Friday, January 22


Wakati vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vikitarajiwa kuanza leo kwa uteuzi wa wajumbe, wabunge wa upinzani tayari wameanza kwa kumtikisa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai, baada ya kususia uchaguzi wa wenyeviti wa kamati hizo.

Dalili za mgawanyiko kwenye kamati hizo zilianza kuonekana juzi, baada ya wabunge hao wa Kambi ya Upinzani kufanya kikao na kuweka msimamo wa kutaka kushirikishwa kwenye uteuzi wa wajumbe.

Kambi ya Upinzani ilisema inataka kushirikishwa katika hatua hiyo ikidai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), imekuwa ikiwapangia watu wa kuongoza kamati zinazosimamia mapato ya serikali ambazo kikanuni zipo chini yao.

Viongozi hao wa kambi ya upinzani walidai kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakipangiwa watu wa kuongoza Kamati ya Hesabu za Serikali za (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ambazo kikanuni zinatakiwa kuongozwa na upinzani.

Baada ya Ofisi ya Bunge kutangaza majina ya wajumbe wa kamati, Kambi ya Upinzani Bungeni ilikutana na waandishi wa habari, lakini wakaahirisha kwa madai kuwa wamegundua kwamba orodha ya majina yaliyotoka, yana matatizo mengi zaidi.

“Tumegundua kwamba matatizo hayapo kwenye kamati ya PAC na LAAC tu, kwenye kamati nyingi kuna matatizo kwa hiyo kwa sasa viongozi wa kambi wanakutana kujadili na kuchambua taarifa iliyotolewa baadaye tutakutana na wabunge wote kisha kesho tutatoa msimamo wetu,” alisema Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, John Mnyika.

Baada ya kauli hiyo, Mnyika aliulizwa inakuwaje wao wanaendelea na vikao wakati wenzao wa CCM wakiwa kwenye uchaguzi:

“Siwezi kujibu chochote, neno lolote nitakalosema, nitaingilia hicho kinachojadiliwa na viongozi. Wewe subiri kwanza tumalize kikao, tutoke na msimamo wa pamoja na kesho tutawaeleza msimamo wetu,” alisema Mnyika.

Awali, kabla ya kutolewa kwa majina hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya, alisema kwa muda sasa wamekuwa wakichaguliwa watu wa kuongoza kamati hizo na CCM.

“Ni sawa na mtu anakupa kitu kwa mkono wa kushoto na kukunyang'anya kwa mkono wa kulia. Ndiyo maana tukataka tushirikishwe kuanzia wajumbe watakaokuwa kwenye kamati hizo,” alisema Sakaya ambaye ni Mbunge wa Kaliua mkoani Tabora.

Kanuni za Kudumu za  Bunge Toleo la Aprili 2013, inasema: “Wenyeviti wa Kamati za Bunge zinazosimamia matumizi ya fedha za Umma ambazo ni Kamati ya Hesabu za Serikali, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, watachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe wa kamati hizo ambao wanatoka katika Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.”

==>Kauli ya Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Zitto Kabwe ambaye bunge lililopita alikuwa mwenyekiti wa PAC ameandika;
  
"Kamati zote za Bunge zina hadhi sawa ndani ya Bunge. Kila mbunge ana haki ya kuwa kwenye kamati yeyote ile na hakuna mbunge bora zaidi ya mwingine.

"Kanuni zimeweka utaratibu wa uteuzi kwenye Kamati ikiwemo maombi ya mbunge, uzoefu na ujuzi wa eneo husika.

"Wanaolalamika leo upangaji wa Kamati ndio usiku wa kuamkia jana walimshinikiza Spika asiwapange mahasimu wao kisiasa kwenye Kamati wanazoona wao ni nyeti.

"Ni unafiki uliopitiliza unapojenga hoja ya uzoefu, chaguo la Mbunge na ujuzi wakati huo huo wenye vigezo vyote hivyo unawapiga vita kwa sababu za kisiasa
 
"Ni dhahiri kuwa mpangilio wa Kamati unajenga Bunge kibogoyo,  Nilitahadharisha toka Bunge la 11 lilipoanza kwamba, "kuna dalili za Serikali kutaka kulidhibiti Bunge ( kumbukeni sarakasi za Tulia Ackson ambaye sasa ni Naibu Spika) . "

"Kiongozi unapokwenda kwa Spika kusema 'fulani asipangwe Kamati fulani kwa sababu atapata sifa' halafu ukataka 'nyumbu' wako ndio wapangwe huko ujue unaisadia Serikali kudogosha Bunge.

"Spika anapoamua Nyote, huyo usiyemtaka na nyumbu wako wasiende huko ujue amekudharau sana.
 
"Unapoona Viongozi wa Serikali wanahangaika kupanga Kamati za Bunge watakavyo wao ujue viongozi hao ni dhaifu, hawana nia njema na hawataki kuwajibishwa.

"Twendeni kwenye hizi hizi Kamati tulizopangiwa kuwafanyia kazi Watanzania. Twendeni tukaonyeshe kuwa Bunge litabaki Bunge tu na Wabunge tusikubali Bunge Kibogoyo. Ni lazima Bunge lidhibiti Serikali hata Serikali hiyo ikiwa inaongozwa na Malaika.

"Serikali ni chombo cha mabavu lazima idhibitiwe, na ndio kazi ya Bunge kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 63."

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali iliyopita, Bernard Membe ameungana na waziri mwenzake wa zamani, Dk Makongoro Mahanga kukosoa sera ya kubana matumizi ya Rais John Magufuli ya kudhibiti safari za nje na kuteua baraza dogo la mawaziri.

Kama ilivyokuwa kwa Dk Mahanga, waziri huyo aliyedumu kwa miaka tisa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje amesema kiuhalisia, Rais hajapunguza idadi ya wizara kama alivyosema bali amepunguza “idadi ya mifuko”, huku akisisitiza kuwa mkuu huyo wa nchi atalazimika kutoka nje “atake asitake”.

Membe amekuwa waziri wa pili wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kukosoa sera ya kubana matumizi ya Serikali ya Awamu ya Tano baada ya Dk Mahanga, ambaye sasa amehamia Chadema, kumkosoa akisema idadi ya wizara inapimwa kwa kuangalia makatibu wakuu na si wizara na hivyo ukubwa wa Baraza la Mawaziri bado uko palepale.

Akiongea na Gazeti la Mwananchi, Membe alikuwa na maoni kama hayo na akaenda mbali zaidi kuzungumzia hata sera ya kudhibiti safari za nje na Rais kujizuia kusafiri, akisema “Tanzania haiwezi kuishi kama kisiwa” katika dunia ya leo.

Membe, ambaye alikuwamo kwenye kinyang’airo cha urais na kufika hadi tano bora, alisema Rais hajabana matumizi yoyote kwa kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri, bali alichofanya ni kupunguza idadi ya mawaziri na siyo wizara.

“Alichofanya ni sawa na kuwa na mayai kumi halafu ukaamua kuyaweka kwenye mifuko kumi, maana yake ni kwamba utakuwa na mifuko kumi yenye mayai,” alisema Membe.

“Lakini unaweza kuwa na idadi hiyo hiyo ya mayai na ukaamua kuyagawanya; mayai matatu unayaweka kwenye mfuko mmoja, mawili kwenye mfuko mwingine na yaliyobaki kwenye mfuko mmoja. Maana yake ni kwamba utaendelea kuwa na mayai kumi lakini idadi ya mifuko imepungua. Hapa sasa utakuwa hujapunguza gharama za kuyatunza hayo mayai.”

Rais aliahidi kwenye kampeni na hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge kuwa atapunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri ili kubana matumizi. Alitekeleza ahadi yake kwa kuunda baraza lenye mawaziri 34 tofauti na lililopita ambalo lilikuwa na mawaziri 55.

Upunguzaji huo wa baraza ulifanywa kwa kuunganisha wizara na hivyo kufanya makatibu wakuu, ambao ni maofisa masuhuli wa wizara kuwa zaidi ya mmoja kwenye baadhi ya wizara.

“Ameendeleza wizara zilezile, lakini akaamua kuzikusanya pamoja. Hiyo haimaanishi kuwa atakuwa amepunguza gharama za uendeshaji wake,” alisema Membe.

“Hilo tutaliona kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka huu. Tuone kama bajeti itaongezeka au itapungua? Kwa sababu kama wizara zimepungua kama tunavyoamini, lazima bajeti ipungue, sasa bajeti ikiongezeka au ikibaki vilevile maana yake hakuna kilichofanyika.”

Membe alitoa mfano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo sasa inaitwa “Wizara ya Mambo ya Nje, Kikanda na Ushirikiano wa Afrika Mashariki”, akisema itapaswa kuwa na bajeti mbili; ya Mambo ya Nje na Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kinyume chake ni vigumu kuiendesha.

Membe alikiri kuwa hata yeye angeingia kwenye mtego wa kupunguza idadi ya wizara kama angefanikiwa kuchaguliwa kuwa Rais kama ilivyokuwa nchini Namibia ambako wizara zilipunguzwa kutoka 32 hadi 20.

“Baadaye nikagundua kuwa hata Namibia yenyewe inajuta,” alisema.

Alisema siku ya kuapishwa Rais Magufuli, alikutana na Makamu wa Rais wa Namibia, Nickey Lyambo na baada ya kusalimiana na kumpongeza kwa hatua ya kupunguza wizara, kiongozi huyo wa Taifa hilo la kusini mwa Afrika alimweleza kuwa uamuzi huo umewasababishia matatizo makubwa bungeni

“Aliniambia katika Bunge la Namibia kuna mjadala mkali wa kutaka wizara ziongezwe,” alisema Membe akimnukuu makamu huyo wa rais wa Namibia.

Membe alibainisha kuwa kwa Tanzania, mfumo huo mpya wa wizara pia unaweza kuathiri uwasilishaji wa bajeti bungeni kwa kuwa mawaziri sasa watahitaji muda mwingi zaidi kuliko ilivyokuwa awali ili kuzungumzia wizara kadhaa zilizounganishwa, jambo ambalo lililalamikiwa pia na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu.
“Kila kitu kina form na content (muundo na maudhui). Alichofanya Rais Magufuli ni kubadili form na siyo content ya wizara, wizara ni zilezile na mzigo ni uleule,” alisema.

Mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi, pia alikosoa udhibiti wa safari za nje, akisema Tanzania si kisiwa.

Alikuwa akijibu swali lililomtaka aeleze uhalisia wa mpango wa Rais Magufuli kubana matumizi kwa kufuta safari za nje za mawaziri na watumishi wengine wa umma.

Mara tu baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli alifuta safari zote za nje ya nchi kwa watendaji na watumishi wa umma, isipokuwa zile tu ambazo zingepata kibali cha Ikulu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kubana matumizi ya Serikali.

Rais Magufuli alisema katika hotuba yake ya kuzindua Bunge kuwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2015, safari hizo ziliigharimu Serikali Sh356.3 bilioni na kwamba kati ya fedha hizo, Sh183.1 bilioni zilitumika kwa ajili ya tiketi za ndege, Sh68.6 bilioni kwa ajili ya mafunzo na Sh104.5 bilioni kwa ajili ya posho.

Bila kugusia madhara ya kufuta safari hizo, Rais Magufuli alijielekeza zaidi kwenye matumizi ya fedha ambazo angeokoa.

“Lakini tujiulize fedha hizo zingeweza kutengeneza zahanati ngapi? Zingeweza kutengeneza nyumba za walimu ngapi? Zingeweza kutengeneza madawati mangapi? Zingeweza kununua dawa hospitalini tani ngapi?” alihoji Rais Magufuli katika hotuba yake iliyotoa mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Lakini Membe, ambaye wizara yake iliwahi kutetea safari za Jakaya Kikwete nje ya nchi baada ya wapinzani kusema ziligharimu zaidi ya Sh4 trilioni, alisema safari za nje zina umuhimu kwa taifa lolote.

“Tanzania si kisiwa, hata ukiwa tajiri namna gani lazima utoke nje ya nchi yako,” alisema Membe ambaye ana shahada ya umahiri ya uhusiano wa kimataifa aliyoipata Marekani.

“Lazima utakwenda mwenyewe au mawaziri wako na hasa Waziri wa Mambo ya Nje kwa sababu kuna vikao nje ya nchi ambavyo mabalozi hawaruhusiwi kuingia.

“Ukijaribu kujifanya kisiwa utakuwa kama Zimbabwe. If you isolate yourself you will be isolated (ukijitenga, utatengwa).”

Membe alisema nchi ina mabalozi 36 tu duniani kote kati ya nchi 194 zinazohitaji uwakilishi huo na kibaya zaidi, mabalozi hawaruhusiwi kuingia kwenye baadhi ya vikao, na hata wakiingia wakifika kwenye hatua ya uamuzi watazuiwa kushiriki.

“Kwa mfano, Uturuki hatuna ubalozi, sasa unapoona ndege inaleta watalii kutoka Uturuki, unadhani Bunge la Uturuki liliketi kutuletea watalii Tanzania? Hapana. Tulitoka nje na kuwashawishi wakaja,” alisema Membe aliyewahi kueleza kuwa wakati wa awamu ya Rais Jakaya Kikwete mawaziri walikuwa wanapishana angani kana kwamba kuna moto ardhini.

“Pia, leo unaposikia gesi, gesi, gesi nayo imepatikana nje ya ubalozi. Mawaziri walitoka nje ya nchi wakatafuta wawekezaji. Ni kazi ya wizara kufanya yote hayo.”

Membe alirudia kauli aliyoitoa siku chache kabla ya kuanza mchakato wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana kuwa lazima waziri wa mambo ya nje awe nje ya nchi kwa muda mwingi na ikitokea yuko ndani ya nchi kwa mwezi mmoja mfululizo, lazima ni mgonjwa.   

Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.

Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya Sanawali, Tekniko, Ngarenalo, Mbauda, Majengo Na Kisongo
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita Barabarani kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine kesho tarehe 23 Januari, anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.

 


Waandishi wawili wa habari, Simon Mkina na Jabir Idrissa walitoka mahabusu juzi, Jumanne jijini Dar es Salaam, ambamo waliswekwa baada ya gazeti lao, Mawio kufutwa na Serikali.
Wamepoteza gazeti. Wakaporwa uhuru kwa kuhojiwa na polisi mchana wote na sehemu ya usiku; na hatimaye kutupwa mahabusu.
Sasa kila siku ni kiguunjia, kuripoti polisi hadi watakapopelekwa mahakamani au kuambiwa ‘yameisha.’
Haya yote yanatokana na Serikali, kupitia Waziri wa Habari, Nape Nnauye kufuta gazeti la Mawio kwa madai kuwa linaandika uchochezi; na hivyo wahariri wake kuitwa wachochezi.
Mawio limekuwa likiripoti yaliyopo kwa njia ya uchunguzi kama wizi, migogoro na taharuki; mengi yakiwa yale yaliyosababishwa na watawala au wenza wao; na lengo likiwa kufahamisha umma na kuhimiza watawala kuchukua hatua.
Zawadi pekee kwa maripota na wahariri kwa jitahada zao za kuanika mambo na kuonya kabla hali haijawa mbaya, ni kuwaita wachochezi, kuwasaka kama wahalifu, kufuta gazeti lao na kuwasweka rumande.
Kumbe Serikali ina maana tofauti ya uchochezi. Tuangalie kauli zifuatazo na kuzilinganisha na maandishi ya gazeti linalotoa hadhari na lililofutwa.
Mara ngapi tumesikia kauli hii: “Ikulu mtaisikia redioni.” Ikiwa na maana kwamba hata mkishinda katika uchaguzi, hamtaingia Ikulu. Haya ni manukato? siyo uchochezi? Wanaoambiwa wajisikie vipi? Wafanye nini?
Umewahi kusikia hili? “Mapinduzi yalikuwa Unguja, hayakuwa Pemba; na Serikali itakuwa ya Unguja!”
Hivi wanaoambiwa kwa kauli ya kibaguzi na jeuri ya kifisadi, wanyenyekee na kusema “Insha Allah?” Wanafikiri nini? Wahusika ‘hawajafutwa’
Hili je? “Serikali ya Zanzibar haikupatikana kwa vikaratasi” na pengine wakisema “hatuwezi kutoa urais kwa makaratasi” – wakiwa na maana ya karatasi za kupigia kura na kuongeza, “Kama nanyi mnataka, basi pindueni.” Kauli chokozi inayotia kidole jichoni. Anayeambiwa ajisikie vipi? Wahusika ‘hawajafutwa.’
“Wewe (Maalim Seif), utaishia umakamu wa rais. Basi!” Anayeambiwa ndiye amekuwa akipigana kisiasa tena kwa utulivu; katikati ya propaganda kuu, kwamba “nchi yetu ni ya kidemokrasia na haina ubaguzi wa aina yoyote!” Soma kishindo cha radi ya kiangazi: “Mmekuja Unguja na njaa zenu; rudini kwenu!” Wanaoambiwa wanajisikiaje? Wafanye nini?
Waweke maneno pembeni na kuanzisha vita vya kuondoa ubaguzi; kwa misaada na ushirikiano kimataifa? Mhusika “hajafutwa.”
Eti nini? Sikilizeni anayejiita mnyofu. “…tutashinda hata kwa bao la mkono…” Ni kauli katikati ya vuguvugu la kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana. Ofisa wa “chama tawala” anatangazia taifa na dunia; kwa kiburi na jeuri isiyomithilika.
Anapeleka ujumbe gani kwa washindani kutoka vyama vingine? Anaeneza demokrasia? Anataka washindani wafanye nini? Anataka Tume ya Uchaguzi ikitangaza kuwa wameshindwa; wafanye nini na Serikali ijibu vipi? Mhusika “hajafutwa.”
Nina zaidi ya kauli 100 za aina hii zilizotoka vinywani mwa viongozi wa Serikali na chama kinachopanga Ikulu. Wahusika wanafyatua maneno kwa jeuri: Maneno ya kukera, kuudhi, kuchukiza, kutisha, kuchokoza, kudhalilisha, kubagua; yote kwa shabaha ya kuchochea majibu kwa njia ya mapigano – vita! Vyombo vya habari vimenukuu baadhi ya kauli hizi na nyingine zimesomwa katika maandiko mbalimbali; katika vijarida na mbao kwenye vijiwe vya vijana na wazee.
Wako wapi walio wakali sana ndani ya Serikali, wawezao kupambana na uchochezi huu, unaoweza kuangamiza Taifa? Uko wapi ‘mkono mrefu’ wa Serikali ambao hutamkwa kwa majigambo pale polisi wanapokuwa wakikimbiza “mwizi wa karanga.”
Upande huu kuna watoa kauli zinazotaka watu wachukie, wakasirike, waghadhibike; wachukue walichonacho na kuanza kumalizana; huku Serikali ikiwaangalia kana kwamba imewafadhili kwa kazi hiyo.
Upande mwingine kuna habari na taarifa za ‘kigazeti’ Mawio, kinachoanika wanaopanda mbegu ya maangamizi na kuonya juu ya mifarakano iwezayo kuleta umwagaji damu.
Waziri Nape anasema Mawio ndilo linafanya uchochezi. Analifuta. Hawezi kujifuta. Hawezi kufuta wengine waliobobea katika uchokozi wa kibabe na uchochezi.
Kufuta chombo cha habari ni kurejesha jamii katika nyakati za ujima. Ni kukataa elimu na maarifa. Ni kupora uhuru wa habari. Ni kupanda mbegu ya woga miongoni mwa wananchi. Ni kuingiza Taifa gizani.
Nape hana tofauti na mawaziri waliomtangulia, waliotumika kudhibiti habari kwa kukaa wamepakata na kubusu sheria ya kidikteta inayotumika kufuta vyombo vya habari, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.
Wasiliana na Meza ya Mhariri wa Jamii kwa simu 0713 614872 au 0763679229    

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group, Robert Kisena      
 Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group, Robert Kisena ameeleza kusikitishwa na taarifa zisizo za kweli zinazoihusisha familia ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) na kusisitiza kuwa yeye ndiye mmiliki halali.
Kisena alidai kwa muda mrefu watu wenye nia mbaya dhidi yake, wamekuwa wakihoji umiliki wa shirika hilo licha ya kuonyesha vielelezo vyote. Alisema taarifa zilizosambaa hivi karibuni zinazodai kuwa anaimiliki Uda kwa ushirikiano na Khalfan ambaye ni mtoto wa Kikwete hazina ukweli.
Alidai kuwa Kampuni ya Simon Group ambayo ilisajiliwa Mwanza 2007, inamilikiwa na watu wanane wa familia ya Kisena isipokuwa Profesa Juma Kapuya ambaye ana asilimia tano ya hisa kwenye kampuni hiyo.
“Kampuni hii inamilikiwa na watu wanane, hata mkisoma hizi nyaraka mtaona majina ya watu hao ambao ni mimi, wanangu; Simon, Gloria, Kulwa na George; mdogo wangu William Kisena, mama yangu Modesta Pole na Profesa Kapuya.
“Hakuna jina la Khalfan Kikwete hapa, sijui hizo taarifa watu wanazitoa wapi,” alihoji Kisena huku akionyesha vielelezo.
Alisema hata wakati kampuni hiyo inaanzishwa, Khalfan alikuwa mtoto mdogo ambaye asingeweza kumiliki kampuni hiyo ambayo inakua kwa kasi.
Kisena alidai taarifa hizo za uongo zinaenezwa na watu ambao ni washindani wake kibiashara na wengine ni maadui wa kisiasa wa Kikwete.
Alisema yeye ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na amekuwa hivyo siku zote, lakini hajihusishi na siasa bali anafanya biashara.
“Kama kuna wanaoichafua familia ya Kikwete waache kuniunganisha na mimi, sifanyi siasa.
Na kama kuna wanaonichafua kibiashara basi waache kuiingiza familia ya Kikwete, wapambane na mimi kwenye biashara,” alisema Kisena.
Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema kampuni yake ya Uda RT ndiyo itakayoendesha mradi wa mabasi yaendayo kasi na kuwa nauli zilizopendekezwa zilitokana na tathmini ya gharama halisi za uendeshaji wa mradi huo.
Alisema baadhi ya vitu vilivyowafanya wapendekeze nauli hizo kuanzia Sh700 mpaka Sh1,200 ni pamoja na kulipia barabara za Dart.
Pia, alisema mabasi hayo yatakuwa hayakai vituoni kwa hiyo huenda wakati mwingine yatakuwa yanatembea bila abiria.
“Sababu hizo ndiyo zimetufanya tupendekeze nauli hizo, lakini tuko kwenye mazungumzo na Serikali ili waondoe malipo ya barabara ili nauli ipungue.
Mazungumzo yanaenda vizuri, ninaamini nauli zitapungua,” alisema.
Kisena alisema ifikapo Machi, mwaka huu, Kampuni ya Uda itaorodheshwa kwenye Soko la Hisa ili wananchi waweze kumiliki wenyewe kampuni hiyo.
Alisema wanaendelea kufanya mipango kwa ajili ya kuuza asilimia 70 ya hisa kwa wananchi wote.    


Mapacha sasa - wakiwa na mama yao kutoka kulia Jo, Carol na Heidi
Pacha wawili kutoka Powys, Wales wanatarajiwa kudai rekodi ya dunia ya pacha wa kwanza kuwahi kuzaliwa katika nchi tofauti katika kipindi cha miaka 40 baada ya kutokea tukio jingine la aina hiyo.
Heidi Gannon alizaliwa katika hospitali ya Welshpool mnamo mwaka 1976, huku dada yake kwa jina Jo Baines akizaliwa eneo la Shrewsbury, England karibu saa mmbili baadaye.
Guinness World Records ilikuwa imewaorodhesha watoto wengine pacha waliozaliwa Scotland na England mnamo mwaka 2012 kama wa kwanza kabisa hadi walipowasiliana na Bi Gannon.
Baada ya kufanya uchunguzi wake, Guinness ilisema kuwa pacha hao kutoka Wales kweli walivunja rekodi hiyo.
Bi Gannon alibaini madai ya vijana wake ya kuvunja rekodi hiyo baada ya kununua kitabu kwa ajili ya kijana wake.
Mapacha wa Powys
Mapacha walipozaliwa mwaka 1976
Alizaliwa 09:00 GMT (saa sita asubuhi Afrika Mashariki) tarehe 23 Septemba mwaka 1976 katika hospitali ya Welshpool eneo la Powys, lakini mama yake Carol Munroe hakufahamu kuwa alikuwa na ujauzito wa watoto wawili.
Dada yake Bi Baines, alizaliwa baadae saa 10:45 GMT (Saa nane kasorobo Afrika mashariki) kilomita 32 ndani ya England, katika jimbo la Shropshire.
Maafisa walithibitisha kuwa walikua wanasubiri rekodi itayarishwe na kwamba walikua wakiwasiliana na Bi Gannon kuhusu hilo.
Msemaji wa Guiness alisema: "tulifahamishwa kuhusu dai la Bi Baines na Bi Gannon la rekodi hii wiki iliopita na baada ya utafiti fulani uliomuhusisha mshauri wetu wa masuala ya mapacha tumeweza
kuthibitisha kwamba kweli hawa ni mapacha wa kwanza kuzaliwa katika nchi tofauti."


 
Watu wakishangilia nchini Korea Kaskazini
Wanasayansi nchini Korea Kaskazini wamegundua aina ya pombe ambayo haisababishi uchovu baada ya mlevi kunywa kunywaji hicho kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
Gazeti la Pyongyang Times nchini humo linasema kuwa pombe hiyo haimletei mlevi uchovu wakati anapoamka asubuhi.
Pombe hiyo inaripotiwa kutengezwa kutoka kwa mmea mmoja wa asili unaofahamika kama insam pamoja na mchele.
Vyombo vya habari nchini Korea kaskazini vinafafahamika kwa kutangaza mambo yasiyokuya ya ukweli kuhusu mafanikio ya nchi hiyo.
Mwaka uliopita korea kaskazini ilisema kuwa madawa yanayotengenezwa kutoka kwa mmea huo wa insam yanaweza kuponya magonjwa yakiwemo Sars na virusi vya ukimwi.

Kenyatta  
Rais Kenyatta ameahidi kuwaandama walioshambulia kambi ya el-Adde
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anawatembelea wanajeshi waliojeruhiwa baada ya wanamgambo wa al-Shabab kushambulia kambi ya wanajeshi nchini Somalia Ijumaa iliyopita.
Rais Kenyatta atatembelea majeruhi hospitali ya Forces Memorial, Nairobi na baadaye kujumuika na jamaa, marafiki na maafisa wakuu wa jeshi kwa ibada ya kuwakumbuka wanajeshi waliouawa.
Majeshi Wanajeshi tayari wamekusanyika ndani ya hospitali hiyo ya majeshi
Serikali ya Kenya bado haijatoa idadi kamili ya wanajeshi wake waliouawa baada ya kambi hiyo iliyoko el-Ade kushambuliwa.
Kundi la al-Shabab awali lilisema liliwaua wanajeshi zaidi ya 60 wa Kenya.
Mamia ya jamaa na marafiki wamekuwa wakifika katika vituo vilivyotengwa na idara ya jeshi nchini Kenya kutafuta habari kuhusu wapendwa wao.
Mkuu wa jeshi Jenerali Samson Mwathethe aliambia wanahabari Alhamisi kwamba jeshi bado linaendelea kukusanya habari kuhusu wanajeshi waliokuwa kwenye kambi hiyo.
Majeshi  
Baadhi ya wanajeshi waliojeruhiwa wanatibiwa katika hospitali ya majeshi
Alidokeza pia kwamba huenda ikabidi uchunguzi wa vijinasaba kufanywa kutambua miili ya baadhi ya wanajeshi waliouawa.
Alisema bomu lililotumiwa na washambuliaji hao kuvamia kambi hiyo lilikuwa na nguvu mara tatu kushinda bomu lililotumiwa kushambulia ubalozi wa Marekani jijini Nairobi mwaka 1998.
Watu takriban 250 waliuawa kwenye shambulio hilo.



Rais John Pombe Magufuli leo Jan 21 2016 aliwasili Arusha ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ameingia madarakani, Rais anatarajia kuwatunuku kamisheni  maafisa wanafunzi wa kundi la 57/15 katika chuo cha mafunzo ya kijeshi (TMA) Monduli.
Ninayo baadhi ya matukio katika picha na nimekusogezea tayari nimekusogezea hapa chini.
DSC_6269
DSC_6298
DSC_6331
DSC_6342
DSC_6343
DSC_6348
DSC_6461
DSC_6483
DSC_6484


Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha kuzalisha umeme na kutoa mafunzo cha Kikuletwa ambacho nchi yake imetoa dala za Marekani milioni 5 kwaajili kukifufua kwaajili matumizi ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)

Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro,Anthony Mtaka,Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika wakikagua vyanzo vya maji eneo la Chemka vitakavyotukika kuzalisha umeme na kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa fani ya Uandisi Umeme wa Chuo hicho.

Mhandisi wa Umeme katika Chuo cha Ufundi Arusha,Merchior Urbanus(kushoto)akimwelekeza jambo Balozi wa Norway wakati akitembelea eneo la Kikuletwa.

Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad akifurahia madhari ya Kituo cha Kikuletwa, amehaidi kuendelea kusaidia sekta ya nishati hapa nchini.

Moja ya mitambo zamani iliyopo kwenye kituo cha Kikuletwa iliyowekwa na Mmisionari wa Kijerumani mwaka 1935 na baadaye kukabidhiwa kwa shirika la umeme nchini Tanesco kisha Chuo cha Ufundi Arusha baada ya kutotumika kwa muda mrefu.

Moja ya chanzo cha maji ambacho pia hutumika kama sehemu ya utalii kutokana na maji yake kuwa ya vuguvugu muda wote.

Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad(wa tatu kutoka kulia)Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Masika wakiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Wakuu wa Chuo hicho na maafisa wa Ubalozi wa Norway nchini katika picha ya pamoja leo.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com


Ndege ya Shirika la Ndege la Qatar ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa na Mwili wa Marehemu Asha Bakari alifariki nchini Dubai akitokea matibabuni Nchini India.Mareheme anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Kianga nje kidogo ya mji wa Unguja na Maiti itasaliwa katika msikiti Mkuu wa Kwamchina saa nne asubuhi. 
Mwili wa Marehemu ukiteremshwa katika ndege kwa ajili ya maandalizi ya mazishi kesho saa nne asubuhi Jangombe Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Pandu Amaer Kificho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud wakiwa uwanja wa ndege Zanzibar wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu
Ndugu na Jamaa wa Marehemu wakiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu Uwanja wa Ndege wa Zanzibar leo jioni
Mwili wa Marehemu ukishusha katika gari baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar wakiubeba wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege Zanzibar. 
Wananchi wakiupokea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Wafanyakazi wa Uwanja huo leo jioni.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho na Viongozi wengine wa Serikali na Vyama vya Siasa na Wananchi wakiuombea dua mwili wa marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Zanzibar leo jioni tayari kwa mazishi kesho katika kijiji cha kiyanga. 

Ndugu na Jamaa wakiwa na huzuni baada ya kuupokea mwili wa marehemu leo jioni 



Wananchi wakishiriki katika kuombeleza msiba wa marehemu Asha Bakari Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar aliyefariki Nchini Dubain wakati akitokea Nchini India katika matibabu.
Ndugu na Jamaa na Wananchi wakishiriki katika dua ya kuuombea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili nyumbani kaka wa marehemu kwa ajili ya matayarisho ya mazishi kesho katika mtaa wa jangombe  
Waombolezaji wakiwa katika msiba jangombe kwa ndugu wa marehemu wakisubiri taratibu za mazishi kesho saa nne asubuhi.
Ndugu wa marehemu wakiomboleza msiba wa ndugu yao nyumbani kwao jangombe Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud akizungumza na Ndg wa c na mareheme baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu Jangombe kwa nduga zake kwa mazishi kesho
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com

-