Saturday, August 29

3X6A6344
Mgombea Urais wa UKAWA Edward LOWASSA muda si mrefu atazungumza na wananchi katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho,Hizi ni Pichaz za awali katika ufunguzi wa kampeni hizo.
3X6A6262

Winga wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Memphis Depay ambaye amesajiliwa katika kipindi hiki cha usajili akitokea klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi, August 28 amenaswa na Camera za mapaparazi akikatisha mitaa ya jiji la Manchester na gari lake la kifahari la Mercedes GLA 45 AMG.
2BBCD27C00000578-0-image-a-1_1440767501556
Depay ambaye ana muda mchache toka ameanza kuishi katika jiji la Manchester ameonekana akiwa mwenye furaha wakati akifanya Shopping katika jiji hilo. Winga huyo aliyeanza vizuri katika klabu ya Man United kwa kuifungia magoli katika mchezo wa kwanza wa mtoano

Thursday, August 27


diva

Loveness Malinzi ‘Diva’
NI mtifuano! Agosti 24, mwaka huu ilikuwa siku mbaya kwa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au baba Tiffah na mtangazaji anayekimbiza kwa sauti tamu hewani, Loveness Malinzi ‘Diva’ kufuatia kupishana lugha ndani ya studio za redio na hivyo, Diamond kumvurumishia matusi mwenzake.
Kupishana kauli huko kuliashiria kuwepo kwa uhasama wa siku nyingi kwa wawili hao huku kila mmoja akiwa anaamini mwenzake ana makosa na ndipo siri tano za Diamond kumtusi Diva zikajulikana.
MCHEZO ULIVYOANZA
Siku hiyo majira ya saa 9:00 alasiri, Diamond alitia timu kwenye studio za redio hiyo zilizopo Mikocheni, Dar kwa lengo la kumtambulisha msanii wake mpya kutoka studio yake ya Wasafi Records iliyopo Sinza-Mapambano, Dar.Mwanyeji wa Diamond alikuwa mtangazaji Hamis Mandi ‘B12’. Lakini ndani ya studio hiyo alikuwepo Diva.


Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa Mshindi wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke Dennis Lwasai wakiwa na bango linalomwelezea mahindi huyo wakati walipojitokeza kumpokea wakati akirejea nyumbani kwao Mambogini Moshi
 
Mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke Dennis Lwasai akiwasalimia wakazi wa mji wa Moshi waliokuwa wakimpongeza wakati akirejea kwao Mambo


Ziona Chana anaishi na wake zake wote katika jengo lenye vyumba 100. Wake zake hufanya zamu kulala naye. 
Hutumia jumla ya kuku  kutengeneza chakula cha usiku.
 
Yeye ni mkuu wa familia kubwa zaidi duniani - na anasema kuwa 'amebarikiwa' kuwa na wake 39.
 
Vile vile, Ziona Chana ana watoto 94, - wakwe 14 na wajukuu 33.
Wanaishi katika nyumba yenye vyumba 100, yenye ghorofa nne ambayo imejengwa katikati ya vilima vya kijiji cha Baktwang katika jimbo la Mizoram nchini India, ambapo wake zake hulala katika vyumba vikubwa vya pamoja.
Familia yote ya Ziona yenye watu 181
Jengo la Ziona lenye vyumba 100 ndio jengo kubwa kabisa lililojengwa kwa kokoto katika kijiji chenye vilima cha Baktawng


 
 
 
 
 
 
53 Votes

1. Bugatti Veyron Supersport:
1. Bugatti Veyron Supersport:
Bugatti Veyron

Ni gari lenye spidi kali kuliko yote duniani, na ndio gari la gharama kuliko yote duniani. nini cha zaidi unacho taka kujua?? ni gari lenye mvuto wa kipekee yenye thamani ya $2.6 milioni za kimarekani ambazo ni sawa sawa na bilioni 5.11 za kitazania, Bugatti Veyron Supersport ni hakika Bugatti, jaribu kitanda kabisa, ni jinsi gani hawa VW engineers walivyo sukuma kutangaza, na kuweka horse power ya 1200 kutoka quad-turbo 8.0 lita W16 engine na imetengenezwa kwa aerodynamics ambayo inasidia kufika spidi 267.81 mph. ukiongezea kutofautiana na magari mengine ya hypercars, veyron itakuwa uluxury mkubwa kupita wakifahari
2. Ferrari 599XX:
Ferrari-599XX
599XX

chukulia Ferrari 599 na ibadilishe kwenye supercar tu na utajikuta una 599xx. inanguvu ya horse power ya 700

.
.


Msanii mkali ni lazima awe na gari kali. Christian Bella amesema anapenda kuwa na magari mengi na ndio maana ameamua kununua gari jipya aina ya Toyota Harrier.
Akizungumza na Bongo5 leo akiwa mwenye furaha, hitmaker huyo wa Nani Kama Mama amesema bado anatamani kuwa na magari mengi zaidi na ya thamani.
Kampeni za Urais, mgombea wa Urais wa Tanzania anayeiwakilisha UKAWA kupitia
Pamoja na kuwepo kwa barua hiyo kutoka kwa mkurugenzi wa Ilala, Umoja wa wadai Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesisitiza kuwa ratiba ya mkutano wao utakuwa kama walivyopanga, eneo, muda na tarehe ile ile.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, James Mbatia aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali imekataa ombi lao la kufanyia mkutano kwenye viwanja vya Jangwani bila ya kuwa na sababu za msingi.

Mbatia amesema waliandika barua ya 22 Agosti, 2015 kutumia viwanja vya Jangwani lakini mkurugenzi amewazuia kutumia viwanja hivyo kwa madai kuwa tayari umeshalipiwa na mtu mwingine, ambaye hakutaka kumtaka kwa sababu zao binafsi.


CARLOS SLIM HELU ni tajiri wa kwanza duniani kutoka kwenye Forbes,. Ni mexico anayemiliki mitandao ya simu anaenesha gari aina ya BENTLEY CONTINENTAL FLYING SPUR yenye thamani ya dola laki 3
Bill Gates nitajiri wapili duniani anaendesha gari aina ya PORSCHE 959 COUPE ambayo n magari 230 yaliyopo duniani kote. Ili bidi raisi Bill Clinton kasaini mkataba wakumruhusu tajiri huyo kuendesha gari hilo ambalo

Tuesday, August 25



Nick Jonas na Kendall Jenner.
New York, Marekani
NICK Jonas na Kendall Jenner awali baada wa kuripotiwa kuwa wanatoka kimapenzi, iliaminika kuwa ingekuwa bonge la kapo, lakini ghafla msanii wa muziki na muigizaji huyo, kachomoa kuwa wala hatoki na mwanadada huyo.



Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha .
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwanachama wa CHADEMA, Lawrence Masha jana alikamatwa na Jeshi la Polisi, leo amefikishwa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar
Anashtakiwa kwa kosa la kuzuia Polisi wasitimize majukumu yao(Obstructrion of Justice)


prison
Nimekutana na stori moja kwenye mitandao inayohusiana na magereza ya zamani ya wafungwa, yamekusanywa magereza 9 ya sehemu mbali mbali duniani na kubadilishwa kuwa kitu tofauti kabisa, na ukiyaona hutoamini kuwa majengo hayo yalishawahi kuwa magereza ya wafungwa!
Kwenye yale maeneo ambayo Serikal

Thursday, August 20

Waziri Kamani balaaWaziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani na maofisa polisi.
KUFUATIA tukio la Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani juzikati kugeuka ‘bondia’ kwa ‘kumwanzishia’ timbwili msimamizi wa uchaguzi wa marudio wa kura za maoni ya ubunge kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Busega, Simiyu na kusababisha matokeo yasitangazwe, wadau wameibuka na kusema yote hayo ni machungu ya kukatwa.
Katika tafrani hiyo, miwani ya Waziri Kamani ilivunjika akiwa katika harakati za kumkabili msimamizi huyo ambaye ni Katibu wa CCM Wilaya ya Meatu, Jonathan Mabihya wakati akitangaza matokeo.
Vurugu hizo zilizozuka majira ya saa 4:18 asubuhi ambapo askari polisi waliwatia mbaroni watu kadhaa, zilisababisha Mabihya kushindwa kutangaza matokeo na kuahirisha kwa muda huku Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya akisema yatatangazwa baada ya utulivu kurejea.
HOUSE GIRL (2)TIMBWILI! Njemba mmoja mkazi wa Kisimani mjini Tunduma wilayani Momba, Mbeya ambaye jina lake halikupatikana mara moja, amejikuta akila kichapo kisa, kudaiwa kumtorosha msichana wa kazi ‘hausigeli’ wa mtu.
HOUSE GIRL (1)Tukio hilo lililokusanya watu kibao, lilijiri juzikati katika maeneo hayo baada ya vijana hao kumtuhumu kijana huyo kwamba amemficha msichana huyo ambaye bosi wake aitwaye Johnson alikuwa akimtafuta.
ASSALAAM aleikum na Bwana Yesu asifiwe wapenzi wasomaji. Ninafurahishwa na jinsi mnavyoniunga mkono kunisoma na kunipa maoni yenu. Hakika nitaendelea kuwaelimisha kwa kila ninachoona kinafaa kuwafikia ili kuwekana sawa ndani ya maisha ya uhusiano.
Leo nimekuja na mada hii; UNAPIGIWA SIMU HUPOKEI, UNASONYA...UNATUMA MESEJI...MPENZI WAKO AKUELEWE VIPI?
Mada hii inawahusu wapendanao wote. Wewe mwanamke na wewe mwanaume. Nimefuatilia kwa makini sana suala lenyewe na kubaini kwamba, ni la kweli na limekuwa likiwakera wengi.

ISHU ILIVYO

mandelaa
Historia ya Nelson Mandela ni historia ya kishupavu iliyosimamia ukweli, usawa na haki na pale mtu anapojaribu kuweka doa kwenye jina la familia ya Nelson Mandela watu hawatakuelewa kabisa.
Mjukuu wa Nelson Mandela, Mbuso Mandela mwenye miaka 25 anaziandika headlines South Africa baada ya kesi ya ubakaji wa msichana wa miaka 15 dhidi yake kufikishwa Mahakamani.
mandela's grandson2
Mjukuu wa Nelson Mandela, Mbuso Mandela.
Kwa taarifa zilizotolewa na ripoti iliyofikishwa polisi zinasema kuwa Mbuso Mandela alimshambulia binti huyo wakati wakiwa kwenye restaurant moja maarufu jijini Johannesburg… na wakati akiwa anapata chakula cha jioni na marafiki

Tuesday, August 18


.
.
Jana nilikusogezea stori kuhusiana na huu mradi wa mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi) sasa hapa ni time ya kuona hizi picha za muonekano wa mabasi hayo kwa ndan na nje..
.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia akiwa katika kiti cha dereva.


Peremende zenye bangi zauzwa Kenya
Wizara ya afya nchini kenya imetoa orodha ya peremende, keki na biskuti bidhaa ambazo inadai zimewekwa bangi.
Katika kile ambacho kinatarajiwa kuwashanga wazazi, barui ambayo ilitiwa sahihi kwa niaba mahabara ya serikali, ilisema kuwa baadhi ya sampuli 176 zilizochukuliwa kwa peremende maarufu , keki na mandazi zilipatikana zikiwa na bangi baada ya kufanyiwa uchunguzi.

Monday, August 17

friendsKipindi cha nyuma kidogo niliwahi kuandika makala juu ya umuhimu wa kila mmoja kuwa na marafiki. Katika makala hayo nilisema wazi kwamba, kuishi bila marafiki ni tatizo na ukijaribu kufuatilia wale ambao hawana marafiki, maisha yao yana upungufu.
Nikashauri kwamba, ili maisha yako yakamilike ni vyema ukachagua marafiki ambao watakuwa ni wenye faida kwako. Lakini wakati nikishauri hivyo, wapo watu ambao naona wazi maisha yao hayana dira, wapo wapo tu kwa sababu ya aina ya watu ambao wamechagua wawe marafiki zao.
Unapochagua mtu wa kumfanya awe rafiki yako, ina maana umeona mnaendana katika mambo mbalimbali. Huwezi kumfanya mtu f’lani awe rafiki yako wakati unajua yeye ni mlevi na wewe si mlevi. Yeye ni mwizi, wewe hupendi kuwa hivyo! Ukiwa karibu na mtu huyo, ni rahisi sana kujiingiza huko.

Scary_Movie_AliensMakala: Sifael Paul
+255 682 105 366
Duniani kuna mambo mengi ya ajabu ambayo umewahi au hujawahi kusikia. Gazeti hili linapanda milima na kushuka mabondeni kisha kupaa angani kukuletea simulizi ya undani wa viumbe wa ajabu waishio au waonekanao angani. Ungana nami katika simulizi hii.
Huko nyuma niliwahi kudokeza kwenye gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa Wikienda lakini sikuingia ndani ili kupata ukweli juu ya viumbe hao wa ajabu waishio angani. Wanaitwa Aliens. Wana muonekano kama binadamu isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao waliogundulika karne kadhaa zilizopita, wameshatengenezewa filamu nyingi na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).

TIFFAH DIAMOND
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mtoto wake Princess Tiffah.
Musa mateja
Kazi ipo mwaka huu! Ndugu wa mzazi mwenzake na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamempa zawadi mtoto wa mastaa hao, Latiffah Nasibu ‘Princess Tiffah’ ndinga aina ya Mercedes Benz MSL Benz lenye thamani ya dola 100,000 (zaidi Sh. milioni 200).
MORO TITI (2)Halima Abdallah, anayedaiwa kucharangwa na mmewe.
Dustan Shekidele, Moro
My God! Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Nigar, mkazi wa Kijiji cha Kinole, Morogoro Vijijini anadaiwa kumcharanga mapanga mkewe, Halima Abdallah (28) na kummyofoa titi kisha kulitafuna na kumgeukia mwanaye Tausi (3) na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.
Tukio hilo lililomfanya mwanahabari wetu kufunga safari hadi kijijini hapo lilijiri Agosti 14, mwaka huu ambapo mwanaume huyo alikuwa kwenye shamba lao la migomba ndipo alipotekeleza unyama huo kabla ya kukamatwa na kufikishwa polisi.
MORO TITI (1)Wakizungumza na gazeti hili kijijini hapo, mashuhuda wa tukio hilo, Msimbe Joseph na Mchilo Agustino walisikitishwa na tukio hilo na kwamba hawakujua nini kilimpata baba Tausi
Screen Shot 2015-08-17 at 4.34.40 AM
Diamond Platnumz na crew yake wakati wa kuingia kwenye party
Sherehe za birthday nazo zina uzito wake, Unaambiwa Romy Jons ambaye ni Ndugu yake na msanii Diamond Platnumz lakini pia ni Official Dj wake alifanya Party yake August 16 2015 wakaalikwa mastaa wengi kutoka Bongo Movie na Bongo Fleva, kiukweli ilipendeza sana.
Diamond Platnumz ambaye ni ndugu pia ni rafiki wa karibu na Romy kwa pamoja walikutana na marafiki zao na kusheherekea party hiyo….. na kwenye list ya mastaa waliotokea walikuwepo pia Barnaba, Vee Money, Queen Darleen, Pipi, Aunt Ezekiel, Jux, Kamikaze, TID, Madee, Shilole, na wengine.

Katika pitapita zangu mtandaoni nimekutana na hii list ya wachezaji warefu zaidi katika Ligi Kuu Uingereza na wafupi zaidi katika Ligi Kuu Uingereza, nimeona nikusogezee Top 5 ya  mastaa wa soka warefu zaidi Uingereza na Top 5 ya mastaa wafupi.
Top 5 ya Mastaa wa fupi
5. Santiago Cazorla González huyu ni kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza yumo katika hii list ya wachezaji wafupi ana urefu wa futi 5’6,
santi-cazorla_g_2496350k
4. Huyu ni kiungo mshambuliaji wa Italia anayeichezea klabu ya Sunderland ya Uingereza Emanuele Giaccherini kuna kipindi aliwahi kuingia katika headlines ya kung’atwa

Saturday, August 15

Vote4Aisha.jpgVote4Daniel.jpg

LEO JUMAMOSI 
Southampton v Everton,  St. Mary's Stadium West Ham United v Leicester City,  Boleyn Ground Watford v West Bromwich Albion, Vicarage Road Swansea City v Newcastle United,  Liberty Stadium Sunderland v Norwich City,  Stadium of Light  Tottenham Hotspur v Stoke City,  White Hart Lane

KESHO JUMAPILI
Crystal Palace v Arsenal, Selhurst Park Manchester City v Chelsea,  Etihad Stadium


Askofu Dk.Allex Malasusa (kushoto) akiwa na mrithi wake Askofu Dk. Fredrick Shoo
****************
MAASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamemchagua Askofu Dk. FREDRICK SHOO kua mkuu mpya wa Kanisa hilo.


Uchaguzi huo uliofanyika jana kufuatia kumalizika kwa muda wa uongozi wa wa Askofu Mkuu wa KKKT Dk. Allex Malasusa. 


Na. Julius Mtatiro -

(TAHADHARI: Kama una Jazba usichangie POST hii - Utakufa kwa Presha Bure, Posti hii inaweza kuibua hisia kali, hofu, wasiwasi na majuto ikiwa unakubaliana na maoni haya au unayapinga na ikiwa mgombea wako amegongwa mahali hapa au ameparazwa, jadili hoja wala usimguse mtoa hoja)
                                        Ndugu zangu, 
Jana Chama Cha Mapinduzi kimetoa orodha ya wagombea wake nchi nzima. Katika orodha hiyo kuna watuhumiwa wengi tu wa masuala ya ufisadi, kuna watuhumiwa wengi wa rushwa na wengine walikamatwa na kuhojiwa na TAKUKURU, kwa kifupi kuna watuhumiwa kibao sana.

Mbunge wa Monduli anayemaliza muda wake, Waziri Mkuu wa zamani na Mgombea Urais aliyepitishwa na CHADEMA pamoja na Umoja wa UKAWA, Edward Lowassa alianza safari ya kuzunguka Mikoani kutafuta Wadhamini ambapo safari yake jana alianzia Mbeya.
IMG-20150815-WA0015
Freeman Mbowe akisindikizwa na Vijana wa Red Brigade baada ya kufika kwenye Viwanja vya Ruanda Nzovwe Mbeya ambapo Mkutano wa CHADEMA ulifanyika.
Tulizipata pichaz za kwanza kutoka huko na hizi ni nyingine pia ambazo zimenifikia nikaona nizisogeze hapa na wewe uone kila kilichoendelea baada ya Mgombea Urais huyo kupokelewa na watu wa Mbeya.
IMG-20150815-WA0030
Mgombea Urais Edward Lowassa akipunga mkono kuwasalimia watu

Monday, August 10

DSC_0613

Headlines za Siasa zinaendelea kubeba uzito wa juu Tanzania, August 10 2015 Mgombea Urais anayewakilisha UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa amefika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kuchukua Fomu yake.
Pichaz za kwanza nilikusogezea msafara uliotoka Makao Makuu wa CUF Buguruni Dar es Salaam, wwengine kwenye maagari, wengine bodaboda.. wengine walifunga safari kwa miguu kumsindikiza Mgombea huyo kutoka Buguruni mpaka Ofisi za NEC Posta alafu safari ikaendelea tena mpaka Makao Makuu ya CHADEMA, Kindondoni Dar.
DSC_0614
Ilionekana watu ni wengi sana, nafasi ya eneo hilo haikutosha… ikabidi umati wote usogee Viwanja vya BIAFRA ambapo Viongozi wa UKAWA walipata nafasi kuongea na Wanachama wao walioshiriki mwanzo mpaka mwisho kwenye safari hiyo.
2Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa na mkewe Josephine Mushumbushi.
Mwandishi Wetu
IMEVUJA! Siri ya kitu kilicho kichwani mwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa kuhusu mustakabali wake wa kisiasa umedaiwa upo kwa mkewe, Josephine Mushumbushi, Ijumaa Wikienda imevujishiwa.

Dr-Wilbroad-Slaa 
Dk. Wilbroad Slaa.
Chanzo cha kuaminika kilicho karibu na mwanasiasa huyo, kimeliambia gazeti hili kuwa mke wa kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania, anafahamu uamuzi uliochukuliwa na mumewe, isipokuwa kinachosubiriwa ni siku ya kutoboa kwa Watanzania.
-