 million French Frans).

Ilipofika muda wa mchana siku ya Jumapili mvua ilianza kunyesha na Spaggiari akahisi mitaro waliyotumia kuingilia inaweza kujaa maji na hivyo kufanya zoezi la kutoka kuwa gumu hivyo basi akawaamuru wenzake waondoke kabla mvua haijawa kubwa. Lakini kabla hawaondoka aliwaambia wenzake kuwa anahitaji kufanya jambo moja la muhimu la mwisho. Huku akionekana akiwa na hisia na msisimko wa hali ya juu, spaggiari alichukua kopo la rangi alilokuwa amekuja nalo pamoja na brashi ndogo ya kapakia rangi, kisha akausogelea ukuta mmoja ndani ya vault na kuandika maandishi makubwa yaliyo someka; "SANS ARMES, NI HAINE, NI VIOLENCE" ("Without weapons, nor hatred, nor violence" ("Pasipo silaha, wala chuki, wala ukatili")).
Hiyo ndio 'falsafa' aliyotaka kuifikisha kwa ulimwengu mzima kujitambulisha yeye ni 'mwizi daraja la kwanza' wa dizaini gani.
Baada ya hapo wakafungasha mizigo yao, wakatokomea.


'Maisha' Baada ya Tukio..

Siku ya jumatatu benki ya Société Générale ilifunguliwa na shughuli ziliendelea kama kawaida pasipo yeyote kung'amua kuwa kuna jambo lilitokea ndani ya vault. Na kama ilivyo ada ilipofika majira saa Tatu na nusu asubuhi wafanyakazi wawili walielekea kwenye chumba cha Vault kukifungua ili kuruhusu wateja kuhifadhi vitu na wengine kuchukua vitu walivyohifadhi. Walipofika mlangoni wakaingiza namba maalumu na kisha kama ilivyo utaratibu wakaingiza funguo mbili katika matundu mawili juu ya mlango na kuzungusha funguo lakini jambo la ajabu mlango haukufunguka. Walihangaika kuzungusha funguo karibia nusu saa lakini mlango haukufunguka.

Baada ya juhudi zote hizo bila mafanikio wakaamua watoe taarifa kwa meneja msaidizi wa benki aliyeitwa Pierre Bigou. Bw. Pierre baada na yeye kuhakikisha kuwa mlango ulikuwa haufunguki ikabidi aagize aitwe muhunzi ili aje kuwasaidia. Dakika chache baadae muhunzi alifika na akaanza kuukagua mlango, na ndani ya dakika kumi na tano akawa ameng'amua kuwa mlango umechomelewa kwa ndani na hakuna namna ambayo wanaweza kuufungua wakiwa nje.

Sehemu ya mapokezi baadhi ya wateja walikuja kwa ajili ya kutumia visanduku vyao vya kwenye vault walianza kupaniki na ilimbidi meneja mwenyewe wa benki ahusike kuwatuliza na kuwaondoa wasiwasi. Meneja alitumia maarifa yake yote ya huduma kwa wateja kuwaondoa hofu wateja wake na kuwataka wawe watulivu, " Nothing to worry about monsieur. A minor technical problem madame. Your valuables are quite safe but there may be a slight delay" ("ondoa hofu muheshimiwa. Ni tatizo dogo tu la kiufundi. Vitu vyenu viko salama ila itachukua muda kidogo kurekebisha.") Meneja wa benki Bw. Jacques Guenet alisikika akiwatuliza wateja wake.

Baada ya muhunzi kugundua kuwa mlango huo hautaweza kufunguka kwa nje akapendekeza kuwa watoboe ukuta ili kuingia ndani. Viongozi wa benki wakakubali na kazi kutoboa ukuta ikaanza. Kutokana na unene wa ukuta na kutoboa kwa makini ili wasisababishe hasara nyingine, ilichukua takribani masaa matatu kutoboa tundu kubwa kiasi la kumuwezesha mtu kupita. Yule muhunzi ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuchungulia ndani na alipochungulia alipatwa na mshangao kana kwamba amepoteza fahamu kwa sekunde kadhaa. Hakuamini alichokuwa anakiona ndani ya vault. Huku bado akiwa na mshangao alimgeukia Meneja wa Benki aliyekuwa amesimama nyuma yake na kumwambia kwa mshangao, "Merde de putain" ("you have been robbed" ("Mmeibiwa")).

Baada ya wote bumbuwazi kuwaisha kutokana na kutoamini macho yao walichokuwa wanakiona mbele ya macho yao, hatimae wakapiga simu polisi na haraka sana polisi wakawasili. Baada ya Polisi kuwasili na kuingia ndani ya vault nao pia hawakuamini kile walichokuwa wanakiona mbele ya macho yao. Wote kwa pamoja macho yao yaliganda kwenye Ujumbe ulioandikwa kwenye ukuta, "sans armes, ni haine, ni violence" (Pasipo silaha, chuki wala ukatili).



KUKAMATWA, KUSHTAKIWA NA KUWA 'HURU' TENA

Ndani ya miezi miwili polisi walifanikiwa kugundua kuwa Spaggiari ndiye muhusika mkuu wa tukio lile. Haijulikana hasa ni namna gani polisi walifanikiwa kugundua kuwa Spaggiari ndiye alikuwa 'mastermind' wa tukio lile, kwani kumekuwa na maelezo mengi sana yanayokinzana lakini angalau ufafanuzi unaoonyesha uhalisia kidogo ni kwamba mmoja wapo wa watu walioshiriki tukio lile alipopewa mgao wake wa fedha pia alipewa na miche kadhaa ya dhahabu (gold bars) na bila kutumia akili au kuwa na subira akauza mche mmoja ndani ya wiki chache baada ya tukio. Baada ya siku kadhaa mtu aliyeununua mche huo aliripoti polisi kuwa ameuziwa mche wa dhahabu unaofanana kabisa na moja ya miche inayoripotiwa kuwa imeibiwa kwenye vault ya benki ya Société Générale.
Polisi wakamfatilia huyo mtu na wakafanikiwa kumtia nguvuni na baada ya kumuhoji kwa siku kadhaa akawataja wenzake wote akiwemo Albert Spaggiari.

Polisi waliposikia kuwa Spaggiari ndiye alikuwa kiongozi wa tukio hilo, walishikwa na butwaa kwani Spaggiari alikuwa ni moja ya watu mashuhuri na anayeheshimika zaidi jijini Nice. Na kipindi wanapata taarifa hii alikuwa yuko safarini mashariki ya mbali akiwa amemsindikiza rafiki yake Meya wa jiji Bw. Jacques Médecin, katika ziara ya kiserikali.

Siku ambayo Meya na Spaggiari wanarejea Nice kutoka mashariki ya mbali, Spaggiari alikamatwa hapo hapo uwanja wa ndege na kufunguliwa mashtaka ya kuhusika kupanga na kushiriki tukio la ujambazi katika benki ya Société Générale.

Kesi hii ilitikisa vyombo vya habati ulimwengu mzima na umaarufu wa Spaggiari ukaongezeka maradufu na mwenyewe alionekana kufurahia haswa jinsi alivyokuwa anazungumziwa kila kona ya Dunia.

Wakati kesi ikiwa inaendelea Spaggiari akatunga hadithi ambayo kwa bahati mbaya Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo aliiamini na akawa anatamani kujua kiundani. Spaggiari aliwaeleza kuwa alifanya tukio hilo ili kukiwezesha kiuchumi kikundi cha siri cha wazalendo kilichoitwa 'Catena' (neno la kifaransa linalomaanisha 'Chain' (mnyororo)).

Spaggiari akawaeleza kuwa hayuko tayari kuwapa taarifa za kikundi hicho Polisi kwani hawaamini bali yuko tayari kutoa taarifa kwa Jaji huyo peke yake. Hivyo basi ikawekwa ratiba maalumu ambayo Spaggiari alikuwa anapelekwa ofisini kwa Jaji na kila walipokutana alikuwa anampa kikaratasi alichokiandika kwa mafumbo (coded message) na ilikuwa inamlazimu Jaji akune kichwa haswa ili kung'amua kilichoandikwa na Spaggiari kuhusu siri za hicho kikundi cha 'Catena'.

Katika moja ya vikao vyao na Jaji, Jaji akiwa 'bize' kung'amua Ujumbe huo wa mafumbo Spaggiari aliinuka kutoka kwenye kiti kana kwamba anataka kumkaribia Jaji ili ampe ufafanuzi. Lakini jambo la ajabu alikimbia kwa spidi ya ajabu mpaka dirishani na kujirusha nje kwa uhodari wa hali ya juu (kumbuka aliwahi kuwa mwanajeshi kitengo cha Parashuti). Ofisi ya Jaji ilikuwa juu ghorofa ya Tatu katika hilo Jengo la mahakama, lakini kutokana na Spaggiari kujirusha kwa uhodari alitua chini juu ya paa la gari bila kudhurika. Kisha akakimbia kuvuka barabara na kulikuwa na piki piki inamsubiri.

Baada ya kukwea juu pikipiki akageuka kuwaangalia juu dirishani maaskari pamoja na Jaji waliokuwa wanachungulia wakiwa hawaamini kilichotokea ndani ya sekunde chache. Spaggiari akapayuka kwa nguvu "Au revoir" (kwaherini). Kisha akatabasamu kwa dharau na inasemekana akawaonesha kidole cha kati. Kisha kwa mwendo wa kasi na uhodari pikipiki ikapotea mbele ya upeo wa macho yao. Hiyo ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa mamlaka za serikali za ufaransa kumuona Spaggiari.

Wiki mbili baadae mtu mwenye gari ambalo Spaggiari alitua alipo ruka kutoka ghorofani alipokea cheki ya thamani ya faranga 5,000 pamoja na kikaratasi kikisema ni kwaajili ya matengenezo ya paa la gari lake.
Pia kuna tetesi ambazo zimeenea mno toka kipindi hicho mpaka sasa kuwa mtu aliyempakia Spaggiari kwenye pikipiki na kumtorosha alikuwa Christian Estrosi bingwa wa Dunia wa mbio za pikipiki ambaye baadae alikuja kuwa waziri katika serikali ya Ufaransa.

Baada ya kutoroka Spaggiari alielekea nchini Argentina na kuishi huko na kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha muonekano (plastic surgery). Inasemekana Spaggiari alikuwa anarudi mara kwa mara nchini Ufaransa kumuona mkewe Audi na Mama yake.

Akiwa nchini Argentia inasemekana kuwa alikuwa karibu sana na CIA akiwasaidia kufanikisha shughuli ambazo CIA hawakutaka kujihusisha nazo moja kwa moja kwa kuhofia jina la idara yao kuchafuka ikitokea siri kuvuja.
Mfano mzuri ni jinsi ambavyo Spaggiari (au daniel jina walilotumia CIA kumtambua (code name)) alishirikiana na Michael Townley afisa wa DINA (kitengo cha ushushushu cha nchi ya Chile) kuchora mchoro na kulipua gari la balozi wa Chile nchini Marekani.

Skandali hii ilichangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha mahusiano ya kidiplomasia kati ya marekani na Chile na hakuna aliyejua uhusika wa CIA mpaka pale mwaka 2000 ambapo CIA waliweka hadharani nyaraka kadhaa za siri baada mda wake wa usiri kupita.

Albert Spaggiari alifariki June 8, 1989 kwa kansa ya koo kutokana na matumizi ya sigara.
Fedha, Vito vya thamani, hati fungani na nyaraka nyingine za siri zilizoibwa na Albert Spagiari na Genge lake havijapatika mpaka leo hii. Tukio hili limebakia katika vichwa vya Wafaransa kama tukio kubwa pekee la wizi wa vitu vya thamani ya juu zaidi na lililotekelezwa kwa umaridadi na akili nyingi au kama Spaggiari mwenyewe alivyolielezea; "Sans armes, ni haine, ni violence" (Pasipo silaha, chuki wala ukatili").



KIDON ni kitengo ndani ya Mossad chenye jukumu la kufanya mauaji dhidi ya wale wenye kuhatarisha usalama wa Israel. KIDON ndio wanaosifika na kuogopwa zaidi duniani katika kufanya assasinations kwa ufanisi na ufasaha wa hali juu


Neno Kidon ni la kiyunani lenye maana ya ncha ya upanga, hili lina akisi jinsi kitengo hiko kilivyo mahiri na hatari katika kufanya mauaji.



Kidon ilianzishwa miaka ya 70 kutoka katika kitengo cha Caesaren kilichokuwa chini ya Mossad kufuatia kuuawa kwa waisrael 11 waliokuwa washiriki katika mashindano ya Olympic mjini Munich Ujerumani mwaka 1972. Mauaji hayo yalifanywa na wapiganaji wa kipalestina, japo waisrael wengi walikufa wakati polisi wa Ujerumani walivyojaribu kuwaokoa mateka. Na mara moja baada ya kuundwa wakapewa kazi ya kuua kila aliyehusikia na mauaji hayo ya waisreal kazi iliyofanyika kwa mafanikio makubwa japokuwa kuna wahanga nao walikufa

Mbali ya kuwa kitengo hiki kuwa chini ya Mossad lakini kutokana na usiri wake mkubwa hakina ofisi ndani ya makao makuu ya Mossad mjini Tel Aviv. hata ma-agent wake ni vigumu kutia mguu makao makuu, hii ni kwa mujibu wa afisa wa zamani wa intelijensia katika kitengo cha Mossad kinachoratibu shughuli za Kidon bwana Mishka Ben-David katika kitabu chake "Duet in Beirut". Anaendelea kusema kuwa hata majina wanayotumia ni majina ya kufikirika na si majina rasmi, na wakiwa shughulini hutumia jina la 3 la mhusika na mara nyingine hadi utambulisho wa 4 na wa 5. kutoka na usiri na ufanisi wa hali ya juu, kitengo hiki kimepachikwa jina la Mossad ndani ya Mossad

Recruitment katika kitengo hichi ni kutoka katika special forces wenye vipaji vya hali ya juu ndani ya
Israel Defence Force (IDF) na hupatiwa mafunzo ya hatari kwa mda wa miaka 2. hawa jamaa wanasifika kwa kutoacha alama yeyote katika assasinations zao na wamekuwa wakifanikiwa kwa miaka mingi

Wauaji hutumia pasi na nyaraka feki za mataifa mbalimbali za kusafiria zilizofojiwa kwa ustadi wa hali ya juu na wataalamu wao au hutumia pasi halisi za mataifa mbalimbali ambazo picha hubadilishwa kiutaalamu ili kufanana na mhusika. Pia wanauwezo mkubwa sana wa kujipenyeza na kuingia nchi yeyote na kufanikisha mauaji.

Katika mauaji wanayoyafanya pale mashariki ya kati, mtindo maarufu ni ule ya wauaji wakishambulia huku wakiwa wanatumia usafiri wa pikipiki. Mtindo huu ndio umetumika kuwaua maprofesa na wanasayansi wa nyuklia wanne wa Irani mpaka sasa. Katika mtindo huu, kawaida timu ya wauaji inakuwa na watu wanne

1.TRACER-huyu anamfatilia mlengwa anayetakiwa kuuawa

2.TRANSPOTER-huyu anaiongoza timu ya wauaji kwa mlengwa huyo anayetakiwa kuuawa

3.HELPER-huyu anaendesha pikipiki, anakuwa amembeba muuaji

4.KILLER-huyu ndio muuaji hasa, anafyatua risasi au kurusha magetic bomb kwa target(hili bomu linaweza kumuua mlengwa tu huku wengine wakijeruhiwa)

Unaambiwa huyu shooter anauwezo wa shoot accurately katika speed yeyote bila kupepesuka hata kidogo yani hakuna hata kutingishika akilenga mwendo kasi wowote ule bila kukosa au kurusha bomu likanasa katika sehemu ya gari anayotaka linase sehemu ambapo mara nyingi huwa ni upande wa gari aliokaa mlengwa na kitendo hiki huwa cha haraka sana kiasi wahusika huwa ngumu kutambua kama kuna kitu kimewekwa au kurushwa kwenye gari. Mtindo huu ndio 'Trade Mark' ya mauaji ya KIDON

haya ni machache katika yale machache,mengi kuhusu kitengo hiki. Kwa machache zaidi vitabu hivi ni vizuri; GIDEON'S SPIES: The inside story of Israel legendary secret service by Gordon Thomas na SPIES AGAINST ARMEGEDDON: Inside Israel's secret wars by Dan Raviv and Yossi Melman .
Vitabu viko hapo chini nime attach


Wednesday, October 18




PABLO NI NANI?
Katika milima inayotazamana na mji wa Medellín nchini Colombia, yapo majengo ya kifahari kabisa ndani ya milima hiyo ambayo kwa sasa majengo haya yanatumika kama nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki lakini kabla ya watawa hawa kupewa majengo haya mwaka 2007, majengo haya yalikuwa ni gereza ambalo lilijengwa mwaka 1991 kumuhifadhi mfungwa maalumu raia wa Colombia.
Gereza hili lilikuwa ni tofauti kabisa na magereza yote ambayo umewahi kuyasikia kwani gereza hili licha ya kuwa mali ya serikali lakini michoro yake ilichorwa na kubuniwa na mfungwa mwenyewe.
Si hivyo tu, bali hata maaskari magereza ambao walikuwa wanalinda gereza hili walichaguliwa na mfungwa mwenyewe na hata polisi wa nchi ya Colombia walikuwa hawaruhusiwi kusogolea gereza hilo hata umbali wa maili 12. Kama hiyo haitoshi gereza hili lilikuwa na uwanja wa mpira wa miguu, lilikuwa na bafu lenye Jaccuzi, lilikuwa na bar, lilikuwa na maporomoko ya maji (water falls) yaliyobuniwa kiustadi, na pia chumba (selo) alicholala mfungwa huyu kilikuwa na kitanda kikubwa cha duara chenye kuzunguka pamoja na televisheni kubwa.
Kama hii haitoshi kwenye gereza hilo pia kulikuwa na chumba maalumu cha michezo ya watoto maalumu kwa ajili ya watoto wa mfungwa huyo pindi akitembelewa na familia yake. Na pia ndani ya gereza kuliwekwa darubini kali (Telescope) ya kumuwezesha mfungwa huyo kuangalia katika mji wa Medellín ambako familia ya mfungwa huyu iliishi na kila siku jioni walitoka nje kibarazani kuongea naye kwenye simu huku akiwatazama kwa darubini.
Gereza hili lilijulikana kama La Catedral (the cathedral) na lilimuhifadhi mfungwa muhimu zaidi duniani na binadamu aliyeifinyanga na kuifanya biashara ya mihadarati iwe jinsi ilivyo hivi leo. Marafiki zake wa karibu walipenda kumuita El Patrón (The Boss) au El Zar de la Cocaína (The Tsar of Cocaine) lakini alipozaliwa wazazi wake walimuita Pablo Emilio Escober Gaviria au kwa kifupi Pablo Escobar kama ulimwengu wote ulivyomtambua.
The Boss
Akiwa mtoto wa tatu kwenye familia ya watoto saba ambapo baba yake alikuwa ni mkulima na mama yeke mwalimu wa shule ya chekechea, Pablo Escobar alikuwa ni mwenye kutamani mambo mazito na mwenye maono makubwa tangu angali mtoto.
Akiwa bado kwenye umri wa makumi (teenage) Pablo mara kwa mara aliwaambia ndugu zake na marafiki zake kuwa anataka awe na utajiri wa kiasi cha Peso Milioni 1 za Colombia (COL$ 1 Million) atakapofikisha umri wa miaka 22.
Ndoto hizi zilimfanya ashindwe kumaliza Chuo kikuu alipokuwa anasoma (Universidad Autónoma LatinoAmericana of Madellín) na kujiingiza katika biashara za halali na haramu na hatimaye aliacha masomo chuoni. Moja ya biashara zake haramu za kwanza kabisa akiwa kijana chini ya miaka 21 ilikuwa ni kutengeneza vyeti bandia vya stashahada vya chuo alichokuwa anasoma na kuwauzia watu waliohitaji kwa ajili ya kwenda kupata ajira.
Pamoja na biashara hiyo pia Pablo alijihusisha na kusambaza mizigo ya sigara zilizokuwa haziruhusiwi nchini Colombia (Marlboro), pia alifanya kazi kama mlinzi binafsi (bodyguard) pamoja na wizi wa magari.
Moja ya matukio muhimu ya ujana wa Pablo yaliyochangia kuamsha ari ndani yake na kumfanya atamani kuwa moja wa manguli wa biashara haramu lilikuwa ni tukio ambalo alipofikisha miaka 26 alifanikiwa kuweka benki (Cash Deposit) kiasi cha Peso Millioni 100 za Colombia (COL$ 100 Million).
Mafanikio haya yaliwasha taa ndani yake na kuamsha ari ya kutaka kuwa ‘Papa’ katika ‘Dunia’ ya siri ya ulimwengu wa biashara haramu.
Katika miaka ya 1970 mamlaka ya kupambana na matumizi mabaya ya madawa nchini marekani (US Drug Enforcement Agency) waliwahi kutangaza kuwa wamewekeza zaidi rasilimali zao kupambana na matumizi na uingizaji wa dawa aina ya Heroin nchini marekani na kwa maoni yao walisema kuwa wanadhani madawa aina ya Cocaine hayakuwa na uwezo wa kuleta uteja (addiction) au kufanya mtumiaji kuwa muhalifu tofauti na dawa aina ya Heroin. Hivyo basi walielekeza nguvu zao zote na rasilimali kupambana na biashara ya usafirishaji wa Heroin kama kipaumbele cha kazi zao.
Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa upande wao. Kwani kijana Pablo aliona mwanya huu na udhaifu huu upande wa DEA au pengine tusema kwamba Pablo alifahamu zaidi kuhusu ulimwengu wa mihadarati kuliko DEA.
Kitu kikubwa ambacho Pablo alikiona na watu wakiwemo DEA hawakukiona ilikuwa ni uwezekano (potential) ya kuifanya Cocaine kuwa moja ya madawa yenye soko zaidi Amerika ya Kaskazini. Katika kipindi hiki kulikuwa na watumiaji wachache sana wa Cocaine nchini marekani lakini Pablo aliona fursa ya kuifanya mihadarati hiyo kuwa moja ya madawa yenye kuhitajika sana nchini marekani na ulimwenguni kiujumla.
Kutokana na uzoefu wake wa ulimwengu wa kihalifu, Pablo aligundua kuwa zao la Coca linalimwa nchini Bolivia ambalo linatumika kutengeneza Cocaine ni bora zaidi kuliko Coca inayolimwa nchini kwake Colombia. Hivyo basi Pablo akadhamiria kuwa kama anaingia kwenye biashara hii ya kusafirisha Cocaine ni lazima mihadarati yake iwe tofauti na bora zaidi kuliko Cocaine nyingine watu waliyozoea kutumia. Akadhamiria kufanya Cocaine yake iwe daraja la kwanza ili kuvutia watumiaji na kufanya soko likue kwa haraka.
Kama sehemu ya mkakati wake wa kuingia rasmi kwenye biashara ya kusafirisha mihadarati aina ya Cocaine, mwaka 1975 kijana Pablo alisafiri mpaka nchini Bolivia kukutana na Roberto Suaréz Goméz ambaye marafiki zake walipenda kumuita El Padrino (The Godfather) kiongozi wa Genge lililoitwa La Corparacíon (The Corporation). Suaréz alikuwa ndiye mtu pekee anayeendesha na kuratibu uzalishaji wa zao la Coca katika nchi ya Bolivia na Peru. Kipindi hiki Suaréz tayari alikuwa na mtandao mkubwa katika America ya kusini na alikuwa na jina kubwa, ushawishi na nguvu ya kijeshi hivyo haikuwa kazi rahisi kwa kijana Pablo kumshawishi Suaréz akubali kufanya naye biashara.
Huyu bwana Suaréz alikuwa na nguvu kiasi kwamba alikuwa na jeshi lake binafsi la anga (Air force) na wanajeshi wa miguu 1,500 ambao walipatiwa mafunzo nchini libya.
Pablo alitumia uwezo wake wa kujieleza na uzoefu wake wa ulimwengu wa kihalifu kumshawishi Suaréz na kumueleza kuhusu mkakati wake wa kuiteka biashara ya mihadarati ya Cocaine nchini marekani na akamdadavulia jinsi ambavyo yeye Suaréz atapata utajiri wa kupindukia kama atakubali kufanya nae biashara.
Pia Pablo alimpa wazo Suaréz kuwa atumie ushawishi wake alionao serikalini (Suaréz alikuwa amefanikiwa kumpenyeza Mdogo wake serikalini na kuwa Waziri wa mambo ya ndani) ahakikishe wanakutana na kiongozi wa Cuba Fidel Castro ili wamuombe kuwa mshirika wao katika mambo kadhaa.
Suala hili lilifanikiwa kwani Pablo na Suaréz walipata fursa adhimu na wakakutana na Fidel Castro na ombi lao kubwa kwake lilikuwa ni kuwaruhusu kupitisha mizigo yao nchini kwake Cuba na nchi za jirani pasipo bugudha. Pia walimuomba aruhusu ndege zao za mizigo zitue kwenye viwanja vya ndege vya Cuba na kujaza mafuta pale inapobidi kufanya hivyo.
Castro akawakubalia kwa masharti mawili, moja ni kwamba atakuwa anawachaji mamilioni ya dola za marekani kwa huduma hizo na pili mihadarati hiyo isiuzwe ndani ya Amerika ya Kusini bali isafirishwe na kuuzwa Marekani ambapo Fidel Castro alisisitiza kuwa atafurahi akiona vijana wa Mabepari wakiharibika na mihadarati.
Masharti yote mawili haya yakakubaliwa na Pablo na Suaréz kisha wakarejea Bolivia. Baada ya kufanya mazungumzo juu ya namna watakavyo fanya biashara hatimae Pablo na Suaréz walifikia muafaka na kwa mzigo wake wa kwanza alioununua nchini Bolivia kutoka kwa Suaréz ulikuwa ni kilo 14 za unga gafi za Cocaine.
Baada ya unga gafi kufikishwa nchini Colombia kwenye mji wa Medellín, Pablo alikuwa ameandaa jengo maalum la ghorofa mbili ambalo alilitengeneza kuwa maabara maalumu ambapo Cocaine gafi kutoka Bolivia ilichanganywa na maligafi nyingine na kuboreshwa zaidi kikemia na hatimaye kupata Cocaine daraja la kwanza aliyoihitaji tayari kusafirishwa nchini Marekani kwa ‘walaji’.
Baada ya Cocaine kutoka kwa Pablo kuingia kwenye soko la Marekani uhitaji na biashara ya mihadarati ya Cocaine ilipaa kwa kasi ya ajabu na Pablo Escobar akaanzisha rasmi genge lake la biashara ya mihadarati na akaliita Medellíne Cartel.
Pablo akatengeneza mtandao madhubuti wa wasambazaji wa mihadarati yake katika miji ya Florida na California pamoja na majimbo mengine ya Marekani.
Pia akabuni njia mpya ya kupitisha mihadarati kupitia Bahamasi katika kisiwa cha Norman’s Cay takribani kilomita 350 kusini mashariki mwa pwani ya Florida.
Ili kufanikisha zaidi azma yake Pablo Escobar alinunua nusu ya ardhi ya kisiwa cha Norman’s Cay na nusu nyingine ikanunuliwa na swahiba wake wa kimarekani aliyeitwa Robert Vesco ambaye pia alikuwa ndiye anashughulikia masuala yake ya kibenki na uhasibu.
Katika Kisiwa hiki Pablo alitengeneza uwanja wa ndege, bandari, hoteli, nyumba za kuishi pamoja na ghala kubwa la jokofu maalumu kwa ajili ya kuhifadhi mizigo ya Cocaine kabla ya kuisafirisha kwenda marekani. Kwa kifupi hapa ndipo kilikuwa kitovu cha kibiashara cha Genge lake la Medellíne Cartel.
Pablo Escobar alikuwa amepania haswa kuliteka soko la Cocaine Amerika ya Kaskazini na hii ilijidhihirisha kutokana na juhudi zake alizozifanya kibiashara ili mda wote awe hatua kadhaa mbele tofauti na washindani wenzake kibiashara.
Ili kufanikisha usafirishaji wa mizigo yake kwa ufasaha na uhakika Pablo alinunua ndege za mizigo 15 za ukubwa wa kati na helikopta 6. Pia alinunua Nyambizi ndogo mbili (submarines) kwa ajili ya kusafirisha mizigo mikubwa ya mihadarati.
Hadi kufikia mwaka 1985 Pablo alikuwa anasafirisha takribani tani 70 mpaka 80 za Cocaine kwa mwezi na alikuwa ameshikilia asilimia 80 (80%) ya soko la mihadarati la Marekani.
Na katika kipindi hiki Genge lake la Medellíne Cartel lilikuwa linaingiza kipato cha cha Dola Milioni 70 kwa siku (Shilingi Bilioni 140 za Kitanzania) na mapato yao kwa mwaka mzima yalifikia Dola Bilioni 21.9. (Shilingi Trilioni 46 za Kitanzania).
Katika miaka ya 1990 utajiri wake binafsi ulifikia kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 30 ambazo ni sawa na Dola Bilioni 54 kwa hesabu za sasa (Shilingi Trilioni 110 za kitanzania)
Ni katika kipindi hiki ambacho Jarida maarufu la Forbes lilimuorodhesha Pablo Escobar kama mtu namba 5 tajiri zaidi ulimwenguni na muhalifu tajiri zaidi katika historia ya Ulimwengu.
Kutokana na nguvu na ushawishi alionao, Pablo aliteuliwa na serikali kama mjumbe wa baraza la wawakilishi la Colombia (Chamber of Representatives of Colombia) kupitia chama cha Kiliberali Cha Colombia (Colombia Liberal Party).
Moja ya majukumu muhimu aliyoyafanya akiwa kama Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kilikuwa ni kwenda kuiwakilisha Serikali ya Colombia katika sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu mpya wa Uhispania Bw. Felipe González mwaka 1982 ambapo Pablo alitumia nafasi hii ya Safari ya kiserikali nchini Uhispania kuanzisha tawi jipya la Genge lake la Medellíne Cartel katika nchi ya Uhispania.
****
Katika miaka ya 1990 utajiri wake binafsi ulifikia kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 30 ambazo ni sawa na Dola Bilioni 54 kwa hesabu za sasa (Shilingi Trilioni 110 za kitanzania)
Ni katika kipindi hiki ambacho Jarida maarufu la Forbes lilimuorodhesha Pablo Escobar kama mtu namba 5 tajiri zaidi ulimwenguni na muhalifu tajiri zaidi katika historia ya Ulimwengu.
Kutokana na nguvu na ushawishi alionao, Pablo aliteuliwa na serikali kama mjumbe wa baraza la wawakilishi la Colombia (Chamber of Representatives of Colombia) kupitia chama cha Kiliberali Cha Colombia (Colombia Liberal Party).
Moja ya majukumu muhimu aliyoyafanya akiwa kama Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kilikuwa ni kwenda kuiwakilisha Serikali ya Colombia katika sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu mpya wa Uhispania Bw. Felipe González mwaka 1982 ambapo Pablo alitumia nafasi hii ya Safari ya kiserikali nchini Uhispania kuanzisha tawi jipya la Genge lake la Medellíne Cartel katika nchi ya Uhispania.
Sasa Endelea….,
Hacienda Nápoles: Pepo Juu ya Uso wa Dunia
Kutokana na utajiri uliopitiliza wa Pablo Escobar alithubutu kutengeneza makazi ya kuishi ambayo namna pekee ya kuyaelezea ni kana kwamba alijitengenezea ‘pepo’ akiwa duniani.
Katika mji mdogo wa Puerto Triunfo, takribani kilomita 150 kutoka katika mji wa Medellín, Pablo alinunua eneo lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 20 na kujenga makazi yake na familia yake na akayaita makazi haya Hacienda Nápoles (Naples Estate).
Licha ya majengo ya kifahari ya kuishi yeye na familia yake pia makazi haya yaliwekwa anasa lukuki zisizomothirika. Ndani ya makazi haya kulikuwa na Uwanja wa ndege binafsi (private airport), bustani maalumu ya sanamu za kuchonga na kufinyanga (Sculpture Park), kulikuwa na sehemu maalumu ya kuhifadhi magari ya kifahari na pikipiki za kifahari kwa ajili ya kutazama tu (collection), kulikuwa na uwanja wa mbio za magari magogo (kart racing track), kulikuwa na uwanja wa mapigano ya ng’ombe (Bullring), na pia ndani ya makazi haya kulikuwa na mbuga ya wanyama ya kutengeneza (Zoo) ambapo Pablo alikusanya aina mbali mbali za wanyama kutoka kila kona ya dunia na kuwaweka humo.
Katika geti la kuingia kwenye ‘pepo’ ya Pablo sehemu ya juu ya geti ilininginizwa ndege (ndege halisi) kama urembo. Ndege hii aina ya Piper PA-18 Super Cub yenye namba ya mkia HK-617-P hii ndio ilikuwa ndege ya kwanza aliyoitumia Pablo kuingiza mzigo wake wa kwanza wa Cocaine nchini Marekani.
Hapa katika ‘pepo’ hii ndipo ambapo Pablo Escobar aliishi yeye na familia yake.
Plata o Plomo
Moja ya vitu muhimu vya kihalifu alivyovifanya Pablo na kufanikiwa kuibuka kama kinara wa uhalifu Amerika ya kusini ilikuwa ni kutekeleza sera yake aliyoianzisha yeye mwenyewe ili kuidhibiti serikali na vyombo vya ulinzi ambapo sera hii aliita “Plata o Plomo” (silver of lead (fedha au risasi)). Akiwa na maana kwamba kama wewe ni mtu wa serikali na ikitokea mmesigana basi atakupa fedha (rushwa) kama ukikataa kupokea fedha basi anakupiga risasi.
Sera hii ilimfanya Pablo aogopwe na watendaji wa serikali pamoja na vyombo vya usalama na ikapelekea wengi kukubali ‘Plata’ (silver (fedha)) wakihofia kupoteza maisha endapo wangekataa fedha kutoka kwa Pablo. Hii ilimsaidia Pablo Escobar kuwa na vibaraka wengi katika serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.
Lakini sera hii iligharimu maisha ya watu wengi sana wale ambao walikataa kupokea fedha kutoka kwa Pablo na mojawapo ya matukio mawili yanayokumbukwa sana ya utekelezaji wa sera ya ‘Plata o Plomo’ ni haya:-
Mosi; Uvamizi wa Mahakama Kuu ya Colombia 1985.
Mwaka 1985 baada ya mabishano ya muda mrefu bungeni kuhusu vifungu vya kikatiba vinavyokataza raia wa nchi ya Colombia kukabidhiwa kwa nchi ya kigeni akiwa kama muhalifu hatimae serikali ikafungua kesi ya kikatiba mahakama kuu ya Colombia ikitaka ruhusu ya kukabidhi baadhi ya wahalifu kwa serikali ya Marekani ikitokea wakikamatwa.
Suala hili lilikuwa linamlenga moja kwa moja Pablo Escobar kwani serikali ya Colombia ilikuwa inapewa shinikizo kubwa na Marekani kuwa wafanye marekebisho ya katiba ili iruhusu raia wa nchi hiyo ambaye ni muhalifu kukabidhiwa kwa nchi ya kigeni. Haya yalikuwa ni maandalizi endapo ikitokea Pablo Escobar akikamatwa.
Pablo akajitahidi kwa juhudi zake zote kuhonga serikalini na hata kutoa onyo kuwa mabadiliko hayo ya kikatiba yasifanyike lakini serikali iliendelea na mchakato kutokana na shinikizo walikuwa wanapata kutoka kwa marekani.
Inajulikana kwamba Pablo mara kwa mara alikuwa akiapa mbele za watu wake wa karibu kuwa kamwe hatokubali kufungwa katika nchi ya marekani na alikuwa na msemo anaoupenda kuusema kwamba “ni heri kuwa kaburini Colombia kuliko kuwa hai kwenye gereza la Marekani”.
Baada ya juhudi zake zote za kuionya serikali kutobadili katiba kushindikana hatimaye Pablo akakodi kikundi cha wapiganaji wa msituni kilichoitwa M-19 ili wasaidie kumaliza tatizo lake.
Siku ya Novemba 6, 1985 majaji 25 wa mahakama kuu walikuwa katika vikao vya mwisho kujadili na hatimae waweze kuridhia mabadiliko hayo ya katiba lakini kabla ya kumaliza vikao vyao na kuridhia mabadiliko hayo walivamiwa na wapiganaji wa kikundi cha M-19.
Wapiganaji hawa walivamia na kuteka mahakama kuu kwa muda wa siku mbili na zaidi ya nusu ya majaji waliuwawa na waliosalia walichukuliwa mateka.
Majaji hawa waliochukuliwa mateka walikuja kutumiaka kama sharti muhimu la kuibana serikali waache kurekebisha katiba ili waweze kuachiwa. Baada ya serikali kukubali kuacha kubadili katiba hasa kipengele cha kukabidhi wahalifu kwa nchi ya kigeni, majaji wote waliotekwa wakaachiwa.
Pili; Mauaji Mgombea Urais Luis Carlos Galán
Tukio la pili linalokumbukwa sana la utekelezaji wa sera ya ‘Plata o Plomo’ lilikuwa ni mauaji ya mgombea Urais wa Colombia aliyeitwa Luis Carlos Galán. Galán alikuwa anaongoza kwenye kura za maoni nchi nzima na alikuwa anatarajiwa kushinda kwenye uchaguzi mkuu wa urais wa Colombia wa mwaka 1990.
Moja ya sera kubwa aliyokuwa anaihubiri kila kona ya nchi ilikuwa ni kupambaa na Magenge ya Mihadarati hasa hasa akililenga Genge la Medellíne Cartel na kiongozi wake Pablo Escobar.
Pablo alimtumia barua kadhaa ambazo ziliwekwa nje ya nyumba yake kwenye kisanduku cha barua akimuonya na kumtaka aachane na sera hiyo ya kumsakama yeye pamoja na washirika wake wa Medellíne Cartel lakini Bwana Galán alionekana dhahiri amezamilia kutekeleza sera hiyo endapo angechaguliwa kuwa rais wa Colombia.
Akiwa katika kampeni Bwana Galán alifanikiwa kufika kwenye mji wa Madellín ambapo Pablo alikuwa na ushawishi mkubwa na wapo wananchi waliojaribu kumuua Galán kwa kumrushia guruneti la kutupa kwa roketi (Rocket Propelled grenade) lakini kwa bahati nzuri Bwana Galán akisalimika.
Baada ya hapo Pablo akakodi wadunguaji maalumu kufatilia nyendo za Galán na akawapa amri ya kumpiga risasi mara tu wakipata upenyo wa kufanya hivyo.
Wiki kadhaa baadae akiwa kwenye kampeni katika mji wa Saocho Kiranga alipokwenda kuhutubia wafuasi wake wapatao 10,000 waliokusanyika wakisubiri kumsikia na mara baada ya kuwasili na kupanda jukwaani kuhutubia kabla hajatoa hata salamu kwa wafuasi wake alidunguliwa na risasi na kupoteza maisha papo hapo.
Tukio hili lilizua taharuki nchi nzima na imekuwa skendali yenye utata mpaka leo hii nchini Colombia kwani kuna tetesi kuwa viongozi wa serikali, polisi, pamoja na mashushushu walishirikiana na Pablo Escobar kutekeleza mauaji haya.
Licha ya Pablo kuonekana kama adui namba moja nchini marekani na baadhi wa watendaji wa serikali ya Colombia hali ili kuwa tofauti kwa raia masikini wa Colombia ambao wengi wao walimuona kama shujaa wao na katika mji aliozaliwa na kushi wa Medellín anaonekana zaidi ya shujaa kwani mpaka leo hii wanamuona kama ni aina fulani hivi ya masihi walipewa.
Hii inatokana na umahiri wa Pablo Escobar katika mahusiano na jamii iliyokuwa inamzunguka.
Pablo alikuwa ni mtu mwenye kusaidia masikini nchini Colombia pengine kuliko hata serikali yenyewe.
Pablo alijitolea kweli kweli katika kuboresha huduma za jamii kama vile kujenga mahospitali, shule, nyumba za wazee, nyumba za kuishi kwa ajili ya masikini na akawekeza fedha nyungi kujenga miundo mbinu ya Kanisa Katoliki na nyumba za kuabudia. Pia Pablo alijenga vya kuendeleza watoto katika mpira wa miguu, alifadhili klabu mbali mbali za wakubwa za mpira wa miguu na alijenga viwanja vya kisasa kabisa vya mpira na michezo mingine.
Ilifikia hatua mpaka Pablo alikuwa anawapa fedha taslimu wananchi wa Madellíne ili waweze kujikimu kimaisha.
Mambo haya yote yalifanya wananchi wampende na kufumbia macho uhalifu wote aliokuwa anaufanya.
Kwa mfano katika mji wa Madellín ilifikia hatua kana kwamba wananchi wote walikuwa ni walinzi wake binafsi kwani walikuwa wakimtonya kila walipoona polisi wageni wakiingia hata kwa siri kwenye mji huo. Au wakati mwingine walikuwa wakitoa taarifa za uongo au kukataa kusema chochote pindi wakiulizwa na vyombo vya ulinzi kuhusu nyendo za Pablo.
Hii ilimfanya Pablo azidi kujizatiti na kuongeza mahaba kwa wakazi wa Medellín na raia wa Colombia kwa ujumla.
VITA KUU YA KWANZA YA MAGENGE YA MIHADARATI.
Kuna msemo wanasema ‘adui wa adui yako ni rafiki yako’! Swali: je, inakuwaje pale adui wa adui yako akitishia maslahi yako??
Adui wa Adui yako (Kikao cha Kwanza)
Hapo baadae nitaeleza kwa kifupi kuhusu kuibuka kwa genge lingine ambalo nalo lilishamiri katika biashara ya Cocaine lililoitwa Cali Cartel hivyo kufanya kuwe na uwepo wa magenge mawili yanayoshindana kibiashara yaani Medellín Cartel chini ya Pablo Escobar na Cali Cartel.
Licha ya ushindani wao wa kibiashara mwaka 1983 iliwabidi washirikiane kwa sababu za msingi kabisa. kuliibuka kikundi cha wahuni waliokuwa wanateka watu na kudai fedha kutoka kwa ndugu ili wawaachie. Baada ya kuteka ndugu kadhaa wa viongozi wa serikali wahuni hawa wakaanza kuteka ndugu wa mabosi wa Cartels na kudai pesa.
Moja ya watu muhimu waliowateka alikuwa ni Marta Nieves Ochoa dada wa moja ya mabosi wa Cali Cartel na watekaji walikuwa wanataka wapewe dila milioni 10 ili wamuachie. Hii ndio ilikuwa sababu kubwa ya mabosi wa Cali Cartel na Medellín Cartel kukutana ili kuweka mkakati maalumu ambao utapeleka ujumbe kwa wahuni na watekaji wote kuwa familia za mabosi wa Magenge ya mihadarati ni mwiko kuzigusa.
Katika kikao hiki cha kwanza Medellín Cartel na Cali Cartel waliunda kikosi kazi maalumu walichokiita Muerte a Secuestradores (Death to kidnappers (Kifo kwa Watekaji)) au kama kilivyojulikana kwa kifupi MAS.
Kila Genge lilichangia fedha, vifaa (silaha), na askari kwa ajili ya kikosi kazi cha MAS.
Kesho yake baada ya kikundi hiki kuundwa ndege ilipita juu ya uwanja wa mpira wa miguu kuliko kuwa na mechi kubwa ikifanyika na kumwaga vipeperushi kuhusu kutangaza zawadi nono kwa yeyeto atakayetoa taarifa kuhusu kufahamu lolote juu ya wahuni wanaoteka watu na kushinikiza wapewe hela. Jioni ya siku hiyo taarifa muhimu kutoka kwa wananchi zikaanza kuletwa na kikosi kazi cha MAS mara moja kikaanza kukamata wahuni wa vikundi vya utekaji na kuwatesa huku wakiwarekodi na kuwatumia wenzao wanaoshikilia dada wa bosi wa Cali Cartel.
Ndani ya siku tatu Marta Naives dada wa bosi wa Cali Cartel aliachiwa akiwa salama salimini na huo ndio ukawa mwisho wa magenge ya wahuni kuteka wanafamilia wa mabosi wa magenge ya mihadarati.
Kama ni rafiki yako, anaweza kuwa mshirika wako: Kikao cha Pili
Licha ya ushindani wa kibiashara kuendelea kuwepo kati ya Medellin Cartel ya Pablo Escobar na Cali Cartel lakini kufanikiwa kwa mkakati wa MAS kuliwapa moyo kuwa yako maeneo mengine mengi wanayoweza kufanya kwa kushirikiana na yakawa na faida kwa pande zote mbili.
Sehemu ya kwanza ambayo waliona inaweza kuwa na faida kwa pande zote mbili ilikuwa ni Cali Cartel kukubali Pablo Escobar aweze kupitisha fedha zake haramu katika benki ya First InterAmericans Bank ambayo ilikuwa inamilikiwa na maswahiba wa mabosi wa Cali Cartel. Hii ilikuwa na faida kwa kubwa kwa Pablo kwani ilikuwa ni njia rahisi na salama kwake kuweza kusafisha fedha zake haramu lakini pia ilikuwa na faida upande wa wamiliki wa benki maswahiba wa mabosi wa Cali Cartel kwani nao wangepata faida kwa kutoa huduma hiyo kwa Pablo kutokana mabilioni ya dola ya dola ambayo atakuwa anayapitisha kwenye benki yao.
Sehemu ya pili waliyokubaliana kushirikiana ilikuwa ni namna ya kuratibu bei ya Cocaine mtaani, kuratibu viwango vya ubora wa uzalishaji na njia salama za kusafirisha mizigo.
Sehemu ya tatu walikubaliana kuhusu kugawana soko. Cali Cartel wakakubaliwa kuendesha biashara kwenye jiji la New York na Medellín Cartel ya Pablo Escobar wakapewa Florida na Miami. Jiji la Los Angels likaachwa kama sehemu huru ambayo yeyote anaweza kufanya biashara.
Kwa pamoja wakasonga na biashara ikashamiri.
Rafiki yako anapotishia maslahi yako: Vita Kuu ya Kwanza (Pablo Escobar VS Cali Cartel).
Biashara ya madawa ya kulevya katika America ya Kusini na duniani kote kwa miaka yote imetawaliwa na vita kati ya magenge yanayopambana ili kumiliki na kujipatia ushawishi zaidi katika soko. Lakini katika historia hakuna vita ya magenge ya mihadarati iliyotisha na kuitikisa Marekani na Amerika ya Kusini kama vita kati Medellín Cartel ya Pablo Escobar dhidi ya Cali Cartel.
Vita hii ilitishia hata usalama wa uwepo wa Taifa la Colombia na kuleta aibu kubwa kwa serikali za Colombia na Marekani.
Lakini kabla sijaeleza chochote kuhusu vita hii, nieleze kwa ufupi tu kuhusu Cali Cartel.
The Cali Cartel
Cali Catel ilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1970 kikiwa kama kikundi maalumu cha wapiganaji kilichokuwa kinatumiwa na Pablo Escobar na kilijulikana kama Las Chemas.
Moja wapo ya kazi walizozifanya kwa mafanikio ilikuwa ni utekaji wa raia wawili wa nchi wa uswisi na wakalipwa kiasi cha dola laki saba.
Baada ya malipo haya washirika wa kikundi cha Las Chemas wakajitenga na Pablo Escobar na kukimbilia kusini mwa nchi ya Colombia katika mji wa Cali na wakatumia fedha hiyo kuanzisha biashara yao ya mihadarati na wakafahamika kama The Cali Cartel.
Baada ya biashara yao kuanza kukua wakafanikiwa kuwashawishi wanajeshi kadhaa waasi na kujiunga nao katika biashara na wakafanikiwa kuwapata wengi.
Uwepo wa wanajeshi katika Cali Cartel unadhihirishwa na mfumo wao wa kibiashara pamoja na uwezo wao wa kufanya upelelezi na ushushushu (counterintelligence).
Kwa mfano mfumo wao wa kibiashara ulikuwa tofauti na Medellín Cartel ya Pablo Escobar ambayo yenyewe ilikuwa ni genge linalomilikiwa na mtu mmoja (Pablo) ambapo Cali Cartel wenyewe walikuwa ni muunganiko wa wafanyabiashara wanaojitegemea wanaounda genge/mtandao mmoja wa mihadarati (Cali Cartel).
Kwa upande wa ushushushu na upelelezi walikuwa mahili kiasi kwamba katika baadhi ya ripoti za CIA walikuwa wanawaita kwa jina la utani “Cali the KGB”, wakiwafananisha na shirika la upelelezi la Urusi ya kipindi hicho.
Turejee kwenye…’Vita Kuu’
Ushindani mkubwa wa kibiashara kati ya magenge haya mawili unaweza kuwa sababu kubwa ya wao kuingia vitani lakini hii iliepushwa kutokana na vikao vya makubaliano walivyokaa awalinkuhusu kugawana soko.
Sababu kubwa zaidi na ya msingi iliyochochea vita hii ilikuwa ni Pablo kuamua kuacha kuheshimu makubaliano akiyoingia na Cali Cartel kutokana na genge hili kujihusisha na vitendo ambavyo Pablo alivipinga kwa nguvu zote.
Haijulikani ni kichaa gani kiliwapata viongozi wa ngazi za juu wa Cali Cartel lakini ilipofika miaka ya kati kati ya 1980 Cali Carteli wakaanza kujihusisha na imani zenye utata za “Kusafisha Kizazi/jamii” (Social Cleansing). Cali Cartel walisimamia mauaji ya mamia ya watu kwenye mji wa Cali pasipo sababu ya msingi wakidai kuwa watu hao wanaichafua Cali.
Mauaji yao yaliwalenga walemavu, machangudoa, watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, watoto wa mitaani, na watu wasio kuwa na makazi.
Baada ya kuwaua waliwaandika maandishi kifuania “Cali limpia, Cali linda” (Clean Cali, beautiful Cali (Cali nadhifu, Cali inayopendeza)
Vitendo hivi vilimkera Pablo na ikampa sababu ya kutokuheshimu makubaliano yake na Cali Cartel kuhusu kugawana soko na akaamuru watu wake wafanye biashara nchini marekani katika mji wowote ule wanaojisikia.
Kitu hiki kikiwakera viongozi wa Cali Cartel na ili kumuonyesha kuwa wamechukizwa wakaanza kutoa ufadhili kwa kikundi cha wapiganaji kilichokuwa kinajiita Los Pepes amacho ni kifupi cha Los Perseguidos por Pablo Escobar (People Persecuted by Pablo Escobar (watu walioumizwa na Pablo Escobar)).
Kikundi hiki kilikuwa kinaundwa na ndugu za watu waliouawa na Pablo au Wapambe wake na walikuwa wamejiapiza kumsaka na kumuua Pablo popote alipo. Kitendo cha mabosi wa Cali Cartel kuanza kukipa ufadhili kikundi hiki kilichochea moto wa vita ya magenge amabao haukuwahi kuonekana hapo kabla.
Katika kipindi hiki Colombia ilishuhudia mauaji ya kutisha ambapo wafuasi wa magenge yote mawili walikuwa wakitafutana usiku na mchana. Mauaji haya yaliwahusu mpaka marafiki, ndugu na wanafamilia wa makundi yote mawili. Katika mwaka 1988 pekee idadi ya vifo ilifikia zaidi ya watu 21,000 na mwaka 1989 idadi iliongezeka mpaka vifo zaidi ya 28,000.
Hiki kilikuwa ni moja ya vipindi vigumu zaidi kiusalama kwa Pablo kwani alikuwa na lundo la maadui waliokuwa wakimtafuta. Kulikuwa na serikali ya marekani inamtafuta, serikali ya Colombia inamtafuta, Kikundi cha Los Pepes kinamtafuta, na genge la Cali Cartel linamtafuta. Kutokana na suala la usalama kuwa tete mno ilimlazimu aame kutoka katika ‘pepo’ yake ya Hacienda Napolés na kwenda kujificha katika nyumba za maficho juu ya milima ya mji wa Madellín.
Ilikuwa inambidi abadili makazi mpaka mara nne kwa siku moja. Nyumba zake nyingi hizi za juu ya milima alikuwa anazitumia kuhifadhi pesa na silaha na ilitokea siku walienda kwenye nyumba yake iliyopo karibia kabisa na kilele cha mlima na ilikuwa iko ndani ya msitu mnene.
Siku hii kulikuwa na baridi lisilomithirika na kutokana na nyumba hii kujengwa maalumu kwa ajili ya kuhifadhi fedha na silaha haikuwa na mfumo wa joto wala umeme. Ilifikia kipindi cha usiku baridi lilizidi na kupitiliza kiwangi cha kawaida mpaka ikaanza kutishia afya ya mtoto wake wa kike aliyekuwa naye pamoja na familia yake.
Kutokana na kutokuwepo na namna nyingine yeyote ya kupasha moto nyumba hiyo ili kupunguza baridi, ili mbidi Pablo achome moto maburungutu ya fedha usiku kucha ili kuipatia joto familia yake na hasa mtoto wake wa kike ambaye alionekana kuathiriwa zaidi na baridi. Mpaka asubuhi kunakucha na baridi kupungua kufikia kiwango cha kawaida Pablo alikuwa ameteketeza maburungutu ya hela ya kiasi cha dola milioni mbili za kimarekani.
Baada ya Juhudi za Cali Cartel kumpata Pablo kutozaa matunda, walitoa kandarasi kwa Jorge Selcado ambaye alikuwa ni muhandisi na Mwanajeshi. Jorge alikuwa maarufu kwa kuandaa timu maalumu za mauaji ya kuratibiwa kiumakini (assassination teams) na mara zote mipango yake inakuwa ya mafanikio.
Baada ya Jorge kupewa ‘ofa’ hii na mabosi wa Cali Cartel aliwasiliana na watu wake ambao walikuwa ni wanajeshi wa kukodi (mercenaries) kutoka nchini uingereza ambao walikuwa wamewahi kutumikia katika jeshi la Uingereza kitengo maalumu cha Anga (SAS – Special Air Services).
Timu hii ilikuwa na watu kumi mbili na iliwasili Colombia na kufanya mazoezi kwa miezi kadhaa ili kujiandaa na zoezi lililopo mbele yao. Walifahamu kuwa kwa kipindi hicho Pablo alikuwa amejificha mahali kusiko julikana kwenye milima, hivyo walisubiri wapate taarifa kuwa amerejea kwenye ‘pepo’ yake ya Hacienda ili wafanye shambulio la kushitukiza.
Siku hiyo haikuchelewa sana kwani timu ya Mpira ambayo Pablo alikuwa anaishabikia na kuifadhili ilifanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Colombia. Hivyo Pablo alirejea jijini Medellín ili ajumuike kusherehekea ushindi huo.
Kikosi hiki kilichotumwa kumuua Pablo walijiandaa na Chopa mbili za kivita zilizobeba silaha nzito na mpango wao ulikuwa wamshitukize Pablo nyakati za asubuhi na kufanya shambulizi nyumbani kwake Hacienda Napolés.
Ili mpango huu uwe na ufanisi walikubaliana kuwa washambulie kutokea nyuma ya milima na chopa ziruke katika mfumo maalumu wa kijeshi wa usawa wa chini chini kabisa (nap-to-earth) ili wasiweze kuonekana kutokea mbali.
Keshi yake chopa ziliruka kuelekea Hacienda Napolés kama walivyopanga wapitie nyuma ya milima huku zikiruka chini chini, lakini wakiwa kwenye milima hiyo kwa bahati mbaya chopa moja ilimshinda rubani kutokana na kuruka chini chini na ikagonga kwenye mlima na kudondoka.
Zoezi ambalo kilipangwa kuwa la kwenda kushambulia na kumuua Pablo likageka kuwa ni zoezi la uokoaji na mpango huu ukaishia hapo hapo.
Baada ya kufeli kwa zoezi hili serikali ya Colombia iliwasiliana na Pablo kujaribu kumuomba ajisalimishe.
Waliharibu kumbembeleza kwa kila namna ambayo waliweza na kumuahidi watakubaliana na masharti yoyote atakayoyasema. Serikali ilifikia kipindi walikuwa ‘desperate’ kutokana na aibu waliyokuwa wanaipata kimataifa kwa kushindwa kumdhibiti muhalifu mmoja aliyeifanya nchi yao ya Colombia mpaka kubatizwa jina la ‘Capital of death’ (mji wa kifo). Hivyo matamanio yao ilikuwa tu kuutangazia ulimwengu kuwa wamemkamata Pablo.
Baada ya Pablo kutafakari kwa kina na kuona jinsi usalama wake na familia yake kuwa ni mdogo kutokana na maadui wanaomzunguka kila kona akakubali ombi la serikali kujisalimisha lakini akawapa masharti matatu.
Kila $1 aliyokua anaweka katika biashara yake alikua anapata profit OR return ya $200.
Alikuwa anakusanya pesa haweki bank, anatunza ndani chini ya ardhi, juu ya dari or ukutani. Adui pekee wa hela zake walikuwa ni Panya wenye njaa kali. Kila mwaka inasemekana alikua anapoteza 10% ya faida ambayo kwa haraka haraka ni $b1, Panya walizokuwa wanakula.
Marekani na Serikali ya Colombia ilitaka Pablo akamatwe na afungwe. Akakubali but Gereza akajenga yeye. Ndani ya gereza kulikuwa ni kama 5star hôtel. Alijiwekea kila kitu, Jacuzi, Bar, Pub, TV,na vitu kibao vya thamani. Pia wanawake wakawa wanaingia na akiwa jela alikuwa ana uwezo wa kutoka na kurudi kisirisiri, coz walinzi wa gereza alikuwa anawahonga vizuri sana.
Baadae, Pablo alichoka maisha ya Jela la Hôtel, anataka kurudi kitaa, akatoroka. Wakati anatoroka akachukua familia yake na walinzi wake wakakimbilia Maporini. Wakati wapo huko vichakani, mtoto akaugua ghafla na kukawa na baridi sana, ukahitajika moto unajua Pablo alochofanya?
Alikuwa ananunua na kutumia Rubber band za $2,500 = tsh 4,050,000 za kibongo kufungia hela zake kila mwezi, so kwa mwaka alikuwa ananunua rubber band za $30,000 = 48,600,000 kufunga tu mihela yake (hata BOT hawatumii rubber band za $2,500 kwa mwezi na haijawahi kutokea kwa mtu wala taasisi)
Alinunua ndege kwa ajili ya kusafirishia hela zake tu, kila trip ndege ilikuwa inabeba $10m. Mwaka 1989, Forbes ilimtaja kama tajiri wa 7 duniani, anakadiriwa kuwa na utajiri wa $25-30b, watu wake wa karibu wanasema alikuwa anazidi hata hapo coz kwa siku alikuwa anatengeneza sio chini ya $60m, coz kwa mwezi alikuwa anasafirisha zaidi ya 80-100t USA.
Na ubabe wake wote, Pablo alikuwa anaogopa sana kufa. Baada ya kutoroka Jela, serikali na jeshi la Colombia wakawa wanamtafuta Pablo, akawa-offer serikali iachane nae na atailipia serikali deni ililokuwa inadaiwa $b10 zaidi ya tirioni 18 za kibongo, ili serikali imalize deni inalodaiwa, lakini serikali ilikataa, msako wa Pablo wakakabidhiwa wamarekani na kumuua December 2/1993.
Mpaka leo hongo/rushwa kubwa duniani kuwahi kutokea ni hiyo ya $10b ya Pablo kutaka kulipa deni la taifa la Colombia, 10b usd = trilioni 18.

Wednesday, October 4

 Image result for fidel castro

Mashushushu hawa ndio wenye mafanikio makubwa kuliko wote Duniani.

Njama 638 za mauaji aliyoepuka Fidel Castro.(Chini ya mashushushu wenye ustadi wa hali ya juu sana(skillful)

Njama ya kutumia sigara kumuua Fidel Castro ambayo ilitibuka inajulikana sana, lakini njama nyengine 637 dhidi ya maisha yake ni zipi?

Shirika la kijasusi nchini Marekani CIA na watu waliotoroka Cuba wakati wa uongozi wa Castro walitumia nusu ya karne moja kufanya njama za kumuua kiongozi ambaye taifa lake lina athari kubwa kwa Marekani, kulingana na balozi wa Marekani nchini Cuba Wayne Smith.

Wakati mmoja kiongozi huyo wa Cuba alinukuliwa akisema, iwapo kuepuka majaribio ya mauaji kungekuwa miongoni mwa michezo ya Olimpiki ningejishindia medali ya dhahabu.

Hatahivyo baadhi ya njama hizo hazikutekelezwa ,kulingana na aliyekuwa mlinzi wa zamani wa Fidel Castro, Fabian Escalante.

Stakhabadhi zilizofichuliwa wakati wa utawala wa Bill Clinton zilionyesha kuwa CIA wakati mmoja walianza kuwafanyia utafiti konokono wa eneo la Carebean.

Njama, ilikuwa kutafuta konokono mmoja ambaye angemvutia Castro anayependa sana kuogelea na kumjaza vilipuzi ndani yake kabla ya kumlipua Castro atakapomshika

Mpango mwengine ulikuwa ule wa kutengeza boya la kuogelea ambalo huvaliwa kama shati na ambalo lingetiwa ugonjwa mbaya wa ngozi ili kumuathiri kiongozi huyo.

Mipango yote hiyo ilitupiliwa mbali.

Ajenti huyo alisikitika na akataka mpango mwengine ambao sio rahisi kuugundua,ripoti hiyo ilisema. Mpenzi wa zamani wa Castro, Marita Lorenz alipewa dawa za sumu kumwekea katika kinywaji chake.

Alipewa dawa zenye sumu ili kuweka katika kinywaji cha Castro.Lakini Castro aligundua jaribio hilo na anadaiwa kumpatia bunduki yake badala yake atumie kumuua.

''Huwezi kuniua. Hakuna anayeweza kuniua,"Bbi Lorenzo alisema Bw Castro alimwambia, alipokuwa anahojiwa na gazeti la New York daily.

Castro alidaiwa kutabasamu na kuendelea kuvuta sigara yake.''Nilijihisi nimetolewa pumzi kwa sababu alikuwa na uhakika juu yangu.Alinikumbatia na tukafanya mapenzi''.

Jaribio jingine lililokuwa maarufu dhidi ya maisha ya Castro ni lile la 2000, wakati ambapo mpango uliwekwa kuweka vilipuzi vingi katika jukwaa ambalo alitarajiwa kuhutubia nchini Panama.

Mpango huo ulitibuliwa na vikosi vya usalama vya Castro.

Watu wanne ikiwemo mtoto mmoja wa Cuba pamoja na ajenti wa CIA kwa jina Luis Posada walifungwa lakini baadaye wakaachiliwa.

Pia kulikuwa na mipango ya kumfanya Castro ambaye pia anajulikana '' The Beared'' aonekana kama chombo cha kukejeliwa badala ya kumuua.

Mpango mmoja ulikuwa kumwagia viatu vyake chumvi ya thallium wakati wa ziara yake ya ughaibuni kwa lengo kwamba anaposhika ndevu zake zingeweza kukatika.

Lakini mpango huo ulitibuliwa baada ya Castro kuahirisha ziara hiyo.Castro alichukua tahadhari ya hali ya juu ili kuwakwepa watu waliopanga mauaji yake.

Mwaka 1979 alipokuwa akielekea mjini New York ili kuhutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa hakuweza kuwazuia wanahabari waliomuuliza iwapo alikuwa amevaa fulana ya ndani ambayo ina kinga dhidi ya risasi, alivua shati lake na kuwaonyesha kifua chake.
''Nimevaa fulana ya kawaida'',alisema.

Miongo kadhaa awali mwaka 1975, tume ya bunge la seneti nchini Marekani ilifichua maelezo ya njama nane dhidi ya maisha ya Castro kwa kutumia vifaa ambavyo tume hiyo inasema ''vinachosha akili''.

Njama moja iliopangwa na ambayo karibu ifaulu mara mbili ilikuwa ile ya kutuma dawa za sumu Cuba na kuwapeleka watu kumuua kiongozi huyo.

Ndevu za Fidel Castro pia zililengwa katika njama hizo za mauaji.

Ulikuwa wakati kama huo ambapo rais Kennedy, ambaye aliruhusu uvamizi wa kumuondoa madarakani rais Castro mwaka 1961 aliuawa, ambapo ajenti wa CIA alikuwa anatoa kalamu yenye sumu ilio na sindano kwa ajenti mmoja wa Cuba ili kumuua kiongozi huyo.

Moja ya habari kubwa iliyotawala vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa mni uzinduzi wa sanamu (statue) ya Mikhail Kalashnikov uliofanyika jijini Moscow Urusi.

Mikhail Kalashnikov, mbunifu wa AK-47 silaha maarufu na moja ya silaha hatari zaidi duniani (world's deadliest guns) ambae kwa sasa ni marehemu, ametunukiwa tuzo ya sanamu katika jiji la Moscow. Ila sio kila mtu kaifurahia tuzo hiyo.

[​IMG]
Luteni Generali Mikhail Timofeyevich Kalashnikov


Mara baada ya kuzinduliwa kwa sanamu yake mnamo September 19 kuliibuka maandamano ya wanaopinga tuzo hiyo kutokana na ukweli kwamba ubunifu wake umesababisha vifo visivyo na idadi. Na ndio maana wanaopinga uwepo wa sanamu yake wanasema Kalashnikov ni mbunifu wa kifo na sio shujaa wa taifa hivyo serikali haikupaswa kumtunuku.

[​IMG]

[​IMG]
Sanamu ya Kalashnikov ikimuonyesha akiwa na silaha yake aliyo ibuni ya AK-47


Katika hafla ya uzinduzi wa statue ya Kalashnikov, Vladimir Medinsky ambae ni waziri wa utamaduni wa Russia amesema "Silaha ya Kalashnikov ni utambulisho/alama sahihi ya utamaduni wa Russia, kwa sababu hiyo, serikali imeamua kuziweka silaha zote za Kalashnikov kwenye makumbusho ya Kremlin". (Makumbusho ya Kremlin ni makumbusho makubwa sana Russia na duniani kwa ujumla, yanayotambuliwa na UNESCO na yapo kwenye list of world cultural and natural heritage).


Baadhi ya wanaopinga tuzo ya sanamu kwa Kalashnikov walikua na mabango yaliyosomeka;

"Mbunifu wa silaha ni sawa na mbunifu wa kifo"

Pia wapo waliotoa mitazamo yao juu ya tuzo hiyo kwa Kalashnikov kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter, na hii ni baadhi tu ya mitazamo yao;

"Ni Moscow ya Putin pekee ndio itakubali kumtuza mbunifu wa silaha inayouwa watu wengi kuliko zote"

" Kama mwenyewe angekua hai asingeipenda sanamu yake, kwakua aliwahi kukiri kua silaha yake umeharibu tawala za nchi nyingi na kusababisha maafa makubwa"


AK-47 ilibuniwa mwaka 1947 na katika miaka 60 iliyopita zimetengenezwa AK-47 zaidi ya milioni 70. Zinatumiwa na majeshi, makundi ya uhalifu, magaidi na waasi.

[​IMG]

Kalashnikov akiwa na AK-47


AK-47 inauwa watu zaidi ya 250,000 kila mwaka. Idadi hiyo ni kubwa zaidi kulinganisha na ile ya silaha zote za kisasa kwa ujumla wake.

Kalashnikov alifariki mwaka 2013, na hivi ndivyo alivyosema muda mfupi kabla hajafa , nanukuu "Can it be that I'm guilty for people's death?"

Bado swali linabaki pale pale "Kalashnikov ni mbunifu wa kifo au ni shujaa"?

Friday, September 15

[​IMG]
Rais Kim Jong-un



Mwaka wa 2010 uliingia katika kumbukumbu za Korea Kaskazini baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Kim Jong-il kuzindua kombora lake ambalo wakakti wowote kuanzia sasa litafanyiwa majaribio.

Baada ya kifo cha rais Kim Jong-il , Desemba mwaka 2011 nchi hiyo ilikabidhiwa mikononi mwa mtoto wake Kim Jong-un aliyeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kulingoza vyema taifa hilo.
Baada ya kuapishwa rasmi Aprili 2012 , Kim Jong-un alichukua jukumu hilo na kuzindua satellite iitwayo "rocket-mounted' kama sehemu ya kumbukumbu ya kuenzi siku ya kuzaliwa kwa babu yake ambaye ni muasisi wa taifa hilo Kim Il-Sung.

Msimamo wa kwanza wa Rais Kim Jong-un ulikuwa ni kupinga msaada wa chakula unaotoka Marekani ili kuondoa kifungo cha kufanya majaribio yake ya silaha za nyuklia.

Kwa sasa taifa hilo la kaskazini limeimarisha vitisho vyake kama hatua ya kujibu mazoezi makali ya kivita, yanayondeshwa na Korea Kusini kwa ushirikiano wa Marekani, sanjari na kupinga vikwazo vilivyowekewa dhidi yake katika hatua yake ya kuimarisha zana za kinyuklia.
Katika ilani yake ya hivi karibuni, Rais huyo wa Korea Kaskazini amesema kuwa mpango wake umelenga makombora ya masafa marefu na yale ya kawaida kwa lengo la kuvamia vituo vya Marekani vilivyo Bahari ya Pacific wakati wowote.

Kim Jong-un ameweka tayari makombora hayo kukabiliana na tishio la mashambulio kutoka kambi za kijeshi za Marekani na ndege zake za kivita.
Rais Kim anasema hatua zake zitakwenda sambamba na kujibu ndege za kivita za Marekani kuruka katika anga ya Rasiya Korea.

Kim amesema kuwa kwa sasa muda umewadia wa kumaliza mgogoro na Marekani. Kwa upande wake Marekani na Korea Kusini zinasema kuwa hadi sasa imefanikiwa kunasa mipango ya ndani kutoka Korea Kaskazini kwamba ina kombora lenye na uwezo wa kushambulia umbali wa kilomita 3,000 likiwa na ujazo wa mafuta, tayari kwa kulipuliwa.

Mgogoro huo ulitokana na Peninsula ya Korea kugombewa na mataifa hayo, hatua iliyowahi kusababisha vita baina ya nchi Korea Kaskazini na Korea Kusini iliyopiganwa kati ya mwaka 1950 hadi 1953 ikijumuisha pia China,Umoja wa Kisovyeti na Umoja wa Mataifa (UN).
Machi 29 mwaka huu, mataifa makubwa duniani, China na Urusi yameelezea hofu ya kukithiri kwa mzozo katika Rasi ya Korea na kutaka pande zote kujiondoa katika majibizano.

Makubaliano ya mkutano huo ilikuwa ni kumaliza mgogoro uliopo kati ya nchi hizo.
Taarifa za kiuchunguzi uliofanywa na Korea Kusini zinaeleza kuwa Korea Kaskazini inajiandaa kukamilisha mipango yake ya kuzindua kombora, baada ya kuhamisha makombora yake mawili upande wa Pwani mwa nchi hiyo.

Katika mipango ya kujibu tishio hilo, Korea Kusini kwa ushirikiano na Marekani, zimeimarisha mitambo yake ya kuchunguza shambulio lolote kutoka kwa Rais Jong. Kufuatia hali hiyo, Korea Kusini nayo imeeleza kuimarisha hali yake ya tahadhari baada ya habari kuwa Korea Kaskazini inajiandaa kufanya jaribio la kombora lake moja la masafa ya kati, lililotarajiwa kufanyika April 15, mwaka huu kama sehemu ya kumbukumbu za kuzaliwa muasisi wa Taifa hilo Kim Ill-Sung.

Rais mpya wa Korea Kusini, Park Geun-Hye, amehimiza Korea Kaskazini kubadilisha mkondo wake wa siasa, ili kutuliza uhasama unaoendelea kukuwa kati ya mataifa hayo mawili.
Hali iliyopo kwa sasa kati ya nchi hizo mbili inadaiwa kutokuwa salama kwani Korea ya Kusini imedai kuwa Korea Kaskazini inawazuia hata raia wake kufika katika upande wa pili wa mpaka.

Wakati Marekani akiunga mkono harakati za Korea Kusini, Januari 25, mwaka huu, China pia imesema itaendelea kutoa ushirikiano wa misaada ya chakula kwa swahiba wake Korea Kaskazini, huku ikithibitisha kushiriki endapo kutatokea vita yoyote kati ya nchi hizo.

Mbali na kauli hizo, Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki moon amemtaka Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kupunguza makali yake kwa mzozo unaoendelea kushika kasi, akidai kuwa umeanza kuvuka mpaka. Ban Ki moon ameeleza kuhuzunishwa na namna ugomvi huo unavyotishia maisha ya wananchi wa kawaida na kutoa wito kwa viongozi wa Korea Kaskazini, kubadili mwenendo wao. Awali, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Urusi alisema kuwa uamuzi wa Korea Kaskazini kuendeleza mpango wake wa kuimarisha uwezo wa zana za kinyukilia, unavuruga mipango ya kuanzisha upya mashauriano yanayohusu mataifa sita ya kupatanisha Korea Kusini na Kaskazini.

Monday, September 4


 [​IMG]
Nimekua msomaji wa mambo mengi mtandaoni ni nimekua nikijifunza mengi na kufahamu pia
Leo nawaulizia hawa rockfeller family ambao inasemekana kama ifuatavyo:-
Kwamba wao ndo wanamiliki uchumi wa dunia kupitia dola na rasilimali zote
Wana maamuzi kuhusu mambo yote duniani
Inasemekana kwao wao ndo wanamiliki federal reserve ya marekani
Rais yoyote akiingia marekani lazima akubaliane nao
Ndo wanacontrol dunia
Wana ajenda ya siri juu ya dunia na ndo wanaitumia UN kama chombo chao.Inasemekana UN ipo kwa ajili yao
Vita vingi duniani wameshiriki kupitia mgongo wa serikali ya marekani ambapo wameiweka wao
Inasemekana marekani kuna visible na invisible gov't na invisible govt ndo wao na ndo kila kitu kuhusu uchumi wa marekani na dunia
Ni waasisi na wapo na mkakati wa new world order
Wao ndio wanaodhoofisha nchi nyingi zinazoendelea na kuzifanya kuwa masikini na tegemezi kupitia mifumo yao ya unyonyaji
Inasemekana asilimia kubwa ya mabenk ni yao
Rockfeller family ndo wanaoendeleza mpango wa depopulation duniani na wanadhibiti idadi ya watu kupungua sambamba na kuandaa mikakati ya kupunguza watu kama vita,njaa na magonjwa.
[​IMG][​IMG]
Nimeambatanisha na baadhi ya links
David Rockefeller: An Immoral Life of Evil and Treason
A Face of Evil dies with David Rockefeller [Videos]
Kuna na hii video ya youtube nilitazama kiukweli ilinishtua sana kuhusu david rockfeller

Wednesday, August 30


[​IMG]
Tahadhari: Makala hii ina maelezo, Picha na Video ambazo zinaweza kuwa za kuogofya au kuchefua kwa baadhi ya watu. Tafadhali soma kwa tahadhari binafsi.

Pia si lengo la makala hii kupinga au kokosoa imani ya mtu yeyote. Hivyo basi epuka kutoa maoni yanayoweza kuleta hisia za kukinzana au kukwaza imani za wengine.

Nashukuru kwa kunielewa!

Deera Square, Riyadh (Saudi Arabia)

Ni takribani saa mbili na nusu asubuhi katika eneo la wazi la Deera Square lililopo kwenye mji wa Riyadh katikati ya nchi ya Saudi Arabia. Polisi maalumu wa kitengo cha Mutaween wanawatawanya watu waliopo eneo hilo ambao wengine wamepumzika tu na wengine wapita njia. Polisi hawa ni maalumu wanatambulika kisheria chini ya muongozo wa Shari'ah (kanuni za Kiislamu) ambayo ndiyo kwa kiwango kikubwa inatumika kuongoza taifa la Saudi Arabia, kazi kuu ya askari hawa maalumu ni kuhahakisha kuwa Sharia ya Kiislamu (kwa mujibu wa wao Saudi Arabia walivyo tafsiri) inafuatwa nchini humo.

Mutaween wanahakikisha kuwa wananchi wanafuata utaratibu wa vitu kama mavazi ya heshima (kwa mujibu wa Sharia), kutouzwa vileo mitaani, kutouzwa vyakula 'haramu' kama vile nyama ya nguruwe, vijana kutosikiliza nyimbo za kimagharibi au filamu, pia kuhakikisha wanawake 'wanajisitiri' na hawaongozani na wanaume ambao si waume zao au ndugu zao. Askari hawa ambao sare zao ni kanzu pamoja na viremba maridhawa vya kiarabu wanazunguka mitaani kila kukicha kuhakikisha kuwa Sharia inafuatwa.

Leo hii wapo hapa eneo la Deera Square wakiwaondoa watu kwenye eneo hili, ili kupisha tukio maalumu ambalo linatarajiwa kufanyika mahali hapa.

Eneo hili la Deera Square ukubwa wake bado kidogo lingeweza kufanana na ukubwa wa kiwanja cha mpira. Upande wa kulia wa uwanja huu kuna msikiti mkubwa sana maarufu ambao watu wengi husali hapo, na upande wa kushoto kuna majengo ya ofisi za askari hawa wa Mutaween.

Majengo yanayozunguka uwanja huu wa Deera Square yote yana kuta maridhawa za rangi ya njano zinazofanya muda wa mchana jua kali likipiga eneo hili kujiakisi kwa rangi fulani kama ya dhahabu ambayo haijapita kwenye moto.

Pia kwenye kingo za uwanja kumepandwa michikichi mirefu ya wastani na imepandwa kwa ustadi kwenye mishari kwa kupendeza kabisa. Na si hivyo tu, eneo hili karibu na msikiti upande wa kulia kuna chemi chemi ya urembo ya maji (water fountain) ambayo inarusha maji hewani kwa madaha na kuleta msisimuko wa kupendeza katika eneo hili la uwanja huu tupu mkubwa.

Kwa mtu mgeni unaweza kujihoji eneo hili kubwa namna hii lina matumizi gani hasa? Uwanja ni mkubwa mno kutaka kukaribia uwanja wa mpira wa miguu, lakini hakuna shughuli zozote zinazoendelea zaidi ya wapita njia tu. Vitu pekee vinavyoonekana kwenye uwanja huu mkubwa ni kama nilivyoeleza, michikichi iliyopandwa kwa ustadi, 'water fountain' na msitikiti upande wa kulia na ofisi za Mutaween upande wa kushoto.

Muda huu wa saa mbili na nusu asubuhi kama nilivyoeleza, askari walikuwa wanajaribu kuwaondoa watu waliokaa eneo hili au wale wanaopita njia. Lengo lao ni uwanja huu ubaki mtupu. Lakini ajabu ni kwamba kadiri askari wanavyojaribu kuondoa watu kwenye eneo hili, ndivyo ambavyo watu wengine wengi zaidi wanazidi kumiminika mahala hapa wakiwa na shauku na morari kana kwamba wanaenda kushangilia timu yao pendwa ya mpira wa miguu.




[​IMG]
Deera Square, Riyadh

[​IMG]
Watu wakiwa wamefurika Deera Square Kushuhudia tukio muhimu la Hukumu

Kutokana na watu kuzidi kumiminika eneo hili baada ya askari kuanza kuwatawanya ni dhahiri kwamba hii inaonyesha kuwa hii si mara ya kwanza na hii ni desturi, kwahiyo walikuwa wanajua fika ni nini kilikuwa kinaelekea kutokea mahali hapa.

Hii inawafanya maaskari waweke uzio wa kamba maalumu ya eneo la tukio ('police' scene tape) ili kuzuia umati wa watu usiweze kusogea mpaka eneo la katikati la uwanja huu.

Kama ni mgeni unaweza kujikuta unavutika kusogea mahali hapa ili uweze kujua ni kitu gani hiki cha kusisimua lilikuwa linajiri. Lakini matumaini yako ya tukio la kusisimua yataanza kuyeyuka ghafla mara baada ya kuona magari yapatayo matatu ya Polisi aina ya jeep yakiwasili mahala hapo na polisi kuanza kushuka.

Kwa kawaida ghafla umati wote uliokusanyika hapo unakuwa kimya baada ya kuona magari haya ya polisi. Ukimya unaogubika ghafla umati huu ni mkubwa kiasi kwamba unaweza kujikuta unatokwa jasho la presha kupanda kutokana na kutokujua ni nini kilikuwa kinafuata. Hakuna mtu anayethubutu hata kutingishika au kukohoa, wote wanakodolea macho tu magari haya matatu ya polisi yaliyowasili.

Ukimya na uoga unaotawala nyuso za watazamaji hawa waliojikusanya unaweza kuhoji ni kwanini wefika mahali hapa kuja kushuhudia jambo hili linalotaka kufanyika.

Katika ukimya huu huu mkubwa, wanashuka mapolisi si chini ya kumi na mbili waliovalia sare, sita kutoka gari la mbele na sita kutoka gari la nyuma. Wakishashuka kila mmoja anaenda kujipanga katika eneo lake kuzunguka eneo lote la katikati ya uwanja.

Katika hatua hii ukimya unaongezeka zaidi kiasi kwamba kama ikitokea labda mtu amedondosha sarafu mita ishirini na uliposimama wewe unaweza kujikuta unasikia. Ukimya unakuwa mkubwa zaidi kiasi cha kuogofya, na kinachoweza kukutisha zaidi ni nyuso za morari za watazamaji hawa waliozunguka uwanja huu wa Deera Square.

Baada ya hapo lile gari moja lililosalia (gari la kati kati) milango inafunguliwa, na kisha wanashuka maaskari wanne ambao nao wanakuwa wamevalia sare za kipolisi, lakini tofauti na maaskari wale kumi na mbili walioshuka mwanzoni, hawa wao wanashuka kwenye gari wakiwa wameongozana na mtu mwingine wa tano ambaye yeye hajavalia kipolisi.

Mtu huyu anakuwa amevikwa mavazi meupe sana, au kama wasemavyo watu, "mavazi meupe peeeee"! Yaani weupe ambao unaweza kuumiza macho jua kali linapoakisi. Lakini mtu huyu anakuwa amefungwa mikono yake kwa kamba kwa nyuma na usoni anakuwa amefungwa kitambaa cheusi.

Maaskari wawili kati ya wale wanne walioshuka kwenye gari, wanamshika mtu huyu na kumuongoza mpaka kati kati ya uwanja na wakiisha kumfikisha katikati ya uwanja jambo la kwanza wanalolifanya ni kumpigisha magoti.

Mara chache baada ya kumpigisha magoti wanaweza kumfunika na fuko la kitambaa jeusi usoni (licha ya kuwa tayari amefungwa litambaa cheusi machoni) lakini mara nyingi wanaweza kumuacha hivyo na kitambaa cheusi tu machoni mara baada ya kumpigisha magoti.

Mpaka kufikia hatua hii mtu huyu aliyepigishwa magoti anakuwa tayari kwa ajili ya kuchinjwa.!! Na ghafla tu utasikia sauti kwenye spika zilizofungwa kwenye pembe za uwanja huu, zikitangaza kosa la mtu huyo na hukumu yake kwa mujibu wa Sharia.

Kisha askari mmoja anamfuata huyu mtu aliyepigishwa magoti na kumuinamisha shingo yake kuelekea mbele, kumuandaa kwa ajili ya mchunjajia maalumu wa serikali kupitisha upanga shingoni mwake.

Kisha umati wote unaoshuhudia, pamoja na polisi… wote kwa pamoja wanabakia kumsubiri mtu maalumu wa kutekeleza shughuli hiyo, mtu ambaye labda ndiye aliyechinja zaidi binadamu wenzake wengi kwenye historia ya dunia kuliko mtu yeyote… umati wote, wakiwa kwenye ukimya huu mkuu, na hofu iliyochanganyika na morali wanamsubiria Muhammad Saad al-Beshi.

[​IMG]
Mchinjaji Muhammad al-Beshi

[​IMG]
Al-Beshi akiwaonyesha waandishi wa Habari jambia lake analotumia kuchinijia, alipofanya mahojiano na Arab News mwaka 2003

SIKU MOJA KABLA

Siku moja kabla ya raia aliyehukumiwa kifo nchini Saudi Arabia kuchinjwa hadharani, kwanza mchinjaji Muhammad Saad al-Beshi hutembelea familia ya muhusika ili kuomba msamaha. Msamaha huu anaomba al-Beshi si kwa ajili yake bali anaomba kwa ajili ya mtu anayeenda kumchinja kesho yake ili ndugu zake wapate kumsamehe aondoke duniani akiwa hana lawama kutoka kwa jamaa zake.

Moja ya swali ambalo binafsi niliwahi kujiuliza au yawezekana pia nawe uko unajiuliza muda huu, ni namna gani al-Beshi alifikia hatua ya kuwa "mchinjaji rasmi" wa serikali ya Saudi Arabia? Kuna sifa gani hasa zinaangaliwa? Al-Beshi anajisikiaje kuondoa uhai wa binadamu mwingine kikatilli namna hii?

Katika mahojiano ya nadra sana ambayo aliyafana na Arab News mwaka 2003 al-Beshi aliwahi kueleza ni namna gani alijikuta anaingia katika ajira hii ya "kipekee".

Al-Beshi alianza kazi ya kuchinja watu mwaka 1998, kabla ya hapo alikuwa anafanya kazi gerezani maeneo ya Taif, na kazi yake ili kuwa kuwafunga mikono na vitambaa vyeusi machoni wafungwa ambao walikuwa wanapelekwa kuchinjwa.

Baada ya muda akajikuta anaanza kutamani na yeye 'kupanda cheo' ili awe mchinjaji.
Ikatokea kuna muda serikali ikatangaza nafasi ya kazi kwa ajili ya mchinjaji na hila kusita akaomba nafasi hiyo na kukubaliwa.

Mara yake ya kwanza kuchinja mtu ilikuwa ni mwaka 1998. Al-Beshi anaeleza kuwa siku hiyo alikuwa na hofu sana na hasa kutokana na umati wa watu uliojitokeza.
Beshi anasema kuwa alipofika eneo la kuchinjia, alimuinamisha mtuhumiwa shingo na kumpiga upanga mara moja shingoni kwa kishindo kikubwa na kumtenganisha kichwa na kiwili wili.

Siku yake hii ya kwanza kuchinja mtu, Beshi anadai kuwa hakupata usingizi usiku, lakini baada ya hapo hajawahi tena kuwa na hofu wala kukosa usingizi.

Mpaka sasa ameshachinja mamia ya binadamu kwa ruhusa ya serikali ya Saudi Arabia na inaelezwa kuwa yeye ndiye anayeongoza kwa kuchinjwa watu wengi na ndiye mchinjaji chaguo la kwanza la serikali pale inapohitajika mtu kuchinjwa hadharani baada ya kuhukumiwa.
Beshi anaeleza kuwa kuna kipindi huwa anachinja mpaka watu kumi kwa siku moja.

Al-Beshi anajitetea kuwa yeye si mtu katili kwa sababu ya kazi anayoifanya, kwani anajisikia fahari kufanya kazi hiyo ya mchinjaji kwa kuwa anaamini anafanya kazi ya mwenyezi Mungu kama ilivyoagizwa kwenye vitabu.

Pia anaendelea kujitetea kwamba kazi yake haimtengi na jamii kwa kuwa ana marafiki wengi msikitini na mtaaani, pia ana ndugu na jamaa ambao wanampenda na kumuelewa juu ya chaguzi yake hiyo ya ajira.

Si hivyo tu, bali pia al-Beshi ni mume ameoa na amejaaliwa kupata watoto saba.

Al-Beshi anaeleza kuwa huwa anawaruhusu watoto wake kumsaidia kusafisha damu sime lake pindi akitoka kazini kwenye kuchinja watu Deera Square.

Moja ya watoto wake anayeitwa Musaed ambaye ana miaka 22, ameanza 'kumtrain' ili aje kufanya kazi hiyo ya uchinjaji miaka ya baadae.

Siku ya kwanza baada ya kukabidhiwa jukumu hili la kuwa mchinjaji wa serikali, al-Beshi alikabidhiwa sime maalumu na serikali kwa ajili ya kutekeleza jukumu hili. Sime hili linaelezwa kuwa na thamani ya Riyal 20,000 za Saudi Arabia (zaidi ya dola 6,000 za marekani).

Al-Beshi anaeleza kuwa sime hili ni moja kati ya vitu muhimu zaidi kwenye maisha yake anavyovitunza kwa uangalifu mkubwa sana kwa kuwa sime anaona ni kama heshima kubwa kwake aliyopewa na serikali ya Saudi Arabia ili aweze kufanya kazi ya Mungu.

Beshi haishii hapo tu, bali pia anaeleza namna watuhumiwa wanavyoandaliwa mpaka kuanzia siku mbili kabla mpaka dakika ya mwisho ya kuchinjwa… pia anaeleza kuhusu saikolojia na jinsi mtuhumiwa anavyokuwa "desperate" dakika chache kabla hajachinjwa…

ADHABU YA KIFO HADHARANI NCHINI SAUDI ARABIA

Saudi Arabia ni moja kati ya nchi nne pekee ambazo bado zinatekeleza adhabu ya kifo hadharani. Nchi nyingine ni Iran, Korea Kaskazini na Somalia.

Nchini Saudi Arabia, serikali ya kifalme inatekeleza adhabu hii kwa msimamo kwamba wanatekeleza shari'ah kama ambavyo imeelekezwa katika Qur'an Tukufu. Hivyo basi ikitokea raia amefanya kosa ambalo linapaswa aadhibiwe kifo, adhabu hii inatekelezwa kwa mtu huyo kuchinjwa hadharani kwa upanga.

Makosa ambayo yanaweza kupelekea mtu kuhukumiwa kifo ni pamoja na Kuua, usagaji, ushoga/ngono kinyume na maumbile, ubakaji, uzinzi, biashara ya mihadarati, ukahaba, uasi wa dini au kisiasa, kuabudu sanamu, ujambazi wa silaha, wizi wa kawaida (akiiba mara nne), kukufuru, uchawi na ulozi.

Japokuwa kumekuwa Ufalme wa Saudi Arabia umekuwa ukijitetea kuwa wanatekeleza hilo kwa mujibu wa maagizo ya vitabu vitukufu, lakini watu wengi wamekuwa wakitafsiri adhabu hizi za kuchinja watu hadharani kama njia ya kujenga hofu mioyoni mwa wananchi ili waweze kutii kila jambo ambalo linaamuliwa na mfalme wa Saudi Arabia na wasiweze kuhoji chochote.

Wajuzi zaidi wa elimu ya dini wanaweza kutujuza zaidi kuhusu hili, lakini binafsi kwa kadiri nilivyotafiti, nilichokiona kwamba hukumu nyingi za watu nchini Saudi Arabia juu ya kuchinjwa hadharani, japo zinatolewa kwa mtazamo wa kidini lakini zinaegemea zaidi katika upande wa aina za hukumu za Tazir badala ya Hudud

Binafsi sina utaalamu sana kuhusu dini, lakini kwa "a, b, c" za dini ninazofahamu, maoni yangu ni kwamba (nakaribisha kusahihishwa kama siko sahihi) niseme natambua kwamba chini ya Shari'ah, kuna aina tatu za hukumu. Tazir, Qisas na hudud.

Qisas ni aina ya hukumu ambazo zinakuwa baina ya pande mbili au mtu na mtu, yaani namna gani ya kumlipizia mtu aliyekutenda jambo fulani baya.

Kwa upande wa Hudud, hizi ni hukumu ambazo zimeonggelewa moja kwa moja kwenye Qur'an. Yaani kwamba mtu akifanya kosa fulani basi adhabu yake ni kifo hadharani. Hukumu hizi na makosa yake zimetajwa moja kwa moja kwenye Qur'an na kwenye hadith.

Chini ya hukumu hizi, kuna angalizo/tahadhari kubwa inatolewa ili kuweza kuepuka adhabu ya kifo hadharani pale inapobidi. Kwa mfano mtu aliyehasi dini anaweza kupewa nafasi ya kutubu na kurejea tena kwenye dini na kuondolewa adhabu ya kuuwawa hadharani.

Halafu pia kuna hukumu za Tazir. Hizi ni zile hukumu ambazo zimempa mamlaka jaji wa mahakama (Kadhi) kutoa hukumu kwa utashi wake kutokana na makosa husika kutotajwa moja kwa moja kwenye Shari'ah kwa mujibu wa maandiko.

Sasa kwa maoni yangu, nchi ya Saudi Arabia wanatumia mwanya huu kushinikiza adhabu ya kifo hadharani ili kujenga hofu kwenye mioyo ya wananchi wake.

[​IMG]
[​IMG]

Jambo hili limekuwa linaleta shida sana kati ya Saudi Arabia na watu wa haki za binadamu. Kuna makosa ambayo raia wa Saudi Arabia wanachinjwa hadharani ambayo hata wanazuoni wengi wanaamini kwamba hayako sawa kidini bali ni juhudi za Ufalme wa Saudia kuwaziba midomo raia 'vimbele mbele'.

Kwa mfano moja ya utata mkubwa kuhusu adhabu hii ya kifo hadharani ikitokea baada ya polisi wa Saudi Arabia kuwakamata vijana wawili walioitwa Ali al-Nimr na rafiki yake Dawoud al-Marhoon kwa kosa la kuandamana mwaka 2011 kupinga utawala wa Kifalme nchini Saudi Arabia. Kipindi vijana hawa wanakamatwa walikuwa na miaka 17 pekee.

Siku chache baadae alikamatwa muubiri wa kiislamu maarufu nchini humo kipenzi cha vijana anayeitwa Sheikh Nimr al-Nimr (mjomba wake Ali al-Nimr) kwa kosa la kutoa mawaidha yenye maudhui ya kupinga serikali.

Wote hawa walikatwa mwaka 20111 na 2012, na mpaka kufikia mwaka 2015 wote walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa kuchinjwa hadharani.

Hukumu hii ili amsha hasira kubwa ya mashirika ya binadamu mpaka kufikia hatua utekelezaji wa adhabu kwa watuhumiwa hawa watatu ukasogezwa mbele, lakini bado wangali gerezani wakisubiria kuchinjwa siku yoyote ile. (Sheikh Nimr al-Nimr walichinjwa mwaka jana, January 2, 2016 pamoja na raia wengine 47 kwa pamoja).

Lakini kila hii haimaanishi kwamba hakuna watu wanaochinjwa kila siku kwa amri ya serikali ya Saudi Arabia.

Tumezoea kuona vyombo vya habari vikiripoti kuhusu ukatili wa kikundi cha ISIS kutokana na kuwachinja mateka wao wakiwa wanawarekodi, lakini uhalisia ni kwamba serikali ya Saudi Arabia inachinja watu wengi zaidi kuliko ISIS. Pengine habari za ukatili huu unaotekelezwa na serikali ya Saudi Arabia haukemewi sana kwenye vyombo vya habari kutokana na uswahiba wa serikali hiyo na mataifa ya kimagharibi yakiongozwa na Marekani.

Mfano mwaka 2011 inakadiriwa kuwa watu 26 walichinjwa hadharani.
Mwaka 2013 zaidi ya watu 78 walichinjwa hadharani.
Mwaka 2015 jumla ya zaidi ya watu 158 walichinjwa hadharani.
Mwaka 2016 zaidi ya watu 153 walichinjwa hadharani, ambapo watu 47 kati ya hao walichinjwa kwa pamoja (mass beheading) siku ya January 2, 2016.

UTEKELEZAJI WA HUKUMU YA KIFO KWA KUCHINJA HADHARANI

Kwa desturi siku ambayo hupendelewa kuchinja watu waliohukumiwa huwa ni siku ya Ijumaa asubuhi kabla ya jua kuwa kali au baada ya swala ya adhuhur.

Mwanzoni nilieleza namna ambavyo raia wengine wanaondolewa kwenye uwanja wa Deera Square ili kupisha zoezi hili.

Pia nimeeleza namna mtu huyu anavyoletwa mpaka hapa uwanjani akiwa amefungwa kitambaa cheusi na kupigishwa magoti. Baada ya kupigishwa magoti, ndipo anaingia mchinjaji ambaye mara nyingi atakuwa ni Muhammad al-Beshi akiwa na jambia lake kiunoni.

Kama mtu huyu anayechinjwa ni mwanamke, basi ni lazima aletwe hapa akiwa amevalishwa hijab na akifika hapa hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kumshika zaidi ya al-Beshi. Lakini kama ni mwanaume basi unafuatwa tu utaratibu wa kawaida wa kufunga kitambaa usoni (hata mwanamke naye lazima afungwe kitambaa).

Al-Beshi anaeleza kuwa katika kipindi hiki, mtu huyu anayetarajiwa kuchinjwa anakuwa dahifu mno kisaikolojia kiasi kwamba karibia mara zote huwa hawaletiushkeli wowote bali wanatij kila wanachoambiwa. Ni kana kwamba wameshaitoa roho zao kwa mauti, yaani hawana tumaini tena. Al-Beshi anaeleza kuwa mtu huyo anakuwa mnyonge katika kipindi hiki kiwango ambacho huwezi kushuhudia binadamu katika maisha ya kawaida.

Japokuwa anaeleza kuwa wapo wachache ambao huongea maneno ya huzuni na kulia kuomba huruma wasamehewe kitu ambacho (msamaha) hakijawahi kutokea.

Baada ya al-Beshi kuchomoa jambia lake kiunoni, anamsomea hukumu ya kosa alilolifanya huyo mtu na kisha kumkumbusha kutaja/kusoma "Shahada" huku awe anainamisha kichwa chake mbele akiwa hivyo hivyo amepiga magoti. Kisha al-Beshi anainua jambia juu na kulishusha shingoni kwa mtu huyo kwa nguvu, na kwa pigo moja tu anatenganisha kichwa na kiwili wili.

[​IMG]
Al-Beshi akiwa anajiandaa kumkata mtu kichwa kwa jambia

[​IMG]
Al-Beshi akiwa ameshamaliza kumkata mtu kichwa kwa jambia... Ukitazama kwa makini hapo chini utaona mwili umelala ukiwa hauna kichwa na kichwa kiko pembeni upande wa kushoto

Pigo hili moja la jambia linalotenganisha kichwa na kiwiliwili, kinakitupa kichwa chini na kubiringika kama kichwa cha mdoli kichodondoka chini huku kikiachwa mzoga wa mwili ukidondoka pembeni yake ukibubujikwa na damu kutoka kwenye shingo ambayo haina kichwa tena.

Ndani ya kama dakika mbili hivi, wasaidizi wengine wanakuja na kuokota mabaki ya mzoga huu wa binadamu na kuupakia kwenye gari inayosubiria pembeni.

Sasa hapa inategemea na hukumu ya huyu marehemu ilivyoandikwa na Kadhi.

Kuna baadhi baada ya kuchinjwa hukumu yao inaamuru kuwa miili yao ininginizwe sehemu ya umma kwenye mti mrefu au 'crane' kwa siku tatu au nne au saba kutegemea na hukumu.
Lakini kama hukumu ya mtu huyu haisemi chochote kuhusu mwili wake kuning'inizwa hadharani basi maiti hii inapelekwa mpaka mochwari ambapo kichwa kinashonwa tena kwenye kiwiliwili kwa Uzi na sindano na kisha mwili unazikwa.

Mpaka hapa hukumu ya kifo cha kuchinjwa hadharani inakuwa imekamilika.

Nikirudi tena nitaeleza visa vya kusisimua vilivyowahi kutokea kuhusiana na utelezaji wa hukumu hii ya kuchinja hadharani…
-