Tuesday, June 30

Mmiliki wa Shule ya Msingi na Awali (International) ya Mount Zion iliyopo Bahari Beach, Dar, Annah Mizighi Mwambili enzi wa uhai wake.

INASIKITISHA! Mmiliki wa Shule ya Msingi na Awali (International) ya Mount Zion iliyopo Bahari Beach, Dar, Annah Mizighi Mwambili, 47, (pichani) ameuawa na mwili wake kutupwa ndani ya shule yake baada ya kupotea kwa zaidi ya miezi sita huku mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Tatu Ntimizi, Said Ntimizi akidaiwa kuwa mmoja kati ya watuhumiwa wa mauaji hayo.
Duru za awali za upelelezi wa polisi, zinamtaja Said kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu na marehemu bila kufafanua alihusikaje na mauaji hayo ya kinyama yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana, siku na tarehe isiyojulikana na mwili wake kutupwa kwenye shimo la maji taka ndani ya eneo la shule aliyokuwa akiimiliki.
Aidha, nyuma ya taarifa hiyo ya mauaji, deni la shilingi milioni mia tisa (900,000,000) ambalo mwanamke huyo alikuwa akimdai mmoja kati ya watuhumiwa hao ambao majina yao yote bado hayajafahamika likitajwa kuwa ndiyo chanzo cha Annah kutolewa uhai.



HUKUMU ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basir Mramba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona imeahirishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam hadi Julai 3, mwaka huu.
LOS ANGELES, CA - JUNE 28:  Professional boxer Floyd Mayweather, Jr. (L) attends the 2015 BET Awards at the Microsoft Theater on June 28, 2015 in Los Angeles, California.  (Photo by Christopher Polk/BET/Getty Images for BET)
Kama wewe ni shabiki wa mastaa wowote wa mbele, basi utapenda kujua wana thamani ya kiasi gani cha pesa mwaka huu. Forbes imeachia orodha ya wasanii 100 wenye pesa zaidi kwa mwaka huu wa 2015, na kwenye orodha hiyo utakutana na watu kama Katy Perry, Beyonce, Kim Kadarshian, Floyd Mayweather, Manny Pacquiao, Taylor Swift na wengine kibao so unaweza ukavuta picha nani kampiku nani kwenye uwezo wa kifedha mwaka huu.
Staa anayeshika kijiti kwenye orodha ya mwaka huu ni Floyd “Money” Mayweather akiwa na thamani ya millioni $300 , Manny Pacquiao kwenye nafasi ya pili akiwa na thamani ya $160 million, Katy Perry akishika nafasi ya 3 akiwa na thamani ya millioni $130.


Hatimaye marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa wameungana na wajumbe wenzao wa Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanza kuwajadili makada waliojitokeza kuwania urais na kutoa ushauri utakaowezesha kupatikana kwa njia bora za kumpata mgombea wa chama hicho.

Tayari vikao vya baraza hilo vilivyokuwa vikisubiriwa kwa hamu vimeshaanza na leo vinaingia katika siku yake ya tatu, kwenye ofisi moja nyeti jijini Dar es Salaam.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya baraza la wazee hao zinaarifu kuwa vikao hivyo vina umuhimu wa pekee katika mchakato huo na kwamba vimepewa eneo tulivu na lenye usalama wa hali ya juu.

Indonesia
Kama uko karibu sana na TV za Kimataifa kama BBC, Sky News na CNN utagundua kwamba kwenye stori kubwa zilizopewa headlines sana iko ya Shambulio la Kugaidi lililotokea Tunisia na kusababisha mauaji ya Watalii.. Breaking News imeingia nayo kwenye stori kubwa zilizo kwenye headlines sasahivi, inahusu Ndege ya Kijeshi kuanguka kwenye makazi ya watu Indonesia na watu 30 wamefariki.
BBC Ajali II

Ndege hiyo ilipata ajali muda mfupi baada ya kuruka kutoka kwenye Uwanja wa Medan Polonia Airport.

kk
Kim Kardashian ni mwanadada ambaye anajulikana kwa kutengeneza headlines nyingi sana na moja kati ya headlines anazoziweka public personality huyu ni zile zinazohusu uzuri wake. Lakini Kim anasema amechoshwa na fikra za watu wengi wanaodhani kuwa yeye ni mwanamke mzuri tuu asiye na akili ya kufikria mbali, na kwa sababu hiyo staa huyu ameweka headlines nyingine kubwa, ametangaza kurudi shule!

Kim Kadarshian amesema anahisi yeye kama mtu binafsi hana uwezo mkubwa wa kutosha kiakili. Licha ya mamillioni na umaarufu wote alionao sasa hivi, Kim ameamua kurudi shule kupanua IQ huku akidai IQ yake haiko kwenye levo anayoitaka na anaona bora arudi kusoma, ameshapata umaarufu na pesa yupo tayari kuwekeza nguvu zake kwenye vitu vingine anavyoona ni muhimu na mume wake Kanye West amekua akimsisitiza Kim kujaribu vitu tofauti haswa kipindi hiki ambacho ana mimba.

Monday, June 29

d43d7e14d47316fadabd07
May 2015 ulikuwa mwezi ambao tulishuhudia maafa yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha mfululizo Dar… mara nyingi hivi vitu vikitokea huku kwetu watu hawaamini kama hata nje ya TZ nako huwa vitu vinatokea hivyohivo.
Mafuriko yametokea China, hapa unaweza kuona kwenye picha hali ilivyokuwa baada ya balaa la mafuriko kuwakuta.
d43d7e14d47316faf2e232
Hivi ndio ilivyokuwa kwenye Chuo kilichopo Nanjing, Jimbo la Jiangsu ndani ya China… Watu zaidi ya 65,000 wameathirika kutokana na mvua hizo.
jr6
Kuna ule msemo wa mtoto wa nyoka ni nyoka, kwa mtoto wa Cristiano Ronaldo iko hivyohivyo… ukimwangalia ana dalili zote kufuata njia ya baba yake kwenye soka.
Ronaldo na mtoto wake huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka mitano wameonekana wakijipumzisha katika ufukwe wa Bahamas huku dogo akiwa busy muda wote  ni yeye na mpira, baba yake alikuwa pembeni pia wakiendelea kula zao good times.
jr8
aunt na iyobo-002 
Mkali wa sinema za Kibongo Aunt Ezekiel akiwa na wafanyakazi wa Globalpublishers walipomtembelea kumuona mtoto wake.
Makubwa! Aunt Ezekiel ameweka wazi kinachotafsirika kuwa ni kuzaa nje ya ndoa huku akishikilia alichokiita ‘hayo ni mambo yake binafsi’, Ijumaa Wikienda liligaragazana naye kwa maswali. 
http://www.bongomovies.com/public/uploads/WEMA_SEPETU66.JPG
Ishu ya  Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutopata ujauzito imeshazungumzwa mara kadhaa na hata yeye mwenyewe alishawahi kujitokeza na kuizungumzia lakini safari hii amelizungumzia kwa njia tofauti.
Wema ambaye pia ni muigizaji wa filamu, awali alisema sababu kubwa ya kutopata ujauzito ni masuala ya kiafya lakini safari hii ametoa kauli tata ambayo inahusiana na imani za nguvu za giza.

Wema ambaye alifunguka hayo hivi karibuni, anadai kuwa yawezekana marehemu Steven Kanumba anahusika kwenye suala hilo.

Steve II
Kwenye list ya mastaa wa TZ waliotangaza kugombea Ubunge kwenye Uchaguzi wa 2015 lipo pia jina la mastaa wa Bongo Movie, Steve Mengere aka Steve Nyerere.
Jamaa alikuwa anamaanisha kabisa kuhusu safari yake kwenye Siasa, hapa nina pichaz kutoka kutoka viwanja vya CCM Bwawani ambapo Steve alikuwa akitangaza nia hiyo.
Screen Shot 2015-06-28 at 10.29.12 PM
Meza kuu iliyokuwa na viongozi wa CCM pamoja na Steve Nyerere mwenyewe.

Saturday, June 27



Diva wa muziki wa Pop, Beyonce Knowles.
New York, Marekani
DIVA wa muziki wa Pop, Beyonce Knowles huenda akashika mimba hivi karibuni baada ya kuweka wazi kuwa yupo mbioni kupata mtoto wa pili na mumewe ambaye pia ni mwanamuziki wa Hip Hop, Shawn Carter ‘Jay-Z’.

Kwa mujibu wa Jarida la In Touch linaweka wazi kuwa Beyonce (33) ambaye ni mama wa mtoto mmoja, Blue Ivy (3), kwa miezi kadhaa yupo katika kutafuta mtoto mwingine lakini anachohofia ni malezi juu ya mtoto huyo ajaye.
“Kwa miezi miwili sasa anamtafuta mwanamke sahihi wa kuweza kumlea mtoto wake ajaye. Tayari wapo katika hatua za mwanzo na mumewe za kutafuta mtoto,” liliandika jarida hilo.

Malaika ,Msanii anayetamba kwa sasa  katika game ya muziki wa tanzania na wimbo wake wa SARE amesema hivi karibuni video ya wimbo wake huo unatarajiwa kuanza kuchezwa katika kituo kikubwa cha kimataifa cha runinga

 TRACE TV
 

Akizungumza na MLIMANI TV malaika amesema walitakiwa wawe wametuma kazi hiyo lakini kuna baadhi ya mambo ambayo uongozi wake unasubiri kuyakamilisha ili kuituma.

.
.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Nyerere ameingia kwenye list ya wagombea ubunge mwaka 2015
Akizungumza na waandishi wa habari  alisema..’Kwanza ninataka kuwahakikishia watanzania sijakurupuka,


Msanii mchanga kutoka Uganda Jeng Jeng ama Rihanna wa Uganda ambaye alizoelewa kutupia picha zake za utupu ili tu awe staa kama Rihanna amerudi upya mtandaoni na kwenye safari hii ameamua kuja na mipango kabambe kuhkikisha kuwa anaiteka uganda kwa mambo atakayo yafanya kwenye mitandao

 

Kwa kuanza amechia video yake moja akifanya majambozi kama kawaida yake iko hapa chini

Kama kifaa chako hakina uwezo bofya hapa chini


Friday, June 26


RUBY BENDI ni bendi ya muziki wa kizazi kipya tanzania inayopatikana katika jiji la dar es salaam.band hii ya vijana wadogo wenye vipaji ni muungano wa wasanii wanne ambao ni ISMAIL YAHYA(SUMALAY),KHALID WAZIRI(KWEAPIPA),LAWRENCE CLEMENT(MAYA) NA SUNDAY MTOLE(C-MINOR).

Jina hili la Ruby Band linatokana na mmiliki wake Ruby Yusuph ambaye anamiliki kampuni ya Ruby International yenye studio ya RUBY RECODS na RUBY VIDEOS inayoshughulika na kurekodi nyimbo pamoja na kufanya video za nyimbo mbalimbali na filamu za kitanzania.

Mwezi june mwaka 2014 bendi hii
Linah 
Staa wa Muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga ‘Linah’ akiwa ameketi na William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo.
Musa Mateja
MREMBO anayefanya poa kunako Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, anadaiwa ‘kujiegesha’ kimahaba kwa shemeji yake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo.IMG-20150602-WA0025 
 Ndani ya Ukumbi wa Triple 7 uliyopo Kawe jijini Dar hivi karibuni, paparazi wetu aliwaona wakiingia sambamba na kukaa beneti kama mtu na mpenzi wake jambo lililozua maswali kibao kutoka kwa wateja waliokuwepo ukumbini hapo.
Linah1 
Linah na Boss Mtoto katika pozi la kimahaba.Mbali na kunaswa siku hiyo, pia paparazi wetu amekuwa akiwashuhudia mara kadhaa wawili hao wakiwa pamoja katika kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar.
nnj 
Mara ya mwisho, Linah na Boss Mtoto walikuwa pamoja kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Kili Music zilizofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, mapema mwezi huu.
Ndani ya Triple 7, paparazi wetu aliamua kumfuata Linah ili ajiridhishe uwepo wake na mwanaume huyo ambapo msanii huyo alijing’atang’ata na kusema:
“Huyu ni mtu wangu huwa natoka naye. Sijui umenielewa? Natoka naye sehemu mbalimbali.Ila kukutoa wasiwasi tambua kwa sasa sina mpenzi na nina haki ya kuwa naye, sina mpaka wa kujiachia na Boss Mtoto,” alisema.

 
Msanii wa Bongo Fleva, Kadja Nito akiwa katika pozi kabla ya kufanya mahojiano na Global TV Online.
 
Kadja Nito akiwasikiliza wanahabari wa Global Publishers (hawapi pichani) wakati wa maswali.



Imeripotiwa kutoka mkoani Simiyu katika Wilaya ya Bariadi kuwa Mkuu wa Wilaya (DC) hiyo Bw. Ponsian Nyami amemuomba Rais Jakaya Kikwete asimwonee huruma na badala yake atengue uteuzi wake kwa maana ameshindwa kusimamia ujenzi wa maabara katika wilaya yake.


Aliyasema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Elaston Mbwilo katika kikao cha majumuisho baada ya kutembelea maabara hizo na kubaini utekelezaji wake ni asilimia 10 tu.

Kabla ya kauli ya Nyami, Mbwilo alitoa lawama kwa DC kwa kushindwa kusimamia ipasavyo agizo la Rais na kueleza kuwa ndani ya Mkoa, Wilaya hiyo ndiyo ya mwisho katika utekelezaji wa agizo husika.

Hata hivyo Mkuu huyo mkoa alisema kuwa viongozi pamoja na watendaji wameshindwa kutekeleza agizo hilo ikiwa pamoja na miundombinu hasa barabara ndani ya wilaya hiyo kuwa chini ya kiwango, ambapo alimtaka Mkuu wa wilaya kuwachukulia hatua watumishi wote walisababisha hali hiyo.


Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio mawili tofauti. 
 
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa watoto hao wameuawa katika matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.
 
Mwaja alisema tukio la kwanza lilitokea juzi ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye aliuawa na fisi wakati akiwa na wenzie wawili wamelala.
 
 “Alikwenda fisi katika eneo hilo na kumvuta (mtoto mmoja) na kumtafuna hadi akamuua,”alisema Mwaja.


Siku chache zimepita tangu hukumu ya kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kutolewa dhidi ya mzazi mwenzake Faiza Ally,baada ya kuiomba mahakama kumchukua mtoto wao, hali iiyopelekea mahakama kutoa hukumu kuwa mtoto achukuliwe na Mbunge huyo,  jambo lililofanya sakata hilo kutinga bungeni.
 
Baadhi ya wabunge na wadau mbalimbali wamedai kuwa mtoto bado ni mdogo sana kuweza kuishi na baba yake na kutoa maoni kuwa mtoto arudishwe kwa mama yake kwa kuwa kila mtu ana mapungufu na kusema kuwa mtoto bado ana haki ya kuwa karibu na mama yake.

Saturday, June 13

bury
Nimekutana na stori hii kutoka Zimbabwe inamhusu Nabii mmoja kutoka nchi hiyo kufariki akiwa kwenye mishemishe za kupata nguvu za ziada ili akemee mapepo.
Nabii huyo Shamiso Kanyama alifatwa na familia moja wakamuomba aje nyumbani kwao ili afanye maombezi kuondoa mapepo yaliyokuwepo kwenye nyumba ya wanafamilia hao.
              
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 16 alimuuliza mama yake: "Mama, utanifanyia nini nikifikisha umri wa miaka 18 (siku yangu ya kuzaliwa)
Mama akajibu:- "mwanangu bado una unasafari ndefu". mtoto yule lifikisha umri wa miaka 17, siku moja ghafla akaanguka chini.
Mama yake akambeba na kumuaisha hospitali, na daktari akasema: "Mama mwanao ana Moyo mkubwa pia limeonekana tundu katika moyo wake."

.
Snoop Dogg
Kwenye headlines kubwa za siku ya leo ipo hii moja inayomhusu Mkurugenzi wa Twitter, Dick Costolo kutangaza kujiuzulu kama mkurugenzi wa Kampuni hiyo kutokana na malalamiko kwamba inajiendesha kihasara.
Headlines sasa hivi sio kuhusu Dick Costolo tena, ni Snoop Dogg.. Ishu unajua ni nini? Jamaa kasema eti yuko tayari kabisa kushika nafasi hiyo!!

Sunday, June 7


neymar
Mashabiki wengi wanawafahamu mastaa wao wa soka kwa sasa lakini hawajui zamani walikuaje? Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na wengine walikuaje wakiwa watoto.
Hapa nimekukusanyia picha za mastaa 15 wa soka Ulaya kabla ya kuwa mastaa kama walivyo sasa.
messi
Lionel Messi wa sasa na wakati akiwa mtoto

AW1A0940
Tayari nimesogea hapa Mlimani City Dar es Salaam… Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Tanga na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba anakuja hapa leo.
Kwenye list ya waliokuwa wakitajwa kuwa wanahitaji ruhusa ya CCM kugombea Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika October 2015, yeye pia yupo.
Leo tukae tayari kusikia kutoka kwake mwenyewe rasmi kabisa.. ninazo pichaz za kwanza kwanza hali ilivyo hapa Mlimani City mpaka sasa mtu wangu.
AW1A0936
AW1A0939

Thursday, June 4

Mandla Mandela, mjukuu wa kwanza wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Mandla akiwa na babu yake Mzee Nelson Mandela.
MANDLA MANDELA, mjukuu wa kwanza wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amehukumiwa kwenda jela au kulipa faini ya kwa kumshambulia na kumtishia kwa bastola mwalimu wa shule moja mwaka 2013.
Mandla, ambaye ni mbunge wa chama tawala cha African National Congress (ANC), alitiwa hatiani kwa kumshambulia mwalimu aitwaye Mlamli Ngudle kutokana na ajali ya barabarani iliotokea huko Mthatha, Jimbo la Cape, Afrika Kusini.
Waziri wa Maendele Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba (katikati) akizungumza na waombolezaji waliofika nyumbani wa Marehemu,Eugen Mwaiposa leo Mchana.
Mme wa Marehemu, ,Ally Mwaiposa (aliyekaa) akifarijiwa na waombolezaji waliofika nyumbani kwake.

Madam Wema Sepetu amkwapua bwana wa Linah Sanga akiongea kwa uchungu msanii huyo wa bongo fleva kwenye kipindi cha Ala za roho,Amedai penzi lake limekwenda na maji baada ya madam kufanya yake.Bwana huyo ndie alikua meneja wake nakufanyia mchakato wa video ya Olitemba South Afrika.Madam Wema juzi juzi tulisikia kaolewa leo tena kasfa nzito ya kuiba bwana wa wawatu.Linah na jamaa huyo wamedumu miaka zaidi ya minne.
Ishu ya imani ni ya mtu binafsi na kila mtu ana uwezo wa kuamini kile anachoona ni sahihi kwa mtazamo wake na mtu anapotokea kumuamini kiongozi wake wa dini kwa asilimia kubwa hutekeleza yale anayofundishwa.Sasa hii ya leo
mooo
Mapema wiki hii millardayo.com iliandika stori ya ajali ya lori la mafuta kuua zaidi ya watu 90 Nigeria ikiwa ni baada ya kuwa kwenye mwendo mkali na kugonga watu na magari yaliyokuwa kwenye kituo cha abiria.
station
Muonekano wa kituo cha mafuta baada ya kulipuka
Lakini leo Ghana nayo imeingia kwenye headlines baada ya kituo cha mafuta kulipuka na kuua watu wanaokadiriwa kuzidi 90 katika mji mkuu wa nchi hiyo Accra.
-