Tuesday, December 1


flevaMwanamuziki Chinedu Okoli ‘Mr Flavour’.
WAKATI wanamuziki Bongo wakiendelea kuiga wanamuziki kutoka nje na kusahau kabisa muziki wao wa asili, wasanii wa Nigeria wamekuwa mfano wa kuigwa kwa kuimba nyimbo zenye vionjo vya ngoma zao za asili huku mwanamuziki Chinedu Okoli ‘Mr Flavour’ akiongoza kwenye listi hiyo.
Mwimbaji huyu mwenye ‘body’ la kutosha,anatajwa kupenda kufanya muziki wa asili ya makabila mbalimbali ya Nigeria kupitia baadhi ya nyimbo zake kama vile Nwa Baby, Adamma, Ololufe, Uyi, Ada Ada na nyingine nyingi.
Flavour anajulikana sana Bongo kupitia wimbo wake wa Ashawo ambao ulimpa umaarufu mkubwa kabla ya Wimbo wa Nana alioshirikishwa na Msanii Diamond Platnumz huku staili yake ya kucheza kifua wazi kwa kukata mauno ikimtofautisha na wasanii wengi wa levo yake


abiria wakisubiri usafiri abiria
Baadhi ya abiria wakisubiri usafiri bila mafanikio.


Kwa wiki ya pili sasa Rais Dkt Magufuli ameendelea kuwa gumzo barani Afrika na sasa hadi nchi za Ulaya zimedata naye.

Gazeti kubwa la Marekani, The Guardian limeandika habari isemayo: What would Tanzania’s cost-cutting president do? Twitter responds.
Pai  gazeti kubwa la  Australia,The Courier-Mail limeandika makala ndefu likimtaka Waziri mkuu wao,  Malcolm Turnbull ajifunze achapakazi toka kwa Rais wa Tanzania,Dr John Pombe Magufuli
Jina lake linatrend muda wote kwenye mtandao wa Twitter na kadri siku zinavyooenda habari za utendaji wake zinazidi kuenea.
Katika mtandao huo wa Twitter, imeanzishwa Verb ya jina la Magufuli iitwayo  magufulify ambayo imepewa maana ifuatayo;


Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akiongea na Waandishi wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7 katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya Stanbink Tanzania.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7 katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya Stanbink Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bwana Assah Mwambene.

Kama uliipata stori ya Mamlaka ya Mapato TRA kunasa makontena tisa eneo la Tanki Bovu Mbezi Dar es Salaam, nina muendelezo wake mtu wangu kuhusu majibu ya TRA walivyonasa mzigo huo.
Hapa ni nukuu ya alichokisema Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu ya Walipa Kodi wa TRA >>> ‘Tulipata taarifa kutoka kwa watu kwamba kuna kontena zinahamishwa kutoka bandari kavu ya Vingunguti usiku wa manane kuja kwenye godown iliyopo eneo la Mbezi Tanki Bovu ambayo sio rasmi na haiko kwenye orodha ya bandari kavu zilizo kwenye uangalizi wa TRA‘>>- Mkurugenzi Richard Kayombo.
IMG-20151201-WA0015
Kwenye sentensi nyingine za Richard Kayombo >>> ‘Tumeshirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha tunafika eneo hili na kuliweka chini ya ulinzi…. Hapa yapo makontena tisa, vilevile tumekuta magari matatu ambayo yalikuwa yanabeba haya makontena, madereva wake wako chini ya ulinzi.’
Baada ya hapo kilichofatia ni hiki >>> ‘Uchunguzi wetu tumemfahamu mwagizaji wa makontena pamoja na wakala wa forodha ambaye alikuwa anashughulikia makontena haya… Makontena yalipata kibali cha kupelekwa eneo la EPZ Ubungo September 17 2015, lakini kibali kimepita muda wake na cha kushangaza ni kwamba kontena hizi zimeletwa huku ambako sio mahali rasmi, ni kiashiria kwamba kuna jambo baya lilitaka kutokea kama ukwepaji wa kodi.’
IMG_20151201_131138
Sentensi za mwisho kwenye ufafanuzi huo hizi hapa >>> ‘Tutabaini kila kitu baada ya kupata nyaraka halisi na kuwapata mwagizaji na wakala wa forodha ambao wanatakiwa kujitokeza ndani ya saa 24… wasipojitokea tutafungua makontena kuangalia kilichomo, kama ni bidhaa halali tutazitaifisha, na kama ni bidhaa haramu zitateketezwa…‘ >>- Richard Kayombo.



Tayari uongozi mpya chini ya Rais Dk. John Magufuli umeanza kazi..ikiwa ni siku chache baada ya uteuzi wa Waziri mkuu Majaliwa Kassim kupewa madaraka, yapo mambo mengi ambayo tayari ameanza kuyatekeleza.
Jana jioni kwenye ofisi ya waziri mkuu kulikuwa na hafla fupi ya makabidhiano kati ya waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda ambaye alimtembelea Waziri  mkuu mpya ikiwa ni pamoja na kumkabidhi ofisi.
Hapa ninazo baadhi ya picha wakati wa makabidhiano hayo..
maja1

maja2

maja3

maja4

maja5

maja6

maja7

maja8

Friday, November 27

Idadi ya makontena 31 yaliyobeba magogo yamekamatwa katika bandari ya Dar es salaam yakidaiwa kutokea Zambia.
Wizara ya Maliasili na Utalii baada ya kupata taarifa hiyo kupitia vyombo vyake vya upepelezi iliamua kufuatilia na kugundua makontena hayo yenye thamani ya zaidi ya milioni 300 yameingizwa nchini kinyemela na makampuni matatu ambayo bado yanafanyiwa uchunguzi.
Utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli umekuwa topic kubwa sana kwenye mitandao mbalimbali ya Tanzania na nchi za jirani… Mwanzoni nilikusogezea tweets za Wakenya zikimgusa Rais Magufuli kwenye kona mbalimbali za utendaji kazi wake ambazo nyingi zilikuwa za kumpongeza.
Leo nimechukua tena time ya kutembelea tena mtandao wa kijamii wa Twitter na huko nimekutana na ‘hashtag’ mpya ya Rais Magufuli, yenyewe inaitwa ‘#WhatWouldMagufuliDo’ (‘#MagufuliAngefanyaNini’) ambayo kuanzia jana ilianza kuweka headlines kwenye twitter kutokana na matumizi yake!

Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.
Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.
“Hazina inazo pesa za kutosha  na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu,  kununua mashine za BVR  kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi  na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu” alisema Bwa. Cheyo.

Monday, November 23

 
 Rapa maarufu wa Marekani, Mathew Matthers Eminem.
UNAWEZA kudhani ni utani lakini hili limetokea nchini Uingereza baada ya jopo la watafiti nchini humo kutoa utafiti wao kuwa nyimbo za rapa maarufu wa Marekani, Mathew Matthers zinaongeza morali ya mazoezi na spidi kwa wanamichezo.


Kwa mujibu wa  Sheria ya Sikukuu za Kitaifa  (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameamua kuwa maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9 Desemba, 2015, yatumike  kwa kufanya kazi.  
 


Uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli kueleza kwa kina namna safari holela za nje ya nchi zinavyoligharimu taifa mabilioni ya fedha, umeianika wazi Serikali iliyopita ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete na kuibua mjadala mkubwa miongoni mwa baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya siasa nchini.

Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kiasiasa wanasema kuwa ujasiri wa Rais Magufuli kueleza bila kificho jinsi safari za nje zinavyogharimu taifa kabla ya kutangaza msimamo mkali wa kuzidhibiti umedhihirisha pasi na shaka kuwa rais huyo mpya amedhamiria kubana matumizi holela ya fedha za serikali na badala yake kuzielekeza katika shughuli za maendeleo kwa nia ya kuboresha maisha ya Watanzania.

Wakati akilihutubia Bunge la 11 Ijumaa iliyopita kisha kulizindua rasmi, Rais Magufuli aliwataka wabunge na Watanzania wote wamuunge mkono katika uamuzi wake wa kupiga marufuku safari holela za nje huku akisisitiza kuwa kwa kufanya hivyo, fedha nyingi zinazopotea zinaweza kutumiwa katika kuboresha huduma za jamii.


KESI ya kuagwa kwa heshima kwa Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Geita, Marehemu Alphonce Mawazo, imefunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Mwanza.

Kesi hiyo namba 10 ya mwaka 2015, imefunguliwa jana na familia ya marehemu Mawazo, imepangwa kusikilizwa kesho baada ya washitakiwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo na mwanasheria mkuu wa Serikali kupelekewa mashtaka.

Kesi hiyo inayosimamiwa na mawakili watatu, John Mallya, James Millya na Paul Kipeja, leo ilikuwa ni mara ya kwanza kusikilizwa mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwanasheria wa Chadema, John Mallya, alidai kuwa kesi hiyo itatajwa leo baada ya washitakiwa hao kupelekewa samansi ya kesi inayowakabili.

“Tunashukru Jaji, Lameck Mlacha, amekubali kuisikiliza, kesi hii tuliofungua kwa hati ya dharura, katika mahakama ya kanda kuu ya Mwanza, kwani ni haki ya msingi kuagwa kwa mtu yeyote,” amesema Mallya.

Wednesday, November 11

Headlines za Mbwana Samatta kutwaa kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora wa michuano ya klabu Bingwa barani Afrika bado zinazidi kuchukua nafasi, baada ya November 11 kurejea Dar Es Salaam akitokea Lubumbashi Congo ambako ndio makao makuu ya klabu yake ya TP Mazembe ambayo Jumapili ya November 8 ilitwaa taji la klabu Bingwa Afrika kwa kuifunga klabu USM Alger ya Algeria kwa jumla ya goli 4-1.
Samatta 3
Hizi ni pichaz za mapokezi ya Mbwana Samatta aliyoyapa kutoka kwa familia yake baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Dar Es Salaam, baada ya kurudi Tanzania Samatta atajiunga na kikosi cha  Taifa Stars ambacho kinarejea leo November 11 saa 12 jioni kutokea Afrika Kusini kilipokuwa kimeweka kambi ya maandalizi ya m
Leo Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe pamoja na aliyekuwa mgombea Urais wa chama hicho Anna Mghwira wamezungumza na waandishi wa habari ikiwa ni mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.
Katika mkutano huo Mwenyekiti wa chama hicho Anna Mgwhira alitumia nafasi hiyo kuweza kuwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kuwasuport katika kipindi chote cha kampeni na kukifanya chama kuzidi kuwa imara zaidi.
Zitto Kabwe naye alizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo kumpongeza Mwenyekiri wake Anna Mgwhira kwa kumsaidia kukitangaza chama hicho na kupandisha taswira ya chama chao mbele ya umma.
“Kazi iliyopo mbele yetu ni kukijenga chama na kukifanya kifike mbali zaidi, tumefanikiwa kupata kiti kimoja cha ubunge lakini tutatumia kiti hicho kupaza sauti ndani ya bunge..ikumbukwe sisi tulisema waziwazi kuhusu rushwa tofauti na vyama vingine vya upinzani ambavyo havikuwa wazi”..Zitto

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli tayari ameapishwa na kuanza kazi… kwa upande wa Wabunge wenyewe bado.
Kinachosubiriwa ni kuitishwa kwa Bunge la 11 ambapo Spika Mteule pamoja na Wabunge wote wataapishwa… kingine kitakachofanyika ni uthibitisho wa jina la Waziri Mkuu, uchaguzi wa Naibu Spika na ufunguzi rasmi wa Bunge la 11.
BungeTZ
Kulikuwa na stori nyingi sana wakati wa mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu ikiwemo matokeo kukataliwa na baadhi ya Wagombea, kwingine Uchaguzi haukufanyika kabisa, kwingine uchaguzi ulisogezwa mbele kwa sababu mbalimbali. Lakini mpaka leo November 11 2015 hapa ninayo majina ya Wabunge 256 ambayo Tume ya Uchaguzi NEC imeyathibitisha kwamba wamepita kwenye Uchaguzi na wanasubiri kuapishwa.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UCHAGUZI WA UBUNGE NA UDIWANI ULIOAHIRISHWA KUTOKANA NA VIFO VYA WAGOMBEA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote kuwa Uchaguzi wa Ubunge na Udiwani katika Majimbo na Kata ambazo hazikufanya Uchaguzi tarehe 25 Octoba 2015 kwa sababu za vifo vya wagombea sasa Uchaguzi huu utafanyika tarehe22 Novemba 2015; 13 Desemba, 2015 na 20 Desemba, 2015.

Majimbo,Kata na tarehe watazofanya Uchaguzi ni kama ifuatavyo:

22 Novemba 2015
Na.
JIMBO
MKOA
1.
LUSHOTO
TANGA
2.
ULANGA MASHARIKI
MOROGORO
IMG-20151110-WA0026 Trela la lori lenye namba za usajili T863 AEF limepinduka mchana wa leo eneo la Polisi Ufundi, Barabara ya Kilwa jijini Dar. Ajali hiyo imetokea baada ya lori lililokuwa likivuta trela hilo kujaribu kukwepa gari dogo lililokuwa likitokea mbele yake.

Sitta 2 Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuchukua fomu za kuwania uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib.
sitta Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akizungumza na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed
2
Mrembo akikatiza katika mitaa ya Jiji la Hong Kong bila kuvaa nguo za ndani.
6
...Akielekea kufanya manunuzi kwenye maduka.
5
...Akinunua tiketi ya treni.

Tuesday, November 10



Siku chache baada  ya  kufuta  safari  za  vigogo  nje ya  nchi,Rais  wa  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  Dr John Magufuli  anakusudia  kufyeka wizara  8  miongoni  mwa  28  zilizopo  sasa  ili  kubana  matumizi.

Hatua  hiyo  ya  Dr  Magufuli  ni  sehemu  ya  utekelezaji  wa  ahadi  alizozitoa  kwa  wananchi  wakati  akijinadi  kwenye  kampeni  zake  za  kuwania  Urais  kupitia  Chama  cha  Mapinduzi-CCM  kwamba  atapunguza  ukubwa  wa  serikali  kwa  kuunda  baraza  dogo  la  mawaziri.

Katika  miaka 10  ya  uongozi  wa  Rais  Kikwete, kumekuwa  na  malalamiko  ya  ukubwa  wa  baraza  la  Mawaziri  huku  baadhi  ya  wizara  zikiwa  na  mawaziri  watatu.


Aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Frederick Mwakalebela amefungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Iringa mjini yaliyompa ushindi Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema huku akiitaja kofia ya M4C katika shtaka lake.

Msajili msaidizi wa mahakama kuu ya kanda ya Iringa , Ruth Massama amesema kuwa Mwakalebela alifungua shtaka hilo mahakamani hapo Oktoba 30 mwaka huu.

Katika shitaka hilo, pamoja na mambo mengine, Mwakalebela anamtuhumu Msigwa kwa kuvunja sheria ya uchaguzi kwa kuvaa kofia yenye nembo ya M4C inayotumiwa na Chadema,  katika siku ya kupiga kura.

Kadhalika, mlalamikaji huyo anamtuhumu mwangalizi wa uchaguzi kwa kukiuka sheria na kanuni za uchaguzi wakati wa zoezi la kupiga na kuhesabu kura.

Katika madai yake, Mwakalebela ameeleza kuwa katika kata ya DaboDabo alikataliwa kuingia katika kituo cha kupigia kura wakati wakati mshindani wake huyo aliruhusiwa kuingia bila kizuizi chochote.

Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Iringa Mjini alimtangaza Mchungaji Peter Msigwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo hivyo kupata nafasi ya kuendelea kuliwakilisha jimbo hilo kwa muhula wa pili.


Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa ushauri wake kwa kiongozi mkuu wa nchi ili kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo.
 
Zitto ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook, japo hakutaja jina lakini maelezo yake yanaonesha kuwa mwenye uwezo wa kufanya maamuzi hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, ndiye mlengwa wa ujumbe huo.
 
Hivi ndivyo alivyoandika:

Justin Bieber.
KAMA wewe ni mdau wa burudani, Jina la JUSTIN BIEBER linaweza lisiwe geni masikioni mwako hasa kutokana na umaarufu mkubwa alioupata kupitia kipaji chake cha uimbaji tangu akiwa kijana mdogo.
Bieber aliyeanza kutambulika mwaka 2008 akiwa na miaka 14 na kujulikana zaidi kupitia kibao chake cha Baby alichomshirikisha mkali wa Hip Hop,Ludacris, ameweza kuwa mmoja kati ya wasanii wenye umri mdogo wanaoingiza mkwanja wa kutosha kupitia muziki wake huku mafanikio yake yakitumika kama mfano wa vijana wengine wanaochipukia kwenye tasnia hiyo.


Mkongwe wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya For You, Abubakari Katwila ‘Q Chillah’.
Mkongwe wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya For You, Abubakari Katwila ‘Q Chillah’ amefunguka kuwa ukubwa wa jina lake ndiyo umemrudisha kwenye gemu kwa kasi na kumfanya ajitume sana kufanya muziki wake.
kizungumza na paparazi wetu, Q Chillah alisema kuwa katika kipindi alichokuwa kimya aligundua kuwa watu wengi walikuwa wakimiss kazi zake jambo ambalo lilimfanya agundue ukubwa wa jina lake hivyo kuamua kupambana kwenye muziki ili arudishe heshima aliyojitengenezea siku za nyuma.
Inawezekana ulikuwa na maswali mengi kuhusu mipango ya harusi ya staa wa Bongo Fleva Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz na Zari sasa basi ameyajibu kupitia kipindi cha Mseto cha Citizen kinachoendeshwa na Willy Mtuva.
Harusi haina muda mre


Utamaduni wa wanafunzi kuwatunga majina waalimu wao ulikuwepo toka zamani na mara nyingi mwalimu anaweza kutungwa jina ambalo yeye akawa halijui ila kutokana na tabia na muonekano wake basi wanafunzi hupenda kumtunga jina linaloendana na tabia zake kama ni mkali usishangae ukisikia akipewa jina la ajabu kama mnoko na kadhalika.
PAY-Man-United-arrive-at-The-Lowry-Hotel
Stori zilizotoka mtandaoni ni kuwa wachezaji wa klabu ya Manchester United wameamua kumtunga jina kocha wao raia wa Uholanzi Louis van Gaal, wachezaji wa Man U
Kwenye countdown zenye headlines za Siasa, bado macho na masikio ya wengi yako kwenye maeneo machache sasahivi, nani ni Waziri Mkuu TZ? Nani Spika wa Bunge TZ?
Majibu yatapatikana soon ila kwa sasa bado… inawezekana Waziri Mkuu akateuliwa toka chama cha upinzani?
tulia ackson
Dk.Tulia Ackson
Nimempata kwenye exclusive Dk.Tulia Ackson ambaye ni Wakili wa Serikali, ana majibu haya kuhusu uwezekano wa Serikali ya Tanzania kuongozwa na

Saturday, November 7

STAA asiyekaukiwa matukio Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewacharukia watu wanaohoji kwa nini anapendeza angali mwanafunzi kwa kuwaambia, ‘kwani akiwa mwanafunzi ni mwiko kupendeza?’
Staa asiyekaukiwa matukio Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Lulu alisema amekuwa akiona maon


-