Umewahi kufikiria manyoya ya kuku yanaweza kutumika kuwa kinga ya kuzuia mbu?hii ni kweli baada ya wataalamu wa mambo ya afya kudhibitisha hilo na kusisitiza ina uwezo huo kama ilivyo kwa vyandarua vinavyotengenezwa viwandani.
Wanasayansi kutoka Taasisi ya Afya Ifakara ‘IHI’ wamegundua mradi wa kutengeneza vyandarua kwa kutumia manyoya ya kuku yaliyorundikwa nyumbani na majalalani ikiwa ni moja ya jitihada za kuendeleza vita dhidi ya ugonjwa wa malaria hasa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti wa kila mwezi iliyotolewa na Taasisi hiyo kwenye Gazeti la NIPASHE,manyayo hayo yatakua yanakusanywa kutoka maeneo ya masoko na kwenye makazi ya watu.