Thursday, March 31


Rais John Magufuli wa Tanzania akitoa hotuba Ikulu Dar es Salaam.

Rais John Magufuli wa Tanzania akitoa hotuba Ikulu Dar es Salaam.
Kufuatia tamko la rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kupunguza mishahara ya wakuu wa taasisi na mashirika ya umma nchini Tanzania baadhi ya wachambuzi wamepokea kwa hisia tofauti nchini humo.

Uamuzi huo utaathiri mashirika mengi ya umma nchini humo ambapo baadhi ya wakuu wake wametajwa kupokea mshahara wa zaidi ya milioni 30 kwa mwezi .
Mchambuzi wa siasa nchini Tanzania na mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kitila Mkumbo, anasema kufanya kazi kwenye mashirika haya ni sehemu ya utumishi wa umma na akisistiza kwamba wakuu wa mashirika haya wasitarajie kulipwa kiasi kikubwa kupita kiasi akipinga wale wanaodai kwamba kupunguza mishahara hiyo kunaweza kupunguza utendaji au morali katika mashirika ya umma.
Pia akiongeza kwamba ili Rais Magufuli na chama chake wafanikiwe lazima wabadilishe mtazamo wa kisera, kiitikadi na kifalsafa bila hivyo mabadiliko hayatakuwa na msingi wowote wa kufanikiwa.


Kwa kipindi cha hivi karibunin kumekuwepo na tuhuma za baadhi ya wabunge kujihusisha na masuala ya rushwa.

Tuhuma hizo zimekuwa zikifanyiwa kazi na vyombo vya dola na kwamba tayari baadhi ya wabunge wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kinasikitishwa sana na tuhuma hizo, hasa pale zinapowahusisha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi  na kinaunga mkono jitihada za vyombo vya dola katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo.

Lazima ifahamike kuwa vitendo vya rushwa havina itikadi,dini, wala kabila na kwamba havikubaliki kwa namna yoyote kwani vina madhara makubwa kwa taifa.

CCM inavishauri vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua stahiki wabunge wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Chama cha mapinduzi kwa upande wake hakitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wabunge wake watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa
**
Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wamefikishwa mahakama ya Kisutu leo kwa tuhuma za rushwa.

Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge wanatuhumiwa kushawishi na kupokea rushwa  ya shilingi Milioni 30 toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo 

Mwendesha Mashitaka wa Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mahela Ndimbo mbele Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,  Thomas Simba amesema tukio hilo lilitokea  Machi 15 mwaka huu  majira saa 2  had saa 4 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Ndimbo alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao wakiwa wajumbe Kamati Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) waliomba  rushwa ya sh.milioni 30 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Gairo, Mbwana  Magota.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,Thomas Simba aliutakaupande wa mashitaka upeleke ushaidi  wa watuhumiwa wa rushwa .

Washitakiwa waliposomewa shitaka la kuomba rushwa wote walikana na dhamana yao kuwa wazi kwa masharti ya kila mmoja kwa na mdhamini wa mmoja wa sh.milioni tano pamoja na hati ya kusafiria ambapo wote walikidhi masharti ya dhamana hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba ameairisha kesi hiyo mpaka Aprili 14 mwaka huu itakapotajwa tena .


Wednesday, March 30




Wanawake wanapenda kuwa wagumu sana kila wakati ikifikia maswala ya kuwatongoza. Ni vizuri kuwa hivyo kwa sababu haitakuwa na maana kwa mwanaume kumpata mwanamke yeyote bila kutoa kijasho.

Wakati mwingine inakuwa rahisi kwa mwanaume kumsisimua mwanamke haswa ikifikia maswala ya kumshawishi.

Kuna njia tofauti tofauti ambazo unaweza kutumia kumshawishi mwanamke yeyote kuingia katika box lako. Hapa tumekurahishia kazi kwa kukuandalia maswali ishirini ambayo ukimuuliza mwanamke yeyote utamfanya azimie. Maswali haya unaweza kuyatumia mkiwa pamoja ama kama mwanamke anaweza kuhisi fedheha kiasi flani basi ni vyema zaidi kutumia maswali haya katika text, mtandaoni ama Whatsapp

Tumia maswali haya kumuuliza aidha mpenzi wako ama ni mwanamke yeyote yule ambaye huwa unamtongoza. Unaweza kuanza na swali lolote lile ilimradi uwe unachat na yeye muda wote. Hakikisha umetumia maswali nyakati za usiku ili uweze kupata matokeo mazuri.

1. Uko pekeako?
Swali hili linaeleweka kuuliza kama yuko pekeake na hana kitu cha kufanya nyumbani. Akijibu yuko pekeake. Mjibu kwa kumwambia kuwa unatamani ungekuwa uko na yeye pale alipo sasa.

2. Unafanya nini sahizi?
Fanya kumuuliza hivi kwa umakini ili ujue kama yuko huru ama vipi. Kama ana kazi basi itakuwa ni vigumu kwake kumakinika na mpango mzima. So hakikisha kuwa hayuko buzy. Wanawake wengi hupenda kusema kuwa wako kitandani hawana kitu cha kufanya.

3.Wapenda kupapaswa wakati umelala kwa kitanda?
Swali hili ni kama changamsha bongo kwake. Hii inatoa nafasi ya kuiweka akili yake kwa chat na kuanza kuongea maswala ya kimapenzi polepole bila kumfanya aingiwe na woga ama kushuku nia yako chafu.

4. Unavalia nini kama unaenda kulala/ umevalia nini sasa hivi?
Hili ni swali lenye shauku kwa mwanamke ambaye tayari amejilaza kwa kitanda. Hili ni swali la kibinafsi na bado halijatimiza kumfanya mwanamke kuingiwa na akili ya kusisimuliwa. Akitaja kile alichovali unafaa kumjibu kwa mfano: "Duh!, sahizi umenifanya nianze kukuwaza vile ambavyo umerembeka".

5. Hivi waona unarembeka / sexy zaidi ukivalia nguo gani?
Mfanye aanze kuongea mambo na nguo ambazo akizivaa zinamfanya akuwe sexy ama zinazomrembesha. Atajieleza vile alivyo yeye. Hapa utakuwa unamsoma akili yake iwapo anaweza kustahimili chat yako. Akitaja anapenda kuvaa kanga, jaribu kuichafua akili yake kwa kumuuliza iwapo amenyeshewa na mvua akiwa amevalia kanga(ama nguo yeyote) angejihisi vipi.

6. Ushawahi hata mara moja kumuona mtu mwengine akifanya ngono kwa bahati mbaya?
Swali kama hili linawaweka nyote katika hisia za kupandwa na nyege lakini mnaliweka swali hili kwa mtu wa tatu ili liwazuie mjiskie huru kuendeleza na chat yenu.

7. Ushawahi kushikwa matiti na mtu yeyote kibahati mbaya wakati mmesimama mahali hadharani penye watu wengi?
Swali kama hili linaweza lisimshangaze mwanamke kwa sababu wanapitia mambo kama haya. Akikubali, mjibu ungetamani kuwa ni wewe umemshika kibahati mbaya. Akijibu kwa kucheka ujue mchezo unaenda sambamba.

8. Ushawahi kufanya ngono na jamaa kwa sababu ya kuwa ulikuwa na nyege?
Fanya kumfahamu kama ni mwanamke ambaye anaweza kufanya ngono na mwanaume wakati ambapo anapoingiwa na nyege. Wanawake wengi wanaweza kukataa kujibu hili swali lakini ukiona amekujibu vizuri basi inaonyesha kuwa mwanamke huyu yuko tayari kujibu swali lolote lile ambalo umemwandalia.
9. Kwa bahati mbaya ukimwona mwanaume akiwa uchi ungependa kuona sehemu gani yake ya mwili kuanzia mabega kushuka chini?
Sasa hapa umeanza kuwa mkorofi kwa kuanza kumuuliza maswali ya kiujanja. Hii itamfanya yeye aonekane ndiye anatumia maneno machafu na wala si wewe.

10. Unapenda gani kati ya boxer ama chupi?
Hili ni swali na kumchanganya tu. Akikujibu anapenda boxer mwambie umevalia nini. Hapa kutamfanya aanze kufikiria vile umevalia. Ataanza kukuwaza ukiwa umevalia boxer ama chupi pekee.

11. Siri yako ni ipi ya kumpagawisha mwanaume kihisia?
Kwa kumuuliza hivi utamfanya yeye kufikiria akifanya mapenzi na mwanaume na atakuwa akikuelezea. Hii itamfanya yeye kuingiwa na mawazo ya ngono. Wakati uo huo anaweza kukueleza zaidi kuhusu kwa nini yeye ni bingwa wa kupagawisha mtu.

12. Kama kuna sehemu ambayo mwanaume anayoweza kukugusa na kukufanya kuingiwa na unyevu ingekuwa ni ipi?
Hili ni swali la moja kwa moja ambalo litamfanya kupandwa na kuingiwa na nyege. Kama atalijibu na ukweli wake wote, basi fahamu ya kuwa atakuwa amepandwa na nyege.

13. Je ukipapaswa mwili mzima unaweza kuingiwa na unyevu?
Wanawake wengi wakipapaswa vizuri kwa kawaida huingiwa na unyevu.  Hivyo unaweza kumjibu kuwa wewe una ustadi wa aina hio so ukikutana na yeye hilo ndilo jambo la kwanza la kumfanya ili kumsisimua.

14. Kama nimekupiga busu kwa bahati mbaya wakati nakuaga, utanichukulia vibaya?
Swali kama hili litamfanya kuanza kufikiria busu lako kama lingekuwaje.

15. Mwili wangu ungeuona wa kuvutia ukiwa na manywele ama ukiwa umenyolewa?
Swali kama hili fasta litampa taswira ya wewe ukiwa uchi kwa madakika fulani akikuona ukiwa na manywele ama umenyolewa.

16. Kama wataka kufanya mapenzi na mwanaume ungependa wewe kuanza ama yeye?
Swali hili litamfanya afikirie akiwa uchi tayari kufanya ngono.

17. Kitu gani mwanaume anachofaa kukufanyia ili uingiwe na unyevu?
Hapa unaingia direct kwa swali ambalo ni tamu. Akikujibu vizuri unafaa urudie tena swali la 12 ili apate kukuelezea kwa kina.

18. Kama ningekuwa nakunongonezea maswali haya yote kwa sikio lako, je ningekusisimua kihisia?
Kama umeifanya hii chat imeenda vizuri, kufikia sasa inafaa kuwa huyo mwanamke ameingiwa na unyevu kitambo. So kwako ni kumsikia mwenyewe kama atakujibu nini.

19. Kama haungekuwa na boyfriend, je mimi na wewe tungeweza kufaana? ? Kama ningekuwa na wewe sahizi tungeweza kulana dende?
Swali kama hili laweza kukufanya ulazwe kwa kitanda, lakini hili swali la mwisho ndio litafunga mchezo
20. Kama mwanaume yeyote muda huu angekuja sehemu unayoishi na kufanya ngono na wewe ungeipenda?
Usijizungumze kuhusu wewe wakati unapomuulizwa maswali kama haya. Lazima uhakikishe ya kuwa anakutaka. Akijibu 'ndio' kimbia fasta kushinda fastjet hadikwa nyumba anayoishi. La sivyo, hakikisha kutumia mbinu nyingine za ushawishi hadi atakapokuruhusu uende nyumbani kwake


Na Mwandishi Wetu, Mahakama ya Tanzania.

Mahakama ya Tanzania ni moja kati ya Taasisi iliyopo katika mchakato wa kuboresha huduma zake. Katika kufanikisha azma hii jitihada/maboresho mbalimbali yameendelea kufanyika ili kuwezesha Mhimili huu muhimu kuwa na mazingira rafiki ya utoaji haki kwa wananchi.

Hivi karibuni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman alitembelea katika Mahakama za mikoa ya Iringa, Njombe pamoja na Ruvuma, lengo la ziara ikiwa ni kukagua na kujionea hali ya utendaji wa Mahakama na mwenendo wa uendeshaji wa mashauri.
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Wilaya ya Songea.
 
Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu alipata nafasi ya kutembelea Mahakama Kuu Songea, Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea, Mahakama ya Wilaya Songea. Mahakama ya Wilaya Mbinga, Mahakama ya Wilaya Nyasa inayotarajiwa kuanza kazi hivi karibuni na baadhi ya Mahakama za Mwanzo.

Mhe. Jaji Mkuu aliongozana na Watendaji wengine wa Mahakama katika ziara yake ambao ni; Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Msajili Mkuu pamoja na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Wote walipata fursa ya kujionea hali halisi ya miundo mbinu ya Mahakama ikiwa ni pamoja na kupata taarifa za Mahakama hizo kutoka kwa Jaji Mfawidhi/Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hizo. 
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (wa kwanza kushoto) akipata taarifa fupi ya Mahakama Kanda ya Songea kutoka kwa Mhe. John S.Mgetta, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Songea (aliyesimama), mara baada ya kuwasili Mahakama Kuu kanda ya Songea.

Akisoma taarifa yake mbele ya Mhe. Jaji Mkuu, Mhe. John Mgetta, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Songea alisema kuwa Kanda yake ina Mahakama Kuu moja (1), Mahakama ya Hakimu moja (1) ya Mahahakama za Wilaya tano (5) ambazo ni Songea, Namtumbo, Tunduru, Mbinga na Mahakama ya Wilaya Nyasa.

Hata hivyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. John Mgetta alikiri Mahakama yake kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi hususani Makarani na ubovu wa majengo ya Mahakama, kwani hayatoshi na ni machakavu.

Mhe. Jaji Mkuu, Kanda ya Songea inakabiliwa na uhaba wa watumishi, hususani makarani. Ukiachia mbali changamoto hii tunakabiliwa pia na uchakavu wa miundombinu ya majengo.
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania (kushoto), Mhe. John S.Mgetta Jaji Mfawidhi Kanda ya Songea (kulia), wakisoma majalada ya kesi katika Mahakama ya Mwanzo Kigonsera mkoani Songea.

 “Mhe. Jaji Mkuu, majengo mengi yanayotumiwa na baadhi ya Mahakama mfano Mahakama Hakimu Mkazi na Wilaya za Songea pamoja na Mahakama nyingi za Mwanzo ni ya kuazima. kwa ujumla hali ya majengo ya Mahakama katika Kanda hii si ya kuridhisha, Mahakama nyingi zina majengo mabovu sana, hasa Mahakama za Mwanzo, ama yanahitaji ukarabati mkubwa au kubomolewa na kujengwa upya,” alieleza Mhe. Jaji Mgetta.

Licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa, Mahakama Kanda ya Songea ni moja ya Kanda inayoongoza nchini kwa umalizaji wa Mashauri yanayofunguliwa katika Mahakama mkoani humo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Tehama, Mahakama ya Tanzania, Bw. Machumu Essaba alisema kwa mujibu wa Takwimu za uondoshaji wa Mashauri nchini, Kanda ya Songea ndio inayoongoza kwa kasi kubwa ya kumaliza kwa wakati kesi zinazofunguliwa.

“Napenda nikiri kuwa Kanda ya Songea ndio Kanda inayoongoza kwa uondoshaji wa Mashauri, hii inatokana na jitihada zifanywazo na Majaji na Mahakimu wa Mahakama katika kanda hiyo,” alisema Essaba.
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Songea ina jumla ya Majaji wawili tu na kuongeza kuwa kila Jaji anawastani wa mzigo wa kazi (work load) wa kesi 215 kwa kila mmoja. 

Alisema; uwezo wao wa kumaliza mashauri yanayofunguliwa (clearance rate) ni 154% na kila kesi iliyofunguliwa ilimalizika kwa wakati kwa asilimia 100% huku wakiendelea kutoa maamuzi ya kesi za zamani kwa asilimia 54%.
Kwa upande wa Mahakama ya Mkoa/Hakimu Mkazi, Mkurugenzi Msaidizi huyo alisema Mahakama hiyo haina kesi yenye Zaidi ya miezi 18 Mahakamani na kuongeza kuwa Mahakama hiyo ina jumla ya Mahakimu wanne (4) wenye wastani wa mzigo wa kazi wa kesi 117 na uwezo wao wa kuondoa mashauri yanayoingia ni asilimia 112, na kuongeza kuwa utendaji huu unarudisha Imani ya Mahakama kwa wananchi.

Bw. Essaba aliendelea kueleza juu ya utendaji wa Mahakama katika Kanda ya Songea, kwa kuongeza kuwa kuna jumla ya Mahakama za Wilaya nne (4) Mahakama zote zikiwa na jumla ya Mahakimu sita (6) na kila mmoja ana wastani wa mzigo wa kazi ‘workload’ wa kesi 186 na uwezo wao wa kuondoa kesi zinazofunguliwa ni asilimia 135 na kupelekea kumaliza mlundikano wa mashauri katika Mahakama hizo.

Bw. Essaba alimaliza kwa kuongelea juu ya Mahakama za Mwanzo zilizopo Kanda ya Songea ambazo jumla yake ni 45 na kuongeza kuwa Mahakama hizo zina jumla ya Mahakimu 52 ambapo kila mmoja ana mzigo wa kazi wa kesi 157 na uwezo wao wa kuondoa kesi zinazofunguliwa kwa Mahakama zote za Mwanzo ni 104.

“Hakuna kesi/shauri lolote lililokaa kwenye Mahakama hizo zaidi ya mwaka mmoja, kwa ujumla Kanda ya Songea ni moja ya kielelezo cha utendaji uliotukuka katika Mahakama ya Tanzania,” alisisitiza Essaba.

Hata hivyo; Mahakama ya Tanzania kwa ujumla wake ipo katika mchakato wa maboresho, ulioanza muda wa takribani miaka mitatu sasa wa kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kuondosha mashauri ya muda mrefu Mahakama na kutoruhusu Mashauri kukaa Mahakamani Zaidi ya miaka miwili (2).

Kwa upande wake Mhe. Jaji Mkuu, aliupongeza uongozi wa Mahakama Kanda ya Songea kwa jitihada zao za dhati katika kuhakikisha wanatoa haki kwa wakati, na kuongeza kuwa hali hii inawapa Imani wananchi na kuifanya Mahakama kuwa kimbilio lao katika upatikanaji wa haki.
Kwa upande wao Watendaji walioambatana na Mhe. Jaji Mkuu katika ziara yake walisema wamefarijika sana na kasi ya Kanda ya Songea kwa uondoshaji wa Mashauri na kudai kuwa hali hii imesababisha hata idadi ya wafungwa/mahabusu gerezani kupungua.
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati, akipitia jalada moja baada ya jingine kuona hali halisi ya utoaji haki kwa Wananchi katika Mahakama ya Mwanzo Kigonsera mkoani Songea.
“Binafsi nimefarijika sana na mabadiliko tuliyoyaona Songea, idadi yawafungwa imepungua ghafla na wananchi walio wengi wanaonekana kufurahia na kusifu jitihada hizi za Mahakama mkoani Ruvuma,” alisema Mhe. Katarina Revokati, Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania.
Pamoja na jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanyika kuboresha huduma za Mahakama nchini, Mhe. Jaji Mkuu aliwasihi watumishi kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi na kanuni zilizowekwa.
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, (katikati), Mhe. John Mgetta, Jaji Mfawidhi- Mahakama Kuu Kanda ya Songea (wa pili kushoto), Mhe. Salima Chikoyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania (wa kwanza kushoto), Mhe. Katarina Revocati, Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu wa Mkoa wa Songea.



Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.


MKOA Mwanza waongoza kuwa na watumishi  hewa 334  ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha kwa kuwa na watumishi hewa 270 ikiwa nchi nzima na watumishi  hewa 2,702.

Hata hivyo Shinyanga na Songwe ni mikoa isiyo kuwa na watumishi hewa kukosekana kwa watumishi hewa katika mkoa wa shinyanya imetokana na mikakati ya mikoa hiyo kila idara kupeleka majina ya watu wanaostahili kulipwa mishahara kila mwezi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Killango kuwa viongozi walioanza katika mikoa huo walijipanga katika kuondokana na watumishi hewa.
Mkoa wa Songwe kukosekana kwa watumishi hewa kunatokana na upya wake na mkuu wake mkoa ameapishwa wiki moja iliyopita.

Akizungumza na Wakuu wa Mikoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene aliwataka wakuu wa mikoa wafanye kazi ikiwemo ubunifu wa miradi ya kuongeza mapato.

Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa kuondokana na matumizi yasio na ulazima ili fedha hizo zitumike katika matumizi ya msingi.

Amesema kuwa zoezi hilo liweze kuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kushughulika na watoro ambao wanalipwa fedha wakati hawafanyi kazi,
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema wote ambao wamehusika na hujuma za mishahara wafikishwe katika vyombo vya dola na mkoa wake umeanza kutekeleza.
 Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Mikoa leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza baada ya kukabidhi majina hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadik  akikabidhi majina hewa kwa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  akizungumza Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene  baada ya kumkabidhi majina watumishi hewa , jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Aggrey Mwanri akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.

Wakuu wa Mikoa na Watendaji wa TAMISEMI wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Balozi Seif Ali Iddi akipeana mkono wa hongera na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi kabla Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kumuapisha kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipeana mkono wa hongera Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid akiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (kushoto) wakati wa kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushika nafasi hiyo leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipitia hati ya kiapo kabla ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kumuapisha rasmi kushika nafasi hiyo aliyomteuwa,hafla ya kiapo ilifanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar(kushoto) Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
Washauri wa Rais wa Zanzibar wa mambo mbali mbali ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Mjini Unguja.
Balozi Seif Ali Iddi akielekea sehemu ya kula kiapo kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipoapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akibadilishana mawazo na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kumuapisha rasmi leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Mwanasheria Mkuu wa zanzibar Mhe,Said Hassan Said (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (katikati) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid wakiwa katika hafla ya kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushika nafasi hiyo leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto) akiwa na Viongozi waliohudhuria kuapishwa kwake leo,(wa pili kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mama Asha Suleiman Iddi baada ya kumuapisha Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar leo katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar,(Picha na Ikulu.]


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.

Mkataba wa pili  unahusu masuala ya kiufundi  yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba uliosainiwa  Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.

Katibu Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.

Balozi Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji  kuwekeza nchini Tanzania.

Adha Balozi Yoshida amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akikisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
==

Wednesday, March 23


Wahariri wa vyombo vya habari za kidini wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya kimafunzo mkoani Pwani, ziara hiyo imeandaliwa na TACAIDS .
Mhariri wa Habari kutoka Radio Maria Bi. Judidh Francis akiongea jambo katika ziara ya wahariri wa vyombo vya habari vya kidini katika kituo cha afya cha utoaji huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze,ziara hiyo imeandaliwa na TACAIDS 
Mhariri wa Habari kutoka Radio Sauti ya Quran Bw. Sadiki Faki akiongea jambo katika ziara ya wahariri wa vyombo vya habari vya kidini katika kituo cha afya cha utoaji huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze,ziara hiyo imeandaliwa na TACAIDS .
Mratibu wa TACAIDS mkoani Pwani Bw. Badru Abdunuru akiwafafanulia jambo wahariri wa vyombo vya kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika mkoani pwani katika Kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze .
Mratibu wa TACAIDS mkoani Pwani Bw. Badru Abdunuru akiwafafanulia jambo wahariri wa vyombo vya kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika mkoani pwani katika Kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze .
Mratibu wa TACAIDS mkoani Pwani Bw. Badru Abdunuru aliyesimama kulia akiwafafanulia jambo wahariri wa vyombo vya kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika mkoani pwani katika Kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze .
Msimamizi wa kituo cha Maarifa kwa ajili ya kutoa huduma za VVU kwa madereva wa masafa marefu wa kwanza kushoto aliyekaa mbele Bi. Amina Chandima akiwafafanulia jambo wahariri wa vyombo vya kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika mkoani pwani katika Kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze .
Wahariri wa vyombo vya habari za kidini walipotembelea kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU mkoani Pwani, Wilayani Kibaha .
Mhariri wa Tumaini Media Bw. Martin Kuhanga akiongea jambo wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari vya kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika katika Kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze .
Msimamizi wa utoaji wa huduma za tiba na ushauri kwa watu wanaoishi na VVU kutoka Wilaya ya Kibaha Daktari Robert Mwakyusa akiongea jambo na wahariri wa vyombo vya habari za kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika mkoani pwani.

 Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya akizungumza na viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini ya mradi wa Maji Yetu uliofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji uliogharimu shilingi Bilioni 14.5 alipokutana nao leo jijini Dar es salaam.
Mshauri wa Ufundi wa DAWASA BTC  Mhandisi Praygod Mawalla akitoa elimu kwa viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji katika jiji la Dar es salaam namna ya kuifanya miradi wanayoisimamia ijiendeshe na kuwa endelevu kwa manufaa ya wananchi.
Mshauri wa Ufundi wa DAWASA BTC  Manjolo Kambili akitoa akitoa ufafanuzi kuhusu Programu ya za utoaji wa mafunzo kwa watumiaji wa Maji katika maeneo yenye miradi hiyo wakati wa mkutano na viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji za jiji la Dar es salaam.

Viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini ya mradi wa Maji Yetu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na watendaji wa DAWASA leo jijini Dar es salaam.

Afisa Uhusiano na Jamii  wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi. Mecktridis Mdaku Mtaalamu kutoka akiwasisitiza viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji katika jiji la Dar es salaam kupanda miti na kuiendesha miradi katika hali ya Usafi ili kulinda afya za watumiaji wa huduma za maji.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa DAWASA Bi. Mary Ntikula akipanda mti mara baada ya mkutano na viongozi wa Jumuiya ya Watumia Maji Dar es salaam kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji na Utunzaji wa Mazingira. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya
Baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji jijini Dar es salaam.


       Na. Aron Msigwa Dar es salaam.

Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) imewataka viongozi wa Jumuiya za watumia maji katika jiji la Dar es salaam na  baadhi ya maeneo ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani kusimamia kikamilifu mapato na matumizi ya miradi ya maji ili kuepuka migogoro inayosababishwa na matumizi mabaya ya fedha jambo linalochangia baadhi ya miradi kushindwa kujiendesha na kuwa kero kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka hiyo Bi.Neli Msuya wakati akitoa elimu kwa viongozi hao kuhusu uendelezaji wa miradi inayosimamiwa na Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini ya mradi wa Maji Yetu kwa ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji.

Amesema DAWASA imekukutana viongozi hao kuwakumbusha wajibu walio nao katika kuhakikisha miradi wanayoisimamia inakidhi matarajio ya wananchi kwa kutoa huduma bora na kujiendesha kwa faida kwa na kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Kwa kuzingatia idadi ya watu zaidi ya Laki mbili (200,000)  wanaohudumiwa na mradi huu kwa kupata maji safi na salama na gharama kubwa iliyotumika kuanzisha mradi huu shilingi Bilioni 14.5 ,tumeona kuna umuhimu wa kuendelea kuweka msisitizo wa uangalizi kwa kuwa miradi hii ni muhimu na iko kwa wananchi Amesisitiza.

Amewaeleza viongozi hao kuwa majukumu ya DAWASA kama mmiliki wa miundombinu ya majisafi na majitaka ni kugharamia matengenezo makubwa na kufanya uwekezaji wa kupanua miundombinu ya majisafi na majitaka jijini Dar es Salaam na maeneo yaliyoainishwa chini ya Sheria ya DAWASA Namba.20 ya Mwaka 2001.

Bi. Neli amefafanua kuwa DAWASA iliingia mkataba wa uendeshaji na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) kutoa huduma ya uondoshaji wa majitaka katikA jiji la Dar es salaam, Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

Aidha, amesema kupitia mkataba huo,  DAWASCO huuza maji kwa wateja, kutayarisha Ankara za maji, kukusanya maduhuli, kulipia gharama za uendeshaji na kufanya matengenezo ya mfumo mzima wa usambazaji maji na uondoshaji majitaka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. 

“Kupitia elimu inayotolewa leo mtagundua kuwa ninyi ni muhimu katika kuwahudumia wananchi, mtaona kuwa ninyi ni DAWASCO ndogondogo kwenye maeneo yenu kwa kuwa mnauza maji kwa wateja, mnatayarisha Ankara za maji , mnakusanya fedha za malipo ya huduma mnafanya matengenezo ya mifumo ya maji kwa wateja wenu” Amesisitiza.

Amesema kwa sasa DAWASA imewekeza kwenye miradi mikubwa na kupanua chanzo cha Maji cha Ruvu chini ambacho huzalisha lita milioni 270 kwa siku, ujenzi wa Bomba kubwa lenye urefu wa Kilometa 56 kutoka Ruvu Chini hadi matenki yaliyopo chuo Kikuu Ardhi jijini Dar es salaam.

Aidha amesema kwa upande wa Ruvu juu maboresho makubwa yamefanyika kwa kupanua mitambo ya uzalishaji ambayo sasa itazalisha lita milioni 196 kutoka milioni 82 kwa siku.

Ameongeza kuwa upande wa maeneo ya kaskazini na kusini mwa jiji la Dar es salaam kuelekea wilaya ya Mkuranga DAWASA inaendelea kuwekeza katika uchimbaji wa visima virefu vya maji na kuweka mifumo ya usambazaji wa maji ili kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake Mshauri wa Miradi ya Maji kutoka DAWASA BTC Bw. Manjolo Kambili amewaeleza viongozi hao kuwa wao kama viongozi wa Jumuiya za watumia maji wanatakiwa kufuata sheria na taratibu za Serikali kwa kuwa miradi hiyo ni ya Serikali.

Ameeleza kuwa jukumu la kusimamia na miradi hiyo liko kisheria hivyo viongozi hao wanapaswa kutekeleza kikamilifu majukumu yao likiwemo la kuhakikisha kuwa miradi yote inaajiri wahasibu wenye taaluma kwa lengo la kuandika na kutunza kumbukumbu za kila siku zinazohusu mapato na matumizi yao.

Naomba nisisitize katika hili, nyie mmepewa jukumu la kusimamia miradi ya maji ya Serikali, lazima mlitambue hili miradi yenu itakaguliwa na wataalamu ndio maana tuliwaomba muajiri wahasibu kwa kuwa vitabu vyenu vitakaguliwa kujua mwenendo wa mapato na matumizi yenu Amesisitiza.
Amewataka viongozi hao kuhakikisha kuwa kila mradi wa jumuiya unakuwa na akaunti ya Benki pamoja na kusimamia suala la utoaji wa risiti halali zenye nembo za jumuiya husika ili kuweka uwazi na imani wa walipiaji Ankara za maji.

Naye Afisa Uhusiano na Jamii wa Mamlaka hiyo Bi. Mecktridis Mdaku amewasisitiza viongozi hao kusimamia suala la Usafi wa mazingira, upandaji wa miti na utunzaji wa  vituo vya miradi, majengo na miundombinu ya maji ili kuwakinga wananchi dhidi ya magonjwa ya milipuko  ikiwemo. 

Ninyi kama viongozi wa Kamati za miradi ya maji lazima msimamie suala la usafi wa mazingira ili maeneo ya miradi yavutie pia kuwakinga wateja wenu na ugonjwa wa kipindupindu  Amesisitiza Bi. Mdaku.Ametoa wito kwa viongozi hao kuepuka kuyatumia majengo ya miradi ya maji ya wananchi kwa shughuli nyingine  nje ya maji ikiwemo kuhifadhi na kufanyia biashara ya mkaa.  
MWISHO.
-