Thursday, April 21

Baada ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans kuondolewa katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya usiku wa April 20 2016 na klabu ya Al Ahly ya Misri kwa jumla ya goli 2-1, sasa wanajiandaa kurudi kucheza Kombe la shirikisho barani Afrika katika hatua ya 16.
Yanga imepangwa kucheza na klabu ya Grupo Desportivo Sagrada Esperança ya Angola katika hatua ya 16 bora ambapo mechi zitachezwa nyumbani na ugenini na baada ya hapo timu nane zitaingia katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Kombe la shirikisho barani Afrika, Grupo Desportivo Sagrada Esperança ilianzishwa December 22 1976 .
gfd
Yanga ataanza kucheza nyumbani kati ya Mei 6-8 na mechi za marudiano zitachezwa kati ya Mei 16-18 2016


Je, Falsafa ya Kuanzishwa kwa Mbio za Mwenge wakati wa Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/1961 imepitwa na wakati??? Je, kuna wakati utafika misingi ambayo taifa hili lilijengwa kwahiyo, itapitwa na wakati? Je, tuachane na mbio za Mwenge kwa sababu za gharama kuwa kubwa - wengine wanasema mwenge ni Jipu na Rais Magufuli alitumbue? Au Mbio za Mwenge zina umuhimu na ni sehemu ya msingi ambao taifa hili lilianzishwa na ni kumbukumbu ya mapambano ya kumletea mabadiliko na maaendeleo Mtanzania? Yote haya nitayatolea ufafanuzi kwenye Penyenye Fupi Fupi.
Falsafa ya Mwalimu Julis Kambarage Nyerere kuhusu mwenge wa Uhuru ilikuwa ni: “Sisi Watanganyika, tunataka  kuuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau”.
Je, Falsafa ya Kuanzishwa kwa Mbio za Mwenge wakati wa Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/1961 imepitwa na wakati??? Ikumbukwe kwamba falsafa hii ni sehemu ya misingi ya Taifa letu..tangu ilipoanzishwa na waasisi wetu. Mataifa yaliyoendelea yameendelea kuenzi misingi iliyojenga Mataifa hayo kwa gharama zozote zile. Tutakubaliana sote kuwa Watanzania bado tunahitaji kujikwamua kutoka kwenye ujinga, maradhi, na umaskini. Tunahitaji kujikwamua kutoka kwenye dhuruma na chuki ambazo, ukizingatia dhana ya mazingira na wakati, zimekuwa ni tofauti zaidi ukilinganisha na wakati wa Uhuru. Japokuwa wakati wa Uhuru kulikuwa na dhuruma, ufisadi, chuki nakadharika, bado hata sasa hivi tuna ufisadi, dhuruma na chuki tena zilizoenda mbali sana. Katika dhama hizi za Magufuli, zilizotofauti kabisa na nyakati za Kikwete, Mkapa, Mwinyi na zile za wakati wa Baba wa Taifa. Tumejionea uozo wa hali ya juu kuliko ambavyo tumewahi kushuhudia. Neno hili siyo geni tena kwetu – “Tanzania ilikuwa ni shamba la bibi”.  Mwenge wa Uhuru unapaswa kutukumbusha kila mara kuwa vita dhidi ya ubadhirifu, chuki, na dharau bado inaendelea. Tena falsafa ya Mwalimu ilikuwa inataka huu Mwenge umulike hadi nje ya mipaka yetu. Hii inanipeleka kwenye penyenye yangu inayofuata – Kuingiliwa kwa Uhuru wa Taifa letu na Mataifa ya Magharibi.
Tutakumbuka kuwa hivi karibuni sakata la MCC 2 lilishika kurasa nyingi sana. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Marudio wa Zanzibar na kuhusiana na ile sharia ya makosa ya Kimtandao. Taasisi ya MCC ni kibaraka wa umagharibi, pia ina kila lengo la kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu. Maitaifa ya Magharibi kuingilia mambo ya ndani ya nchi za kiafrika limekuwa ni jambo la kawaida sana. Tumekuwa ni nchi ya amani isiyokiuka haki za binadamu, sasa kuiingiliwa kwenye mambo ya ndani ya nchi ni jambo linakiuka hadhi yetu ya kuwa Sovereign State. Mwenge wa Uhuru unatukumbusha maneno ya Mwalimu Julius Nyerere kuwa “… tunataka kuuwasha Mwenge na kuuweka juu yam lima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu...” Je msingi huu wa kuanzishwa kwa Taifa letu umepitwa na wakati, hasha.. msingi huu bado uko na unaendelea. Na kama taifa lazima tusimame kidete. Mwenge huu inabidi tuumulike ili sisi kama Watanzania tujikumbushe, na hayo mataifa ya nje yaliyo karibu nasi na yaliyo Magharibi au Mashariki. Pia ninaungana na kauli ya Mh. Rais Dk. John Joseph Magufuli kuwa ni bora kuishi kwa kula mihogo kuliko kula mkate ya masimango.
Je, kuna wakati utafika misingi ambayo taifa hili lilijengwa kwayo, itapitwa na wakati?
Mwalimu Julius Nyerere, alipohutubia Watanganyika kwa mara ya kwanza kama Waziri Mkuu wa Tanganyika, alielekeza kuwa Tanganyika iko vitani dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini. Ni nukuu baadhi ya maneno yake: “…matatizo haya, hayanitishi mimi, hayawatishi wenzangu, na wala hatuombi kwamba yawatisheni ninyi. Tunayaona kwamba ni jaribio tu…Mara nyingi sana, nimesema nayi juu ya umaskini, ujinga, na maradhi, lakini kwa kweli adui yetu mkubwa ni umaskini. Tukiweza kumshinda adui huyu, tutakuwa tumeweza kupata silaha itakayotuwezesha kuushinda ujinga na maradhi. …tunaweza kupigana vita vya umaskini. Namuomba kila raia wa Tanganyika, aape kiapo cha kuwa adui wa umaskini. Amshambulie adui huyo mahali popote atakapoonekana.”
Japokuwa Tanganyika ilipata Uhuru wake bila mapambano dhidi ya mkoloni yaliyohusisha kumwaga damu. Msingi tuliachiwa na Baba wa Taifa ni kuwa nchi iko kwenye mapambano dhidi ya umaskini. Kila Mtanzania anapaswa kuwa vitani wakati wowote. Nikiiweka hoja hii kwenye muktadha wa Mwenge wa Uhuru ambao unajengwa kwenye msingi wa kumulika ubadhirifu na dhuruma. Tumeshuhudia ambavyo viongozi au watumishi wetu katika kada mbalimbali wakiwa mstari wa mbele kwenye ubadhirifu wa mali za umma. Kuingia mikataba isiyokuwa na tija wala maslahi ya Taifa. Watu hawa wamekuwa wakiturudisha nyuma sana kwenye vita dhidi ya umaskini ambao mwalimu alitutaka kila Mtanzania kuapa kupambana nao kila sehemu atakapoukuta. Ila katika juhudi za Mtanzania maskini kujitafutia njia za kutoka kwenye umaskini na wengine kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi, wachumia tumbo wamekuwa na mtindo wa kujinufaisha wao na vizazi vyao. Kinyume kabisa na misingi ya Taifa letu. Kila Mtanzania akiwa vitani dhidi ya umaskini inamaanisha kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato na serikali itatimiza wajibu wake kuwaletea wananchi bidhaa za umma. Ndiyo maana katika dhama hizi za Magufuli utumbuaji wa majipu unaturudisha kwenye ile vita dhidi ya dhuruma, ufisadi, na uonevu. Mwenge lazima uendelee kumulika, falsafa na itikadi ya kuwa tuko katika mapambano lazima iendelee kumulikwa.
Je, tuachane na mbio za Mwenge kwa sababu za gharama kuwa kubwa - wengine wanasema mwenge ni Jipu na Rais Magufuli alitumbue? Au Mbio za Mwenge zina umumhimu na ni sehemu ya msingi ambao taifa hili lilianzishwa kwayo na ni kumbukumbu ya mapambano ya kumletea mabadiliko na maaendeleo Mtanzania?
Kama nilivyelezea hapo juu nia, falsafa na matokeo ya kuwepo kwa mbio za Mwenge wa Uhuru bado hazijabadilika. Changamoto ambazo zilikuwepo wakati wa Uhuru wa Tanganyika, bado zipo katika kipindi cha Tanzania ya karne ya 21, na inawezekana Tanzania ya vizazi vijavyo itakutana na changamoto zinazofanana na hizi lakini kadika mazingira na wakati wa vizazi vya wakati huo.
Kama Taifa misingi ya kuanzishwa kwa Taifa lazima iendelezwe, kwani wanaosema kuachana na misingi hiyo huwezi fahamu ajenda yao iliyojificha ni mimi. Taifa lisilo na misingi ya kuanzilishwa kwake ni dhaifu. Taifa linaloweza kutupilia mbali misingi ya kuanzilishwa kwake, linaweza kuwa katika hatari kubwa sana ya siku moja kutoweka, au kuingia katika virugu na matatizo ambayo ni vigumu kuweza kurudi katika hali ya awali. Bado tunaihitaji misingi ya Taifa letu. Bado tunaipenda misingi ya Taifa letu. Gharama ya mbio za Mwenge siyo hoja, maana misingi ya kuanzishwa kwa Taifa lazima ilindwe kwa gharama zozote zile. Ufisadi uliokuwa unaendana na kukimbiza mbio za Mwenge wa Uhuru ndiyo unaotakiwa kupigwa vita kwa juhudi zote. Mwenge kwa sababu unamulika na kuangaza palipo na ufisadi, udharimu, dharau, na chuki. Mbio za Mwenge wa Uhuru zitumike kutumbulia kila linapokuwa limemulikwa jipu, kwenye miradi ambayo imekuwa ni utamaduni kutumika kuizindua nchi nzima yaani mikoa 31 na Halimashauri 173.
Kumbukumbu ya kumletea Mtanzania mabadiliko ya kiuongozi na uundwaji wa mfumo wa utawala bora utakao ridhishwa kizazi hadi kizazi, ni jambo linalopaswa kuwa sehemu ya ujivuni wa kuwa na Mwenge wa Uhuru. Mwenge ni alama ya Uhuru wetu kuona mapungufu yetu. Mwenge ni alama ya kutuunganisha Watanzania na kupambana na uovu, udharimu, wizi, na ufisadi. Mwengi ni alama ya Uzalendo na kila Mtanzania nia akiuona anapaswa kuukumbuka wakati wa uhai wake wote, na kuwafundisha watoto na watoto wa watoto wake kuwa hiyo ndiyo ishara ya Uzalendo wa Mtanzania. Ndiyo ishara la tumaini la Mtanzania lilioanza tangu na kabla baada ya kupata Uhuru na lilikuwepo kabla ya kupata Uhuru. Wanaoupiga vita Mwenge wa Uhuru wamepoteza tumaini na wanataka Watanzania nia pia wapoteze tumaini pamoja nao. Ninachoamini mimi ni kuwa mtu aliyepoteza tumaini safari yake inapaswa kuishia kaburini. Tena kwa sisi tuliona tumaini la kizazi hiki na kutambua ukuu wa Mungu, tunaamini hata baada ya Kaburi tunatumaini kuwa siku moja tunauna uso wake. Sasa iweze sisi Watanzania tukubali mawazo haya finyu kuwa Mwenge ni Jipu, ninadhani kupoteza Tumaini ni Jipu, na dawa ya jipu ni kulitumbua na Mwenge unamwangaza kwa kutosha kumulika wakati wa Utumbuaji wa Jipu hilo.
Mnyela Jonathan N.


 Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akisalimiana na wawakilishi wa mashirika ya WHO na UNICEF alipowasili katika kambi ya maafa kuona mazingira ya Kambi hiyo iliyopo Skuli ya Sekondari ya Mwanakwerekwe C nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman akiongozwa na Afisa Msaidizi wa kambi ya maafa Makame Khatib Makame kutembelea kambi hiyo iliopo  Skuli ya Mwanakwerekwe C.
 Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmany Andemichael akiangalia dawa za Shirika la Msalaba mwekundu  alipofika  Ofisi yao waliofungua kutoa huduma katika kambi hiyo.
 Afisa kutoka Shirika la WHO Zanzibar Michael Habtu akichunguza maji yanayotumika katika kambi ya maafa kujua ubora wake.
  Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar Ali Juma Hamad vidonge vya waterguard na maji ya ORS kwa ajili  kambi ya maafa, wa kwanza (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Afya Halima Maulid Salum.
 Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhi katika kambi ya maafa Mwanakwerekwe C.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Na Ramadhan Ali-Maelezo Zanzibar.
MAAFISA wanaoshughulikia wananchi waliohifadhiwa katika kambi ya maafa Mwanakwerekwe C wameshauriwa kutoa elimu ya Afya kwa wananchi hao ili kuwaepusha na maradhi ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Naibu Waziri wa Afya Bi. Harusi Said Suleiman ametoa ushauri huo alipoitembelea kambi ya maafa kuona mazingira  na matatizo yanayowakabili katika kambi hiyo akiambatana na wawakilishi wa Mashirika ya WHO na UNICEF waliopo Zanzibar.

Amesema  kambi inakusanya watu wengi wenye desturi na taratibu za maisha tofauti hivyo suala la kutoa elimu ya Afya itakayosaidia maambukizi ya maradhi ni kitu muhimu .
Amewata wananchi hao  kufuata taratibu na maelekezo ya maafisa wa kambi hiyo ikiwemo  kunywa maji yaliyotiwa dawa na kukosha mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula ili wawe walimu wazuri watakaporejea kwenye makaazi yao.

Afisa Msaidizi wa Kambi ya maafa Makame Khatib Makame amemueleza Naibu Waziri wa Afya kwamba hivi sasa kambi inawatu 420 wakiwemo wanawake 240.

Amesema huduma zote muhimu zinatolewa ndani ya kambi hiyo na wameanzisha utaratibu wa kuwapeleka  na kuwarejesha watoto wanaosomo katika skuli zao.

Wananchi wanaohifadhiwa katika kambi ya maafa wameiomba Serikali kuweka utaratibu wa kuwasaidia watakaporejea katika makaazi yao kwa vile wamepoteza vifaa vingi vya matumizi baada ya nyumba zao kujaa maji.

Tuesday, April 19



 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkazi Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bibi. Mary Kawar akizungumza na vijana (hawapo pichani) wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na shirikila hilo leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa mada wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.
 Mtaalam wa ajira kutoka ILO Bw. Jealous Chirore akichangia mada wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika hilo na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi kutoka YUNA – Chuo cha Bogamoyo akiuliza swali wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bibi. Mary Kawar baada ya kufungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.

Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo

Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akizungumza kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu ya droo hiyo pamoja na ofa mbalimbali zinazoendelea kutolewa kwa wateja wa DSTV 
Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo akichanganya droo hiyo kwa njia ya kielektoniki kupitia kompyuta. wengine wanaoshuhudia ni maafisa wa MultiChoice Tanzania. Kulia ni mwakilishi kutoka Bahati Nasibu ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Millao.
Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akihakiki moja ya majina ambayo yameingia kwenye droo ya ushindi kwa wateja wa DSTV 
Droo hiyo ikiendelea.
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionyesha majina ya washindi kwenye 'sreen' kubwa (Haipo pichani) wakati wa tukio hilo.
Droo hiyo ya JISHINDIE NA DSTV ikienndelea huku maafisa wa MultiChoice Tanzania na Mwakilishi wa Mchezo wa kubahatisha Tanzania pamoja na wanahabari wakishuhudia tukio hilo mapema leo Aprili 19.2016, Makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam.
 (Picha zote na Andrew Chale.)
Kampuni ya MultiChoice Tanzania inayosambaza vifaa vya ving’amuzi vya DSTV hapa nchini mapema leo Aprili 19.2016 imechezesha droo maalum na kuwapata washindi wa “JISHINDIE NA DSTV” katika tukio lililofanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbay, barabara ya Ali Hasan Mwinyi, Jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.

Awali katika droo hiyo, Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo alieleza kuwa, droo hiyo ilianza tokea mwezi wa kwanza ambapo wateja walitakiwa kuwa na malipo kwenye ving’amuzi vyao vya DSTV bila kukatika kuanzia hiyo Januari hadi mwezi Machi.

Wateja ambao hawajakatiwa ving’amuzi vyao katika promosheni hiyo ya JISHINDIE NA DSTV, waliotangazwa leo ambaoo ni wateja waliojiunga mwezi wa kwanza na kuweza kulipia DSTV zao bila kukatiwa matangazo kwa muda wa miezi mitatu wameweza kujishindia zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar wakiwa wao na familia zao.

“Washindi wawili ambao kila mmoja atapata nafasi ya kupelekwa Zanzibar na kukaa huko kwa siku mbili katika hoteli huku akilipiwa kila kitu kuanzia usafiri, malazi, chakula yeye na familia yake ikiwemo baba, mama na watoto wawili. Washini hao ni Mwelly Nyakusaima ambaye ni mkazi wa Igoma-Mwanza na mshindi mwingine ni Evarist Ndambo mkazi wa Tabataa Jijini Dar es Salaam.” Alisema Bi. Hilda Nakajumo.

Aidha, alibainisha kuwa, washindi wengine waliojishindia droo hiyo ambao ni wa kipengele cha pili ni wale wateja ambao tayari walishajiunga na DSTV huku wakitakiwa wasikatiwe malipo yao kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa tatu.

Ambapo wateja 50 wamejishindia DSTV EXPLORA Decoders huku wateja 90 wao wakibahatika kupata kuunganishwa malipo ya bure ya mwezi ikiwemo ya mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita na miezi 12 bure.

Aidha, washindi hao wote walioshinda MultiChoice ilibainisha kuwa, watapigiwa simu na kuelekezwa namna ya kuchukua zawadi zao hizo kuanzia sasa kwa muda hadi June mwaka huu.

Kwa upande wake, Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu aliwakumbusha wateja wa DSTV kuendelea kulipia malipo ya ving’amuzi vyao huku wakitoa ofa mbalimbali sambamba na vipindi vizuri ikiwemo vya uhondo wa soka la kimataifa, filamu na muziki..

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafnyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, na kufanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam Aprili 19, 2016. Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kwa viongozi hao juu ya shughuli za Mfuko na faida ya wafanyakazi kupatiwa fidia endapo patatokea madhara awapo kazini. Wengine pichani ni mgeni rasmi, Pendo Z.Berege, (Mwakilishi wa Msajili wa vyama vya afanyakazi na waajiri, na Peter J. Mbelwa kutoka Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii, (SSRA).

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umeendesha semina ya siku moja kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kuwalipia michango ya mwezi.

Semina hiyo iliyofanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Aprili 19, 2016, ilifunguliwa na mwakilishi wa Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri, Bi.Pendo Z.Berege.Katika hotuba yake, Bi. Berege alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatwapo na majanga wakiwa kazini.

Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni taasisi ya serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi No. 20 ya mwaka 2008.Akiwakaribisha wana semina kwenye semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Msomba alisema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi na kwa kutambua kuwa viongozi wa wafanyakazi ndio wadau wakuu wa Mfuko huo, semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.

Akitoa mada juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi waumiapo kazini.
Naye Bi.Amina Likungwala kutoka WCF, amesema katika mada yake ya Wajibu wa Vyama vya Wafanyakazi ambapo alisema, ni wajibu wa vyama kutoa elimu kwa wanachama wao ambao ni wafanyakazi lakini pia kuwaeleza waajiri umuhimu wa kutoa michango kwa wakati 

Mshiriki akisoma kijitabu chenye maelezo ya kina kinachofafanua majibu ya maswali ya mara kwa mara ambayo wadau wanataka kujua kuhusu WCF.
Bi. Pendo Berege, akifungua semina hiyo 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA, Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA, Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba.
Mzee Mchafu Chakoma, mwakilishi wa viongozi wa wafanyakazi akitoa neno la shukrani
Bw. Chakoma (kushoto), akibadilihana mawazo na Bi. Pendo Berege
Bi Amina Likungwala kutoka WCF, akitoa mada kuhusu wajibu wa vyama vya wafanyakazi
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence, akitoa mada "Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).







Idadi ya wafanyakazi hewa katika mkoa wa Shinyanga ambao awali ulidaiwa kutokuwa na wafanyakazi hao kabisa, imeongezeka na kufikia 226.

Hayo yamebainishwa leo na Rais John Magufuli katika uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, ambapo alisisitiza kuwa serikali yake haitawafumbia macho viongozi ambao kwa namna moja au nyingine wataruhusu mianya ya ubadhirifu wa fedha katika maeneo yao.

”Mkoa wa Shinyanga kwa taarifa nilizonazo hadi sasa wameshapatikana wafanyakazi hewa 226 kutoka ‘zero’ hivyo ni lazima tuwajibike kwa watanzania wanyonge,” amesema Rais Magufuli.

Wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mikoa Serikalini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela alisema mkoa wake hauna mtumishi hewa hata mmoja jambo lililopelekea Rais Magufuli kuunda tume iliyobaini watumishi  hewa  45 katika awamu ya kwanza.

Baada ya kubainika uwepo wa watumishi hao, Raisi alitangaza kutengua uteuzi wa Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutokuwa makini na taarifa anazopewa na wasaidizi wake.


Rais Magufuli amemsimamisha kazi mchana huu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe kutokana na ufisadi wa kutisha katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji  na  kuisababishia  serikali  hasara  ya  sh. bilioni 3.

Rais Magufuli amechukua uamuzi huo mchana huu wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda alitoa Hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo.

Akieleza zaidi, Makonda  amesema, Kamati aliyounda  ilibaini kuwa pale ubungo kunatumika sheria ndogo mbili za ukusanyaji mapato moja ya mwaka 2004 na nyingine ya mwaka 2009  ambazo zote zilisainiwa na Wilson Kabwe.

Amesema  kuwa Sheria  ya Mwaka 2004 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa kila basi  linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 4,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 42 kutokana na mabasi 350 yanayoegeshwa kituoni hapo   na   Sheria  ya Mwaka 2009 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa kila basi  linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 8,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 82  kwa mwezi

Makonda amesema kwamba, Kabwe alisaini mikataba miwili, wa 2004 na wa mwaka 2009  ambapo ule wa mwaka 2004  ulipelekwa jiji  na  ule wa 2009 ukapelekwa kwa mzabuni, hivyo jiji wanajua kuwa kila basi linatozwa sh. 4000 kwa  siku wakati mzabuni  anatozwa  8000 kwa siku

Makonda pia ameongeza kuwa Mkurugenzi huyo vilevile amekiuka sheria ya kutoa zabuni baada ya anayefanya kazi ya kutoza kodi za 'packing' katika jiji la Dar es salaam kumaliza muda wake lakini Mkurugenzi alimuongezea muda wa miezi minne kwa barua na baadaye miezi 6 kwa kisingizio kwamba mchakato unaendelea wa kumpata mtu mwingingine bila ya kutangaza dhabuni jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Kutokana  na  maelezo hayo, Mheshimiwa Rais ametangaza kumsimamisha kazi bwana Kabwe ambaye  ni  Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam  na ameagiza vyombo vya dola vianze uchunguzi mara moja ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa

“Kama vyombo hivyo vitamsafisha mimi sitakuwa na neno,” alisema Rais Magufuli huku akisisitiza kuwa ni muda wa watu waliowafanya wananchi kulia kwa muda mrefu, na wao waanze kulia ili wananchi wacheke. 
Wilson Kabwe

Daraja la kisasa la Kigamboni linalounganisha eneo la Kigambonina upande wa Kurasini likikatisha bahari ya Hindi. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kulizindua rasmi daraja hilo  leo Jumanne Aprili 19, 2016. 
Akina mama na watoto wao wakilishangaa daraja hilo la kisasa
Barabara inayoelekea kwenye daraja hilo

Kwa mwaka wa nne mfululizo uwanja wa Ndege wa Singapore Changi  umekuwa ndio uwanja wa ndege bora zaidi duniani ukishika nafasi ya kwanza na ulichukua tuzo zaSkyTrax World Airport Awards 2016 ambapo ulitangazwa huko Gologne Germany, Tuzo za Skytrax zinategemea kura zinazokusanywa kutoka kwa mamillioni ya abiria.

LIST YA TOP 10 YA VIWANJA BORA VYA NDEGE  DUNIANI  2016

1. Singapore Changi Airport
1
2. Incheon International Airport (South Korea)
2
3. Munich Airport (Germany)
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
4. Tokyo International Airport Haneda
4
5. Hong Kong International Airport
5
6. Chubu Centrair International Airport (Nagoya, Japan)
6
7. Zurich Airport (Switzerland)
7
8. London Heathrow Airport
8
9. Kansai International Airport (Osaka, Japan)
9
10. Hamad International Airport (Doha, Qatar)
10

-