Tuesday, December 1


flevaMwanamuziki Chinedu Okoli ‘Mr Flavour’.
WAKATI wanamuziki Bongo wakiendelea kuiga wanamuziki kutoka nje na kusahau kabisa muziki wao wa asili, wasanii wa Nigeria wamekuwa mfano wa kuigwa kwa kuimba nyimbo zenye vionjo vya ngoma zao za asili huku mwanamuziki Chinedu Okoli ‘Mr Flavour’ akiongoza kwenye listi hiyo.
Mwimbaji huyu mwenye ‘body’ la kutosha,anatajwa kupenda kufanya muziki wa asili ya makabila mbalimbali ya Nigeria kupitia baadhi ya nyimbo zake kama vile Nwa Baby, Adamma, Ololufe, Uyi, Ada Ada na nyingine nyingi.
Flavour anajulikana sana Bongo kupitia wimbo wake wa Ashawo ambao ulimpa umaarufu mkubwa kabla ya Wimbo wa Nana alioshirikishwa na Msanii Diamond Platnumz huku staili yake ya kucheza kifua wazi kwa kukata mauno ikimtofautisha na wasanii wengi wa levo yake


abiria wakisubiri usafiri abiria
Baadhi ya abiria wakisubiri usafiri bila mafanikio.


Kwa wiki ya pili sasa Rais Dkt Magufuli ameendelea kuwa gumzo barani Afrika na sasa hadi nchi za Ulaya zimedata naye.

Gazeti kubwa la Marekani, The Guardian limeandika habari isemayo: What would Tanzania’s cost-cutting president do? Twitter responds.
Pai  gazeti kubwa la  Australia,The Courier-Mail limeandika makala ndefu likimtaka Waziri mkuu wao,  Malcolm Turnbull ajifunze achapakazi toka kwa Rais wa Tanzania,Dr John Pombe Magufuli
Jina lake linatrend muda wote kwenye mtandao wa Twitter na kadri siku zinavyooenda habari za utendaji wake zinazidi kuenea.
Katika mtandao huo wa Twitter, imeanzishwa Verb ya jina la Magufuli iitwayo  magufulify ambayo imepewa maana ifuatayo;


Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akiongea na Waandishi wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7 katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya Stanbink Tanzania.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7 katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya Stanbink Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bwana Assah Mwambene.

Kama uliipata stori ya Mamlaka ya Mapato TRA kunasa makontena tisa eneo la Tanki Bovu Mbezi Dar es Salaam, nina muendelezo wake mtu wangu kuhusu majibu ya TRA walivyonasa mzigo huo.
Hapa ni nukuu ya alichokisema Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu ya Walipa Kodi wa TRA >>> ‘Tulipata taarifa kutoka kwa watu kwamba kuna kontena zinahamishwa kutoka bandari kavu ya Vingunguti usiku wa manane kuja kwenye godown iliyopo eneo la Mbezi Tanki Bovu ambayo sio rasmi na haiko kwenye orodha ya bandari kavu zilizo kwenye uangalizi wa TRA‘>>- Mkurugenzi Richard Kayombo.
IMG-20151201-WA0015
Kwenye sentensi nyingine za Richard Kayombo >>> ‘Tumeshirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha tunafika eneo hili na kuliweka chini ya ulinzi…. Hapa yapo makontena tisa, vilevile tumekuta magari matatu ambayo yalikuwa yanabeba haya makontena, madereva wake wako chini ya ulinzi.’
Baada ya hapo kilichofatia ni hiki >>> ‘Uchunguzi wetu tumemfahamu mwagizaji wa makontena pamoja na wakala wa forodha ambaye alikuwa anashughulikia makontena haya… Makontena yalipata kibali cha kupelekwa eneo la EPZ Ubungo September 17 2015, lakini kibali kimepita muda wake na cha kushangaza ni kwamba kontena hizi zimeletwa huku ambako sio mahali rasmi, ni kiashiria kwamba kuna jambo baya lilitaka kutokea kama ukwepaji wa kodi.’
IMG_20151201_131138
Sentensi za mwisho kwenye ufafanuzi huo hizi hapa >>> ‘Tutabaini kila kitu baada ya kupata nyaraka halisi na kuwapata mwagizaji na wakala wa forodha ambao wanatakiwa kujitokeza ndani ya saa 24… wasipojitokea tutafungua makontena kuangalia kilichomo, kama ni bidhaa halali tutazitaifisha, na kama ni bidhaa haramu zitateketezwa…‘ >>- Richard Kayombo.



Tayari uongozi mpya chini ya Rais Dk. John Magufuli umeanza kazi..ikiwa ni siku chache baada ya uteuzi wa Waziri mkuu Majaliwa Kassim kupewa madaraka, yapo mambo mengi ambayo tayari ameanza kuyatekeleza.
Jana jioni kwenye ofisi ya waziri mkuu kulikuwa na hafla fupi ya makabidhiano kati ya waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda ambaye alimtembelea Waziri  mkuu mpya ikiwa ni pamoja na kumkabidhi ofisi.
Hapa ninazo baadhi ya picha wakati wa makabidhiano hayo..
maja1

maja2

maja3

maja4

maja5

maja6

maja7

maja8

-